WABUNGE MLICHANGIA CHAMA AMA SACCOS?
Ni ukweli kuwa kuna michango ya wabunge inayopelekwa ofisi ya chama makao makuu.
Ni ukweli kuwa kumekuwepo _minong'ono_ Dodoma kuhusu michango hiyo kwamba iko wapi na inafanya nini?
Sasa kwamba Kigogo ameipata hiyo, sioni ubaya. Wala sioni ubaya yeye kuibandika jukwaani na hadharani.
Ni ukweli kwamba Kigogo si mbunge wa CHADEMA wala si mtumishi makao makuu. Kwa hiyo hana popote atakakopata taarifa hii ya siri. Lazima amepelekewa na mmoja wa wabunge. Lwa hiyo Kigogo hana kosa lolote katika hatua ya sasa. Labda hapo baadaye.
Sasa tujiulize; kama ilikuwa sahihi wabunge kuchangia chama chao hela kama shukrani kwa kuwadhamini na kukiimarisha chama kimfumo.
Nashindwa kujua ni nini makubaliano baina ya wabunge wetu na chama nyuma ya michango hiyo. Ikumbukwe kuwa michango hii ni takwa la katiba ya chama. Hakuna kwenye katiba inapoelezwa kwamba wabunge wakiisha changa watauliza iliko hela waliyochanga.
Kama kweli maelezo yanayotolewa ni kwamba walikuwa wakichangia katika mfuko wa chama kwa ajili ya uchaguzi ujao 2020, kwa nini maulizo haya yanakuja leo?
Sijui kama wabunge wetu wanachanga ili warudishiwe hizo hela ama wanachanga ili hela zitumiwe na chama kwa mujibu wa mipango yake?
Je, wabunge wanaona sadaka yao ya fedha ni kubwa kiasi kwamba haiwezi kujadiliwa ndani ya chama bali nje kulikojaa maadui zetu? Je ni kweli chama kilichowajenga na kuwapa ubunge sasa kinapokea fadhila ya kubomolewa na ninyi mlioshiba na kung'aa kwa jina la chama?
Kuna anayefikiri mnamkomoa Mbowe. Lakini niwaambie sisi wenzenu tuliofanya kazi miaka nenda rudi. Usiku na mchana tukawajengea mtandao imara ambao kwao mlikuja kushinda ubunge. Sisi tuliopoteza fursa nyingi kwa kuwa tulijitambulisha na upinzani. Sisi tuliopoteza mali nyingi kwa kugharamikia upinzani. Sisi tulionyang'anywa mali na kuhatarishwa maisha yetu kwa kuwa tumeamua kukipigania chama chenu. Sisi tuliojazwa madonda kutoka kwa watawala wanaokasirishwa na uimara wa chama chetu; leo mnaongezea pilipili kwenye madonda yetu. Hakika ukatili huu ni mkubwa sana.
Hivi wabunge wanapodai sehemu ya mshahara wao wanaouchanga kwa ajili ya chama walituambia lini sehemu inayobaki wameitumia vipi kwa ajili ya majimbo na chama katika mikoa na kanda zao.
Nilibahatika kusikia mahali kuhusu harakati ndani ya chama dhidi ya Mbowe. Harakati hizi pia zilikuwa dhidi yake kama KUB.
Wabunge wetu hawa nilinusa habari kuwa katika kikao kimoja cha kambi walisimama na kumpongeza Mhe. Zitto kwa kazi nzuri aliyofanya ya kumhudumia Lissu bila kumtaja Mbowe popote. Ilipikwa fitina dhidi ya Mbowe kwamba katika tukio la kishambuliwa kwa Lissu, Mbowe ndiye "wasiojulikana". Hii si ile propaganda ya CCM bali ni ya ndani ya chama na iliyoasisiwa bungeni.
Chama kimenyamazia wabunge hawa kwa muda mrefu. Wamejiona wafalme wa chama. Wanajua kosa la kupeleka habari za chama nje ya vikao rasmi vya chama. Je huu si uvunjifu wa kanuni na katiba ya chama kwa makusudi?
Kwa hapa walipotufikisha, Nitashangaa sana:
1. Kama tutawanyamazia. Hatuhitaji msaada wa Kamati Kuu wala Baraza Kuu. Tuwapa vidonge vyao huku huku.
2. Tuwajazie taarifa za imani yetu kwa Mbowe. Na tahadhari kwamba titawashambulia kushoto, kulia, mbele na nyuma wakiendelea na majaribio yao haya.
Waheshimiwa makamanda. Mti wenye matunda ndiyo utupiwao mawe. Hawa wabunge nani amewasikia majimboni ama katika harakati za kumaanisha za kujenga chama?
Mbowe kwa ajili yetu na taifa amepitia madhila mangapi? Mali zake zilizoharibiwa ni za bei gani? Akaunti zake zilizofungwa ni za thamani gani? Amepoteza vingapi ili kutufikisha hapa tulipo.
Kwa nini wabunge wetu wachague kumlipa fedheha badala ya fadhila kwa harakati zote alizofanya hadi kufikia hapa tulipo!
Naogopa kumadress Mbowe katika hili. Ila nitawashanga mkiwanyamazia wabunge hao wanaoiona sadaka yao kuwa ni kubwa kuliko za watu wengine ambao hawajalipwa mishahara na posho za kibunge kama wao.
Hivi mimi nimekuwa katibu wa mkoa kwa miaka 10. Sijawahilipwa mshahara miaka yote hiyo. Je sadaka yangu hii ambayo niliitoa ili wapatikane wabunge nani alitakiwa ailipe? Mmeniletea lini mafuta pipa moja la kufanya ziara mkoani kwangu. Aje hapa Katibu mwenzangu yeyote wa mkoa aonyeshe anavyolipwa fadhila na wabunge aliowapigania.
Nasema semeni yote muyatakayo, fanyeni yote muyawezayo, nendeni popote mtakako:
Mwenyekiti wetu ajaye ni *FREEMAN AIKAEL MBOWE.*