Wabunge Wa CCM: Msimpotoshe Rais Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge Wa CCM: Msimpotoshe Rais Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mchambuzi, Feb 5, 2012.

 1. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Kumekuwa na taarifa kwenye vyomba vya habari kuhusu ufa unaojitokeza baina ya Rais na Bunge, hasa wabunge wa CCM. Kuna kila sababu ya kuamini kwamba, ufa huu kwa kiasi kikubwa unaechochewa na uamuzi wa Rais Kikwete kupingana na suala la nyongeza la posho za wabunge. Kinachoendelea ni nia ya wabunge kumkomoa Rais Kikwete, kwa kupinga miswaada mbalimbali, hivyo kuiwekea serikali ya Rais Kikwete katika hali ngumu ya kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Hii ni tofauti na kipindi cha huko nyuma, ambapo bunge lilitawaliwa na kauli za “Ndiyoooo”, zikiambatana na makofi kwenye meza hata kwa hoja za kutia aibu. Lakini muhimu zaidi ni kitendo cha wabunge wa CCM kuja na msimamo wa kumpinga Rais Kikwete kuhusu msimamo wake juu ya marekebisho ya muswada wa sheria wa mchakato wa katiba mpya, hasa baada ya Rais kukubaliana na viongozi wa Chadema juu wa umuhimu wa kuufanyia marekebisho muswada huo. Lengo la mada yangu ya leo ni juu ya suala hilo.

  Madai ya wabunge wa CCM ni kwamba, marekebisho waliyopewa Dar-es-salaam hayafanani na yale ya Bungeni. Kwa mfano, wabunge hawa wanapinga kuondolewa kwa Wakuu wa Wilaya kushiriki katika mchakato wa Katiba mpya, na badala yake, kazi hiyo kupewa wakurugenzi wa halmashauri, kwa madai kwamba, Wakurugenzi wa halmashauri nchini ni wanachama wa Chadema. Sasa kwavile to everything there is an opposite, ni muhimu wakahojiwa, Je, Wakuu wa Wilaya Wapo Kwa ajili ya wana CCM au Watanzania? Pia kuna wabunge wanaojenga hoja kwamba, kwa vile walishawapelekea wananchi majimboni taarifa kuhusu mchakato wa katiba mpya, itawawia vigumu kurudi majimboni na taarifa mpya. Ni kwa sababu hizi Wabunge wa CCM wanaona Rais Kikwete amewadharau, wakidai kwamba, wao walipitisha muswada wa sheria, lakini Rais akaja kuwasaliti baada ya “kukutana na Chadema kwa dakika chache na kukubaliana nao kwa hoja”.

  Ni jambo lisilo pingika kwamba, msimamo wa Rais Kikwete kuhusu umuhimu wa marekebisho ya muswaada huu, una maslahi kwa taifa, bila ya kujali vyama vya siasa. Kwa kufuata kanuni ya ‘To Everything There is an Opposite”, msimamo wa wabunge wa CCM kuhusiana na msimamo wa Rais Kikwete, ni dhahiri hauna maslahi kwa taifa bali maslahi kwa CCM. Rais amekuwa makini kuepuka siasa za vyama katika suala hili muhimu. Ameelewa vyema kwamba muswada uliopitishwa bungeni mwaka jana ulijaa mapungufu ambayo ni hatarishi kwa mustakabali wa taifa letu. Inastaajabisha kwa wabunge wa CCM kutoliona hili. Rais Kikwete anastahili pongezi kwani kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, Kikwete ni Rais wa kwanza kuonyesha ukomavu mkubwa wa kisiasa wa kuamini katika siasa zlizo juu ya vyama vya siasa, na badala yake, kusimamia siasa zenye maslahi ya taifa. Bila Taifa imara litokanalo na katiba imara, vyama vya siasa sio mali kitu, kwani taifa imara na vyama imara haviwezi kuwepo chini ya mzaingira ya katiba isiyokuwa na uhalali mbele ya umma. Ndio maana, katika mchakato wa katiba mpya, sio CCM wala Chadema watakaoibuka washindi, bali Watanzania kama Taifa.

  Ni muhimu wabunge wa CCM waelewe kwamba, pamoja na Kikwete kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Kikwete sio Rais wa CCM pekee bali ni Rais wa Chadema, NCCR, CUF, CCK, na watanzania wasiokuwa na vyama vya siasa. Na katika mkutano wake na Chadema Ikulu, pamoja na maamuzi aliyoyafikia, Rais alikuwa amevaa kofia hiyo, sio kofia ya CCM.

  Udhaifu wa katiba ya Sasa umechangiwa sana na kukosekana kwa umakini miongoni wa wabunge wa CCM miaka ya nyuma. Wabunge wa CCM walipata nafasi nyingi za kurekebisha mapungufu ya katiba hii, lakini kutokana na sababu wanazozijua wenyewe, hawakujali kufanya hilo. Kama wangekuwa ni viongozi makini zaidi, wabunge wa CCM wangetambua kwamba, safari kuelekea katiba mpya ilikuwa ni safari isiyoepukika, hasa baada ya muungao na pia baada ya ujio wa vyama vingi vya siasa. Hili lilizidi kudhihirishwa zaidi na tume ya Nyalali ambayo ilipendekeza mabadiliko mengi ya sheria zilizokuwa za kikandamizaji na za kikoloni. Pia maamuzi mengi ya kesi mbalimbali katika mahakama yalitoa ishara ya muda mrefu sana kwamba kuna umuhimu wa Taifa kupata katiba mpya. Lakini katika kipindi chote hiki, wabunge wa CCM walidharau umuhimu huu.

  Bunge la CCM ni Kigeu Geu

  Ili kufafanua hili, tuanze na tukio la bungeni la miaka ya 1990 – uamuzi wa Zanzibar Kujiunga na OIC. Tukio hili lilizaa vilio vingi miongoni mwa wabunge wengi wa CCM. Wabunge walidai kwamba kitendo kile kilivunja katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lakini wabunge wa CCM hawakujali jinsi gani katiba ile iliwapunja wazanzibari haki zao. Pia walisahahu jinsi gani wao pamoja na viongozi wa serikali walivyokuwa mara kwa mara, waki-kiuka katiba ya nchi, wakishindwa kusimama katiba iliyopo, wakivunja sheria mbalimbali, na kupelekea wananchi wengi (hata wa majimboni mwao), kupata tabu, kunyanyasika, na hata kupoteza maisha. Lakini mapungufu yote haya hawakuyaona, bali suala la Zanzibar na OIC. Pamoja na Tume ya Nyalali kuweka wazi masuala haya, bado Bunge la CCM liliendelea kulifungia macho tatizo hili. Ni wazi kwamba Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haikuwatendea haki wazanzibari, na hata sasa, haiwatendei haki Watanzania bara.

  Ni tabia hii ya wabunge kupinga hili, na kuunga mkono lile kuhusu katiba yetu, ndiyo inanipelekea mimi kuwaita wabunge kigeu geu. Ni dhahiri kwamba wabunge wa CCM wamekuwa wamekosa uthabiti (consistency), kiutendaji na kimaamuzi katika kusimamia, kutunga na kurekebisha sheria zilizokuwa just, fair and equitable kwa watanzania wote.

  Mbunge yoyote makini, bila ya kujali Chama Cha Siasa, anatakiwa awe na ndoto zifuatazo juu ta Taifa lake:

  1. Kuwakilisha wananchi wake katika kupigania/kudai serikali ya ki-katiba, yenye utawala wa haki, na inayoendeshwa kwa mujibu wa sheria.

  2. Lakini muhimu zaidi ya hilo hapo juu ni wabunge kuhakikisha kwamba sheria zilizopo ni sheria ‘fair’, 'just and ‘equitable’, kwa watanzania wote.

  Jambo la kwanza hapo juu haliwezi kuwa na maana bila ya jambo la pili. Ni lazima yote yaende sambamba. Vinginevyo, taifa haliwezi kuwa na Katiba na Sheria zenye uhalali mbele ya umma. Kwa maana nyingine – a Pre-requisite ya serikali inayoendeshwa kwa mujibu wa katiba, ni uwepo wa Katiba na Sheria zinazotoa haki sawa kwa wananchi wote – ‘fair, just and equitable’.

  Msimamo wa Wabunge wa CCM kumpinga Rais Kikwete kuhusu umuhimu wa marekebisho wa muswada wa sheria, yatapelekea kuzaliwa kwa katiba mpya isiyolinda fairness, justice and equity kwa watanzania wengi, hivyo kukosa uhalali mbele ya umma.

  Nini Ni Madhara Kwa Taifa, iwapo Rais Kikwete Atakubaliana na Wabunge wa CCM?

  Iwapo Rais Kikwete ataungana na Wabunge wa CCM, ni dhahiri kwamba nchi yetu itaingia katika machafuko mkubwa ya kijamii na kisiasa siku za mbeleni. Nitafafanua.

  Iwapo serikali ya CCM itajikita zaidi kutupatia katiba itakayozaa serikali ‘inayotawala’ kwa mujibu wa katiba, bila ya kujali iwapo sheria hizo ni Just, Fair na Equitable, Serikali hiyo haitakuwa na uhalali mbele ya umma, na itaweza kabisa kuporomoshwa kwa nguvu ya umma. Iwapo wanachotaka wabunge wa CCM ni uwepo tu wa katiba na serikali kwa mujibu wa sheria, bila ya kujali sheria zilizopo zipo fair, just na equitable kiasi gani, basi hata serikali ya Makaburu ya Afrika ya Kusini ingekuwa bado ni serikali halali na kuwepo madarakani hadi leo, chini ya katiba ya kikaburu. Kwani, serikali ya makaburu ilitokana na Katiba na iliendeshwa kwa mujibu wa Sheria, Katiba na sheria zake zili heshimiwa na kuzingatiwa kwa hali ya juu, katika shughuli za kila siku za utendaji wa serikali ya Makaburu. Lakini pamoja na haya yote, bado ilikuwa ni kichekesho kwa chama cha ANC kuendelea kuheshimu katiba hiyo na kufuata sheria hizo: Eti tu kwa vile nchi ina katiba na serikali inaendeshwa kwa mujibu wa katiba na katiba, basi ANC iheshimu katiba na sheria zilizopo. Hiki nikichekesho ambacho Rais Kikwete na wasaidizi wake wamekigundua, hivyo kutoa msimamo juu ya umuhimu wa mabadiliko katika mswaada husika.

  Ni muhimu kwa watanzania waelewe kwamba, iwapo Rais Kikwete ataungana na wabunge wa CCM katika msimamo wao, basi watambue kwamba huko majimboni na kwingineo, wananchi wataendelea kuwepo chini ya mfumo mbovu, mfumo wa kikandamizaji, na ambao hauwapatii fursa ya kuendesha harakati za kudai haki zao za msingi za kijamii, kisiasa na kiuchumi, kwani katiba ya sasa inawapunja haki hizi zao hizi msingi. Pili, ni muhimu kwa wananchi huko majimboni wakaelewa kwamba chini ya mfumo unaolibdwa na wabunge wa sasa wa CCM, wananchi hawataweza kupata fursa za kuendesha harakati zao za kutafuta ‘self determination’ ya taifa lao, kwani katiba ya sasa inawapunja fursa hiyo kwa kiasi kikubwa sana.

  Ni muhimu kwa wabunge wa CCM wakatambua kwamba ubora na utiifu wa katiba ya nchi do not exist in a vacuum, bali ndani ya msingi ya fairness, equity and justice to all. Vinginevyo hakuna umuhimu wa wananchi kutambua na kuheshimu Katiba inayopwaya katika masiala haya. Ni dhahiri kwamba wabunge wengi wamesoma katika historia kwamba Mashujaa wa mataifa mengi duniani walikuwa wale waliovunja sheria na kukiuka katiba zilizokuwepo. Mifano ni Mwalimu Nyerere, Mahatma Gandhi, Nelson Mandela etc. Kwa mfano, Mahatma Gandhi alijizolea umaarufu mkubwa na baadae kuwa Baba wa Taifa la India, kwa kuwaongoza wahindi kwenda ‘ziwani’ kujitengenezea chumvi kwa ajili ya matumizi yao, jambo ambalo lilikuwa ni Marufuku chini ya sheria za kikiloni la Mwingereza. Vitendo vya kina Nyerere, Ghandi, Mandela vya kuvunja sheria na kukiuka katiba, vilipelekea serikali ya kikoloni ziwaone watu hawa kuwa ni wahuni na wa-ahini, chini ya sheria za kikoloni. Wabunge wa CCM wanatakiwa waongeze umakini hasa pale viongozi wa upinzani, kwa mfano, John Mnyika na Freeman Mbowe wanapotoa kauli kwamba wapo tayari kulipa faini zote na kufungwa jela kwa kuvunja sheria inayokataza watu kujiingiza katika kampeni za elimu ya umma, katika mchakato wa kutafuta katiba mpya. Wabunge wa CCM wakikosa umakini, wao ndio watageuka kuwa tanuri la kuwazalishia watanzania viongozi mashujaa wa taifa la Tanzania, wenye kufanana na kina Nyerere n.k.

