Wabunge, Rais na Makamu wake wakatwe mishahara na Posho kulipa Dowans

Mi naona pia wanasheria wakatwe kuanzia chenge, werema , kina jaji mkuu wote pia waongezwe kny list ya kuilipa fidia dowans
 
Kama nakumbuka vizuri, Sita ile siku akifunika kombe pale Dodoma alisema mjadala umefungwa na ni kosa la kanuni kuujadili tena, hivyo nina mashaka ya kutumiwa zuio la kanuni kuuibua upya.

Hivi nyie mliowasikia Werema na Ngeleja, mnadhani wanaongea kwa authority ya nani?, si ni mkuu wa kaya, ndiye aliyeamua hili lisiende cabinet, lipite juu kwa juu, lipeni!, sasa cabinet gani itajadili wakati uamuzi wa kuwalipa umeshapishwa?.

Msisahau, rais wetu ni executive president mwenye mamlaka ya mwisho, haamrishwi kufanya lolote wala halazimiki kuukubali ushauri wa yoyote, na maamuzi yake ni ya mwisho, yaani final, kaamua tunalipa, na kweli tunalipa, huku tukilipa, wengine wakijua tunawalipa hao Dowans, huku sisi wengine tukijua ni hakika, wanajilipa!.
 
Mzee MMK sitaacha kusema tena na tena dawa ta Tanzania ni kuiondoa CCM kwa nguvu tu, hiyo ya kukatana mishahara haitasaidia lolote. Wakilipa tu, sote twende barabarani kama walivyofanya wenzetu Tunisia. Wamezi kutuchezea hawa!!!
 
Mzee MMK sitaacha kusema tena na tena dawa ta Tanzania ni kuiondoa CCM kwa nguvu tu, hiyo ya kukatana mishahara haitasaidia lolote. Wakilipa tu, sote twende barabarani kama walivyofanya wenzetu Tunisia. Wamezi kutuchezea hawa!!!

Hili ndio suluhisho tosha na muafaka
 

Mkuu unamaanisha wabunge wa CCM na baraza la mawaziri! au pamoja na wabunge wa upinzani? :shock:
 
Deni tumelipa
 
Ndugu sijakuelewa sawasawa hapo kwenye RED unamaanisha sisi wananchi wenye kipato duni ndio tunaostahili kubeba mzigo huo? naomba ufafanuzi.
N:b; naunga mkono hoja ya Mzee mwanakijiji kwa asilimia 200%.
Kumbe zamani ulikua na kipato duni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…