Wabunge wa CCM Waomba Ushauri Kuhamia CHADEMA! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wa CCM Waomba Ushauri Kuhamia CHADEMA!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Buchanan, Nov 15, 2009.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Nov 15, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mivutano ndani ya CCM imewafanya baadhi ya wabunge wa CCM kuomba ushauri toka kwa wahadhiri wa fani ya Siasa wa UDSM ili kukabiliana nazo ikiwemo uwezekano wa kuhamia CHADEMA! Wabunge hao wa CCM (majina yao hayajafahamika) wamedai kuwa kuna kampeni za chini chini majimboni mwao kwa kuwa kuna wanaogawa fedha ili kuwabwaga, hali ambayo imekuwa tete kwao!

  SOURCE: HabariLEO, tr 15/11/2009.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Na bado....
  Hiki chama kama kimelaaniwa vile.
  Wakome kupitisha sheria ya kuzuia mgombea binafsi...
  Sasa linawarudia...
   
 3. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #3
  Nov 15, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Completely agree with you. Wenzetu wanamsemo kuwa "what goes around come around." walipokuwa wanapitisha hayo mawzo ya kijinga kabisa hawakuwa wanafikiri siku moja yatawarudi
  Ila kama ni ushauri wangu wabaki huko huko maana aliywezea kutoka na kupata ubunge ni Dr Slaa tu vinginevyo wamuulize njelu Kasaka. Hata kama watakuwa wanapendwa na wadanganyika lichama lao litawapora ushindi.
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Nov 15, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,566
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  Kuhamia Chadema siyo suluhisho, tunataka tujue ni akina nani hao, usije ukakuta ni EL, RA na Chenge! ebo

  Tunataka tujue lengo la kwenda Chadema ni kuwa wagombee nafasi zao, au ku-comply na Chadema's policies?

  Chadema as I stated earlier lazima intelijinsia yenu iwe makini sana nyakati hizi, it could be another 'SPYGAME'

  Chadema, if you will welcome these guys, you may need to put on the H1N1 (swine flu) mask, is not only that they are stinking, they may spread disease as well.

  Chadema is not a church!
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Nov 15, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,227
  Trophy Points: 280
  .

  Kuna wenye-chama, wala-chama na wanachama kama ilivyo kwa wenye-nchi, wala-nchi na wananchi.

  Hawandio wenye chama, kina JK ni wala chama tuu kuwaongoza wanachama, wahame na chama ni chao kiko mkononi mwao, sasa hiki chama wamwachie nani!?.
   
 6. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #6
  Nov 15, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Kati ya Chadema na CUF, nadhani CUF ni better. CHADEMA kuna ugomvi sana. Chadema wanaweza kujirekebisha, na muda upo wa kujirekebisha,lakini sasa wana siasa za kutwangana makonde ndani ya Chama.
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Nov 15, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  waende chama kingine CHADEMA should not open a room kwa majizi haya
   
 8. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #8
  Nov 15, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni wabunge gani hao waweke hadharani tuwajue na kuwapa ushauri sahihi.kuhusu vyama ,katika siasa za tanzania ya leo.
   
 9. P

  Paullih Member

  #9
  Nov 15, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 85
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu hujui kuwa wagombanao ndio wapatanao?
   
 10. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #10
  Nov 15, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Hii thread ni uzushi, hakuna kitu kama hicho CCM. Kutoka CCM na kuhamia chadema ni kujimaliza kisiasa
   
 11. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #11
  Nov 15, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  A sieve has to be used in admiting them in!
  Hatutaki pessimist na waliotumwa kutuvuruga.
   
 12. M

  MaMkwe JF-Expert Member

  #12
  Nov 15, 2009
  Joined: Sep 5, 2007
  Messages: 284
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwani walipojiunga na CCM waliomba ushauri wa kitaalaam? Kwa hiyo wanachotaka si chama ila kuendelea kupokea posho mbilmbili. Nikiwa Rais kupitia CHADEMA 2010 Posho za vikao vya Bunge nitazifutilia mbali. Wabunge kazi yao ni kuhudhuria vikao vya Bunge. Wanalipwa per diem kwa kuwa nje ya vituo vyao vya kazi (majimbo yao) kwa nini tena walipwe posho kwa kufanya kazi yao?

  Wafanyakazi wengine wa umma wakitumwa nje ya vituo vyao vya kazi wanalipwa tu perdiem lakini hawalipwi posho nyingine kwa kufanya kazi aliyoajiriwa.
   
 13. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #13
  Nov 15, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Msishangae kukuta ni wale wale ambao wananchi wanataka kuwabwaga majimboni kwao kwa kushindwa kutimiza ahadi zao.

  Vilio vingi vinavyotokea sasa ni vya kutaka kuonewa huruma. Kwa mtu aliyetimiza wajibu wake, hata nani aende kumwaga mapesa, huyo mbunge atashinda tu. Lakini kwa wale ambao waliyahama majimbo yao kwa miaka minne, hata waende chama gani watadondoshwa tu.
   
 14. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #14
  Nov 15, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145

  Hakuna kitu kama hiki Mtanzania.
   
 15. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #15
  Nov 15, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  FairPlayer,

  Mimi namjua mbunge mmoja ambaye analia lia na kila anayetaka kugombea jimbo lake anamwita fisadi, anadai kuna mapesa yanamwagwa. Sasa kama kuna mapesa yanamwaga si aende polisi? Si aende PCCB? Si awataje majina hao wanaomwaga pesa? Si awataje majina hao wanaodhaminiwa? Si awataje majina wananchi hao wanaopewa pesa?

  Nitakuwa wa mwisho kuamini vilio vya wabunge kama hao kwasababu wengine hata tumehusiswa na ufisadi wakati ukweli uko tofauti kabisa.

  Wacha kipenga kilie na tutawaambia mbele ya wananchi wathibitishe hizo tuhuma zao. Kuchafua watu bila sababu zozote ni ufisadi mkubwa kuliko hata huo wanaojifanya wanaupigania.

  Amani inajengwa na fairness na uongozi wa haki na sheria. Haiwezekani nchi ikaruhusu watu wachache kwasababu wanadhaminiwa na wamiliki wa vyombo vya habari, wakaamua kuwachafua wapinzani wao bila kuwa na ushahidi wowote. Huo sio uongozi, ni ujambazi wa kisiasa.
   
 16. E

  Ex-Fisadi Member

  #16
  Nov 15, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii thread, source yake ni gazeti la Habari Leo ambalo licha ya kuwa linamilikiwa na serikali ya CCM limekuwa likiwabeba sana Mafisadi na kujipambanua kuwa ni gazeti la Kifisadi vilevile. Stori kwenye gazeti lile haina kichwa wala miguu na imeandikwa na watu wa usalama wa Taifa ikiwa ni njia ya kiuokoa chama kinachoyumba sasa. Hakuna mbunge yeyote aliyeomba ushauri na kama ni ushauri asingekwenda kwa wasomi bali wangemtafuta DK. Slaa.
  Tunapochangia kwenye thread hii tunakuwa tumejiingiza kwenye mtego wa kumtisha yeyote ambaye anafikiria kuhama!
   
 17. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #17
  Nov 15, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160

  Mipasho hii.....una undugu na mh Sophia Lioness? Kwanini usimtaje huyo Mbunge kama una guts? Ifikie wakati tuende na facts....MBUNGE MMOJA....Mbunge fulani duuuuuuuuuuuu Mkuu vipi bwana!
   
 18. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #18
  Nov 15, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Labda kumbukumbu zako ni mbovu; Sophia amewataja kwa majina anaowatuhumu.

  Kama unataka kujua watu wengine wana guts, njoo Kyela filimbi ikilia. Tutawaambia ukweli huo huko huko kwa wananchi ambao ndio waliwachagua. Siasa za majimbo hazipiganiwi JF.
   
 19. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #19
  Nov 15, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Unafanya nini JF wewe Fisadi mchanga? Unapata shida gani kuandika Dr H. Mwakyembe unaishia namjua Mbunge mmoja duuu eti uwe Mbunge wa Kyela.....nitahama wilaya hadi kipindi chako kiishe!
   
 20. M

  Mkodoleaji JF-Expert Member

  #20
  Nov 15, 2009
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 454
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaani ningependa wabunge kama 20 tu hivi watoke CCM wajiunge na upinzani kwa mkupuo. Yaani watabadilisha sura ya kisiasa na CCM kwa kweli watashika adabu. Muulizeni Prof. wa Siasa wa Afrika Mashariki (Baba Moi) siku akina Raila, Mudavadi, Saitoti na akina Musyoka walipotangaza rainbow yao. Kwa hiyo kama wapo tuwatie moyo watoke na wawashawishi na wengine wote hapo demokrasia inaweza kutanuka. Pamoja na kwamba nao ni mafisadi, lakini ni kweli kwamba mafisadi wanapokuwa kambi tofauti wanasaidia kuongeza demokrasia. Kwa hiyo wabunge wa CCM kama mpo mnaotaka kutoka tokeni mje mtie joto la mapambano nje ya CCM.
   
Loading...