  Pia ni muhimu kwa wabunge wa CCM waelewe kwamba uwepo wa serikali kwa mujibu wa katiba na serikali inayotawala kwa mujibu wa sheria, maana yake ni uwepo wa serikali ya kidemokrasia, inayotawala chini ya katiba halali, katiba iliyotokana na mawazo ya wengi, na katiba inayoheshima haki za raia wake. Vinginevyo watanzania hawata kuwa na haja ya kuheshimu katiba itakayokosa sifa hizi. Wabunge ndio watunga sheria za nchi hii, lakini ka miaka mingi sana, wabunge wa CCM walikosa umakini waa kutunga sheria zenye kusimamia equity, fairness na justice. Wabunge hawa hawakuwa makini kushinikiza serikali kufanya mabadiliko ya sheria zilizokuwa bado ni za kikoloni n.k, hata pale Tume ya Nyalali iliyotoa mapendekezo yake. Badala yake, kama ilivyo ada kwao, walikuwa ni mabingwa wa kupiga makofi kwenye meza zao kwa kila sheria hata kama ilikuwa ni ya kumkandamiza mwananchi jimboni kwake, huku wakitamka kwa kauli moja “NDIYOOO”. Vinginevyo wengi tulishukuru ujio wa tume ya Nyalali kwani ilitufungua wengi juu ya jinsi gani Katiba ya Nchi yetu ilivyokuwa ya ovyo ovyo.
  Lakini cha kuchekesha zaidi ni kwamba, ni wabunge wale wale ndio walikuja kuona ndugu zetu wazanzibari kwamba ni wahaini, waasi, na waliokosa Uzalendo, kuhusu suala la OIC. Ama kweli mkuki kwa nguruwe mchungu, kwani kwa miaka yote ya muungano, wabunge hawa hawakujali jinsi gani katiba iliyopo ilivyokuwa ina wanyima haki wazanzibari na watanzania bara. Ni kutokana nahaya, ndiyo maana wazanzibari wakafanya uamuzi ule, ambao kimsingi, kwa vile kwa muda mrefu hawakuwa wanasikilizwa na madai yao, walikuwa na uhalali wa kuja na mikakati ya kuondokana na mfumo wa kinyonyaji.

  It is ‘prudent wabunge wa CCM waanze kuwa ‘consistent’ katika maamuzi yao. Muhimu zaidi ni haja ya wao kuuunga mkono msimamo wa Rais Kikwete kuhusu marekebisho ya muswada husika kutokana na sababu ambazo nimeshazijadili. Mwisho niseme tu yafuatayo:

  1. Wabunge wa CCM wanatoa tafsiri kwamba wao wachotaka ni Bora Katiba, sio Katiba Bora. Ni muhimu waungane na Rais Kikwete pamoja na wabunge wa vyama vyote vya upinzani katika kuwatafutia watanzania “KATIBA BORA” badala ya “BORA KATIBA”, kwani kitendo hiki hakina uhusiano na tofauti zetu za vyama vya siasa, bali mshikamano kama taifa. Vinginevyo Katiba mbovu itakuja kuwang’ata hata wao kama wastaafu, pamona na familia na vizazi vyao vya baadae.

  2. Kuna sheria nyingi za kikoloni ambazo Tume ya Nyalali iliziorodhesha kwamba hazimtendei haki mtanzania chini ya katiba ya sasa. Kwa miaka mingi sana, wabunge wa CCM ndio wamekuwa wakizipitisha sheria hizi, huku nyingine wakiziongezea meno zaidi ili ziwakandamize zaidi watanzania. Wabunge wa CCM wana mzigo mkuwa wa kuutua – ukweli kwamba katiba mbovu ya sasa ni zao la CCM. Vinginevyo wakiwa makini hivi sasa, wana nafasi ya kuacha legacy, hasa wakiweka maslahi ya taifa kwanza, katika kipindi hiki cha kuelekea katiba mpya, hasa kwa kujikita zaidi kuihoji serikali, na kumtaka mwanasheria mkuu wa serikali kuleta bungeni sheria zote zilizobainishwa na tume ya nyalali kwamba ni oppressive and unconstitutional, ili zifanyiwe marekebisho, na wabunge hao wawe ni sehemu ya mafanikio hayo.

  3. Wabunge wa CCM wajikite zaidi kupinga utamaduni wa bureaucracy yetu ambayo inachukulia suala la ‘fairness’ katika kutoa huduma kwa umma kama vile ni ‘privilege’, badala ya ‘right’. Tunaliona hili katika huduma mbalimbali za serikalini kuu na za mitaa.

  4. Wabunge wa CCM waunge mkono msimamo wa Rais wa kuwatoa wakuu wa wilaya katika kuendesha na kusimamia mchakato wa kutafuta katiba mpya. Ni lazima watambue kwamba, haat Rais anajua kwamba, chini ya katiba ya sasa, wakuu wa wilaya wana mamlaka ya kuweka mtu ndani kwa muda wa masaa 24 bila ya hatia au sababu yoyote ya msingi. Chini ya katiba ya sasa, mkuu wa wilaya ana uwezo wa kukuweka ndani hata kutokana na chuki tu binafsi, kisha asubuhi akatoa amri uachiwe huru. Waheshimiwa Wabunge, sasa hawa ndio wa kupewa jukumu la kusimamia mchakato wa katiba mpya kweli?

  Mwisho, waheshimiwa wabunge wa CCM, muda sio mrefu mtarudi uraiani, aidha kutokana na kustaafu au kupoteza viti vyenu majimboni. Nina uhakika kabisa kwamba kila mmoja wenu atapendelea sana yeye na familia yake aishi chini ya mazingira ya katiba yenye kutoa haki na fursa sawa za kiuchumi, kijamii, na kisiasa kwa raia wote. Masuala Kama vile mafao yenu ya uzeeni, haki za kiuchumi, kisiasa na kijamii kama wastaafu, na pia za familia zenu, yote haya yanawezekana iwapo kwa pamoja mta muunga Mkono Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambae ameamua kuvua koti la CCM na kuvaa koti la Tanzania kama Taifa, kulisimamia suala hili.
  Mungu Inariki Tanzania.

  Mchambuzi,

  Mwanachama Hai wa CCM na Mwanachama Hai wa JamiiForums.
   
 2. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Wewe ni lini wabunge wa CCM walikwambia wana mpango wa kukwamisha marekebisho ya sheria ya kutungwa katiba mpya? Au unazungumzia tetesi tu? Wabunge wa CCM ni wachumia tumbo and I can bet, hawawezi kuikwamisha hayo marekebisho. Wakithubutu Kikwete anavunja bunge halafu wote wanapigwa chini!!!!! Nani yuko tayari kuuacha ulaji wa posho? Thubutu.

  Tiba
   
 3. M

  Makupa JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Jk chonde chonde hawa wabunge wa chama chetu ni janga ,cha muhimu ni kufanya kile watanzania wanachotaka na si vinginrvyo
   
 4. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  wabunge wa ccm ni viazi tu hakuna kitu kila kitu wao kuiga 2015 piga chini wote!
   
 5. Kikarara78

  Kikarara78 JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,164
  Likes Received: 514
  Trophy Points: 280
  Mchambuzi na Wana JF,
  Mkuu tumekusoma na ninafikiri Ujumbe na Uchambuzi wako Wahusika wataufanyia kazi, mimi yangu nafikiri Wabunge wa CCM wataacha Ushabiki wao wa Chama na waweke Utaifa mbele, sijakataa kuonyesha au kushabikia Chama au Jambo lolote lile, kikubwa hapa mwisho wa siku tuwe kitu kimoja na Utaifa mbele.
  Nawakilisha

   
 6. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,161
  Likes Received: 1,250
  Trophy Points: 280
  Ila kweli JK kama anataka kujisafisha mbele ya watanzania wasiomwamini kama mimi, wabunge wakikwamisha huu mswada wa mabadiliko ya sheria ya katiba awapige chini, kwa sababu hawana faida yeyote kwa watanzania zaidi ya wao kuzidi kuwaza posho na kusinzia bungeni
   
 7. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Mkuu quote yako imeniacha hoi:
  TUMETHUBUTU, TUMESHINDWA NA TUMEKWAMA HAPA HAPA
   
 8. B

  Bambwene Member

  #8
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu shukrani kwa uchambuzi wako yakinifu, naomba uchambuzi huu upeleke kwenye makala malumu gazetini kwani nina hakika sio wabunge wote wa ccm wanaoingia humu jamvini hivyo wanaweza wasinufaike na ushauri wako, pia kwa faida ya wananchi walio wengi ambao nao hawana nafasi ya kuingia kwenye mtandao
  UBARIKIWE SANA.
   
