Wabunge, Rais na Makamu wake wakatwe mishahara na Posho kulipa Dowans

Mi naona pia wanasheria wakatwe kuanzia chenge, werema , kina jaji mkuu wote pia waongezwe kny list ya kuilipa fidia dowans
 
hapana.. Pasco; hawa waliopo sasa hivi ndio wanaweza kuzuia na kuwawajibisha wahusika wote. Nguvu ya Bunge au kuwajibika kwa Bunge hakuishi pale wabunge wengine wasipochaguliwa. Vinginevyo, mambo yanayofanywa na Bunge yangekuwa yanaisha nguvu pale Bunge moja linapoisha na lingine kuingia. Kwani baraza la mawaziri litakaloamua suala hili ndilo lililokuwepo wakati mkataba unaingiwa?
Kama nakumbuka vizuri, Sita ile siku akifunika kombe pale Dodoma alisema mjadala umefungwa na ni kosa la kanuni kuujadili tena, hivyo nina mashaka ya kutumiwa zuio la kanuni kuuibua upya.

Hivi nyie mliowasikia Werema na Ngeleja, mnadhani wanaongea kwa authority ya nani?, si ni mkuu wa kaya, ndiye aliyeamua hili lisiende cabinet, lipite juu kwa juu, lipeni!, sasa cabinet gani itajadili wakati uamuzi wa kuwalipa umeshapishwa?.

Msisahau, rais wetu ni executive president mwenye mamlaka ya mwisho, haamrishwi kufanya lolote wala halazimiki kuukubali ushauri wa yoyote, na maamuzi yake ni ya mwisho, yaani final, kaamua tunalipa, na kweli tunalipa, huku tukilipa, wengine wakijua tunawalipa hao Dowans, huku sisi wengine tukijua ni hakika, wanajilipa!.
 
Mzee MMK sitaacha kusema tena na tena dawa ta Tanzania ni kuiondoa CCM kwa nguvu tu, hiyo ya kukatana mishahara haitasaidia lolote. Wakilipa tu, sote twende barabarani kama walivyofanya wenzetu Tunisia. Wamezi kutuchezea hawa!!!
 
Mzee MMK sitaacha kusema tena na tena dawa ta Tanzania ni kuiondoa CCM kwa nguvu tu, hiyo ya kukatana mishahara haitasaidia lolote. Wakilipa tu, sote twende barabarani kama walivyofanya wenzetu Tunisia. Wamezi kutuchezea hawa!!!

Hili ndio suluhisho tosha na muafaka
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Nimefikiria kuwa kwa vile Dowans watalipwa no matter what kama nilivyosema miaka karibu mitatu iliyopita na kwa vile malipo haya inaonekana yatatokea kabla ya kikao kijacho cha Bunge kwa vile haiwezekani kutokulipa. Nimeona nije na pendekezo jepesi lenye mantiki kuwa Wabunge, Rais na Makamu wake wakatwe mishahara na posho zao kulipia Dowans. Kwa sababu moja kubwa kwamba Rais ndiye anahusika na kuja kwa Dowans na Wabunge kwa sababu walishindwa kuisimamia serikali na kuiuzia kuliingiza taifa kwenye gharama hizi.

Hili litakuwa fundisho kwa sehemu zote hizo mbili kuwa waangalifu. Na wasitafute namna ya kuongeza mishahara na posho kwa wakati huu baada ya kuilipa Dowans. Hesabu zangu za haraka haraka zinaonesha kuwa wabunge na Rais wote wakianza kulipa kila mwaka watalipa dola 30,000 hivi kwa mwaka kwa kila Mbunge. Hii ni chini kidogo ya posho yao ya magari mapya!

Na hii iwe kanuni mpya kuwa wakati wowote serikali inaingizwa mikataba mibovu ni wabunge na Rais ndio watakuwa wanalipia adhabu za kijinga kama hii ya Dowans! Kama hawako tayari (au wazo hili litakuwa baya) basi JK aamue kusitisha ongezeko la mishahara kwa wabunge mawaziri na watendaji wote wakuu wa serikali akiwemo na yeye mwenyewe kwa miaka mitano ijayo!!

MMM(BGM)

Mkuu unamaanisha wabunge wa CCM na baraza la mawaziri! au pamoja na wabunge wa upinzani? :shock:
 
Mzee Mwanakijiji, this will be too little too late, wabunge walioileta Dowans na serikali iliyoileta Dowans, ni wabunge lililopita na serikali, iliyopita, huwezi kuihukumu serikali hii kwa makosa ya serikali iliyopita, hata kama baadhi ya wahusika ni wale wale, serikali ilishavunjwa hawa waliopo ni wapya, wameapisdhwa tena na mambo mapya.
Deni tumelipa
 
Ndugu sijakuelewa sawasawa hapo kwenye RED unamaanisha sisi wananchi wenye kipato duni ndio tunaostahili kubeba mzigo huo? naomba ufafanuzi.
N:b; naunga mkono hoja ya Mzee mwanakijiji kwa asilimia 200%.
Kumbe zamani ulikua na kipato duni
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom