Wabunge wa upinzani hamjatumwa bungeni kuzomea

Zekidon

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2013
Posts
1,903
Reaction score
569
Naona aibu sana kwa nchi yangu.

Unapotazama bunge na kuona jitu zima kabisa na akili zake, tena limepata kura elfu 30, ili kuwawakilisha wana nchi wa jimbo lake anaishia kusema "buuuu" , hiyo sio sifa wala akili ni matope.

Kwa bahati mbaya sana, wabunge waliochaguliwa kwa tiketi ya ukawa wanadhani upinzani ni kupiga kelele bungeni, kutukana, kubishia kila kitu na pia kutoka nje.Sidhani waliowachagueni waliwapa dhamana hiyo, mkafanye mnayoyafanya sasa.

Mkiwa majukwaani mbona hampigi makelele hovyo au kutukana au kuzomea au kukimbia majukwaa kama mnavyofanya mkiwa bungeni.Mkiwa mnaomba kura mnaigiza busara za hali ya juu, kumbe hamnazo hata chembe.

Acheni ujinga na kudhalilisha bunge letu na pia wananchi waliowapigia kura wananchi angalieni wabunge mliowachagua, wanawaaibisha.
 
Mkuu unatak kwenye watu zaidi ya 300 wawe na akili moja?penye wengi pana mengi lazima tujifunze kuvumiliana.
 
wache wanafikiri safari hii bungeni kwenye bahari ya pesa na kuchezea magari ya kifahari
 
Tunapoelekea itakuwa huwezi kutizama bunge na mtu unayemuheshimu,maana jana yale matusi waliyokuwa wanayatoa ukikaa na mtu unayemuheshimu unaona hata aibu.
 
Kawaida mtu mbishi huwa ana akili ila anyekubali kila kitu huwa punguani.
 
Huoni Aibu kuona wananchi wanakufa nakipindu pindu kutokana na uchafu,huoni aibu nchi kuagiza magari yapolisi 700+ ile hali ct scan na ambulance hatuna,huoni aibu zec kutotangaza matokeo kwa mshindi Zanzibar,huoni alieshinda kwakumtandika fimbo mgombea mwenzake kuwa spika wa bunge,acha ushabiki tunaua nchi kwa tabia za kinafiki
 
Sijawahi kuona mafanikio katika kuzira na kutoka nje au kuzomea. Hawawezi kubuni mbinu nyingine?

mbinu nyingine ni moja tuu ambayo hawajawahi kuifanya ni kuchapana makonde .nyie mwajifanya wastaalabu sana ni bora kutukana kuliko mafindofindo yanayofanyika.
ww waona aibu kutukana usha wahi angalia bunge LA kenya watu walichapana makonde wazi wazi mwanzo mwisho.
 
Huoni Aibu kuona wananchi wanakufa nakipindu pindu kutokana na uchafu,huoni aibu nchi kuagiza magari yapolisi 700+ ile hali ct scan na ambulance hatuna,huoni aibu zec kutotangaza matokeo kwa mshindi Zanzibar,huoni alieshinda kwakumtandika fimbo mgombea mwenzake kuwa spika wa bunge,acha ushabiki tunaua nchi kwa tabia za kinafiki

kwahiyo suluhisho la ukosefu wa dawa mahospitalini kutokana na ukawa ni matusi na kuzomea bungeni. kama ndio hivyo basi wananchi walikosea kuwaamini.
 
mbinu nyingine ni moja tuu ambayo hawajawahi kuifanya ni kuchapana makonde .nyie mwajifanya wastaalabu sana ni bora kutukana kuliko mafindofindo yanayofanyika.
ww waona aibu kutukana usha wahi angalia bunge LA kenya watu walichapana makonde wazi wazi mwanzo mwisho.

swala ni uhalali wa kilichofanyika na si nani kafanya. kwahiyo jirani yako akijisaidia sebuleni nawe utafanya hivyo kwakua jirani yako kalifanya.
 
mbinu nyingine ni moja tuu ambayo hawajawahi kuifanya ni kuchapana makonde .nyie mwajifanya wastaalabu sana ni bora kutukana kuliko mafindofindo yanayofanyika.
ww waona aibu kutukana usha wahi angalia bunge LA kenya watu walichapana makonde wazi wazi mwanzo mwisho.

Tunataka mbinu mpya kama hizo ili tujue kweli wako kwa maslahi ya Watanzania na siyo yao pekee.
 
Naona aibu sana kwa nchi yangu.

Unapotazama bunge na kuona jitu zima kabisa na akili zake, tena limepata kura elfu 30, ili kuwawakilisha wana nchi wa jimbo lake anaishia kusema "buuuu" , hiyo sio sifa wala akili ni matope.

Kwa bahati mbaya sana, wabunge waliochaguliwa kwa tiketi ya ukawa wanadhani upinzani ni kupiga kelele bungeni, kutukana, kubishia kila kitu na pia kutoka nje.Sidhani waliowachagueni waliwapa dhamana hiyo, mkafanye mnayoyafanya sasa.

Mkiwa majukwaani mbona hampigi makelele hovyo au kutukana au kuzomea au kukimbia majukwaa kama mnavyofanya mkiwa bungeni.Mkiwa mnaomba kura mnaigiza busara za hali ya juu, kumbe hamnazo hata chembe.

Acheni ujinga na kudhalilisha bunge letu na pia wananchi waliowapigia kura wananchi angalieni wabunge mliowachagua, wanawaaibisha.

Hebu Toa Ushuz Wako Hapo! Unataka Ukjamba Tukushanglie? Na Akil Zenu Za Kuunga Mkono Kila Ki2 Mpaka MITA MIA 200? hapo ndo mlitoa ushuz
 
we ni kiaz angalia ulaya huko mpaka wanadundana,ulaya mbali bunge la kenya unalijua wewe,bunge sio kanisa wala msikiti.tatizo watu mumeanza kufuatilia siasa mwaka huu
 
ipo haja ya kupanua lango la kuingia bungeni gari la washawasha liweze kuingia kwa urahisi.
 
Back
Top Bottom