Wabunge wa Upinzani walipuka bungeni, waimba wana imani na Mkapa, Kikwete

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,509
2,000
Bunge limezizima kwa makofi baada ya hotuba ya mpango wa bajeti ya kambi rasmi ya upinzani.

Wabunge wa upinzani ambao ndiyo wengi waliobaki ukumbini baada ya wengi kwenda kufuatilia ripoti ya kamati ya pili ya Rais John Magufuli kuhusu usafirishaji wa makinikia.

Wabunge wamesimama na kuanza kuimba huku wakipiga makofi, marais wa awamu zilizopita; Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete wametajwa.

"Tuna imani na Mkaaapa...oya oya oya

Mkapa kweeeli...kweli

Kweli, kweli, kweli Mkapa.

Tuna imani na Kikweeetee...oya oya oya

Kikwete kweeli

Kweli, kweli, kweli Kikwete."

Wimbo huo umeimbwa baada ya Waziri Kivuli wa Fedha na Mipango, David Silinde kulitaka Serikali kuileta bungeni mikataba yote ya madini ili ijadiliwe.

Upinzani walipuka bungeni, waimba wana imani na Mkapa, Kikwete
 
Attachments

  • tmp_30070-IMG_20170612_134229-1152207625.jpg
    File size
    56.9 KB
    Views
    102

Bufa

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
6,226
2,000
Hawa wapinzani kama watoto hawajui wanataka nini na njia zao za kitoto badala ya kutoa hoja. Leo wanamsifia JK wakati kwa miaka 10 walishinda wanamkashifu. Wanaamini maana ya upinzani ni kupinga kila kitu. Smh
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,562
2,000
Hawa wapinzani kama watoto hawajui wanataka nini na njia zao za kitoto badala ya kutoa hoja. Leo wanamsifia JK wakati kwa miaka 10 walishinda wanamkashifu. Wanaamini maana ya upinzani ni kupinga kila kitu. Smh
Hujaelewa wewe umedandia treni kwa mbele. JPM kule Ikulu kamwambia Ndugai kuwa style yako ya kuwatoa wabunge na kuwafungia iendelee na ana iunga mkono. N akuwa wakija huku nje na wakiongea wanayoonge kule bungeni atawashughulikia. Ndio maana wameimba hivyo kama kejeli.
Muwe mnafuatilia mambo kwa kina sio kuchukua juu juu
 
fattys

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
669
500
Hawa wapinzani kama watoto hawajui wanataka nini na njia zao za kitoto badala ya kutoa hoja. Leo wanamsifia JK wakati kwa miaka 10 walishinda wanamkashifu. Wanaamini maana ya upinzani ni kupinga kila kitu. Smh
Soma katikati ya misteri kwenye ujumbe huo wa Wabunge wa Upizani. Kwamba Marais hao Wastaafu yaani Mkapa na Kikwete nao wanahusika na hizi kashfa za uchimbaji wa Madini.
Siyo kuwa wanawasifa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom