Wabunge wa CCm waliotia sahihi maisha yao hatarini.

Mukama ameishiwa baada ya kushindwa hata kupambana na kivuli cha Yusuf Makamba. Inashangaza ule ujasiri aliokuwa nao wakati akiwa Mkuu wa jiji umeyeyukia wapi.

CCM iko kwenye hatua za mwisho kuelekea kufa, ni ngumu sana kuinusuru. Nimemsifu Lugola kwa kuliweka hilo hadharani ili wananchi wajue kwamba CCM inaongozwa na watu wa namna gani.

Mukama alipopewa kuongoza Kamati ya kuchunguza CCM kufanya vibaya alimkandia sana Makamba. JK akasema ngoja nimpe yeye mwenyewe ili aje anyooshe mambo. Alipokabidhiwa mikoba akakuta ni ya moto. Kauli alizotoa Dodoma baada ya NEC zilianza kubadilika taratibu na mpaka sasa hata hajui Operation Vua Gamba ilikuwa inahusu nini.

Sasa anavyomtishia Lugola ina maana anahalalisha ufisadi ambao amekuwa akituaminisha kila siku kwamba CCM inapiga vita ufisadi?

Kwa kadri wanavyochelewa kuchukua hatua ndio wanavyozidi kujipaka matope. Maana Wizara ya Viwanda na Biashara washapakana matope tayari na Ekelege naye kashasilibwa.

Wizara ya Uchukuzi nayo vingunge wake wote wa juu wameishapakana matope. So, kama kufanya mabadiliko, then Waziri, Naibu Waziri na Katibu Mkuu wote wanatakiwa kuondolewa. Kaazi kweli kweli! Hapo bado hawajaenda kwenye Management ya TPA na Bodi yake.
 
Marehemu Kijana Wamalwa aliyewahi kuwa makamu wa Rais wa Kenya,aliwahi kutoa maneno haya katika kampeni wakati wa uchaguz wa kuking'oa chama cha Kanu na Moi.Alisema hivi;
"Ng'ombe akitaka kuzaa cha kwanza kujitokeza huwa ni miguu ya ndama,na ikishafika hiyo steji atazaa tu,huwezi kumzuia asizae" Sasa hawa akina Mkama bado hawaoini miguu ya ndama ishajitokeza,wataweza kuirudisha hiyo miguu tumboni ili ng'ombe asizae? Hivi karne hii bado kuna mtu anamzuia mwenzake kuongea?Wasubiri kilichompata Gadaffi na Mubarak.
 
Kama hatafungua mashtaka, then ntajua ni yaleyale ya magamba, perepete nyingi, kazi kiduchu

Huwa vigumu kufungua mashtaka kama maongezi yalikuwa kwa simu, ingawa wenzetu wangeweza kuchukua record kwenye mitambo ya simu na kuwa kielelezo cha kupeleka mahakamani.
 
Mukama ndiye anae iangamiza ccm,bora Mzee Makamba alikuwa ana pambana kisawasawa na Dr.SLAA.ULIKUWA UNAMSIKIA MAKAMBA LEO YUKO ZIARANI HUKU NA KULE,LAKINI MZUZU WA KAMBALE NI ZOBA.
Mkuu it is true, CCM wanajimaliza wenyewe, sioni kama Mukama anakisaidia chama badala yake chama kinazidi kufanya vibaya kuliko enzi za Makamba, at least Makamba alikuwa anazunguka Mikoani kukijenga lakini huyu aliyesema ataongoza kisayansi amekaa Lumumba tu kama ofisa ugavi, anadhani cheo cha siasa ni kukaa ofisini na kuagiza wengine watende, kwenye siasa unatakiwa ujitume uingie mwenyewe vijijini. Lakini ngoja tuone anakokipeleka chama. Enzi za Makamba hata kama kulikuwa na kutishana lakini si kwa wazi namna hii.
 
Kama hatafungua mashtaka, then ntajua ni yaleyale ya magamba, perepete nyingi, kazi kiduchu

mashtaka yatafunguliwa vipi na hakuna kielelezo? hakuna utaratibu wa kurekodi maongezi ya simu tanzania
 
Jamani wala msimlaumu Mkama kwamba anakiua chama. Chama chenyewe ndicho kimejiua chenyewe. Hicho chama kwa hatua kilichofikia hata mngempa Dr. Silaa asingeweza kukinusuru. Chama chenyewe kiko mautiuti, aka mahututi.
Pili mchango mkubwa wa kukiua umetolewa na mwenyekigoda wao. Mwenyekiti wao ndo mbovu. Hamwoni hata nchi alipoifikisha, hoi bin taabani?
 
Watanzania bana! Hawa wabunge ni watunga sheria na wana ufahamu mzuri wa sheria za Tz. Hii reaction yao kwa sim kutoka kwa mkama ni aibu tupu. Mtu anakutishia maisha, ushahidi unao, badala ya kuwahi polisi wewe unatoka nduki hadi Dar tena usiku wa manane! Hizo sheria tunatunga za nini kama hatutaki kuzifuata?
 
Jamani wala msimlaumu Mkama kwamba anakiua chama. Chama chenyewe ndicho kimejiua chenyewe. Hicho chama kwa hatua kilichofikia hata mngempa Dr. Silaa asingeweza kukinusuru. Chama chenyewe kiko mautiuti, aka mahututi.
Pili mchango mkubwa wa kukiua umetolewa na mwenyekigoda wao. Mwenyekiti wao ndo mbovu. Hamwoni hata nchi alipoifikisha, hoi bin taabani?
Ndio tunajua chama kinakufa lakini Mukama kama kiongozi lazima aonekane anakisaidia, mbona kuna wengine wamo humo humo wanaonekana?
 
