Wabunge ruksa kutukanana na kutukana kwa mujibu wa sheria ya JMT

Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,334
1,461
Wakili wa Serikali: Lema arudishiwe ubunge
NA HELLEN MWANGO
5th December 2012

lema%20na%20lissu.jpg

Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Godbless Lema (kushoto), akimsikiliza wakili wake, Tundu Lissu, nje ya Mahakama ya Rufaa jijini Dar es Salaam baada ya kesi yake ya kupinga kuvuliwa ubunge kuahirishwa jana. Lissu pia ni Mbunge wa Singida Mashariki kupitia chama hicho.


Wakili wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Vitalis Timon, ameiambia Mahakama ya Rufani kuwa waliopinga matokeo ya ubunge wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, hawakuwa na haki ya kufanya hivyo kisheria na kwamba matusi, kejeli na kashfa haviwezi kumvua nafasi hiyo.

Alidai kuwa matusi hayawezi kumvua ubunge Lema kwani wabunge wenyewe walitunga sheria namba nane ya mwaka 1995 ikiruhusu matusi baada ya kuona awali kuwa walikuwa wakibanwa na mahakama.

Wakili Timon alitoa madai hayo katika Mahakama ya Rufani mbele ya jopo la majaji watatu lililowajumuisha Jaji Nathalia Kimaro, Salum Massati na Benard Luanda, waliposikiliza rufaa iliyowasilishwa na Lema akipinga uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Arusha wa kumvua ubunge.

Lema alivuliwa ubunge Aprili 5 mwaka huu kufuatia kesi iliyofunguliwa na wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel.

"Wapiga kura hawawezi kupinga matokeo ya uchaguzi wakati yanayotokea katika kampeni hayawahusu, mpiga kura si sehemu ya kamati ya maadili na hana haki katika kampeni...katika ushahidi walalamikaji walidai kwamba walimshauri Batilda (aliyekuwa mgombea wa CCM) kwa muda mrefu afike mahakamani, alikataa ndipo wakaamua kwenda wao mahakamani," alidai na kuongeza kuwa:

"Julai 31, 1995 Bunge lilipitisha sheria namba nane wakisema kwamba matusi si sababu ya kutengua matokeo, wenyewe Wabunge waliruhusu watukanane katika sheria waliyotunga, wanapenda kutukanana, wabunge walijipendelea wakati wakitunga sheria hiyo baada ya kuona mahakama inawabana katika eneo hilo, waacheni watukanane waliyataka wenyewe," alidai wakili huyo mwandamizi wa serikali.


Timon alidai kuwa wanaohusika wakati wa kampeni ni wagombea, vyama vya siasa, mawakala wa wagombea na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) na kwamba wapiga kura wanahusika kulalamikia hatua za usajili wa wapiga kura na wakati wa kupiga kura.

"Waheshimiwa majaji, waliokuwa na maslahi binafsi katika kesi hii ni waliopoteza jimbo. Baada ya uchaguzi CCM walikaa kikao na kuazimia kulirudisha jimbo kwa kufungua kesi, walikuwa na nia mbaya walipofungua shauri hili," aliendelea kuieleza mahakama.

"Sioni kwa nini Jaji wa Arusha aseme Lema alikuwa na maslahi binafsi katika ushahidi wake kwa kuleta wanachama wa Chadema kutoa ushahidi, angewaleta watu gani zaidi ya hao waliokuwapo wakati wa kampeni?" alihoji.

"CCM walileta mashahidi wa CCM, lakini hawakuambiwa kwamba walikuwa na maslahi binafsi, naunga mkono rufaa na naomba uamuzi wa kumvua Lema ubunge utenguliwe," aliiambia mahakama.

Wakili wa Lema, Method Kimomogolo, akizungumzia hoja 18 za kukata rufaa hiyo, alidai kwamba Jaji aliyetoa hukumu ya kumvua ubunge Lema, Gabriel Rwakibarila, alikosea kisheria kuvutiwa na njia walizotumia shahidi wa 11 na 14 badala ya kuzingatia uzito wa ushahidi waliotoa.

"Alivutiwa na shahidi wa 11 Amina Ally ambaye anaishi kwa kuuza mitumba na shahidi wa 14 ambaye alitumikia jeshi nje ya nchi na akastaafu kwa kuogopa kupelekwa tena nje ya nchi," alidai Kimomogolo.

"Jaji alikosea kuegemea katika ushahidi usioaminika na ushahidi wa mdomo bila kutafuta ushahidi mwingine wa kuunga mkono hivyo kuifanya hukumu kutokidhi vigezo vya kuitwa hukumu," alidai Kimomogolo.

Kimomogolo alidai kuwa Jaji Rwakibarila wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Sumbawanga katika hukumu yake hakutumia mifano ya kesi mbalimbali zilizoamuliwa na Mahakama ya Rufaa, japo alipelekewa ili azirejee na mawakili wa pande zote mbili.

Kimomogolo aliendelea kulieleza jopo hilo la majaji kuwa Jaji Rwakibarila hakuchanganua wala kupima ushahidi licha ya kuwasilishiwa viini vikuu vilivyokuwa vinabishaniwa.

"Mrufani hakuwahi kukamatwa na Polisi wakati wa kampeni kwa kutukana na jaji hakusema makosa gani ya jinai yalitendwa na mrufani katika kampeni zake," alidai.

Alidai kuwa uamuzi uliomvua ubunge Lema ukikubaliwa na kuruhusu kila mtu apinge matokeo ya uchaguzi kwa kufungua kesi, hali itakuwa mbaya na kuongeza kuwa mtu afike mahakamani kwa malalamiko yanayomhusu.

"Jukumu la kutetea maslahi ya Taifa ni la Mwanasheria Mkuu wa Serikali, si wanachama wa CCM waliopinga ubunge, kama wanaona AG hafanyi kazi vizuri, wananchi wamwajibishe," alidai.

Wakili Kimomogolo alirejea kesi mbalimbali zinazofanana na kesi ya Lema ikiwamo ya Joseph Warioba dhidi ya Stephen Wassira, Basil Mramba dhidi ya Leonce Ngalai, William Bakari dhidi ya Mgonja na kesi ya Walid Kabourou iliyoamuliwa miaka 16 iliyopita na watu waliwasilisha hadi `tape' mahakamani.

"Kwa nini katika kesi ya Lema wajibu rufani hawakuwasilisha hata ushahidi wa `tape' kuonyesha matusi aliyotukana?" alihoji Kimomogolo.

Wakili wa wajibu rufani, Alute Mughway, alidai mashahidi wao walieleza kila kitu mahakamani na jaji alikuwa anajua nani mwenye jukumu la kuthibitisha kesi.

Alidai kuwa ushahidi uliotolewa haukupaswa kuungwa mkono na ushahidi wowote na kwamba siasa za uchaguzi zinatakiwa kuwa safi kwani hata katika kanuni za uchaguzi wanaonywa kuhusu matusi, kejeli na kudhalilishana.

"Siasa za matusi ni siasa za maji taka zilikatazwa, kanuni zilizokataza zilisainiwa na vyama vyote, watu wanachaguliwa kwa hoja si kungurumisha matusi na kuwadhalilisha wagombea wengine," alidai Mughway.

Alidai kuwa hukumu ilikidhi viwango vyote na kuomba rufaa itupiliwe mbali kwa sababu zilizotolewa na mrufani hazitoshelezi kutengua uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

"Waheshiwa, tunaomba uamuzi wa Mahakama ya Arusha ubaki kama ulivyokuwa na warufani waamuriwe kulipa gharama za kesi," alidai. Kesi iliahirishwa hadi tarehe ya hukumu itakapopangwa.

Akizungumza katika viunga vya mahakama hiyo baada ya kuahirishwa kesi hiyo, Lema aliwasihi wanachama wake kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu wakati wanasubiri hukumu.

"Hiki ni kipindi kigumu wakati tunasubiri hukumu kutolewa kuliko tulipokuwa tunasubiri usikilizwaji wa rufaa hii, nawasihi muwe na utulivu kwani kila mmoja amesikia mahakamani mawakili walivyotoa hoja zao," alidai Lema.

Aliwataka kuwa watulivu waiachie mahakama ifanye kazi yake kwa mujibu wa sheria na kwamba haki itatendeka.

Mapema saa 2:00 asubuhi, viunga vya mahakama hiyo vilifurika wafuasi wa Chadema wakiongozwa na Lema waliofika kusikiliza kesi hiyo pamoja na wananchi mbalimbali.

Ukumbi namba moja wa mahakama hiyo ulifunguliwa saa 2:30 asubuhi na saa 3:00 asubuhi jopo hilo liliketi chini na kuanza kusikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi jopo litakapopanga tarehe ya hukumu kama Lema atarudishiwa ubunge wake
ama la.

CHANZO: NIPASHE

NB: Naomba wanasheria wa JF mtuwekee hivyo vifungu vya sheria bunge letu tukufu liloviruhusu kurushiana matusi ili nisisikie mtu mwingine akifunguliwa kesi ya lugha za Lusinde.
 

SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,611
7,788
NB: Naomba wanasheria wa JF mtuwekee hivyo vifungu vya sheria bunge letu tukufu liloviruhusu kurushiana matusi ili nisisikie mtu mwingine akifunguliwa kesi ya lugha za Lusinde.
Kimsingi hakuna sheria au vifungu katika sheria "vinayoruhusu" kurushiana matusi. Sheria ya uchaguzi ya mwaka 1985 ilikuwa imeorodhesha mambo au matendo ambayo yanaweza kupelekea mgombea aliyeshinda kunyang'anywa ushindi ("declared void") (Section 108 (3)) na hili la kurusha maneno ("matusi") lilikuwamo. Sasa hiyo sheria ya kufanyia mabadiliko sheria ya uchaguzi ya mwaka 1995 iliondoa hiyo ibara ndogo ya 3 katika ibara ya 108 ya sheria ya uchaguzi ya mwaka 1985. Naamnini ni kwa kuondolewa kwa kifungu hicho ndio maana mwanasheria huyu wa serikali anadai "waliruhusu" matusi.

Unaweza kusoma ibara ya 20 ya sheria ya mwaka 1995 kwa pamoja na ibara ya 108 ya sheria ile ya mwaka 1985 hapa:
http://polis.parliament.go.tz/PAMS/docs/8-1995.pdf
http://polis.parliament.go.tz/PAMS/docs/1-1985.pdf

NB: Mimi sio mwanasheria!
 

Bobuk

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
5,870
3,262
Duuuu hawa ndiyo wabunge wagonga meza wa CCM. Kama kweli walipitisha SHERIA hiyo inayoruhusu MATUSI wakati wa kampeni, watakuwa wabunge wa hovyo ambao hawajawahi kutokea tangu dunia iumbwe.

Lakini pia hii itakuwa FARAJA kwa akina Livingstone Lusinde na Mwigulu Nchemba maana wao wana viwanda vya kutengeneza matusi.
 

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
47,034
64,120
waachae watukanane............hahahaaaaaaaaaaaaa
 

ojoromong'o

Member
Nov 6, 2012
91
38
Duuuu hawa ndiyo wabunge wagonga meza wa CCM. Kama kweli walipitisha SHERIA hiyo inayoruhusu MATUSI wakati wa kampeni, watakuwa wabunge wa hovyo ambao hawajawahi kutokea tangu dunia iumbwe.

Lakini pia hii itakuwa FARAJA kwa akina Livingstone Lusinde na Mwigulu Nchemba maana wao wana viwanda vya kutengeneza matusi.

...mkuu mbona walisha pitisha sheria nyingi tu za kijinga,unaikumbuka ile sheria ya kukonyeza?(haijalishi unamatatizo ya macha au la,ni kwamba ukionekana tu unamkonyeza mwanamke bila ridhaa yake imekula kwako)...
 

kelao

JF-Expert Member
Sep 24, 2012
8,136
5,763
Wangemwomba lusinde awapeleke hao wabunge semina ya matusi kwani yeye ana uzoefu wa kutosha.
 

ezra1504

Member
Nov 2, 2010
55
12
Hawa jamaa ni wamshitaki na Lusinde? Maana yule ndo anatukana mpk basi au wakishindwa ndo wanajua tulitukanwa ila wakitukana wao haina madhara? Wapi Wassira?
 

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,780
Na James Magai | Decemba5 2012

WAKILI wa Serikali Mkuu Timon amedai kuwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ilikosea kutengua ubunge wa aliyekuwa Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema, kwa madai ya kutumia lugha za matusi kwa kuwa Bunge limeruhusu wanasiasa kutukanana kwenye kampeni.

Wakili Vitalis alitoa madai hayo jana, wakati wa usikilizwaji wa rufaa ya Lema, aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),katika Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam.

Wakati wakili huyo wa serikali akitoa madai hayo, Wakili wa wajibu rufaa, ambao walishinda katika kesi ya msingi, Alute Mughway, naye alidai kuwa Mahakama Kuu, Arusha ilikosea katika uamuzi wake, pamoja na mambo mengine, kwa kukataa baadhi ya madai yao.

Lema alivuliwa ubunge April 5, 2012, katika hukumu iliyotolewa na Jaji Gabriel Rwakibalia, kufuatia kesi iliuyofunguliwa makada watatu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel, wakipinga ushindi wake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Lema kupitia kwa Wakili wake Method Kimomogoro alikata rufaa Mahakama ya Rufani, lakini Novemba 8, 2012 mahakama ilitupilia mbali rufaa hiyo baada ya kuini kuwepo kwa dosari za kisheria, kutokana na pingamizi lililowekwa na upande wa wajibu rufaa.

Hata hivyo mahakama hiyo ilimpa nafasi nyingine ya kukata rufaa tena baada ya kumpa siku 14 kufanya marekebisho ya dosari hizo za kisheria na kuiwasilisha mahakamani ndani ya muda huo, amri ambayo aliitekeleaza.

Wakati Lema akikata rufaa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu kumvua ubunge, wajibu rufaa nao walikata rufaa (Cross Appeal) kupinga uamuzi wa mahakama hiyo, huku wakibainisha hoja nne.

Katika hoja ya kwanza hadi ya tatu walidai kuwa Jaji alikosea katika hukumu yake kwa kuchanganya vituo vilivyotolewa ushahidi na mashahidi wanne na hatimaye akakataa ushahidi wapo, pamoja na tarehe za ratiba ya kampeni ya CCM nay a Chadema.

Hoja ya nne walidai kuwa Jaji alikosea kwa kuamua kuwa hata kama Lema kwenye kampeni zake alidai kuwa Dk. Buriani ni mkazi wa Zanzibar hatafaa, wakidai kuwa ukazi si sifa ya kuchaguliwa kuwa mbunge.

Hatimaye rufaa hizo zilisikilizwa jana na jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani, lililoundwa na Jaji Salum Massati, Jaji Bernard Luanda, chini ya uongozi wa Jaji Nathalia Kimaro.

Wakati wa usikilizwaji wa rufaa hiyo, mawakili wawili ambao ni ndugu, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu na kaka yake Mghway, walipambana vikali kwa hoja za kisheria.

Lisu, Kada wa Chadema ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alikuwa akimtetea Lema mrufani (Lema), akisaidiana na Wakili Method Kimomogolo, huku Mughway akiwatetea wajibu rufani ambao ni makada wa CCM.


[/COLOR]Hata hivyo Wakili Vitalis, aliyemwakilisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), ambaye pia alikuwa upande wa Lema, alidai kuwa wajibu rufaa hawakuwa na haki ya kufungua kesi kupinga ushindi wa mrufani (Lema) kwa kasoro zilizotokea wakati wa kampeni.

Wakili Vitalisi alidai kuwa wajibu rufani hao hawakuwa wahusika katika katika mchakato huo kampeni na kwamba hata kama kulikuwa na lugha ya matusi kama walivyodia katika ushahidi wao mahakama haikuwastahili kumvua ubunge kwa kuwa Bunge liliruhusu matusi kwenye kampeni.

Akifafanua zaidi Wakili Vitalis alidai kuwa anayepaswa kufungua kesi mahakamani kwa madai ya lugha ya matusi ni yule aliyetukana kwa kuwa hayo ni maumivu ya mtu binafsi na kwamba hata anapokufa, madai yake nayo hufa wala hayawezi kuendelezwa na mtu mwingine.

"Sasa iweje kwa mtu ambaye yuko hai lakini watu wengine ndio waje mahakamani kufungua kesi?", alihoji Wakili wa Serikali Vitalisi.

Aliongeza kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 108 cha Sheria ya Uchaguzi Sura ya 313 ya mwaka 2010, matusi si miongoni mwa mambo ambayo yanaweza kutengua matokeo ya uchaguzi.

Hata hivyo Wakili huyo wa Serikali alidai kuwa Bunge liliruhusu kutukana na baada ya kufanya marekebisho katika sheria ya uchaguzi, mwaka 1995 kufuatia hukumu ya kesi kati ya AG na Aman Waridi Kaburu.

Alidai awali sharia ilikuwa inaruhusu matokeo ya uchaguzi kutenguliwa kutokana na lugha za matusi, lakini baada ya hukumu ya kesi ya Kaburu Januari , 1995, mwezi Julai mwaka huo Bunge lilifanya marekebisho na kuondoa suala la matusi katika mambo yanayoweza kutengua uchaguzi.

"Hapa Bunge liliifunga mikono mahakama, hakuna kutengua matokeo ya uchaguzi kwa mambo amabayo hayajatajwa. Kwa uamuzi huu waliamua kutukanana, kwa hiyo nasi hatuwezi kuwakatalia.", alidai Wakili Vitalisi.

Pia alidai kuwa kifungu cha 108 (2) cha Sheria ya Uchaguzi kinaeleza aina ya za ubaguzi zinazokatazwa ni pamoja na wa kidini na kikabila na kwamba aina nyingine kama makazi (Uzanzibar, Ubara) hazijatajwa.

Awali Wakili wa Lema Kimomogoro aliainisha sababu 18 za rufaa hiyo kuwa ni pamoja na Jaji kuamua kuwa Sheria zinazotumika katika Nchi za Jumuiya ya Madola (hususan Uingereza), hazitumiki katika kesi za uchaguzi nchini.

Sababu nyingine alidai kuwa ni Jaji kutokujieleza vyema kama wajibu rufaa waliwajibika katika hati yao ya madai kwa kutaja maneno dhahiri ya ubaguzi dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk Batlida Burian.

Sababu nyingine alidai kuwa Jaji alikosea kuamua kuwa mtu yeyote aliyejiandikisha kupiga kura ana haki isiyo na mpaka ya kufungua kesi kupinga matokeo.

Alidai kuwa hoja yao ni kwamba mtu anakuwa na haki hiyo pale ambapo haki yake imevunjwa au inaelekea kuvunjwa na si pale aliyeathirika na ukikwaji wa haki hiyo ni mtu mwingine.

Sababu nyingine alidai kuwa Jaji hakutolea uamuzi baadhi ya hoja ambazo zilitakiwa kujibiwa na kwamba hakujielekeza vyema kwenye wajibu wa kuthibitisha madai kwa kueleza kama walalamikaji walithibitisha madai yao bila kuacha mashaka yoyote.

Sababu nyingine ni kwamba Jaji alitumia ushahidi wa mdomo bila kungwa mkono na ushahidi mwingine, na kwamba Jaji alijielekeza vibaya katika kupima ushahidi wa pande zote na badala yake akaegemea ushahidi wa walalamikaji na mashahidi wao tu.

Pia alidai Jaji alikose kusema kuhusu hoja ya vitendo vya kijinai na kwamba hakuvitaja hivyo vitendo vilivyofanywa na mrufani, huku akisisitiza kuwa hukumu hiyo haikukidhi vigezo vya kisheria.

Hata hivyo akijibu hoja hizo, Wakili Mughwa alidai kuwa hukumu hiyo imekidhi vigezo vya kuwa hukumu kwa kuwa inaeleza mambo yote yanayopaswa kuwepo.

Wakili Mughwa alidai kuwa walalamikaji katika kesi ya msingi kwenye ushahidi wao walieleza maneno yaliyokuwa yakilalamikiwa huku akidai kuwa mawakili wa utetezi wanaipotosha mahakama kwa kuwa mambo mengine aliyopinga yako kwenye kumbukumbu za mahakama.

Kuhusu matumizi ya Sheria za Nchi za Madola, huku akitoa orodha ya kesai mbalimbali, alidai kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 2 (3) cha Sheria ya Uchaguzi kesi za uchaguzi zinaendeshwa kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi na kwamba Jaji alikuwa sahihi kuamua hivyo.

Akizungumzia haki ya mpiga kura kufungua kesi, Wakili Mughway alidai kuwa haki hiyo inaelezwa katika kifungu cha 111 (1) (A) cha Sheria ya Uchaguzi (2010) pamoja na katiba
 

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,780

Siasa za CHAMA TAWALA ni za CHUKI; Kama HAUPENDWI watayafanya MAISHA yako NDANI ya KUNDI GHALI haswa na SHIDA kutaka kurudi KUNDINI...
 

Naytsory

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
2,192
789
Yawezekana Jaji Gabriel ni mbumbumbu wa sheria, alishinikizwa au alikula fedha chafu. Siyo makosa ya kawaida haya, kama inawezekana achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kuidhalilisha taaluma ya sheria.
 

Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,998
1,156
Yawezekana Jaji Gabriel ni mbumbumbu wa sheria, alishinikizwa au alikula fedha chafu. Siyo makosa ya kawaida haya, kama inawezekana achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kuidhalilisha taaluma ya sheria.
Hivi hayumo kwenye ile list ya Lissu na majaji wa kutliwa shaka?
 

Naytsory

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
2,192
789
Jiulize ni watanzani wangapi wameathirika na majaji kama Gabriel na kwa kutokuwa na uwezo wa kukata rufaa sasa wako magerezani na wengine kudhulumiwa haki zao? Pili ikiwa mahakama kuu ina majaji kama Gabriel, je, mahakama za mwanzo, wilaya na mkoa zina hali gani? Mh. Rais wa JMT tafakari chukua hatua.
 

KIJOME

JF-Expert Member
Jun 7, 2012
3,084
732
Duh!!Haya ni majanga,hivi huyu jaji rwakibalia hayupo kwenye ile list ya majaji vilaza wa jeyikeyi?kAZI IPO...
 

Mpwechekule

JF-Expert Member
Jul 8, 2012
221
55
Wampe ubunge wake haraka kwani ukiitishwa uchaguzi itakuwa aibu kwa ccm na unaweza kuwa ndio mwanzo wa kupelekwa icu
 

Mheshimiwa Mwl Steve

Senior Member
Nov 3, 2012
139
40
Nchi iko kimagumashi zaidi.Ukimpendezesha mkulu unalamba cheo sio kwa sababu ya compency yako.Tunawashukuru akina tundu lissu kwa kutupa mawe kwenye kichaka,hakika watakurupuka wengi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom