Wabunge waasi CHADEMA hawa hapa

Wabunge waasi CHADEMA hawa hapa

WABUNGE MLICHANGIA CHAMA AMA SACCOS?

Ni ukweli kuwa kuna michango ya wabunge inayopelekwa ofisi ya chama makao makuu.

Ni ukweli kuwa kumekuwepo _minong'ono_ Dodoma kuhusu michango hiyo kwamba iko wapi na inafanya nini?

Sasa kwamba Kigogo ameipata hiyo, sioni ubaya. Wala sioni ubaya yeye kuibandika jukwaani na hadharani.

Ni ukweli kwamba Kigogo si mbunge wa CHADEMA wala si mtumishi makao makuu. Kwa hiyo hana popote atakakopata taarifa hii ya siri. Lazima amepelekewa na mmoja wa wabunge. Lwa hiyo Kigogo hana kosa lolote katika hatua ya sasa. Labda hapo baadaye.

Sasa tujiulize; kama ilikuwa sahihi wabunge kuchangia chama chao hela kama shukrani kwa kuwadhamini na kukiimarisha chama kimfumo.

Nashindwa kujua ni nini makubaliano baina ya wabunge wetu na chama nyuma ya michango hiyo. Ikumbukwe kuwa michango hii ni takwa la katiba ya chama. Hakuna kwenye katiba inapoelezwa kwamba wabunge wakiisha changa watauliza iliko hela waliyochanga.

Kama kweli maelezo yanayotolewa ni kwamba walikuwa wakichangia katika mfuko wa chama kwa ajili ya uchaguzi ujao 2020, kwa nini maulizo haya yanakuja leo?

Sijui kama wabunge wetu wanachanga ili warudishiwe hizo hela ama wanachanga ili hela zitumiwe na chama kwa mujibu wa mipango yake?

Je, wabunge wanaona sadaka yao ya fedha ni kubwa kiasi kwamba haiwezi kujadiliwa ndani ya chama bali nje kulikojaa maadui zetu? Je ni kweli chama kilichowajenga na kuwapa ubunge sasa kinapokea fadhila ya kubomolewa na ninyi mlioshiba na kung'aa kwa jina la chama?

Kuna anayefikiri mnamkomoa Mbowe. Lakini niwaambie sisi wenzenu tuliofanya kazi miaka nenda rudi. Usiku na mchana tukawajengea mtandao imara ambao kwao mlikuja kushinda ubunge. Sisi tuliopoteza fursa nyingi kwa kuwa tulijitambulisha na upinzani. Sisi tuliopoteza mali nyingi kwa kugharamikia upinzani. Sisi tulionyang'anywa mali na kuhatarishwa maisha yetu kwa kuwa tumeamua kukipigania chama chenu. Sisi tuliojazwa madonda kutoka kwa watawala wanaokasirishwa na uimara wa chama chetu; leo mnaongezea pilipili kwenye madonda yetu. Hakika ukatili huu ni mkubwa sana.

Hivi wabunge wanapodai sehemu ya mshahara wao wanaouchanga kwa ajili ya chama walituambia lini sehemu inayobaki wameitumia vipi kwa ajili ya majimbo na chama katika mikoa na kanda zao.

Nilibahatika kusikia mahali kuhusu harakati ndani ya chama dhidi ya Mbowe. Harakati hizi pia zilikuwa dhidi yake kama KUB.

Wabunge wetu hawa nilinusa habari kuwa katika kikao kimoja cha kambi walisimama na kumpongeza Mhe. Zitto kwa kazi nzuri aliyofanya ya kumhudumia Lissu bila kumtaja Mbowe popote. Ilipikwa fitina dhidi ya Mbowe kwamba katika tukio la kishambuliwa kwa Lissu, Mbowe ndiye "wasiojulikana". Hii si ile propaganda ya CCM bali ni ya ndani ya chama na iliyoasisiwa bungeni.

Chama kimenyamazia wabunge hawa kwa muda mrefu. Wamejiona wafalme wa chama. Wanajua kosa la kupeleka habari za chama nje ya vikao rasmi vya chama. Je huu si uvunjifu wa kanuni na katiba ya chama kwa makusudi?

Kwa hapa walipotufikisha, Nitashangaa sana:
1. Kama tutawanyamazia. Hatuhitaji msaada wa Kamati Kuu wala Baraza Kuu. Tuwapa vidonge vyao huku huku.
2. Tuwajazie taarifa za imani yetu kwa Mbowe. Na tahadhari kwamba titawashambulia kushoto, kulia, mbele na nyuma wakiendelea na majaribio yao haya.

Waheshimiwa makamanda. Mti wenye matunda ndiyo utupiwao mawe. Hawa wabunge nani amewasikia majimboni ama katika harakati za kumaanisha za kujenga chama?

Mbowe kwa ajili yetu na taifa amepitia madhila mangapi? Mali zake zilizoharibiwa ni za bei gani? Akaunti zake zilizofungwa ni za thamani gani? Amepoteza vingapi ili kutufikisha hapa tulipo.

Kwa nini wabunge wetu wachague kumlipa fedheha badala ya fadhila kwa harakati zote alizofanya hadi kufikia hapa tulipo!

Naogopa kumadress Mbowe katika hili. Ila nitawashanga mkiwanyamazia wabunge hao wanaoiona sadaka yao kuwa ni kubwa kuliko za watu wengine ambao hawajalipwa mishahara na posho za kibunge kama wao.

Hivi mimi nimekuwa katibu wa mkoa kwa miaka 10. Sijawahilipwa mshahara miaka yote hiyo. Je sadaka yangu hii ambayo niliitoa ili wapatikane wabunge nani alitakiwa ailipe? Mmeniletea lini mafuta pipa moja la kufanya ziara mkoani kwangu. Aje hapa Katibu mwenzangu yeyote wa mkoa aonyeshe anavyolipwa fadhila na wabunge aliowapigania.

Nasema semeni yote muyatakayo, fanyeni yote muyawezayo, nendeni popote mtakako:

Mwenyekiti wetu ajaye ni FREEMAN AIKAEL MBOWE.

Update 2:

Anaandika Halima James Mdee (Mb), Mjumbe Wa Kamati Kuu CHADEMA.

Sisi wabunge tunaochangia PESA na ambao ni WAJUMBE wa KAMATI KUU tunaopata fursa ya kupata taarifa za MAPATO na Matumizi ya CHAMA TUNATHIBITISHA hakuna hata 100 iliyoliwa na MTU..Wakongwe katika hiki CHAMA tunajua kila mwaka wa UCHAGUZI ukifika kuna CHOKOCHOKO nyingi zinazohusu FEDHA. Najiuliza tu, hivi kama hizo pesa za UMMA zinapigwa na WATU kwenye CHAMA namna hiyo mbona SERIKALI ya CCM tena MAGUFULI anavyotuchukia ASITUFUNGULIE MASHTAKA YA UHUJUMU UCHUMI??

Hivi MNAVYOONA SHUGHULI za CHAMA zinaendelea NCHI nzima yenye ukubwa wa sQuare KM 945,087 mnadhani pesa inatoka wapi? Mnavyoona Pikipiki zinakwenda nchi NZIMA sio mara moja au mbili mnadhani pesa zinatoka wapi? Mnapoona M4C mpya zinanunuliwa mnadhani pesa inatoka wapi?? Sasa hivi CHAMA kiko kwenye Chaguzi NCHI nzima mnadhani pesa zinatoka wapi? Mnajua gharama za Matibabu ya KAMANDA wetu mpaka sasa hivi IMEGHARIMU kiasi GANI na CHAMA kimeshatumia KIASI gani ??Mnataka SASA tuanze kurusha Twitter AU INSTAGRAM au kwenye HIZI groups???mapato na matumizi ya chama?? Wenyeviti na MAKATIBU wa KANDA zenu WAJUMBE wa KAMATI KUU, wanajua TAARIFA zote za FEDHA. Wafuateni KWENYE ofisi zao wawape Ufafanuzi wa jambo lolote mnalodhani linahitaji ufafanuzi. Ni kweli kuna wabunge ambao UTEKELEZAJI wa TAKWA la KATIBA la KUCHANGIA chama umekuwa ukiwauma SANA.

Hawajawahi kutaka toka awali, hawa ndio walienda kulalamika kwa NDUGAI na Hawa ndio wanafanya kazi na CCM Bungeni kuumiza au kuwachonganisha wabunge wenzao na MHIMILI. Miaka yote kabla 2015, tumekuwa tukichanga kwa kukatwa moja kwa moja na ofisi ya katibu ya Bunge.

Baada ya 2015 tumeendelea kukatwa mpaka hao WAPUUZI wanaojulikana hawajaenda kwa ADUI yetu kumwambia CDM haitetereki sababu wabunge tunachangia na kwamba AKIZUIA CHAMA kitasota, na KWELI YULE PIMBI akazuia. Kumbe wabunge WALIOPELEKA HUO uzushi wamesukumwa na UBINAFSI wao wa KUKOPA mpaka kupitiliza... mpaka kufikia hatua ya kuona MCHANGO HALALI wa KIKATIBA ni HISANI kwa CHAMA.

Wamesahau na SISI huko nyuma tukiwa WACHACHE tulichanga kwa UAMINIFU MKUBWA ndio maana WAO wakapatikana. Tuna wabunge WAFIA CHAMA, lakini pia tuna wabunge MASLAHI . Ni ukweli mchungu!! Tukiimarishe CHAMA , tupate WAWAKILISHI wanaotanguliza MASLAHI ya UMMA na CHAMA kabla ya MASLAHI yao BINAFSI. Nashukuru MUNGU MAGUMU tunayoyapitia MSIMU HUU yanatukomaza na kutufanya TUJUANE ZAIDI.
Nimesoma mpaka mwisho sijaona majina yao!
 
Nyie kukosoa ni haki,mkikosolewa nyie, wanaowakosoa ni wasaliti.😂😂​
Hakuna ukosoaji wowote zaidi ya utapeli wa kutaka kugombanisha chama.Tumewagundua mchana kweupe
 
Akiwemo Mbowe,baada ya kuwasaliti wenzake na kumteua lowassa pandikizi la ccm
Kura zaidi ya mil 6 hakuwa za Lowassa,ni za Chadema.Zuruku yao ikaongezeka sana.Kama alikuwa pandikizi basi ni pandikizi lenye faida.Kamanda wao wa anga alicheza kama pele.Kwa mtazamo wangu,Mbowe ni mwanasiasa bora kabisa kwa sasa.
 
Hakuna ukosoaji wowote zaidi ya utapeli wa kutaka kugombanisha chama.Tumewagundua mchana kweupe
Acheni ujanja ujanja mkuu vinginevyo mtapoteza uhalali wa kuikosoa serikali ya CCM.​
 
Kura zaidi ya mil 6 hakuwa za Lowassa,ni za Chadema.Zuruku yao ikaongezeka sana.Kama alikuwa pandikizi basi ni pandikizi lenye faida.Kamanda wao wa anga alicheza kama pele.Kwa mtazamo wangu,Mbowe ni mwanasiasa bora kabisa kwa sasa.
Sidhani kama atarudi tena
 
Tutawaondoa wasaliti wote
Halafu nyie ndio mnataka mpewe nchi muongoze?😂😂

Mwanachama akihoji matumizi ya pesa za chama anakuwa MSALITI.

Mwanachama akitaka mabadiliko ya uongozi anakuwa MSALITI.

Raia wakihoji mnavyotumia kodi zao si mtawamaliza?
​
 
Halafu nyie ndio mnataka mpewe nchi muongoze?[emoji23][emoji23]

Mwanachama akihoji matumizi ya pesa za chama anakuwa MSALITI.

Mwanachama akitaka mabadiliko ya uongozi anakuwa MSALITI.

Raia wakihoji mnavyotumia kodi zao si mtawamaliza?
​
Hawa watu hawawezi kuongoza nchi hata wao wanajua! Siku moja nilimuuliza kada mtiifu was chadema kuhusu mwenyekiti wao kushika nyazifa hiyo kwa mda mrefu alinijibu kwamba hayupo mwingine jasiri swali likaja nikajiuliza kama akiwa raisi Kuna hatari ya kuwa life president kulingana na sifa anayopewa na historia aliyonayo ya kuwa mwenyekiti wa mda mrefu huyo jamaa abatukuzwa kwenye chama hatari na anayehoji uenyekiti wake hufukuzwa chamani hata tundu lisu analijua Hilo!poleni makamanda endeleeni kusifu na kumpigia mapambio mwenyekiti wenu hiyo demokrasia mnayoitaka nashauri ianze chamani#2020# tutaelewana tu
 
WABUNGE MLICHANGIA CHAMA AMA SACCOS?

Ni ukweli kuwa kuna michango ya wabunge inayopelekwa ofisi ya chama makao makuu.

Ni ukweli kuwa kumekuwepo _minong'ono_ Dodoma kuhusu michango hiyo kwamba iko wapi na inafanya nini?

Sasa kwamba Kigogo ameipata hiyo, sioni ubaya. Wala sioni ubaya yeye kuibandika jukwaani na hadharani.

Ni ukweli kwamba Kigogo si mbunge wa CHADEMA wala si mtumishi makao makuu. Kwa hiyo hana popote atakakopata taarifa hii ya siri. Lazima amepelekewa na mmoja wa wabunge. Lwa hiyo Kigogo hana kosa lolote katika hatua ya sasa. Labda hapo baadaye.

Sasa tujiulize; kama ilikuwa sahihi wabunge kuchangia chama chao hela kama shukrani kwa kuwadhamini na kukiimarisha chama kimfumo.

Nashindwa kujua ni nini makubaliano baina ya wabunge wetu na chama nyuma ya michango hiyo. Ikumbukwe kuwa michango hii ni takwa la katiba ya chama. Hakuna kwenye katiba inapoelezwa kwamba wabunge wakiisha changa watauliza iliko hela waliyochanga.

Kama kweli maelezo yanayotolewa ni kwamba walikuwa wakichangia katika mfuko wa chama kwa ajili ya uchaguzi ujao 2020, kwa nini maulizo haya yanakuja leo?

Sijui kama wabunge wetu wanachanga ili warudishiwe hizo hela ama wanachanga ili hela zitumiwe na chama kwa mujibu wa mipango yake?

Je, wabunge wanaona sadaka yao ya fedha ni kubwa kiasi kwamba haiwezi kujadiliwa ndani ya chama bali nje kulikojaa maadui zetu? Je ni kweli chama kilichowajenga na kuwapa ubunge sasa kinapokea fadhila ya kubomolewa na ninyi mlioshiba na kung'aa kwa jina la chama?

Kuna anayefikiri mnamkomoa Mbowe. Lakini niwaambie sisi wenzenu tuliofanya kazi miaka nenda rudi. Usiku na mchana tukawajengea mtandao imara ambao kwao mlikuja kushinda ubunge. Sisi tuliopoteza fursa nyingi kwa kuwa tulijitambulisha na upinzani. Sisi tuliopoteza mali nyingi kwa kugharamikia upinzani. Sisi tulionyang'anywa mali na kuhatarishwa maisha yetu kwa kuwa tumeamua kukipigania chama chenu. Sisi tuliojazwa madonda kutoka kwa watawala wanaokasirishwa na uimara wa chama chetu; leo mnaongezea pilipili kwenye madonda yetu. Hakika ukatili huu ni mkubwa sana.

Hivi wabunge wanapodai sehemu ya mshahara wao wanaouchanga kwa ajili ya chama walituambia lini sehemu inayobaki wameitumia vipi kwa ajili ya majimbo na chama katika mikoa na kanda zao.

Nilibahatika kusikia mahali kuhusu harakati ndani ya chama dhidi ya Mbowe. Harakati hizi pia zilikuwa dhidi yake kama KUB.

Wabunge wetu hawa nilinusa habari kuwa katika kikao kimoja cha kambi walisimama na kumpongeza Mhe. Zitto kwa kazi nzuri aliyofanya ya kumhudumia Lissu bila kumtaja Mbowe popote. Ilipikwa fitina dhidi ya Mbowe kwamba katika tukio la kishambuliwa kwa Lissu, Mbowe ndiye "wasiojulikana". Hii si ile propaganda ya CCM bali ni ya ndani ya chama na iliyoasisiwa bungeni.

Chama kimenyamazia wabunge hawa kwa muda mrefu. Wamejiona wafalme wa chama. Wanajua kosa la kupeleka habari za chama nje ya vikao rasmi vya chama. Je huu si uvunjifu wa kanuni na katiba ya chama kwa makusudi?

Kwa hapa walipotufikisha, Nitashangaa sana:
1. Kama tutawanyamazia. Hatuhitaji msaada wa Kamati Kuu wala Baraza Kuu. Tuwapa vidonge vyao huku huku.
2. Tuwajazie taarifa za imani yetu kwa Mbowe. Na tahadhari kwamba titawashambulia kushoto, kulia, mbele na nyuma wakiendelea na majaribio yao haya.

Waheshimiwa makamanda. Mti wenye matunda ndiyo utupiwao mawe. Hawa wabunge nani amewasikia majimboni ama katika harakati za kumaanisha za kujenga chama?

Mbowe kwa ajili yetu na taifa amepitia madhila mangapi? Mali zake zilizoharibiwa ni za bei gani? Akaunti zake zilizofungwa ni za thamani gani? Amepoteza vingapi ili kutufikisha hapa tulipo.

Kwa nini wabunge wetu wachague kumlipa fedheha badala ya fadhila kwa harakati zote alizofanya hadi kufikia hapa tulipo!

Naogopa kumadress Mbowe katika hili. Ila nitawashanga mkiwanyamazia wabunge hao wanaoiona sadaka yao kuwa ni kubwa kuliko za watu wengine ambao hawajalipwa mishahara na posho za kibunge kama wao.

Hivi mimi nimekuwa katibu wa mkoa kwa miaka 10. Sijawahilipwa mshahara miaka yote hiyo. Je sadaka yangu hii ambayo niliitoa ili wapatikane wabunge nani alitakiwa ailipe? Mmeniletea lini mafuta pipa moja la kufanya ziara mkoani kwangu. Aje hapa Katibu mwenzangu yeyote wa mkoa aonyeshe anavyolipwa fadhila na wabunge aliowapigania.

Nasema semeni yote muyatakayo, fanyeni yote muyawezayo, nendeni popote mtakako:

Mwenyekiti wetu ajaye ni FREEMAN AIKAEL MBOWE.

Update 2:

Anaandika Halima James Mdee (Mb), Mjumbe Wa Kamati Kuu CHADEMA.

Sisi wabunge tunaochangia PESA na ambao ni WAJUMBE wa KAMATI KUU tunaopata fursa ya kupata taarifa za MAPATO na Matumizi ya CHAMA TUNATHIBITISHA hakuna hata 100 iliyoliwa na MTU..Wakongwe katika hiki CHAMA tunajua kila mwaka wa UCHAGUZI ukifika kuna CHOKOCHOKO nyingi zinazohusu FEDHA. Najiuliza tu, hivi kama hizo pesa za UMMA zinapigwa na WATU kwenye CHAMA namna hiyo mbona SERIKALI ya CCM tena MAGUFULI anavyotuchukia ASITUFUNGULIE MASHTAKA YA UHUJUMU UCHUMI??

Hivi MNAVYOONA SHUGHULI za CHAMA zinaendelea NCHI nzima yenye ukubwa wa sQuare KM 945,087 mnadhani pesa inatoka wapi? Mnavyoona Pikipiki zinakwenda nchi NZIMA sio mara moja au mbili mnadhani pesa zinatoka wapi? Mnapoona M4C mpya zinanunuliwa mnadhani pesa inatoka wapi?? Sasa hivi CHAMA kiko kwenye Chaguzi NCHI nzima mnadhani pesa zinatoka wapi? Mnajua gharama za Matibabu ya KAMANDA wetu mpaka sasa hivi IMEGHARIMU kiasi GANI na CHAMA kimeshatumia KIASI gani ??Mnataka SASA tuanze kurusha Twitter AU INSTAGRAM au kwenye HIZI groups???mapato na matumizi ya chama?? Wenyeviti na MAKATIBU wa KANDA zenu WAJUMBE wa KAMATI KUU, wanajua TAARIFA zote za FEDHA. Wafuateni KWENYE ofisi zao wawape Ufafanuzi wa jambo lolote mnalodhani linahitaji ufafanuzi. Ni kweli kuna wabunge ambao UTEKELEZAJI wa TAKWA la KATIBA la KUCHANGIA chama umekuwa ukiwauma SANA.

Hawajawahi kutaka toka awali, hawa ndio walienda kulalamika kwa NDUGAI na Hawa ndio wanafanya kazi na CCM Bungeni kuumiza au kuwachonganisha wabunge wenzao na MHIMILI. Miaka yote kabla 2015, tumekuwa tukichanga kwa kukatwa moja kwa moja na ofisi ya katibu ya Bunge.

Baada ya 2015 tumeendelea kukatwa mpaka hao WAPUUZI wanaojulikana hawajaenda kwa ADUI yetu kumwambia CDM haitetereki sababu wabunge tunachangia na kwamba AKIZUIA CHAMA kitasota, na KWELI YULE PIMBI akazuia. Kumbe wabunge WALIOPELEKA HUO uzushi wamesukumwa na UBINAFSI wao wa KUKOPA mpaka kupitiliza... mpaka kufikia hatua ya kuona MCHANGO HALALI wa KIKATIBA ni HISANI kwa CHAMA.

Wamesahau na SISI huko nyuma tukiwa WACHACHE tulichanga kwa UAMINIFU MKUBWA ndio maana WAO wakapatikana. Tuna wabunge WAFIA CHAMA, lakini pia tuna wabunge MASLAHI . Ni ukweli mchungu!! Tukiimarishe CHAMA , tupate WAWAKILISHI wanaotanguliza MASLAHI ya UMMA na CHAMA kabla ya MASLAHI yao BINAFSI. Nashukuru MUNGU MAGUMU tunayoyapitia MSIMU HUU yanatukomaza na kutufanya TUJUANE ZAIDI.
hhaahahahaaha wacha wafu wawazike wafu wenzao...wabunge wamestuka fedha zao zinaliwa hovyo bila maendelek yoyote..mnataka muwanyamazishe midono eeeh...hivi si chama cha demokrasia hicho au mlishazika demokrasia...mnamsemaga mheshimiwa Rais ananyamazisha midomo hataki watu waongee ovyo lakini kumbe nyinyi ndio mnaongoza katika hili..shwainnnnnnny
 
Hawa watu hawawezi kuongoza nchi hata wao wanajua! Siku moja nilimuuliza kada mtiifu was chadema kuhusu mwenyekiti wao kushika nyazifa hiyo kwa mda mrefu alinijibu kwamba hayupo mwingine jasiri swali likaja nikajiuliza kama akiwa raisi Kuna hatari ya kuwa life president kulingana na sifa anayopewa na historia aliyonayo ya kuwa mwenyekiti wa mda mrefu huyo jamaa abatukuzwa kwenye chama hatari na anayehoji uenyekiti wake hufukuzwa chamani hata tundu lisu analijua Hilo!poleni makamanda endeleeni kusifu na kumpigia mapambio mwenyekiti wenu hiyo demokrasia mnayoitaka nashauri ianze chamani#2020# tutaelewana tu
Haya ndio mambo tunapigia kelele kila siku. Hii nchi inahitaji taasisi imara na sio kiongozi imara.

CHADEMA katika kuifanya taasisi yao iwe imara wameshindwa kwa kiasi kikubwa mno, hawaamini katika uimara wa chama bali katika uimara wa Mwenyekiti. Wale MATAGA wanaotaka JPM atawale mpaka achoke wametoa huo ujinga CHADEMA, ajabu CHADEMA tena wanawaona wajinga.
​
 
Habari ya mbowe kuendelea na uongozi ni upuuzi wa kiwango cha PhD, ameshafanya yake na kutoa mchango mkubwa sana lakini inatosha, mwenyekiti awe Tundu Lissu, otherwise hatutaelewana
 
Hawa watu hawawezi kuongoza nchi hata wao wanajua! Siku moja nilimuuliza kada mtiifu was chadema kuhusu mwenyekiti wao kushika nyazifa hiyo kwa mda mrefu alinijibu kwamba hayupo mwingine jasiri swali likaja nikajiuliza kama akiwa raisi Kuna hatari ya kuwa life president kulingana na sifa anayopewa na historia aliyonayo ya kuwa mwenyekiti wa mda mrefu huyo jamaa abatukuzwa kwenye chama hatari na anayehoji uenyekiti wake hufukuzwa chamani hata tundu lisu analijua Hilo!poleni makamanda endeleeni kusifu na kumpigia mapambio mwenyekiti wenu hiyo demokrasia mnayoitaka nashauri ianze chamani#2020# tutaelewana tu

Mkakati wa utawala wa CCM ni kununua wapinzani au kuwaangamiza hata kwa mauaji. Wasiofika bei kama Lissu na Mbowe ni changamoto kubwa sana. Yaliyompata Lissu hayana mjadala. Majuzi Mbowe kakoswa na shaba iliyoishia kumtoa roho binti Akwilina ndani ya dala dala kisha Mbowe kung’ang’aniwa na kesi ya kuhamasisha maandamano “yaliyosababisha” kifo cha Akwilina! A strange twist of sacrifices! I just wonder if Mbowe paid homage to Akwilina and her family for taking the bullet meant for him!

Hii ni enzi ya ajabu sana. Najaribu kufikiri Zitto angekuwa ndiye mwenyekiti wa CHADEMA chama kingekuwaje leo hii. Unconventional circumstances call for unconventional approach. Wanaong’ang’ania Mbowe apishe uongozi wa CHADEMA kwa kigezo cha demokrasia wanaishi kwenye nchi ya kusadikika - sio Tanzania hii ya leo. Au ni wanafiki wa kutupwa. Talk is cheap. Eti Mbowe hawezi kuhamasisha maandamano? Hiyo kesi aliyonayo leo ni kuhusu nini? Labda akilazwa na risasi ndipo mtaelewa tuko nchi gani awamu hii. That’s if you’ve got a good measure of integrity.
 
Back
Top Bottom