Wabunge wa CCM sasa wanatembea kifua mbele

Kazi yote uliyo jipa kuandika uchafu huu ungekuwa umefikiria mambo ya msingi ya sana kama kumuongezea mkeo pea nyingine ya yebo
Basi Onyesha usafi wako badala ya kuonyesha uchafu wako
 
JF Salaam!

Kwa namna ya pekee naomba kutoa maoni yangu juu ya mabadiliko makubwa yanayoendelea kufanywa na serikali ya awamu ya 5 ya JPM na Khassim Majaliwa (KM).

Niwapongeze kwa dhati watu hawa wawili kwa jinsi walivyofanikiwa kufanya mabadiliko makubwa ndani ya mda mfupi sana.

Mmewapa heshima wabunge wenu na wanachama wenu kwa ujumla japo yawezekana wengi wao bado hawajaanza kutambua hili.

Kwa kipindi cha nyuma kwa namna ufisadi ulivyoshamiri ilikuwa ni vigumu mtu kujitambulisha kuwa ni mwana ccm watu wakaacha kumshangaaa.

Kwenye daladala ilikuwa ni kawaida kuzomewa huku magwanda yakivaliwa kama sifa.

Mwaka 2010 wakati wa kampeni za uchaguzi kuna wagombea wa ccm walikuwa wana vaa nguo za chama wakipanda jukwaani na mara baada mkutano wanaingia ndani ya magari yao na kuvua nguo zile. Aibuuuuu!

Kwa maaeneo mengi ilikuwa ni nadra kuvaa nguo za chama au kusimama kutetea chama ukatoka salama.

Ufisadi ufisadi ufisadi ulitamalaki.
Mwanzo mwa mwaka 2007/8 nyoka mwenye kengeza alipiga shilingi bil.2 basi watu wakaona ajabu kweli wakapiga kelele sana na yeye akajibu hivyo ni vijisenti. Basi tukapigwa butwaa!!

Baadae kiwango cha ufisadi kikapanda daraja kutoka bil.2 mpaka mabilioni yasiokuwa na idadi, taarifa za mara kwa mara za wizi mkubwa mkubwa zilitoka kila siku mpaka watu wakazoe. Ilipotolewa bil.321 za escrow ilikuwa kawaida sana nazo zikaliwa.

Kamati ikaundwa ikiongozwa na mpinzani mpiga dili, akaharibu repoti kwa kuficha majina muhimu ya wahusika. Walaaaniwe!

Labda kwa kuwaburudisha tu nishare ujumbe mfupi sana kutoka kundi moja la whatsaap leo;

MZEE TUNAKUMISI. RUDI TENA. KWA NINI TUNAKUMISI!?
1. Tulizoea kupiga dili sasa tumebanwa.
2. Tulikuwa na nyumba ndogo lakini viwezeshi hatuns
3. Tulizoea rushwa sasa ni kimbembe
4. Tulijitawala maofisini sasa ni HAPA KAZI TU
5. Tulitafutiana kazi kindugu na kirafiki lakini mambo yamebadilika
6. Tulizoea kukwepa kodi na misamaa dezo sasa ndo mwisho
7. Tulizoea uwongo sasa dhubutu ukione
8. Tulikuwa ma uhuru usio na mipaka sasa panya hajitawali
9. Tulizoea...
KWA NINI TUSIKUMISIIIIII???

Mwisho wa kushare.

SASA KATIKA MABALIKO YA CHANYA!!

Kubadilisha haya mazoea yaliyokwepo kipindi cha nyuma ni kazi sana ni lazima watu wengine waumie, wengine waugue na wengine watachanganyikiwa kabisa kama tulivyokwisha anza kuona wakilia kutafuta huruma kwa wananchi.

Tuliowafahamu kama wapinga ufisadi ndio hao hao leo wanakuwa vikwazo kwa vita dhidi ya ufisadi na madawa ya kulevya.

Mh. Nape aliongoza mapambano dhidi ya mzee lowasa akiwa na ajenda yake ya kisiasa (kuachiana jimbo na BCM) lakini leo hii uwezi amini kama ni Nape yule yule wa kuwavua magamba wenzake.

CHADEMA kwa upande mwingine nao hawaeleweki tena hata kidogo. Ilikuwa ni sifa kwa mtu kujitambulisha kuwa ni mpinzani kwa sababu upinzani ulikuwa unaongoza vita dhidi ya rushwa, ufisadi na ulinzi wa rasilimali zetu. Kwa bahati mbaya sana leo wametugeuka kabisaaaaaa. Wamekuwa watetezi wa wapiga dili, madawa na hata wezi wa rasilimali zetu.

Tuseme sasa basi, wapinzani hawatufai tena, na sio salama tena kuaminiwa na wanananchi. Hawana ajenda tena, kazi yao kubwa ni kwenda matukio ya kitoto ya wasanii wanaotafuta watoke vipi kimziki.

"We need a new crop of opposition leaders and not mbowe, not lipumba and not zito".

Hawa walishazoe kutumia nafasi zao kupiga dili na viongozi mafisadi wa kipindi kileeee!. Ni mda muafaka sasa kudai viongozi wapya wa upinzani. Kwa hawa tulionao wameishiwa mpunzi ( kwa sauti ya mzee wetu) na come 2020 Magufuli lazima atapata zaidi ya 85% ya kura.

Mwisho kabisa ni mwiko kunipiga biti inbox,wapo wanaojifanya mitandao ya jamii ni madaftari yao.
Mkuu upo sahihi kabisa, ila manyumbu bado hawaelewi ulichoandika, kwani wao wanaishi kwa kukaririshwa.
 
Hizo mil.50,mikopo ya elimu,madawa hospitalini,maslahi watumishi na michango ya wana Kagera kuwa hadithi na kitendawili ndo watembee kifua mbele?! Mnachekelea upole wa watz eti
 
Mmmmh mbona mambo madogo sana hayo kwa single button yanaweza kumalizika kwa siku moja tu. Ufisadi ulikuwa kwenye damu na kuumaliza haikuwa rahisi
 
Katika wanalumumba wenye roho ngumu warue na Bashite mnaongoza, hivi unapata wapi ujasiri wa kuandika thread kama hii kwa hali ilivyo? Chama kiko dhoofu kuliko wakati wowte ule na nyie roho za paka msokuwa na weledi bado mnasimama kutetea ujinga huu!
 
kwani hawajalipwa posho zao?
Sidhani kama kuna mbuge hajalipwa posho, serikali iko makini. Kama bunge lilirudisha bil.12 leo washindwe kulipa posho. Acheni kutudanganya
 
Jadili kwa hoja na sio matusi mkuu kiogwe.
Unapo sema wanatembea kifua mbele unamaanisha nini yaani wewe kura waje kuaomba kwetu wananchi tena wengine mpaka magoti walipiga leo nanunua nyanya sado shilingi elfu kumi, unga ungaa narudia kuonyesha msisitizo unga wa mahindi kilo shilingi elfu mbili sukari 2200, mafuta ya taa , mkaa nao bei juu gesi ndio usiseme hivi wewe umeandika kutukebehi wananchiii au dharauuu yaani ungekuwa karibu na mimi ungekula makofi
 
Utter crap
Watu wanalia ugumu wa maisha nchi mzima na wengi wanaona afadhali ule ufisadi wa awamu ya nne kuliko adha, tabu na dhiki iliyopo nchini sasa
Nani anafurahia sembe na maharage sasa hivi inakimbilia shs3000 kwa kilo,huku karibu biashara zote zinakufa
 
Hata sasa kijana kuvaa gamba la ccm ni fedheha kwani tumezoea kuona wazee na vikongwe ndio wamepiga tisheti,kofia na kanga za ccm kama ishara ya rushwa waliyopewa kipindi cha uchaguzi
 
Sidhani kama kuna mbuge hajalipwa posho, serikali iko makini. Kama bunge lilirudisha bil.12 leo washindwe kulipa posho. Acheni kutudanganya
Wewe nadhani lile neno la Mdee ndio linakustahili.
Unapingana na ukweli ulio wazi? Au umelewa?
 
JF Salaam!

Kwa namna ya pekee naomba kutoa maoni yangu juu ya mabadiliko makubwa yanayoendelea kufanywa na serikali ya awamu ya 5 ya JPM na Khassim Majaliwa (KM).

Niwapongeze kwa dhati watu hawa wawili kwa jinsi walivyofanikiwa kufanya mabadiliko makubwa ndani ya mda mfupi sana.

Mmewapa heshima wabunge wenu na wanachama wenu kwa ujumla japo yawezekana wengi wao bado hawajaanza kutambua hili.

Kwa kipindi cha nyuma kwa namna ufisadi ulivyoshamiri ilikuwa ni vigumu mtu kujitambulisha kuwa ni mwana ccm watu wakaacha kumshangaaa.

Kwenye daladala ilikuwa ni kawaida kuzomewa huku magwanda yakivaliwa kama sifa.

Mwaka 2010 wakati wa kampeni za uchaguzi kuna wagombea wa ccm walikuwa wana vaa nguo za chama wakipanda jukwaani na mara baada mkutano wanaingia ndani ya magari yao na kuvua nguo zile. Aibuuuuu!

Kwa maaeneo mengi ilikuwa ni nadra kuvaa nguo za chama au kusimama kutetea chama ukatoka salama.

Ufisadi ufisadi ufisadi ulitamalaki.
Mwanzo mwa mwaka 2007/8 nyoka mwenye kengeza alipiga shilingi bil.2 basi watu wakaona ajabu kweli wakapiga kelele sana na yeye akajibu hivyo ni vijisenti. Basi tukapigwa butwaa!!

Baadae kiwango cha ufisadi kikapanda daraja kutoka bil.2 mpaka mabilioni yasiokuwa na idadi, taarifa za mara kwa mara za wizi mkubwa mkubwa zilitoka kila siku mpaka watu wakazoe. Ilipotolewa bil.321 za escrow ilikuwa kawaida sana nazo zikaliwa.

Kamati ikaundwa ikiongozwa na mpinzani mpiga dili, akaharibu repoti kwa kuficha majina muhimu ya wahusika. Walaaaniwe!

Labda kwa kuwaburudisha tu nishare ujumbe mfupi sana kutoka kundi moja la whatsaap leo;

MZEE TUNAKUMISI. RUDI TENA. KWA NINI TUNAKUMISI!?
1. Tulizoea kupiga dili sasa tumebanwa.
2. Tulikuwa na nyumba ndogo lakini viwezeshi hatuns
3. Tulizoea rushwa sasa ni kimbembe
4. Tulijitawala maofisini sasa ni HAPA KAZI TU
5. Tulitafutiana kazi kindugu na kirafiki lakini mambo yamebadilika
6. Tulizoea kukwepa kodi na misamaa dezo sasa ndo mwisho
7. Tulizoea uwongo sasa dhubutu ukione
8. Tulikuwa ma uhuru usio na mipaka sasa panya hajitawali
9. Tulizoea...
KWA NINI TUSIKUMISIIIIII???

Mwisho wa kushare.

SASA KATIKA MABALIKO YA CHANYA!!

Kubadilisha haya mazoea yaliyokwepo kipindi cha nyuma ni kazi sana ni lazima watu wengine waumie, wengine waugue na wengine watachanganyikiwa kabisa kama tulivyokwisha anza kuona wakilia kutafuta huruma kwa wananchi.

Tuliowafahamu kama wapinga ufisadi ndio hao hao leo wanakuwa vikwazo kwa vita dhidi ya ufisadi na madawa ya kulevya.

Mh. Nape aliongoza mapambano dhidi ya mzee lowasa akiwa na ajenda yake ya kisiasa (kuachiana jimbo na BCM) lakini leo hii uwezi amini kama ni Nape yule yule wa kuwavua magamba wenzake.

CHADEMA kwa upande mwingine nao hawaeleweki tena hata kidogo. Ilikuwa ni sifa kwa mtu kujitambulisha kuwa ni mpinzani kwa sababu upinzani ulikuwa unaongoza vita dhidi ya rushwa, ufisadi na ulinzi wa rasilimali zetu. Kwa bahati mbaya sana leo wametugeuka kabisaaaaaa. Wamekuwa watetezi wa wapiga dili, madawa na hata wezi wa rasilimali zetu.

Tuseme sasa basi, wapinzani hawatufai tena, na sio salama tena kuaminiwa na wanananchi. Hawana ajenda tena, kazi yao kubwa ni kwenda matukio ya kitoto ya wasanii wanaotafuta watoke vipi kimziki.

"We need a new crop of opposition leaders and not mbowe, not lipumba and not zito".

Hawa walishazoe kutumia nafasi zao kupiga dili na viongozi mafisadi wa kipindi kileeee!. Ni mda muafaka sasa kudai viongozi wapya wa upinzani. Kwa hawa tulionao wameishiwa mpunzi ( kwa sauti ya mzee wetu) na come 2020 Magufuli lazima atapata zaidi ya 85% ya kura.

Mwisho kabisa ni mwiko kunipiga biti inbox,wapo wanaojifanya mitandao ya jamii ni madaftari yao.
Time will tell kijana warue,coz siamin kama unayosema yana ukweli ndani
 
1. Tulizoea kupiga dili sasa tumebanwa.
2. Tulikuwa na nyumba ndogo lakini viwezeshi hatuns
3. Tulizoea rushwa sasa ni kimbembe
4. Tulijitawala maofisini sasa ni HAPA KAZI TU
5. Tulitafutiana kazi kindugu na kirafiki lakini mambo yamebadilika
6. Tulizoea kukwepa kodi na misamaa dezo sasa ndo mwisho
7. Tulizoea uwongo sasa dhubutu ukione
8. Tulikuwa ma uhuru usio na mipaka sasa panya hajitawali
9. Tulizoea...
KWA NINI TUSIKUMISIIIIII???
Kwa hiyo ukibanwa kupata huduma kama hizo ambazo ulikuwa unazipata unaanza kutembea kifua mbele?au unajuta kwa kunyang'anywa ulaji uliokuwaunapata?.
 
Kwa wale wote wanaobisha mniambie Mh. Magufuli awatendee nini muwezi kumkubali??
Mpaka JPM amefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana
 
Back
Top Bottom