Wabunge wa CCM ndio waliotuuza, wasikwepe lawama

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
Hili bunge hili nalo linataka tuliamini kwenye sakata la madini nchini kwetu?liaminiwe kwa lipi?

1.Ni mhimili huu huu mwaka 1997,ulipitisha kwa dharura sheria mbili,ile ya kodi na ya uwekezaji,sheria zilizohalalisha wawekezaji kukwapu madini yetu,sheria ambazo zilifuta kodi nyingi kwenye sekta ya madini,mhimili huu huu ukiitika ndiyooo,kuhalalisha wawekezaji kusamehewa na kufutiwa kodi!.

2.Ni hawa hawa mwaka 2007,walimfukuza bungeni Zitto Kabwe baada ya kutaka ufanyike uchunguzi kwenye mkataba kati serikali na huyuhuyu Acacia wakati huo akiitwa Barrick,hawahawa walitetea huo mkataba uliowaruhusu Barrick kusafirisha haya Makinikia,hawahawa walikataa waziri aliyesaini mkataba huo asijadiliwe bungeni na kumuadhibu aliyeibua hoja kuhusu Mkataba huo ulioidhinisha wana Kahama wafukuzwe kwenye maeneo yao kuwapisha hawa Acacia!.

Tena waliotetea mkataba huu uliovuja mpaka kwenye vyombo vya habari,baadhi yao bado wamo bungeni,wengine ni viongozi bungeni!.

3.Ni hawa hawa,na wengine wamo bungeni tena ni viongozi,mwaka 2010 waliitetea sheria ya madini na kupiga kura za ndiyooo sheria hii inayowapunja wazawa kwenye malipo ya fidia baada ya kuhamishwa kupisha wawekezaji wakiwemo Acacia!.

Hii sheria ya ajabu inayosema eti mtanzania yeye anamiliki sehemu ya juu ya ardhi ,huko chini siyo mali yake,ni mhimili huu huu ndiyo mwaka 2010 ulitunga sheria ya kuwafanya watu wanaoishi pembezoni mwa migodi wawe masikini wa kutupwa pamoja na kuishi sehemu yenye utajiri!

4.Ni mhimili huu huu,mwaka 2009,ukifumbua macho unyama wa Barrick pale wananchi wa Nyamongo walipotiririshiwa sumu,baadhi wakababuka,wengine wakapoteza maisha,mifugo ikafa,ardhi ikachafuliwa na sumu,mhimili huu huu uliunda kamati mwaka 2009,kamati ambayo mwisho wa siku iliwakumbatia wawekezaji na kuwaita waathirika wa sumu kuwa ni wavamizi/wizi,kinachonidikitisha baadhi ya wajumbe wa kamati ile bado wamo bungeni,waliwasaliti wana wa wanyongo kwa kuwaambia wamejitakia kwa kuwavania wawekezaji,leo wanaidai kuongea kwa hasira wakati mwaka 2009 waliwasaliti watanzania na kuwatetea wawekesaji,leo wanataka tuwaone vinara wa kwenye wizi huu wa madini!.

5.Mwaka 2004,watanzania waliokuwa wanaishi kijiji cha Mtakuja,wakihamishwa kinyama,usiku wa manane,kamati ya mhimili huu ilikwenda Geita,ikashuhudia watanzania wakiishi kwenye jengo chakavu la mahakama eneo la Sofia town,baadhi yao mpaka leo wamo bungeni,walifumbia macho unyama huu,waliwaita watu wa mtakuja wavamizi,leo wanataka tuwaamini kuwa wana uchungu na wizi huu!.

6.Hivi hawa wabunge hawajui chochote kinachoendelea Geita?hawajui kinachoendelea Nyamongo ,hawajui kinachoendelea Mererani?.Wanasubiri nani aseme kinachoendelea huko?je wao wanachojua ni makinikia tu?

7.Huu mhimili huu umekaa kimya miaka yote,kamati ya Bomani,kamati ya Lau,kamati ziliundwa zaidi ya tatu kabla ya hii,ripoti mbali mbali zimetoka zikithibitisha uporwaji wa mali zetu,huu mhimili ulikuwa unatazama tu,nakumbuka baada ya mto Tigithe kumwagiwa sumu,kamati ya viongozi wa dini iliinda timu ya wataalam kuchunguza kama kweli mto tigithe ulichafuliwa na sumu kutoka Barrick,ripoti ilitoka,ikathibitisha kuwa mto ulichafuliwa na sumu,huu mhimili kimyaaaaa,haukuwahi hata itumia tafiti hiyo kusaka haki ya waathirika wa sumu za Tigithe!.

8.Ni mhimili huu huu ndiyo ulitunga sheria ya sisi kupata mrahaba/mrabaha wa asilimi 4 tu,ni hawa hawa walipitisha sheria hii,sasa wanataka tuwaamini kwa lipi?

Mhimili huu ujitafakari unapojadili mambo mazito ya nchi hii,ujipime uzalendo wake,ujipime uwezo wake kuisimamia serikali,ujipime uwezo wake kuwawakilisha watanzania!.

Huu mhimili huu?any way!usiku mwema!.
 
Ukiwasikia wanavyolia kule bungeni kama waigizaji wa bongo movie vile hawa watu walipaswa kuwa magerezani au makaburini
 
Hii ni sawa na kozimeni anasema jamaa namchungulia ni mzinifu,halafu katikati ya ngono asiporidhishwa na partner wake,wewe upige kelele dirishani ati waendelee,hii CCM ndiyo walianzisha mkababa wakiona haifai au wanaibiwa nyie msipige kelele subirini akipata mwingine mtaenjoy.
 
Back
Top Bottom