Wabunge toka Zanzibar wasiruhusiwe vikao vya wizara sisizo za muungano bungeni

Pamoja na kwamba title yako inaleta matiki, siiungi mkono kwa sababu tutaishia kuwaambia na wabungue wasijadili maswala yasiyotoka majimboni kwao.
Mkuu unaonekana hujamwelewa. Jifunze kwanza muundo wa muungano ndipo utaweza kuelewa anachokisema mtoa mada.
 
Hili jambo limeshazungumzwa sana lakini katiba ndiyo inalilea. Tusubiri serikali tatu labda litapita. Muundo wa muungano ndio uliopo wenye kuleta utata wote huo.
 
Mleta uzi kanichekesha sana, the way alivyoandika ni kama vile ameshtukia kitu fulan hivi, anyway hoja yako itakuwa na mashiko tukiwa na serikali ya TANGANYIKA!
 
Ndiyo maana kasema washiriki mijadala kwenye wizara za muungano tu hizi nyingine ambazo si za muungano wawaachie wabunge wa Tanganyika peke yao kama ilivyo kwao ambapo watanganyika hawaingii

Ngoja nikukumbushe Historia Kidogo

Tanganyika na Zanzibar ziliungana Kuunda Tanzania...

Cha ajabu Zanzibar iliendelea Kubaki kama nchi lakini Tanganyika ikapotea katika mazingira ya Kutatanisha...

Kwa hiyo basi Kila Mzanzibari ni Mtanzania ...

Kwa mujibu wa katiba ya Tanzania Mzanzibari (Mtanzania) anaweza kuwa waziri katika wizara yoyote ya Jamhuri wa muungano...

Lakini Mtanganyika hawezi kuuongoza katika wizara Zanzibar (Nchi Jirani)...


Suluhisho ni kuridisha serikali ya Tanganyika tuwe na serikali Tatu ili wazanzibari wabaki katika Bunge la Tanzania tu...

Au tuwe na Serikali moja kuondoa purukushani zote hizi...
Au tuvunje muungano kila mtu afate lake....
 
Back
Top Bottom