Wabunge wa CCm waliotia sahihi maisha yao hatarini. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wa CCm waliotia sahihi maisha yao hatarini.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbaga Michael, Apr 23, 2012.

 1. Mbaga Michael

  Mbaga Michael Verified User

  #1
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 2,914
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  BAADHI ya wabunge wa Chama cha Mapinduzi, walioshiriki kusaini hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa nia ya kushinikiza kujiuzulu kwa mawaziri wanaotuhumiwa kufuja mabilioni ya fedha, wametishiwa maisha.

  Habari za kuaminika zilizothibitishwa na mmoja wa wabunge hao, zimesema kuwa wabunge wawili kati ya wanne wa chama hicho wamelazimika kuukimbia mji wa Dodoma na kujificha kwa muda kusikojulikana. Wabunge hao (majina yao tunayo) waliondoka mjini Dodoma mara baada ya kupewa taarifa na watu wao wa karibu kuwa walikuwa wakisakwa kwa vile baadhi ya wakubwa ndani ya CCM walikuwa wamechukizwa na kitendo hicho.

  Akizungumza na Tanzania Daima, mmoja wa wabunge waliokimbia na kujificha, amedai kuwa alilazimika kufanya hivyo baada ya kushauriwa sana na rafiki zake, ingawa awali aligoma kuondoka akisema angekuwa tayari kukabiliana na lolote hata kufa kwa vile anaamini hajafanya kosa lolote la kuhatarisha amani ya nchi. "Ni kweli niko nje ya Dodoma, nimefanya hivi baada ya kuwepo kwa hisia hizo, maana naziita hivyo kwa sababu binafsi siogopi kutishwa," alisema mbunge huyo.

  Kwa upande wake, Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe (CCM) ambaye ni mmoja wa wabunge
  wa chama hicho waliotia saini hoja hiyo, alikiri kupigiwa simu za shutuma na lawama kwa madai ya kukisaliti chama na kuunga mkono hoja ya wapinzani ya kutaka kuwawajibisha mawaziri wanaoitumikia serikali ya chama hicho. Filikunjombe alisema ingawa hajapata vitisho rasmi, lakini alijua hatua hiyo ingemgharimu. Alisema kuwa hajutii hatua hiyo kwa sababu ndiyo mahali pekee pa kusemea na kwamba kama asipoyasema yeye machungu ya Watanzania, hajui nani atayasema.

  Mbunge huyo machachali na asiye na woga aliongeza kuwa ni wajibu wake kukisadia chama chake kwa moyo mnyoofu na kuwasilisha kilio cha Watanzania na cha wananchi wa Ludewa. Alizidi kumshambulia Waziri wa Kilimo na Chakula, Jumanne Maghembe, kwa kuzembea na kupeleka mbolea ya kupandia
  jimboni kwake Ludewa mwezi Machi badala ya mwezi Oktoba, tena ikiwa feki. "Katika hali ya hovyo kiasi hiki, walitaka nicheke na kutetea upuuzi eti kwa sababu nalinda chama? Nimechaguliwa na watu kuwalinda na kuwaletea maendeleo sio umaskini. Kibaya wamewakopa hata mawakala. Badala ya kunisaidia na kuwawajibisha waliofanya uzembe huu eti nalaumiwa mimi," alisema.