 9. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #9
  Feb 5, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Nashukuru sana kwa kunipa moyo. Nitajitahidi kufanya hivyo, hasa kutokana na ushauri wako kwamba hii content ni nzuri, hivyo ina stahili kuwafikia watanzania wengi zaidi.
   
 10. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #10
  Feb 5, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Laiti uchambuzi huu ungeupeleka gazeti la Uhuru wallah wangekusikiliza.
  Sasa hivi watasema wewe ni mchadema hata kama yaweza kuwa ndio Mukama mwenyewe.

  Naukubali uchambuzi wako 110%
   
 11. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #11
  Feb 5, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Shabaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaash , Ameeeeeeeeeeeeeeeeen Makupa ni wewe umeona haya unampa JK ushauri ni kweli ukombozi ni huu sasa umewakubali Chadema kwamba wako kikazi zaidi na kwa ajili ya Watanzania ? Heko sana na JK anasoma hapa atakusikia .
   
 12. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #12
  Feb 6, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mchambuzi naomba nikupongeze kwa kuandika vitu vya maana na vyenye maslahi kwa taifa.

  Una hoja nzuri lakini bado zitakuwa ngumu kueleweka kwa wanaCCM wenzako walioacha maslahi ya taifa nyuma na kutanguliza ya chama mbele
   
 13. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #13
  Feb 6, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,785
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Penye kustahili sifa na pongezi lazima zitolewe,nampongeza Rais Kikwete kwa kutambua umuhimu wa maridhiano ktk jambo nyeti kama Katiba. Ambaye anaona rais amekosea huyo ni adui yetu watanzania na hatutakii amani.
   
 14. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #14
  Feb 6, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Real Man,
  Shukrani. Gazeti la Uhuru, Jambo Leo n.k wana haki ya kuchukua mawazo yoyote humu ili mradi wanatoa credit kwa jamiiforums, sio lazima kwa wanachama humu individually kwani wengi wetu hatuna majina humu. lakini nashukuru umeliona hilo. Mukama alianza kwa kasi nzuri lakini hakika hivi sana ameshalowa na CCM isiyo na dira. Na kuhusu mimi na uchadema, mimi ni mwana CCM, lakini kuna nyakati huwa naona umuhimu wa kuvuka 'kimtazamo', na kuungana na watanzania wenzangu waliopo CUF, CHADEMA, NCCR n.k, katika masuala yenye maslahi ya taifa, kwani nina amini katika siasa zilizo juu zaidi ya vyama. Siasa za vyama huja baadae. Kwani hata UK, USA, ni kawaida kwa wabunge/wanasiasa to cross the 'aisle' na kwenda kwa wenzao iwapo suala husika ni suala kuhusu maslahi ya taifa. Kwa hili kuhusu Katiba, Nipo na Chadema mia kwa mia, na mimi, kama alivyo Mnyika na Mbowe, nipo tayari kufungwa na kulipa faini hata ikibidi niuze viazi kukidhi gharama ya faini hizi, ili mradi naelimisha watanzania wenzangu ambao hawakupata bahati ya kuelewa mengi ya ulimwengu, kuhusu umuhimu wa katiba mpya Tanzania.
   
 15. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #15
  Feb 6, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Mkuu, hata kama nime-quote nukuu hiyo hapo juu, lakini niliyokusudia zaidi ni main post....hata hivyo si kwamba nimekosea, la hasha; nisingeweza ku-quote post ndefu kiasi kile. Kimsingi, nakubaliana na wewe kwa 98%. Asilimia mbili nilizoacha ni kwavile hukuzungumzia umuhimu wa vyama vya upinzani nao kufanya mchakato huu kuwa ni kwa ajili ya katiba yenye manufaa kwa taifa zaidi kuliko kuwa ni katiba ya kisiasa. Hofu niliyokuwa nayo kwa CCM ndiyo hiyo hiyo niliyonayo kwa upande wa upinzani; kwamba wote kwa ujumla wao wangependa kuona katiba yenye ku-favor zaidi itikadi zao badala ya maslahi ya taifa. Hata hivyo, pamoja na kwamba hofu niliyonayo kwa CCM ndio hiyohiyo niliyonayo kwa upinzani; bado uchambuzi wako nimeupa 98% badala ya 50% (i.e. 50% political favor kwa CCM, 50% political favor kwa upinzani) kwavile nafahamu fika kwamba ushabiki wa CCM kwenye suala la katiba ni hatari zaidi kutokana na uwingi wao bungeni kuliko ushabiki ambao unaweza kuletwa na upinzani kutokana na uchache wao.

