Wabunge wa UKAWA wagomea Miswada ya Petroli na Gesi, Bunge laahirishwa ghafla

Ingekuwa Spain serikali ingekuwa haina chake.... Waziri mkuu angepigiwa kura ya kutokuwa na Imani.

Tusipoondoka chini ya ccm tusitegemee lolote. Tunapenda sana ukada kuliko uzalendo kwa rasilimali za nchi. Mbwembwe za kupitisha mswaada wa Gesi na Mafuta hakuna asiyejua yaliyotokea.
 
hii habari niya tare 2/Jul/ 2015
hivi raisi si alikuwa ni nani ?
spika wa bunge alikuwa ni nani ?
chama kilichokuwa madarakani kilikuwa ni kipi ?
alafu ndo tutambue kuwa tunachomwa kidole cha mknd alafu tunadanganywa hio ni Sindano
 
Sasa nimeelewa kwa nini taarifa ya kamati ilipokelewa nje ya bunge, kumbe serikali na bunge waliogopa kulamba hansadi zao.!

Hii ingekuwa aibu kwa bunge na serikali kwa ujumla....bila shaka upinzani ungewachapa na hansadi zile zile za 2015.

Wabunge wale wale, chama kilekile serikali ile ile....cha ajabu wanakishangaa walichokipitisha miaka miwili nyuma..

Hii aibu sana kama Taifa.!
 
Siri ya ripoti kupokekewa nje ya bunge sasa iko hadharani. Nilishangaa ripoti ya bunge kupokelewa nje, na utetezi ukawa eti ni kamati ya spika. Kamati ya spika ilijua hilo suala likijadiliwa ndani watu wataficha sura zao.
 
Back
Top Bottom