ÇCM mmefikia hatua mbaya sana,lakn zaidi tumshukuru Mungu kwa kuendelea kuonesha upeo mzuri kwa wananchi kutambua yupi ni kiongozi bora kwao kwa sasa
 
Kanji Lugola wa Mwibara alidai jana kwamba usiku wa kuamkia Jumapili, siku moja baada ya kusaini hati kwa Zito Kabwe alipokea simu kutoka kwa Mukama akimtolea maneno makali kutokana na hatua yake hiyo. "Alizungumza maneno mengi ya vitisho kwa mfululizo bila hata kunipa nafasi ya kujieleza, akasema, ‘nakuja huko wewe na huyo mwenzako mliosaini mtanitambua,' kuona hivyo tukaondoka Dodoma usiku huohuo," Lugola alieleza.

Nami nilimwambia kwa kuwa sina kosa na nimetumia haki yangu, afanye lolote analoweza.""Hata
wakiniua, sitaogopa naamini katika ukweli na ni kilio cha wengi.
Lakini wengi wananiunga mkono, na wamenipigia simu na wanakubali kuwa wako nyuma yangu.

Alisema walisafiri hadi Dar es Salaam na kwamba walihudhuria kikao cha Bunge cha Jumatatu iliyopita wakitokea mafichoni.Alipotakiwa kuthibitisha madai hayo Mukama alisema: "Siwezi kutoa habari kwa simu."

Alipopigiwa tena na kuombwa afuatwe ofisini alisema, "Kwa leo haitawezekana maana niko njiani natokea Dodoma sasa hivi nimefika Gairo, kama unaweza njoo kesho."


Chanzo: Tanzania Daima na Mwananchi

Aaaah Mh. Lugola yaani mwanamume mwenzio anakuambia nikifika huko mtaniatambua basi wewe unakimbia!! Mngekaaa tu na kumsubiri kwani angewapiga? Natamani angemwambia maneno hayo mtuu yeyote anayetoka kule Tarime nadhani angefika Dodoma akakuta jamaa anamsubiri. Si ni ndugu yako huyo? Nadhani mnatoka wote Mwibara.

Ukiamua umeamua na shujaa halilii bunduki na hakuna haja ya maficho! Unajifichia nini kwani si haki yako kusaini. Yaani unajificha lakini ukikumbuka posho unatoka mafichoni!
 
Kanji Lugola Halikuwa hana njia zaidi ya kusini hiyo karatasi, Jimbo lake la Mwibara ni ngome ya Chadema na alilipata hilo jimbo kwa hila kubwa sana, Kusaini kwake ni kujijengea uhaminifu na kujielezea kuwa yeye anaunga mkono hoja za Chadema
hangekuwa yupo kwenye ngome ya CCM wala asingesaini hiyo karatasi
 
hicho chama ndo kimefika ukingoni wakumbuke kauli za JK nyerere
 
Aaaah Mh. Lugola yaani mwanamume mwenzio anakuambia nikifika huko mtaniatambua basi wewe unakimbia!! Mngekaaa tu na kumsubiri kwani angewapiga? Natamani angemwambia maneno hayo mtuu yeyote anayetoka kule Tarime nadhani angefika Dodoma akakuta jamaa anamsubiri. Si ni ndugu yako huyo? Nadhani mnatoka wote Mwibara.

Ukiamua umeamua na shujaa halilii bunduki na hakuna haja ya maficho! Unajifichia nini kwani si haki yako kusaini. Yaani unajificha lakini ukikumbuka posho unatoka mafichoni!

Kangi Lugola na Wilson Mukama wanajuana hao, wote wanatokea wilaya ya bunda na wote kabila moja.
Kusema kwamba walikimbia mji kwa kuogopa vitisho inawezekana kuna mambo mengi mazito alimueleza kuliko tunavyoweza kufikiria, nimesikia hata vyombo vya dola vilitumika kuwatisha wabunge wa ccm wasisaini petition, huenda wale waliosaini ndio walichimbwa mikwara mikubwa hadi wakaamua kuhama mji.
 
Yalishasemwa na Tanzania Daima waccm humu jamvini wakasewa "source" mara umbea.

Naamini kauli ya Upepo ni kweli Jk kasema
 
ÇCM mmefikia hatua mbaya sana,lakn zaidi tumshukuru Mungu kwa kuendelea kuonesha upeo mzuri kwa wananchi kutambua yupi ni kiongozi bora kwao kwa sasa
 
Lugola na Masters yako yote ya usalama ni mtu wa kumwogopa fisadi Mukama? jeka nchi achana na waliyofilisika mawazo
 
Mbona hawamtishi Filikunjombe au Mkono? Labda wanaona hapo ni mdebwedo lakini piga ua garagaza kama mbunge atamnyooshea Mukama ni wazi Mkama ataufyata mkia.

Sitaki kuamini kuwa hawa hawajatishwa, Ila inaonekana huyu Kanji Lugola ni mwoga, namshahuri aache papara atulie kwani yeye ni mwanaume!
 
Hivi huko CCM kuna nini? kwa nini usichukue uamuzi mgumu wa kurudisha kadi na kujiunga na wapambanaji?
Mnatishwa kwenye chama,wananchi wanawachukia,mnaonekana wezi,wauaji na mafisadi but mpo tu,tena na vikao unahudhuria kutoka mafichoni....huoni kina Mrema wako huru,hawapigiwi simu au kuandikiwa barua....mbona mleta hoja aka Zitto anatamba tu?
Mwenye macho haambiwi tazama na dereva hafundishwi kuona....yaani namaanisha akili za mukama changanya na zako..utapata uamuzi wa J.Millya.
 
Back
Top Bottom