  All in all, well said na ninaunga mkono kwa 100% endapo post ingechapishwa gazetini.
   
 16. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #16
  Feb 6, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  nampongeza sana Mchambuzi kwa nondo za ukweli na zilizotulia......

  naunga mkono kuwa nondo hii ni vyema ikatoka kwenye magazeti mengi iwezekanavyo....ila rahisisha lugha kidogo kwa manufaa ya wengi, pia usiache kubold kwenye msisitizo....

  nampongeza sana JK kwa nia yake ya dhati!!! sisi katika jf tuko pamoja katika hili....

  mungu mbariki JK, mungu ibariki tz!

  NB: mchambuzi, wewe ni CCM?
   
 17. K

  KIGIGI Member

  #17
  Feb 6, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  binafsi nampongeza sana jk kwa uamzi wake huo. swala la katiba ni kwa niaba ya taifa na siyo chama kimoja! hao wabunge wa ccm wajiangalie sana 2015 siyo mbali!
   
 18. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #18
  Feb 6, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Kimsingi nakubaliana na wewe. Ndio maana nikasema katika my original post kwamba, atakaye ibuka mshindi katika mchakato huu sio CCM wala Chadema bali Watanzania kama taifa kwani wao ndio watakuwa wamiliki wa katiba husika na waajiri wa serikali itakayokuwa madarakani kutokana na katiba husika. Umaarufu wa kusema fulani alianzisha wazo hili na lile ni umaarufu wa kupita, kwani hata umaarufu wa Nyererem kutuleta uhuru wa kisiasa, with all due respect, umeshapitwa na wakati, kwani hivi sasa tupo zaidi mkao wa kusubiria uhuru wa kiuchumi.
   
 19. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #19
  Feb 6, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  jk is also a smart politician

  he was sending messages to wabunge wa ccm...japo kati yao ni wenye ufahamu tu watakuwa wamemuelewa...

  leo mwanza alikuwa anahutubia....WANACCM, MASHABIKI WA CCM, WANACHAMA WA CCM, WAPENZI WA CCM...NA WANANCHI KWA UJUMLA.....

  at some point alimnukuu mzee makamba na usemi wake...NGUVU YA MAMBA KU-MAJI!!!!!

  kimsingi alikuwa anawakumbusha wanaccm wenzie na hasa wabunge kuwa....

  1. yeye ni raisi wa inchi na ana kura za makundi yote...

  2. CCM isiyo na hoja zenye mashiko itakufa very fast!!!!

  3. katika hili la katiba anatarajia zaidi nguvu ya umma na wazalendo...

  4. wawe makini, kwani huenda nguvu wanayoringia n kwa kuwa wako ndani ya chama tu!!
   
 20. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #20
  Feb 6, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Asante sana mkuu,

  Mimi ni mwana CCM ninayeamini kauli yetu kwamba Kukosoa na Kukosoana Ndio Silaha ya Mapinduzi, unlike wanachama wengine ambao pengine wanaamini katika kulindana, unafiki, na unafsi kwamba ndio silaha ya Kupata Vyeo na Kufaidi Posho. Na moja ya sababu kubwa kwanini bado nina mapenzi na CCM ni uwepo wa viongozi kama Nape Mnauye. Movement zake ndani ya CCM zinatoa mwanga wa matumaini (hata kama kwa sasa mwanga huu bado ni hafifu), kwamba ipo siku, hata kama ni miaka 20 tokea sasa, CCM itarudi katika misingi yake, kwani mageuzi aliyoyaanzisha Nape, ingawa yanaonekana ni kama ya mwendawazimu, mageuzi haya hayawezi tena kurudi nyuma, whether Nape awepo au asiwepo, msingi umeshawekwa. Ni suala la muda tu, na suala la kurithishana silaha za mapinduzi ndani ya chama.
   
Loading...