Wabunge toka Zanzibar wasiruhusiwe vikao vya wizara sisizo za muungano bungeni

East African Eagle

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
3,759
2,205
Kuna wizara chache ambazo ndizo tumeungana katika mmungano.Hivyo wabunge wa Zanzibar waruhusiwe kuhudhuria na kulipwa posho vikao hivyo tu vinavyohusu wizara za kimuungano.Hizo zingine wasihudhurie kabisa maana haziwahusu kama vile ambavyo wizara zao zilizoko kule Zanzibar sizizo za kumuungano ambavyo haihusu Tanzania bara.

Pia iwe marufuku wabunge wa Zanzibar kushiriki kujadili na kupitisha miswada ya Sheria inayohusu mambo ya Tanzania Bara tu.

Pia mijadala ya bunge iwe inaanza na wizara za Muungano zikishamalizika wabunge wa Zanzibar waondoke wapande meli au ndege warudi zanzibar waache wabunge wa Bara waendelee na mijadala ya wizara zao zinazohusu mambo ya bara tu.
 
Na UVUNJWE tu. Tumechoka. Nasema tena TUMECHOKA

Na sio tumechoka bali tum'majii !

Sasa huyu mbutwai mleta mada nae atuambie ni wapi kwenye Katiba kuna sehemu imeandikwa Tanzania Bara ,hivi Tanzania Bara ni nchi gani au Taifa gani ? Ni Wizara gani zisizo za Muungano ? Na kama si za Muungano ni za nchi gani ?

Labda ni msaidie tu akae atulie ,Kila Mzanzibari ni Mtanzania ila kila Mtanzania si Mzanzibari ,wasio WaZanzibari wanaishi chini ya kivuli tu,ila hawana Utaifa wamehifadhiwa ndani ya Muungano.
 
Sawia kabisa. Hakuna mahali panaitwa Tanzania bara. Zanzibar iliungana na Tanganyika sio bara.
 
Kuna wizara chache ambazo ndizo tumeungana katika mmungano.Hivyo wabunge wa Zanzibar waruhusiwe kuhudhuria na kulipwa posho vikao hivyo tu vinavyohusu wizara za kimuungano.Hizo zingine wasihudhurie kabisa maana haziwahusu kama vile ambavyo wizara zao zilizoko kule Zanzibar sizizo za kumuungano ambavyo haihusu Tanzania bara.

Pia iwe marufuku wabunge wa Zanzibar kushiriki kujadili na kupitisha miswada ya Sheria inayohusu mambo ya Tanzania Bara tu.

Pia mijadala ya bunge iwe inaanza na wizara za Muungano zikishamalizika wabunge wa Zanzibar waondoke wapande meli au ndege warudi zanzibar waache wabunge wa Bara waendelee na mijadala ya wizara zao zinazohusu mambo ya bara tu.
Mkuu umeibua hoja nzuri sana,ina maana kumbe haifanyiki hivyo? Huu ni ujinga na ufujaji wa mali ya umma isivyo stahili,unajua tatizo sisi wa bara tunawachukulia wazenji poa poa tu,ilihali wao kule kwao wanatuchukulia tofauti kabisa ... we regard them like children,lazy affair fulani,mimi naona huu uwe mjadala mpana bungeni,wajitokeze wabunge jasiri waibue hoja hii hata kama watapigwa sana mawe ... huu ni ujinga sana.
 
Tolea maelezo na haya.
Rais akiwa mzanzibar afanyeje kazi?
Makamu wa Rais afanyeje kazi
 
Hoja nyepesi sana. Bunge ni la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na si bunge la Tanganyika. wale wabunge kutoka Zanzibar ni wabunge wa Tanzania kwa hiyo lazima washiriki mijadala yote na sivinginevyo.
 
Kuna wizara chache ambazo ndizo tumeungana katika mmungano.Hivyo wabunge wa Zanzibar waruhusiwe kuhudhuria na kulipwa posho vikao hivyo tu vinavyohusu wizara za kimuungano.Hizo zingine wasihudhurie kabisa maana haziwahusu kama vile ambavyo wizara zao zilizoko kule Zanzibar sizizo za kumuungano ambavyo haihusu Tanzania bara.

Pia iwe marufuku wabunge wa Zanzibar kushiriki kujadili na kupitisha miswada ya Sheria inayohusu mambo ya Tanzania Bara tu.

Pia mijadala ya bunge iwe inaanza na wizara za Muungano zikishamalizika wabunge wa Zanzibar waondoke wapande meli au ndege warudi zanzibar waache wabunge wa Bara waendelee na mijadala ya wizara zao zinazohusu mambo ya bara tu.

You are a brain, there is no reason for them being in the house for non union matters as they just misuse tax payers money - pesa wanazolipwa posho kwa kuhudhuria mijadala isiyowahusu zingetumika kutekeleza miradi ya maendeleo iliyokwama kea visingizio vya kutokuwa na fedha
 
Pia mijadala ya bunge iwe inaanza na wizara za Muungano zikishamalizika wabunge wa Zanzibar waondoke wapande meli au ndege warudi zanzibar waache wabunge wa Bara waendelee na mijadala ya wizara zao zinazohusu mambo ya bara tu.

Kwani kuna serikali ya tz bara au tanganyika? Huu muungano ni complex kweli kweli hata sielewi
 
Wazanzibari walio wengi hapa nakusudia 90% tunaukataa muungano ila Tanganyika ndio yenye kulazimisha lakini yote haya yasingelikuwepo. Nyinyi WaTanganyika badala ya kulalamika katika mitandao eti ZANZIBAR ndio yenye kunufaika kwenye muungano, badala yake wapeni shinikizo viongozi wenu waiachie ZANZIBAR iende kivyake. Lakini ujasiri huo hawana.
 
Ni bunge la Jamhuri ya Muungano. Hoja yako haina mashiko.

Mvivu wa kufikiri!Hoja ni nzuri na nzito.Kimsingi ilitakiwa ifanywe hivyo vinginevyo ni matuizi mabaya ya fedha na kukosa uzalendo.
 
Back
Top Bottom