Wabunge wa CCM upo tayari kufa na SITA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wa CCM upo tayari kufa na SITA?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ELNIN0, Jan 4, 2010.

 1. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,767
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Ningependa kuwauliza wabunge wa CCM na wana JF kwa ujumla mtazamo wao kama kweli wapo nyumba na spika wao Samweli Sita katika kutekeleza maamuzi mazito ya nchi au kutetea maslahi ya taifa hili kwa ujumla. kwa mafano kama Sita angenyanganywa uananchama kwenye CCM je nyie wabunge mngekufa pamoja na spika wenu? au yangekuwa yale yale ya kutosana. (Kheri mimi sijasema..)

  Tatizo linakuja pale ambapo serikali itashindwa kutekeleza mapendekezo ya kamati za bunge, je wabunge mtakuwa sambamba na spika wenu kufa kifo kimoja kwa maslahi ya taifa letu?


  Kwa mtazamo wangu Samweli anakuwa Spika wa kwanza kufanya kazi yake vyema, binafsi nampongeza sana, si kazi rahisi ukizingatia anatoka humo humo ndani ya chungu cha CCM, naunga mkono kwamba ukitaka kummaliza adui yako mmalize humo humo ukitoka nje hutamweza.

  Unaongoza bunge kwa usawa, hoja ndizo zimetawala na hili ni zuri mno kwa sisi wananchi wa hali ya chini, tunapata watetezi.

  Watu walifuatilia sana mambo yako hadi ulipokwenda Urambo iliuwa talk of the town, wakuu wako wa chama wakashituka wakakufuata huko huko kuomba msamaha na kuweka mambo sawa, wewe muungwana na IQ ipo juu.

  Samweli usije kuwa Mbuzi wa kafara kaka yangu, haya mambo yaangalie kwa makini, nachoomba mungu akujaze roho ya ujasiri, akulinde na ututumikie sisi watanzania wanyonge.

  Sipati picha kama wewe Samweli ungekuwa pamoja na hawa mafisadi, kweli tungekuwa pabaya sana, leo hii tunaongea Richmood, Buzwagi, Kiwila na mengineyo bila kuogopa. Pia kwa mara ya kwanza serikali inajiuzuru mikononi mwako, spika mwoga angesema anaumwa anaenda kutibiwa nje ya nchi lakini ukasema nitalikabili hilo, si jambo rahisi.

  Mengine machache yapo kama EPA mfano kagoda , Mwananchi gold na meremeta bado yana kizuizi sasa sijui kwa maslahi ya nani maanayake taifa si ni sisi wenyewe na nyie ndiyo mnatuwakilisha.

  Nakupa hongera sana ila naomba wabunge wenzako wawe pamoja na wewe na mungu akubariki sana spika wangu - ukirudi 2010 tumalizie kazi iliyobaki ili uingie kwenye vitabu vya kumbumbu ya taifa letu.

  Mwsho wakikukaba sana humo, basi hata sisi tunakuhitaji uje tuongeze mashambulizi

  Asante.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Wapi hao?...Ni wachache sana wanaoaminika pale mjengoni, mi nakisia asilimia 15 tu!

  Mambo ya kifisadi yanapoongelewa wengine wanainamisha vichwa chini na kukosa ujasiri utadhani wako slaughter-house!..wanaogopa kunyooshewa vidole na mabwana zao!...huh!
   
 3. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Unalosema ni kweli kabisa! Nguvu ya fedha imetawala fikra za watu wazima na wake/waume zao na familia zao! Hukaa na kuwafikiria watu kama Wabunge ama Waandishi wa habari ambao ukiwatazama wanaonekana ni watu wenye heshima zao lakini kumbe wameishanunuliwa na kuwekwa mifukoni mwa watu wenye pesa. Ni aibu iliyoje endapo itadhihirika kwamba baba/mama amewekwa mfukoni mwa fisadi!
   
 4. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Ni wazi kwamba ili watu wawe na msimamo mmoja lazima wawe na kitubinding kinachowaweka pamoja na kwa upande wa wanasiasa mara nyingi itikadi moja ndio inawafanya wawe wamoja. Sasa hawa wabunge ambao wanapigia kelele ufisadi itikadi yao ni tofauti na itikadi ya hao waliobaki wasiokemea ufisadi? Sitta na hao wanaojiita wapambanaji wa ufisadi wote ni CCM na kama kweli walikuwa si wabinafsi wa kutaka kutumia hii vita ya ufisadi kwa manufaa yao binafsi, wangetoka CCM na kujiunga na watanzania wengine wanaozulika na vitendo vya ufisadi!! Huko bungeni wote ni wagagnga njaa tu na mwenye fedha [ Mafisadi] ndio watakaoungwa mkono na wengi wa hao wachumia tumboni; wengine wamekwishaanza kujihami kuwa wanafuatwa fuatwa hukomajiomboni kwao lakini wao eti hawajawahi kuwasakama Mafisadi!! Hivyo ndio vihoja tutakavyoviona mwaka huu.
   
 5. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2010
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nadhani kusema kuwa wabunge wanaopiga vita ufisadi wanafanya hivyo wakiwa ndani ya chama chao kwa uoga ni kauli isiyo na tathmini ya kutosha. Nilidhani ingekuwa kinyume chake. Kwamba wanafanya hivyo bila kuogopa viongozi wao watawachukulia hatua gani. Maana wanaweza kupoteza nafasi zao kisiasa kama watakosea katika mapambano yao.

  Kuna wanaosema kuwa ni rahisi kupambana vita ukiwa ndani kuliko ukiwa nje. Inaweza kuwa kweli kwa upande mmoja na ikawa sio kweli kwa upande mwingine.

  Mathalan, unapigana vita na bomu likalipuka ukiwa ndani (
  Unadhani utasalimika?), au ikarushwa kitu cha ncha kali na kwa kuwa kuna sehemu finyu ya kukwepa, ukashindwa kijiokoa. Ukweli ni kwamba vita salama hupiganwa nje (kwenye uwazi). Maana ukiwa nje, si tu kuwa unakuwa na nafasi kubwa ya kupigana na hata kujiokoa (kwa kukimbia ikibidi), bali pia unakuwa na zana nyingi zaidi na uwezekano wa kupata support. Lakini vita zinatofautiana.

  Vita iliyopo ndani ya CCM (kama kweli ni vita) ni ya kisiasa zaidi. Ni mapambano ambayo yanaweza yakawa ya kiungwana kwa kuwa kinachopiganiwa ni kitu kinachokubalika kwa misingi na maongozo ya chama chenyewe.

  Wakuu, kwa maana hiyo hapo juu, ndio maana mimi nadhani ni vyema kwa wabunge wanaotoa kauli zinazoonekana kuwa tishio kwa wenzao kuendelea kufanya hivyo wakiwa ndani ya chama chao. Kwani kwa mtazamo wangu, wanachofanya si kupambana na chama, bali kukisafisha na kurudisha misingi imara iliyokuwepo (kama iliwahi kuwepo) ambayo iliwafanya kukiamini na kukitetea katika harakati mbalimbali za kisiasa. Ni vigumu kufanya usafi wa nyumba yako ukiwa nje. Ila watakapoamua kuwa wapambanaji, itawabidi watoke nje, kwakuwa watakuwa wanakiuka misingi na imani ya chama chao. Wakibaki ndani kwa wakati huo, watalipuka na mabomu yoyote yatakayokuwa ndani ya chama hicho.

  Mhe. Sita anajua anachokitaka katika kutetea nafasi ya chama chake na kila mbunge anajua anachotaka katika chama chake. Hivyo si sahihi kulinganisha matarajio ya kila Mbunge kwa kigezo cha Speaker wa Bunge. Speaker atatetea yake, na kama yanawiana na mategemeo ya wengi, atapata support inayohitajika.

  Mwisho, ningependa kusema tu kuwa, katika siasa kuna jinsi ya kufanya maamuzi. Kuna maamuzi ambayo yanaweza kukuondoa kabisa katika siasa, na kuna maamuzi ambayo yanaweza kukujenga. Ila maamuzi yote yanahitajika kufanyika kwa wakati maalum. Napata hisia kuwa, kadiri mambo yanavyokwenda, ni dhahiri kuwa kutakuwa na wanasiasa watakaoona nafasi zao kisiasa zikiwa matatani (wakiwa ndani ya chama chao), na hivyo kujaribu kujiokoa kwa kuingia kwenye vyama vingine vya siasa. Wapo kati yao watakaotoka CCM na wapo watakaotoka kwenye kambi ya Upinzani. Hii ni kawaida inapofika kipindi cha karibu na Uchaguzi Mkuu. Kitakachoamua ni lini wanapoweza kufanya hivyo, ni muda. Uchaguzi wa wakati wa kuamua ni muhimu sana kwa wanasiasa makini.
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,548
  Likes Received: 18,218
  Trophy Points: 280
  Naungana nawe Elnino, Spika Sitta pamoja na maroroso yake, he is so far the best speaker Tanzania had ever have, but he could do better akiweza kucontrol his emotions ambazo sometimes zinaleta over reactions or sometimes ana overdoing things na hivyo kujikuta anaunganisha sensessional kwenye baadhi ya maamuzi yake, other wise he is an asset against mafisadi, that might be turned into a liability na mafisadi hao hao au na ufisadi huo huo.
   
 7. m

  miner Member

  #7
  Jan 4, 2010
  Joined: Dec 14, 2009
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni dhahiri spika Sitta ametimiza wajibu wake kama spika. Nadhani Sitta atashinda tena uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu jee CCM watarudisha tena jina la Samwel Sitta kugombea tena Uspika? Tusubiri tuone nina mashaka sana
   
 8. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #8
  Jan 4, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Bulesi: Kumbuka kwamba hata hiyo katiba ya ccm hakuna mahali imehalalisha viongozi kuwa wezi hizi ni hulka tu za kibinadamu, na hivyo wanahitajika viongozi wenye uthubutu kama wa Sitta ili mambo yarudi sawa.
  Kinachotokea pale mjengoni ni ule utamaduni kama wa panya wa kuuma na kupuliza. Kwamba mtu anajua kwamba anakosea lakini anajua maswahiba watamlinda, kwa hiyo uwepo wa watu kama akina Sitta hata kama nao wanafanya siasa lakini angalau practice of their position inaonekana kuliko hao wanaokwenda kulala wakati nchi inateketea.

  Kwa hili kama Sitta utamuona anafanya pretence au anatafuta political influence, kwa mwananchi wa kawaida Sitta na kundi lake ni wabora mara 100 ya hao wengine, maana wakiachwa bila ya gavana ya kina Sittta, sisi kama taifa kutakuwa hakuna kitu kabisa kuanzia maadili ya uongozi hadi rasilimali za nchi hii. Muombeeni Sitta jamani angalau kama unafanya tathmini ya wabunge pale na kazi zinazofanyika, yeye ni rahisi zaidi kumtathmini kuliko walio wengi.
   
 9. Mlango wa gunia

  Mlango wa gunia Senior Member

  #9
  Jan 5, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 123
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana na wewe mkuu [​IMG]
   
 10. A

  Amanikwenu Senior Member

  #10
  Jan 5, 2010
  Joined: Dec 1, 2009
  Messages: 187
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Namshauri agombee Urais kupitia chama chake.
   
 11. N

  Nanu JF-Expert Member

  #11
  Jan 5, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sitta is good for being a Speaker......something else not sure for now....
   
 12. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #12
  Jan 5, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,767
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Thanks kwa mchango wako, Nafikiri mawazo yako ni muhimu na wana JF na wabunge pia watayapitia

  hizi quote mbili pia zimezibeba...
   
 13. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #13
  Jan 5, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,767
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Chief utaanzisha vita kuu ndani ya CCM, huo moto hautazimika, umesahau ya mzee wetu wa Mtera maswahibu yaliyomkuta 2005?
   
 14. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #14
  Jan 5, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Kwa sababu nchi yetu inaongozwa na demokrasia na mojawapo ni kuwa huru na maamuzi basi Sitta namshauri aanzishe chama cha CCM mzalendo ambao ni ule mpasuko ndani ya CCM. Nina imani akigombea Urais kupitia kundi hili halafu wapambane na mgombea pekee wa sasa(gazeti leo limesema JK Mgombea pekee 2010) nina imani Hon. Sitta atashinda. Akiongea anaonekana ni mtu wa authority, tumjaribu kwa term moja jamani watanzania wazalendo wenye uchungu na nchi yetu.

  Hon. Sitta amekuwa mstari wa mbele kupigania maslahi ya taifa hili kitendo ambacho kimempelekea kuonekana kuwa ni spika msaliti!!! Huyu ndiye hero wa taifa na huwa haogopi kusema waziwazi kuwa kuna migogoro na mipasuko wakati wengine wanajifanya migogoro ndani ya chama na utendaji wa serikali hakuna.

  Hon. Sitta, please, dare!!! We will be your followers. Kura utazipata kwa wingi. Kwanza watanzania wengi wanakufahamu kwa sasa kwa msimamo wako na uzalendo. Wewe ni mtu wa watu, japo mafisadi wanakuchukia kwa sababu unazijua vema sheria na kanuni za bunge na kuruhusu mijadala ile inayowachoma mikuki ya moto.

  Viva Hon. Samweli Sitta.
   
 15. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #15
  Jan 5, 2010
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mwanasiasa yeyote akianzisha chama wakati huu, hawezi kushinda uchaguzi mkuu ujao. Labda kama anajiandaa na uchaguzi wa 2015. Na ukifika wakati huo, watakuwa wamemchafua vibaya kiasi kwamba hatapendeza kwa yeyote.

  Kinachoweza kuleta mabadiliko ya maana ni wanasiasa wenye imani kuwa chama chao kimekuwa na misingi mibovu, kutafuta chama kingine kati ya vilivyopo.

  Uchaguzi wa chama cha kujiunga nacho pia ni muhimu. Ila ni vyema wakatafuta chama kisicho na umaarufu sana au ambacho hakijachafuliwa sana na siasa za nchi. Vyama kama UDP, na vinginevyo. Wakiingia huko, wataweza kuanzisha moto mpya wenye kuvuma sana.

  Kuna wanaodhani kuwa vyama hivyo kwakuwa havijulikani, si rahisi kupata ushindi. Ila watanzania wengi huchagua mtu kabla ya chama. Umaarufu wa wanasiasa hao pamoja na sababu zao kujitoa kwenye vyama vyao ndizo zitakazo wapa ushindi mkubwa. Watakuwa gumzo kwa wengi, na gumzo hilo huenea kwa kasi na kuzaa matunda.
   
 16. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #16
  Jan 5, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama kusingelikuwa na MIZENGWE ndani ya CCM kama ilivyokuwa huko nyuma SITA angeweza kuwa Rais mtarajiwa/ajaye 2015!
   
 17. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #17
  Jan 5, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,767
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Mtu yoyote anayefanya kazi nzuri lazima asifiwe hapo hapo, lazima tukubali kwamba kwa sasa Hon. Samweli yupo juu...anaheshimika na watu wengi kwa sababu kajitoa kwa watanzania maskini wasio jua kesho yao ni ipi, na ndiyo maana ndani ya CCM anapigwa vita eti mchochezi na anaruhusu mijadala hatarishi kujadiliwa bungeni.

  Hii mijitu ( Mifisadi) haosomi alama ya nyakati, inafikiri watanzania siku zote watakuwa wajinga?

  Among all CCM leaders I dare to say Hon Sita is the Herro leader for 2005 - 2010. Bravo.
   
Loading...