Wabunge toka Zanzibar wasiruhusiwe vikao vya wizara sisizo za muungano bungeni

bopwe

JF-Expert Member
Oct 1, 2013
1,769
2,000
Tatizo lenu mlopoambiwa mkatoe maoni ya katiba watu wana fanya fujo na kutukana viongozi mfano tundu always akilaumu lakini alishindwa kusema mchango wake nini kifanyike au kipi kibaya kiondolewe
Leo rasimu imekamilika lakini mchango wa wasomi na kama wewe kwenye maoni hauridhishi
So hayo yalitakiwa uyatoe kwa warioba
Hii rasimu nadhani iyakuwa na mapungufu
Mfano kuna kuondosha wakuu wa mikoa
Na shughuli hizi zikachukuliwa na mayor wa kuchaguliwa na wananchi
Wakuu wa wilaya nao wakawa manainu mayor wakuchakuliwa
Mkurugenzi wa jiji nao nafasi ziyangazwe na muhimu ni qualification sio kisiasa
Kuna mambo mengi yalisemwa ila hayakupata bataka za wanasiasa hasa wa upinzani isipokua znz wao walipigania sana wana chotaka ila huku hamna kitu
 

bopwe

JF-Expert Member
Oct 1, 2013
1,769
2,000
Chuki tuliyofundishwa na wazanzibari ni kuwa kero za muungano inabidi zichukiwe na zisemwe wazi bila kumeza maneno kwa ujasiri.Sasa hii ya bungeni ni kero kubwa isiyoweza kunyamaziwa.Mbunge wa Zanzibar kuweko kwenye kikao cha wizara au kamati ya bunge isiyo ya muungano hilo sikubali.Mimi kama mlipa kodi naona hasira kulipia hela yangu mtu aliyekaa kikao kisichomhusu.Siyo nina wivu na wabunge wa zanzibar kuwa wanapata posho.Hivi mimi kama mlipa kodi ninayemlipa hiyo posho unadhani naona wivu au nina hasira kulipia kitu ambacho hakina VALUE FOR MONEY KWANGU kwa kulipa asiyehusika? Kama ni kuchukia kweli nachukia kama mlipa kodi.

Unacho sema sawa kabisa ndio maana walitaka serikali tatu ya znz ya tanganuika na tanzania
Znz watakua na bunge lao kwa mambo yao na pia tanganyika watakua na bunge lao na mambo yao na upande wa tanzania nalo litakua na wabunge kutoka pande mbili watajadili yale yanayohusu muungano tu badi
Huu ndio mwatubaini wa wazo lako
Lakini kwa sasa tanganyika imejificha na kujifanya wao ni muungano na wao mdio kila kitu
Haya yalikua yashamaliza wakati ule mswaada wa tanganyika ulipopitishwa bungeni
Lakini mwalimu nyerere akaupinga lakini wangemwambia mzee kwa hili unakosea wacha tuliibadilishe
Lakni fikra za zidumu hawakuweza kufumbua midomo yao
Leo warioba anasema aahg serikali tatu 3 ndio dawa
 

Statesman

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
23,891
2,000
kuna tatizo pia la sheria zilizopo ambazo zinatumika jamhuri ya muungano wa tanzania kwa mambo ambayo si ya muungano, nadhani ni muda muafaka wa kufanya amendments katika applicability ya sheria hizo ili kuepuka mgongano wa kimaslahi na kukiuka katiba..
 

12STONE

JF-Expert Member
Mar 16, 2013
1,109
1,475
Hili jambo ni zuri na lakupendeza sana hawa wazenji wamekuwa na midomo mirefu sana ya kutusemea hata yale yasiyo wahusu-Tukifanikiwa kuendesha bunge kwa mtindo huu tutakuwa tumevifunga vinywa vya Ujinga.
Watanganyika tunapunjwa sana na kundi dogo kutuamuliwa mambo nyeti.NAUNGA MKONO HOJA YAKO INALIPA.
 

mandili

Senior Member
Mar 16, 2013
141
195
Issue apo ni katiba tu ndo twaweza pata suluhu, mengine utapigadomo lakin jibu huwez pata. kwasababu bara hatuna raisi zenj kuna rais na balaza la mawazir na serikali yote. pia watu wa Zenj wanaongoza wizara zisizo za muungano lakin wa bara hawawez. ie mzenj ni mTZ lakin M'bara ni wa bara tu zenj hakumhusu
 

Eric Cartman

JF-Expert Member
May 21, 2009
6,815
2,000
It has never been the aim of our Government to reduce Government expenditures. Asilimia kubwa ya Bajeti ya Serikali ni mishahara na posho. Unaweza kupunguza gharama kubwa kiasi gani kwa kuwatoa wabunge wa Zanzibar kwenye mijadala ya Wizara sizizo za Muungano?! Yapo maeneo ya kupunguza matumizi lakini sio hapa.
I thought that was i said, nevertheless if the intention is to cut costs do you think creating three house would be the solution.
 

Msingida

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
7,456
2,000
Hii hoja ni nzito inataka tafakuri ya kina.Nafanya rejea ya mambo ya muungano nitarudi baadaye..........
 

jerrytz

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
5,943
2,000
I thought that was i said, nevertheless if the intention is to cut costs do you think creating three house would be the solution.

Happy Feet,

Three Assemblies will definitely increase the cost however there is an issue to addressed here. The kind of Union we have is not taking us anywhere in development,we have alot of senior leaders who are doing nothing but to fill political posts which are needless
 

ITEGAMATWI

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
4,869
2,000
Hili litawezekana tu pale tutakapokuwa na serikali tatu! Ngoja tuone hiyo Tar 30 rasimu ya pili inasemaje kuhusu muundo wa serikali. Nafikiri hapa muafaka ni serikali tatu tu haya yote hayatatuumiza kichwa vinginevyo basi tukubali hakuna marefu yasiyo na ncha then tubaki na Tanganyika yetu wabaki na Zanzibar yao.
 

nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,520
2,000
Na sio tumechoka bali tum'majii !

Sasa huyu mbutwai mleta mada nae atuambie ni wapi kwenye Katiba kuna sehemu imeandikwa Tanzania Bara ,hivi Tanzania Bara ni nchi gani au Taifa gani ? Ni Wizara gani zisizo za Muungano ? Na kama si za Muungano ni za nchi gani ?

Labda ni msaidie tu akae atulie ,Kila Mzanzibari ni Mtanzania ila kila Mtanzania si Mzanzibari ,wasio WaZanzibari wanaishi chini ya kivuli tu,ila hawana Utaifa wamehifadhiwa ndani ya Muungano.
teh teh,mbavu mie!
 

nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,520
2,000
Mkuu umeibua hoja nzuri sana,ina maana kumbe haifanyiki hivyo? Huu ni ujinga na ufujaji wa mali ya umma isivyo stahili,unajua tatizo sisi wa bara tunawachukulia wazenji poa poa tu,ilihali wao kule kwao wanatuchukulia tofauti kabisa ... we regard them like children,lazy affair fulani,mimi naona huu uwe mjadala mpana bungeni,wajitokeze wabunge jasiri waibue hoja hii hata kama watapigwa sana mawe ... huu ni ujinga sana.
pamoja sana mkuu!
 

Maswala

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
560
225
Pamoja na kwamba title yako inaleta matiki, siiungi mkono kwa sababu tutaishia kuwaambia na wabungue wasijadili maswala yasiyotoka majimboni kwao.
 

mzenjiboy

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
878
500
Nyerere kakuwezeni sana nyie Wadanganyika i.e. Watanganyika. Kakufanyeni muikane nchi yenu ya asili Tanganyika nanyi mukakubali na badala yake akakubatizeni Utanzania nanyi mukafurahia. Wengi wenu kuitwa Watanganyika munaona aibu eti ni Watanzania. Mimi nawashauri ndugu zangu wa Tanganyika kuweni na uchungu na nchi yenu Tanganyika mutupilie mbali maneno ya wana siasa hasa nyie wasomi muache kuburuzwa. Huu muungano uliopo ni tambara bovu wakati wowote linaweza kuchanika.
 

Hydrobenga

JF-Expert Member
Jun 24, 2012
1,123
1,195
Haha na siku Raisi akiwa Mzanzibari Kama alivyokuwa Mzee Mwinyi...?
Lile ni Bunge La Jamhuri ya muungano wa Tanzania...
wabunge wa Zanzibar wana haki ya Kuhudhuria vikao vyote kama alivyo na haki Mbunge wako SUGU...

Inonekana huwapendi wazanzibari kupita kiasi...

SULUHISHO NI KUVUNJA MUUNGANO ...tubaki na BUNGE LA TANGANYIKA
 

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
13,392
2,000
Kuna wizara chache ambazo ndizo tumeungana katika mmungano.Hivyo wabunge wa Zanzibar waruhusiwe kuhudhuria na kulipwa posho vikao hivyo tu vinavyohusu wizara za kimuungano.Hizo zingine wasihudhurie kabisa maana haziwahusu kama vile ambavyo wizara zao zilizoko kule Zanzibar sizizo za kumuungano ambavyo haihusu Tanzania bara. Pia iwe marufuku wabunge wa Zanzibar kushiriki kujadili na kupitisha miswada ya Sheria inayohusu mambo ya Tanzania Bara tu. Pia mijadala ya bunge iwe inaanza na wizara za Muungano zikishamalizika wabunge wa Zanzibar waondoke wapande meli au ndege warudi zanzibar waache wabunge wa Bara waendelee na mijadala ya wizara zao zinazohusu mambo ya bara tu.
Well thought out mkuu. Mimi naongezea pia kuwa wabunge wa Zanzibar wasiwe mawaziri wa wizara zisizo za muungano ambazo ni za Tanganyika tu kama ilivyo sasa ambapo waziri wa afya ambayo siyo wizara ya muungano kwa upande wa Tanganyika imeshikwa na mbunge kutoka Zanzibar na ambaye ni mzanzibari. Hivi inawezekana mbunge kutoka Tanganyika akapewa wizara isiyo ya muungano ambayo ni ya Zanzibar? Kikwete sijui aliishiwa wabunge kutoka Tanganyika wenye sifa ya kuwa waziri wa afya? Au alikuwa anajikomba kwa mzee ruksa? This is unfair!
 

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
13,392
2,000
Haha na siku Raisi akiwa Mzanzibari Kama alivyokuwa Mzee Mwinyi...? Lile ni Bunge La Jamhuri ya muungano wa Tanzania... wabunge wa Zanzibar wana haki ya Kuhudhuria vikao vyote kama alivyo na haki Mbunge wako SUGU... Inonekana huwapendi wazanzibari kupita kiasi... SULUHISHO NI KUVUNJA MUUNGANO ...tubaki na BUNGE LA TANGANYIKA
Ndiyo maana kasema washiriki mijadala kwenye wizara za muungano tu hizi nyingine ambazo si za muungano wawaachie wabunge wa Tanganyika peke yao kama ilivyo kwao ambapo watanganyika hawaingii
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom