Wabunge wa CCM aibu

Wabunge wa CCM aibu

Ewe punguani haujuwi kuwa pale kuna wanachama wa kambi tofauti?

Sasa mbunge wako kama anaakili anachotakiwa awakinashe wa chama kingine wamuunge mkono. Na tumeshawahi kuona kuna hoja wabunge wa vyama vyote wanaziunga mkono wakiona zina maslahi ya jumla kwa Taifa. Hujayaona wewe?

Lakini hivi vi hoja vya mradi tu mpinzani anapinga kwa kuwa ni mpinzani, hivyo tunawahenyesha tu.

Sawasawa.... Unafanya kazi yako safi kabisaa....!
 
CCM lazima watazidi kumchukia maana amewapa " MAKAVU LIVE" bila kupepesa macho

Acha wachukie maana wameamua kujitoa ufahamu wenyewe hivyo kuitwa vichaa ni jina sahihi kwao.
 
Tatizo la waheshimiwa wa CCM wana lala sana wakisikia wanao afiki waseme ndio wao wanadakia tuu bila kujua chanzo cha hoja na hili ni tatizo sana kwani waje wabadilike kuangalia wingi wa watu badala ya point
Hata kama hoja ni ya kijinga watu wanashabikia kwa kuangalia wingi badala ya kuangalia uzito wa hoja
Ndo maana ya hii nchi hsitakaa isonge mbele
 
ndaniya bunge kinachosemwa na wabunge wa ccm hata kama ni cha hovyo utasikia ndioooooo
 
Mliyapenda wenyewe kwa kuwapa ridhaa nyie wenyewe. Kama mnaona sio sawa mwezi wa kumi hauko mbali. Wamalizieni wasirudi ili wabaki kujifunza namna ya kuwakilisha wananchi.
 
Wameonyesha wamo bungeni kwa masilahi ya chama na siyo kuwawakilisha wananchi.
 
it is so called "kali ya mwaka"
mambo bado. Mungu ataenda kufunua kila kilichojificha kutokana na maombi ya kilio cha watu wake. Subirini muone ukuu wa mungu
Ni hatua kwa hatua. wahusika wenyewe wanashangaa inakuaje aje... mbona siku zinavyosogea tunaumbuka na hili mara lile. WENYE MACHO ONENI
 
Huitaji kuwa na degree kutambua upumbavu wa wabunge wa CCM.. Hichi kisa kimetokea muda huu bungeni.

Baada ya Ester Matiko kutoa hoja, sasa Naibu Spika anahoji bunge..

Naibu Spika : Wanaohafiki hoja ya Ester Bulaya (alikosea jina) waseme NDIO..

Wabunge wa CCM: Ndioooooooooooo

Naibu Spika : Samahani sio Ester Bulaya, ngoja nihoji tena "Wanaohafiki hoja ya Ester Matiko wasime ndio"

Wabunge wa CCM : "kimya"

Naibu Spika : wasiohafiki hoja ya Ester Matiko wasime sio.

Wabunge wa CCM : Siooooooooo

Ina maana wao wanapiga kura kwa kusikiliza mijadala au kusikiliza majina?? Ina maana kama jina ni la mpinzani jibu ni sio hata kama hoja hiyo inafaa. Maana mwanzo walipohoji kwa jina la Ester Bulaya waliikubali hoja..




[/SIZE]
HUU NDIO UJINGA UNAOANGAMIZA TZ!Bila kutoka kwenye mawazo mfu nchi itaendelea kuangamia,mabunge yote ulimwenguni hujadili hoja iliyoko mezani!haijalishi nani aliyeitoa so long as ni kwa masilahi ya nchi,mtajifunza lini enyi wabunge?Vyama vitapita ila TZ alioicha mwalimu itakuwepo kwa hiyo TZ KWANZA NA SIO USHABIKI WA KIJINGA WA VYAMA...
 
Back
Top Bottom