WABUNGE wa CCM na SPIKA wao ndiyo adui wa kwanza wa Watanzania...

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Haiwezekani kila hoja ikiletwa bungeni muiunge mkono hata kama ni upupu kwa wananchi huku mkisingizia kuwa mmetumwa na wananchi. Nani kawatuma? Msitusingizie, tangu mlipofanya mikutano yenu ya mwisho ya kampeni hamjarudi tena majimboni kujua wapigakura wenu wanahitaji nini? Halafu naomba tabia hii muache mara moja. Kukosoa muswada au hoja iliyo mezani hali mwishoni mnasema naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja ni ujinga. Huwezi kukosoa jambo halafu ukaliunga mkono kwa asilimia mia moja. Halafu kwa nini huwa mnakejeli hoja za wapinzani hata kama ni muhimu na zenye tija kwa Taifa? Kuweni wazalendo basi japo kidogo. Pia mnasema mmetumwa na wananchi! Nani kawatuma kudai posho? Tunataka wabunge wa kweli siyo wabunge wa kudai posho na kutafuta umaarufu kupitia ubunge. Halafu wewe mwanamke ni nani kakwambia gharama za maisha mjini Dodoma zimepanda kwa wabunge tu? Pale Chako ni chako huwa mnaenda kufanya ni nini kila siku. Mbona wengine huwa mnaondoka mkitembelea magoti? Hizo hoteli mnazotaka kulala zina hadhi gani? Wakati wa kampeni mbona huwa mnalala kwenye vibanda tunavyolala sisi wananchi wenu. Acheni usanii, nyinyi ni waheshimiwa. Heshima ambayo mmeipata kupitia kura zetu. Halafu we mama hebu acha kukataa miongozo ya wabunge, hivi unafikiri utakalia kiti hicho milele? AU MNATAKA TUAMUE NA KUWAFANYA KUWA NDIO MAADUI WETU NAMBA MOJA.
 
Bunge la kenya ndio linaongoza kwa malipo makubwa duniani, huenda baada ya hii nyongeza tukawa tumeshawapiku lakini msisahau ya kuwa Kenya wanajitegemea kwa asilimia tisini na tano
 
Haiwezekani kila hoja ikiletwa bungeni muiunge mkono hata kama ni upupu kwa wananchi huku mkisingizia kuwa mmetumwa na wananchi. Nani kawatuma? Msitusingizie, tangu mlipofanya mikutano yenu ya mwisho ya kampeni hamjarudi tena majimboni kujua wapigakura wenu wanahitaji nini? Halafu naomba tabia hii muache mara moja. Kukosoa muswada au hoja iliyo mezani hali mwishoni mnasema naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja ni ujinga. Huwezi kukosoa jambo halafu ukaliunga mkono kwa asilimia mia moja. Halafu kwa nini huwa mnakejeli hoja za wapinzani hata kama ni muhimu na zenye tija kwa Taifa? Kuweni wazalendo basi japo kidogo. Pia mnasema mmetumwa na wananchi! Nani kawatuma kudai posho? Tunataka wabunge wa kweli siyo wabunge wa kudai posho na kutafuta umaarufu kupitia ubunge. Halafu wewe mwanamke ni nani kakwambia gharama za maisha mjini Dodoma zimepanda kwa wabunge tu? Pale Chako ni chako huwa mnaenda kufanya ni nini kila siku. Mbona wengine huwa mnaondoka mkitembelea magoti? Hizo hoteli mnazotaka kulala zina hadhi gani? Wakati wa kampeni mbona huwa mnalala kwenye vibanda tunavyolala sisi wananchi wenu. Acheni usanii, nyinyi ni waheshimiwa. Heshima ambayo mmeipata kupitia kura zetu. Halafu we mama hebu acha kukataa miongozo ya wabunge, hivi unafikiri utakalia kiti hicho milele? AU MNATAKA TUAMUE NA KUWAFANYA KUWA NDIO MAADUI WETU NAMBA MOJA.

CCM hawajarudi, CDM wamerudi kila baada ya kikao Wenje hurudi kuleta mrejesho wa kilichokubaliwa bungeni
 
Bunge limefanywa kuwa kama kundi la ZE COMED, tena afadhali ya kina Masanja wanaonekana wenye akili kuliko wabunge walio wengi!
Wabunge wenye akili ni wachache sana!
 
Back
Top Bottom