  Lugola apigiwa simu ya vitisho Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola, alipigiwa simu juzi saa saba za usiku na kiongozi mmoja wa juu wa CCM akimtaka ajiandae kwa mapambano kwa kile kilichoelezwa kuwa amekisaliti chama. Akithibitisha tukio hilo, Lugola alisema kuwa kiongozi huyo mzito (jina tunalo) ambaye ni bingwa wa kufoka na kutukana vyombo vya habari vinavyomkosoa, alimwita mbunge huyo mnafiki, mzandiki na kwamba kwa hatua yake ya kusaini hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu atambue kuwa ametangaza vita. "Ni kweli nilipigiwa simu na.. (anamtaja) na kuanza kunifokea na kunitukana. Nilishindwa kuamini kama kiongozi mzito kama yeye anaweza kuniambia maneno hayo. Nami nilimwambia kwa kuwa sina kosa na nimetumia haki yangu, afanye lolote analoweza." Mbunge huyo alisema pamoja na kuambiwa kuwa leo kigogo huyo wa CCM atafika Dodoma kumshughulikia na wale wote tuliotia saini, haogopi lolote na yuko tayari kukabiliana na
  magumu kwa ajili ya maslahi ya Watanzania. "Hata wakiniua, sitaogopa naamini katika ukweli na ni kilio cha wengi. Lakini wengi wananiunga mkono, na wamenipigia simu na wanakubali kuwa wako nyuma
  yangu.

  Alisema maisha ya Watanzania ni mabaya, shuleni hakuna walimu wala madawati, hospitali ziko taabani kwa kukosa dawa huku madaktari wakililia maslahi, na kila wakati serikali imekuwa ikidai haina fedha kumbe, zipo na zinaliwa na wajanja. "Hakuna cha kunitisha katika hali kama hii. Wanaonitisha ndiyo wasioitakia mema CCM na Watanzania na hao lazima tuwashughulikie mchana kweupe. Na katika hili, lazima wote bila kujali wao ni nani lazima wajiuzulu bila kusubiri eti wajipime na kutafakari," alisema
  Lugola.
   
 2. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Mkuu hii sio breaking news!! sawa sawa??
   
 3. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Za asubuhi mkuu naonando unaamka mchana huu
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Umechelewa. Hii habari ipo humu
   
 5. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Copy n paste bila hata kuedit!!!
   
 6. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Hii sio Breaking News bali ni HABARI ILIYOVUNJIKA VIPANDE VIPANDE...

  We unategemea nini katika kundi la wachawi anapotokea mmoja ameokoka watamuacha, watatumia kila hila kumuangamiza ili siri zao zisivuje
   
 7. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kweli itasimama daima waendelee kupambana sisi wananchi tunawaunga mkono.
   
 8. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #8
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  ipe jina basi
   
 9. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Heshima kwa wabunge waliotia saini. Mungu anajua mlichofanya.
   
 10. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #10
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  edit mwenyewe unataka utafuniwe kila kitu, acha uvivu!!
   
 11. LESIRIAMU

  LESIRIAMU JF-Expert Member

  #11
  Apr 23, 2012
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 4,010
  Likes Received: 2,225
  Trophy Points: 280
  Mungu husimamia haki kila wakati. Msiwe na mashaka coz hamna atake ishi milele
   
 12. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #12
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  hajaiona mwenzio ,...............hata hivyo tunashukuru
   
 13. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #13
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Kakopi kwenye hard copy nini?
   
 14. Mbaga Michael

  Mbaga Michael Verified User

  #14
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 2,914
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  uvivu wa watanzania upo mpaka kwenye macho.
   
 15. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #15
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,702
  Trophy Points: 280
  Mukama anataka kumshughulikia Lugola?! Mukama hajipendi...
   
 16. Mbaga Michael

  Mbaga Michael Verified User

  #16
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 2,914
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  kweli.
   
 17. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #17
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,702
  Trophy Points: 280
  Sawa editor wa Uhuru
   
 18. Mbaga Michael

  Mbaga Michael Verified User

  #18
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 2,914
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  imeandikwa uckizoeze kinywa chako kutamka maneno ya ovyo ndani yake kuna matusi na maudhi
   
 19. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #19
  Apr 23, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Katika lichama la majambazi kama ccm ulitegemea nini kitokee? Wauaji wakubwa hawa!
   
 20. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #20
  Apr 23, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  habari iko kwenye magazeti hii jamani MWANANCHI,hususan
   
Loading...