Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,335
- 72,800
Kuna njama za kuhakikisha Wabunge wa Upinzani hawaingii bungeni kwa Naibu Spika kung'ang'ania kuongoza vikao peke yake akijua kuwa kwa vile kusudio la kumuondoa katika kiti hicho halijafikia hatua ya mwisho hawatakubali kuingia ukumbini.
Mkakati huo ambao unaonyesha una mkono mrefu wa serikali, lengo lake ni kuwafanya wabunge wa CCM peke yao ndio wajadili Budget na ipite kwa ulaini.
Jee wabunge hawa wa ccm ambao kama tulivyoona kwenye Bunge la katiba walibaki wenyewe na kushindwa kutupatia Katiba mpya kwa kukosa kwao umakini wataweza kutupatia Budget makini kwa manufaa ya nchi au tunapoteza tena pesa za umma kwa kukaa kwao hapo Dodoma na kupiga makofi huku mambo ya msingi wakiogopa kuyahoji?