Wabunge wa CHADEMA tuachane na Bunge tuungane Arusha

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,555
8,552
Tunaomba Wabunge wa Chadema kuachana na Kikao cha 5 kinachoendelea Hapa Dodoma na kuelekeza nguvu Arusha kwakuendeleza harakati na Juhudi zilizo anzishwa huko Arusha kwakushinikiza serikali kumuachia Mbunge wa Arusha Godbless Lema achiwe huru bila masharti na kushinikiza serikali kuwafutia mashitaka yote yanayowakabili viongozi wa CHADEMA kwakuwa hii ni dhahiri huu ni udharirishaji wa hali ya juu dhidi ya viongozi wakitaifa wa chama cha CHADEMA.
Tunamwomba Rais wa Jamuhuri ya Muungano aingilie kati kwani Amani tunayoiimba kila siku inaweza kutoweka kwa Dakika na kuirudisha ikawa zaidi ya miaka 10!Kwani watu wakichoka juu ya uonevu na uvumilivu ukawatoka mambo yaweza kuwa kama kwingine tunakokusikia kuna machafuko kwani nako kulianza kama hivi kwakukiuka haki za binadamu na unyanyasaji wa kidemokrasia uliokithili!
 
Lema alienda kwa mapenz yake huko jela sisi 2napiga kelele za nini?alijiona anahatia ndiyo maana akajipeleka mwenyewe,kila siku wana wa maandamano mnasisitiza sheria zifuatwe,halaf nyie ndio wa kwanza kupindisha,halaf mbunge anawakilisha wananch wa jimbo lake wakitoka wote kero za wananch wa majimboni mwao zitawakilishwa na nani?.
 
Hapo umesema kweli mkuu na kama watafanya hivyo itasaidia kuishikiza serikali iache uwendawazimu wake na ubabe usio na maana.
 
Lema alienda kwa mapenz yake huko jela sisi 2napiga kelele za nini?alijiona anahatia ndiyo maana akajipeleka mwenyewe,kila siku wana wa maandamano mnasisitiza sheria zifuatwe,halaf nyie ndio wa kwanza kupindisha,halaf mbunge anawakilisha wananch wa jimbo lake wakitoka wote kero za wananch wa majimboni mwao zitawakilishwa na nani?.

kwani ulitaka awekewe dhamana kwa kosa gani?je hata mahakamani alijipeleka?usiwe na mawazo mafupi kama maisha ya funza.mia
 
Wrong move...

Wakiliacha bunge tu na kwenda Arusha, huku nyuma muswada wa katiba utasomwa kwa mara ya pili kwa shinikizo la kichama(CCM).

Hata wabunge wa CCM wenye kutaka kupinga watakua wamefungwa kamba na chama. Na mnajua muswada ukishasomwa mara ya
pili kupindua ni ngumu. Watanzania tulio wengi tunataka katiba mpya sio sarakasi za kitoto za Mh. Lema (Mr. MISIFA), maana kila leo anawaza
afanye kituko gani kitachompa news coverage kuliko jana yake!

Watulie wafikirie kwa vichwa na sio mioyo yao.
 
Waache MAPOSHO na MARUPURUPU yote kwa ajili ya ujinga wa mahabusu LEMA?.CDM hawawez kutema posho hata kidogo.
 
Hapo ndo huwa nawashangaa watu wenye jazba na mapenzi ya kupitiliza kwa vyama na viongozi.
CDM MPs wanakula bata taratiiiiiiiiiiiiiiiiiiibu kule Bungeni wakati wapambe wananyeshewa kule Arusha.
Waache posho wachekwe, alafu famillia zile nini?
Tafakari vizuri unaposhabikia mambo ya vyama.
 
Tunaomba Wabunge wa Chadema kuachana na Kikao cha 5 kinachoendelea Hapa Dodoma na kuelekeza nguvu Arusha kwakuendeleza harakati na Juhudi zilizo anzishwa huko Arusha kwakushinikiza serikali kumuachia Mbunge wa Arusha Godbless Lema achiwe huru bila masharti na kushinikiza serikali kuwafutia mashitaka yote yanayowakabili viongozi wa CHADEMA kwakuwa hii ni dhahiri huu ni udharirishaji wa hali ya juu dhidi ya viongozi wakitaifa wa chama cha CHADEMA.
Tunamwomba Rais wa Jamuhuri ya Muungano aingilie kati kwani Amani tunayoiimba kila siku inaweza kutoweka kwa Dakika na kuirudisha ikawa zaidi ya miaka 10!Kwani watu wakichoka juu ya uonevu na uvumilivu ukawatoka mambo yaweza kuwa kama kwingine tunakokusikia kuna machafuko kwani nako kulianza kama hivi kwakukiuka haki za binadamu na unyanyasaji wa kidemokrasia uliokithili!
Hii ni ews alert?
 
Nasikia Kikwete jana "katembea" na mwana wa mfalme wa uingereza prince Charles, vp habari hizi ni za kweli?
 
nadhani wabunge wa chadema bado wanahitajika bungeni the only way ni kujipanga ili tupate wawakilishi bungeni lasivyo bunge litakosa wawakilishi kama chadema hawataingia wote
 
Naunga hoja yako ,ni vizuri mh Mnyika na wenzake waendeleze hoja zao bungeni.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom