Wabunge, Rais na Makamu wake wakatwe mishahara na Posho kulipa Dowans | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge, Rais na Makamu wake wakatwe mishahara na Posho kulipa Dowans

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 19, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Na. M. M. Mwanakijiji

  Nimefikiria kuwa kwa vile Dowans watalipwa no matter what kama nilivyosema miaka karibu mitatu iliyopita na kwa vile malipo haya inaonekana yatatokea kabla ya kikao kijacho cha Bunge kwa vile haiwezekani kutokulipa. Nimeona nije na pendekezo jepesi lenye mantiki kuwa Wabunge, Rais na Makamu wake wakatwe mishahara na posho zao kulipia Dowans. Kwa sababu moja kubwa kwamba Rais ndiye anahusika na kuja kwa Dowans na Wabunge kwa sababu walishindwa kuisimamia serikali na kuiuzia kuliingiza taifa kwenye gharama hizi.

  Hili litakuwa fundisho kwa sehemu zote hizo mbili kuwa waangalifu. Na wasitafute namna ya kuongeza mishahara na posho kwa wakati huu baada ya kuilipa Dowans. Hesabu zangu za haraka haraka zinaonesha kuwa wabunge na Rais wote wakianza kulipa kila mwaka watalipa dola 30,000 hivi kwa mwaka kwa kila Mbunge. Hii ni chini kidogo ya posho yao ya magari mapya!

  Na hii iwe kanuni mpya kuwa wakati wowote serikali inaingizwa mikataba mibovu ni wabunge na Rais ndio watakuwa wanalipia adhabu za kijinga kama hii ya Dowans! Kama hawako tayari (au wazo hili litakuwa baya) basi JK aamue kusitisha ongezeko la mishahara kwa wabunge mawaziri na watendaji wote wakuu wa serikali akiwemo na yeye mwenyewe kwa miaka mitano ijayo!!

  MMM(BGM)
   
 2. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  hapo utakuwa umewahukumu wabunge wote, na wale wasiohusika hasa wale wa upinzani ambao sauti yao ni ndogo hata pale wanapopinga jambo ikipigwa kura watashindwa na mswada utapita
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,280
  Trophy Points: 280

  Ndugu sijakuelewa sawasawa hapo kwenye RED unamaanisha sisi wananchi wenye kipato duni ndio tunaostahili kubeba mzigo huo? naomba ufafanuzi.
  N:b; naunga mkono hoja ya Mzee mwanakijiji kwa asilimia 200%.
   
 4. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Mzee MM hunadhani kuwakata mishahara hao wakubwa itawapa pinch yoyote! sijui maana nadhani watakuwa kama wamechangia harusi za Dar es Salaam; na huyo Mkuu wa kaya labda ndio hatosikia hata kama kaguswa maana kama ana mgawo wake akatoa kidogo kurudisha sio tabu ni kama kutoa sadaka, sijui; mimi siyo mtaalam wa sheria kwani hiyo hukumu haiwezi kukatiwa rufaha maana sijasikia wakiongelea hili, tuangalie tuone mwisho wa picha itakuwa ajabu sana kama serikali haito chukua hatua zozote juu ya hii, hasa kukata rufaha kama inaruhusiwa, pamoja na hatua kali kwa watu wote waliohusika katika kuleta hiyo company hapa nchni.

  Itakuwa historia mbaya sana juu ya serikali, na nina kwambia mara tu baada ya kulipa utasikia maneno kutoka kwa wafadhili hasa wanaochangia Miradi ya maendeleo na Budget yetu hawato kaakimia kuchangia maendeleo alafu kunafedha zinachukuliwa kufisadi huku wakiona.

  Regards
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Jan 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280

  tunapanua tu maana ya "collective responsibility"
   
 6. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Hili linawezekana wakitaka lakini hawatataka kamwe

  Sarkozy aliahirisha kufanya sherehe ya kitaifa ili kusave dola laki tisa licha ya kuwa hakuwa na sababu ya msingi zaidi ya kubana matumizi

  Serikali ya Japan imetangaza kukata asilimia kumi ya mishahara ya baraza lake lote la mawaziri ili tu kubana matumizi
   
 7. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,994
  Likes Received: 3,743
  Trophy Points: 280
  Nani awakate?
   
 8. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #8
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Kwanza niulize, Hivi PAYE wanakatwa? maana kama hawajazoea kukatwa kodi patakua hapatoshi.
   
 9. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #9
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  mm anasugest wabunge wote wakatwe hata kwa baadae kwa kupitisha mikataba mibovu sasa wale ambao hawatapitisha na mswada ukapita kwa wingi wa kura utakuwa umewahukumu bila sababu!
   
 10. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  anaewalipa maposhoz
   
 11. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #11
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji; nadhani umetoa pendekezo zuri sana kuhusiana na jambo hili. Key players ndio walipe au watumikie kifungo chini ya sheria ya uhujumu uchumi
   
 12. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #12
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  kuna wabunge wengine hawakurudi baada ya uchaguzi na pia kuna wabunge wengine wapya hawakuusika na upangaji wa mikataba hiyo kwa hiyo watalalamika kuwa kwanini wakatwe wakati hawakuwepo katika bunge lililopita
   
 13. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #13
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,994
  Likes Received: 3,743
  Trophy Points: 280
  Anayewalipa maposhoz aliwekwa hapo alipo na nani?
   
 14. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #14
  Jan 19, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,622
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji, this will be too little too late, wabunge walioileta Dowans na serikali iliyoileta Dowans, ni wabunge lililopita na serikali, iliyopita, huwezi kuihukumu serikali hii kwa makosa ya serikali iliyopita, hata kama baadhi ya wahusika ni wale wale, serikali ilishavunjwa hawa waliopo ni wapya, wameapisdhwa tena na mambo mapya.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Jan 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  hapana.. Pasco; hawa waliopo sasa hivi ndio wanaweza kuzuia na kuwawajibisha wahusika wote. Nguvu ya Bunge au kuwajibika kwa Bunge hakuishi pale wabunge wengine wasipochaguliwa. Vinginevyo, mambo yanayofanywa na Bunge yangekuwa yanaisha nguvu pale Bunge moja linapoisha na lingine kuingia. Kwani baraza la mawaziri litakaloamua suala hili ndilo lililokuwepo wakati mkataba unaingiwa?
   
 16. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #16
  Jan 19, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Ingewezekana kukatwa huko kuendane na kuchapwa bakora 2 kila siku hadi deni litakapoisha!
   
 17. Chifunanga

  Chifunanga JF-Expert Member

  #17
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 291
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  MM, hao wakuu wanajilipa mishahara wenyewe, hiyo hoja yako haiwezekani, labda wananchi tugome kulipa kodi.

  kama wao ndio waliosababisha DOWANS ije, basi hawana nguvu ya kujipunguzia mishahara hata kidogo, maana itakuwa inapingana na yaliyopo mioyoni mwao.
   
 18. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #18
  Jan 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,684
  Likes Received: 21,946
  Trophy Points: 280
  Kichuguu,kilichopaswa kufanywa ni hicho tuu. Mengine ni kuzuga tuu.
   
 19. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #19
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,994
  Likes Received: 3,743
  Trophy Points: 280
  Tatizo langu liko kwenye practicality ya hili wazo.
  Nani atakaye-enforce ukatwaji huu?
  Wakatwaji watarajiwa wakikataa??
   
 20. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #20
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  hata wakikatwa wabunge na rais bado mishaara yao na posho zao zinatoka kwa sisi wananchi na kodi zetu, indirect way bado tutalipa sisi
   
Loading...