Wabunge wa CCM sasa wanatembea kifua mbele

Warue

JF-Expert Member
Aug 9, 2012
424
810
JF Salaam!

Kwa namna ya pekee naomba kutoa maoni yangu juu ya mabadiliko makubwa yanayoendelea kufanywa na serikali ya awamu ya 5 ya JPM na Khassim Majaliwa (KM).

Niwapongeze kwa dhati watu hawa wawili kwa jinsi walivyofanikiwa kufanya mabadiliko makubwa ndani ya mda mfupi sana.

Mmewapa heshima wabunge wenu na wanachama wenu kwa ujumla japo yawezekana wengi wao bado hawajaanza kutambua hili.

Kwa kipindi cha nyuma kwa namna ufisadi ulivyoshamiri ilikuwa ni vigumu mtu kujitambulisha kuwa ni mwana ccm watu wakaacha kumshangaaa.

Kwenye daladala ilikuwa ni kawaida kuzomewa huku magwanda yakivaliwa kama sifa.

Mwaka 2010 wakati wa kampeni za uchaguzi kuna wagombea wa ccm walikuwa wana vaa nguo za chama wakipanda jukwaani na mara baada mkutano wanaingia ndani ya magari yao na kuvua nguo zile. Aibuuuuu!

Kwa maaeneo mengi ilikuwa ni nadra kuvaa nguo za chama au kusimama kutetea chama ukatoka salama.

Ufisadi ufisadi ufisadi ulitamalaki.
Mwanzo mwa mwaka 2007/8 nyoka mwenye kengeza alipiga shilingi bil.2 basi watu wakaona ajabu kweli wakapiga kelele sana na yeye akajibu hivyo ni vijisenti. Basi tukapigwa butwaa!!

Baadae kiwango cha ufisadi kikapanda daraja kutoka bil.2 mpaka mabilioni yasiokuwa na idadi, taarifa za mara kwa mara za wizi mkubwa mkubwa zilitoka kila siku mpaka watu wakazoe. Ilipotolewa bil.321 za escrow ilikuwa kawaida sana nazo zikaliwa.

Kamati ikaundwa ikiongozwa na mpinzani mpiga dili, akaharibu repoti kwa kuficha majina muhimu ya wahusika. Walaaaniwe!

Labda kwa kuwaburudisha tu nishare ujumbe mfupi sana kutoka kundi moja la whatsaap leo;

MZEE TUNAKUMISI. RUDI TENA. KWA NINI TUNAKUMISI!?
1. Tulizoea kupiga dili sasa tumebanwa.
2. Tulikuwa na nyumba ndogo lakini viwezeshi hatuns
3. Tulizoea rushwa sasa ni kimbembe
4. Tulijitawala maofisini sasa ni HAPA KAZI TU
5. Tulitafutiana kazi kindugu na kirafiki lakini mambo yamebadilika
6. Tulizoea kukwepa kodi na misamaa dezo sasa ndo mwisho
7. Tulizoea uwongo sasa dhubutu ukione
8. Tulikuwa ma uhuru usio na mipaka sasa panya hajitawali
9. Tulizoea...
KWA NINI TUSIKUMISIIIIII???

Mwisho wa kushare.

SASA KATIKA MABALIKO YA CHANYA!!

Kubadilisha haya mazoea yaliyokwepo kipindi cha nyuma ni kazi sana ni lazima watu wengine waumie, wengine waugue na wengine watachanganyikiwa kabisa kama tulivyokwisha anza kuona wakilia kutafuta huruma kwa wananchi.

Tuliowafahamu kama wapinga ufisadi ndio hao hao leo wanakuwa vikwazo kwa vita dhidi ya ufisadi na madawa ya kulevya.

Mh. Nape aliongoza mapambano dhidi ya mzee lowasa akiwa na ajenda yake ya kisiasa (kuachiana jimbo na BCM) lakini leo hii uwezi amini kama ni Nape yule yule wa kuwavua magamba wenzake.

CHADEMA kwa upande mwingine nao hawaeleweki tena hata kidogo. Ilikuwa ni sifa kwa mtu kujitambulisha kuwa ni mpinzani kwa sababu upinzani ulikuwa unaongoza vita dhidi ya rushwa, ufisadi na ulinzi wa rasilimali zetu. Kwa bahati mbaya sana leo wametugeuka kabisaaaaaa. Wamekuwa watetezi wa wapiga dili, madawa na hata wezi wa rasilimali zetu.

Tuseme sasa basi, wapinzani hawatufai tena, na sio salama tena kuaminiwa na wanananchi. Hawana ajenda tena, kazi yao kubwa ni kwenda matukio ya kitoto ya wasanii wanaotafuta watoke vipi kimziki.

"We need a new crop of opposition leaders and not mbowe, not lipumba and not zito".

Hawa walishazoe kutumia nafasi zao kupiga dili na viongozi mafisadi wa kipindi kileeee!. Ni mda muafaka sasa kudai viongozi wapya wa upinzani. Kwa hawa tulionao wameishiwa mpunzi ( kwa sauti ya mzee wetu) na come 2020 Magufuli lazima atapata zaidi ya 85% ya kura.

Mwisho kabisa ni mwiko kunipiga biti inbox,wapo wanaojifanya mitandao ya jamii ni madaftari yao.

Update!!

Sasa tumeona maana ya wapinzani wapiga dili kama Zito Kabwe. Hakika wabunge wa CCM Wanafarijika.
 
Yapo mambo tunayokubaliana nayo kama taifa. lakini pia kuna uozo mwingi na dhulma pia. Nakubaliana na kubana mianya ya ukwepaji kodi pale bandarini na kwenye maeneo mengine. Lakini hatukubaliani na matabaka yanayo jengwa na serikali. Kuwalinda wahalifu hadharani, lakini pia kuwadhulumu wafanyakazi wa umma haki zao halikubaliki. Ccm wameshindwa kukemea hayo so wanaunga mkono dhulma hizo.
 
JF Salaam!

Kwa namna ya pekee naomba kutoa maoni yangu juu ya mabadiliko makubwa yanayoendelea kufanywa na serikali ya awamu ya 5 ya JPM na Khassim Majaliwa (KM).

Niwapongeze kwa dhati watu hawa wawili kwa jinsi walivyofanikiwa kufanya mabadiliko makubwa ndani ya mda mfupi sana.

Mmewapa heshima wabunge wenu na wanachama wenu kwa ujumla japo yawezekana wengi wao bado hawajaanza kutambua hili.

Kwa kipindi cha nyuma kwa namna ufisadi ulivyoshamiri ilikuwa ni vigumu mtu kujitambulisha kuwa ni mwana ccm watu wakaacha kumshangaaa.

Kwenye daladala ilikuwa ni kawaida kuzomewa huku magwanda yakivaliwa kama sifa.

Mwaka 2010 wakati wa kampeni za uchaguzi kuna wagombea wa ccm walikuwa wana vaa nguo za chama wakipanda jukwaani na mara baada mkutano wanaingia ndani ya magari yao na kuvua nguo zile. Aibuuuuu!

Kwa maaeneo mengi ilikuwa ni nadra kuvaa nguo za chama au kusimama kutetea chama ukatoka salama.

Ufisadi ufisadi ufisadi ulitamalaki.
Mwanzo mwa mwaka 2007/8 nyoka mwenye kengeza alipiga shilingi bil.2 basi watu wakaona ajabu kweli wakapiga kelele sana na yeye akajibu hivyo ni vijisenti. Basi tukapigwa butwaa!!

Baadae kiwango cha ufisadi kikapanda daraja kutoka bil.2 mpaka mabilioni yasiokuwa na idadi, taarifa za mara kwa mara za wizi mkubwa mkubwa zilitoka kila siku mpaka watu wakazoe. Ilipotolewa bil.321 za escrow ilikuwa kawaida sana nazo zikaliwa.

Kamati ikaundwa ikiongozwa na mpinzani mpiga dili, akaharibu repoti kwa kuficha majina muhimu ya wahusika. Walaaaniwe!

Labda kwa kuwaburudisha tu nishare ujumbe mfupi sana kutoka kundi moja la whatsaap leo;

MZEE TUNAKUMISI. RUDI TENA. KWA NINI TUNAKUMISI!?
1. Tulizoea kupiga dili sasa tumebanwa.
2. Tulikuwa na nyumba ndogo lakini viwezeshi hatuns
3. Tulizoea rushwa sasa ni kimbembe
4. Tulijitawala maofisini sasa ni HAPA KAZI TU
5. Tulitafutiana kazi kindugu na kirafiki lakini mambo yamebadilika
6. Tulizoea kukwepa kodi na misamaa dezo sasa ndo mwisho
7. Tulizoea uwongo sasa dhubutu ukione
8. Tulikuwa ma uhuru usio na mipaka sasa panya hajitawali
9. Tulizoea...
KWA NINI TUSIKUMISIIIIII???

Mwisho wa kushare.

SASA KATIKA MABALIKO YA CHANYA!!

Kubadilisha haya mazoea yaliyokwepo kipindi cha nyuma ni kazi sana ni lazima watu wengine waumie, wengine waugue na wengine watachanganyikiwa kabisa kama tulivyokwisha anza kuona wakilia kutafuta huruma kwa wananchi.

Tuliowafahamu kama wapinga ufisadi ndio hao hao leo wanakuwa vikwazo kwa vita dhidi ya ufisadi na madawa ya kulevya.

Mh. Nape aliongoza mapambano dhidi ya mzee lowasa akiwa na ajenda yake ya kisiasa (kuachiana jimbo na BCM) lakini leo hii uwezi amini kama ni Nape yule yule wa kuwavua magamba wenzake.

CHADEMA kwa upande mwingine nao hawaeleweki tena hata kidogo. Ilikuwa ni sifa kwa mtu kujitambulisha kuwa ni mpinzani kwa sababu upinzani ulikuwa unaongoza vita dhidi ya rushwa, ufisadi na ulinzi wa rasilimali zetu. Kwa bahati mbaya sana leo wametugeuka kabisaaaaaa. Wamekuwa watetezi wa wapiga dili, madawa na hata wezi wa rasilimali zetu.

Tuseme sasa basi, wapinzani hawatufai tena, na sio salama tena kuaminiwa na wanananchi. Hawana ajenda tena, kazi yao kubwa ni kwenda matukio ya kitoto ya wasanii wanaotafuta watoke vipi kimziki.

"We need a new crop of opposition leaders and not mbowe, not lipumba and not zito".

Hawa walishazoe kutumia nafasi zao kupiga dili na viongozi mafisadi wa kipindi kileeee!. Ni mda muafaka sasa kudai viongozi wapya wa upinzani. Kwa hawa tulionao wameishiwa mpunzi ( kwa sauti ya mzee wetu) na come 2020 Magufuli lazima atapata zaidi ya 85% ya kura.

Mwisho kabisa ni mwiko kunipiga biti inbox,wapo wanaojifanya mitandao ya jamii ni madaftari yao.
Kazi yote uliyo jipa kuandika uchafu huu ungekuwa umefikiria mambo ya msingi ya sana kama kumuongezea mkeo pea nyingine ya yebo
 
Back
Top Bottom