Wabunge na Waziri wanamnadi Mtulia | Page 5 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge na Waziri wanamnadi Mtulia

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Hivi punde, Feb 11, 2018.

 1. Hivi punde

  Hivi punde JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2018
  Joined: Apr 1, 2017
  Messages: 1,326
  Likes Received: 2,994
  Trophy Points: 280
  Wabunge na mawaziri kutoka CCM wamejitokeza katika mkutano wa hadhara wa kampeni kumnadi mgombea ubunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia.
  Waliohudhuria mkutano huo uliofanyika leo Februari 11,2018 katika mtaa wa Idrisa, Magomeni ni Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson; Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako; na Naibu Waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile.


  Wabunge waliohudhuria ni Hussein Bashe wa Nzega Mjini, Azzan Zungu (Ilala), Livingstone Lusinde 'Kibajaji’ (Mtera), Halima Bulembo (Viti Maalumu) na Oliver Semuguruka (Viti Maalumu).
  Wengine ni Sixtus Mapumba (Mbinga Mjini), Steven Ngonyani 'Profesa Majimarefu' (Korogwe), Joseph Musukuma (Geita Vijijini) na Rita Kabati (Viti Maalumu).


  Kabla ya viongozi hao kupanda jukwaani, burudani ilitolewa na vikundi vya ushereheshaji huku waliohudhuria mkutano huo wakisimama kucheza na kuwatuza waliokuwa wakiburudisha.


  Halima amesema mwanzoni Mtulia alikuwa mbunge wa upinzani na katika baraza la madiwani hakuweza kushauriana na meya lakini sasa yuko CCM hivyo kuwaomba wananchi wamchague.
  Mapunda amesema wananchi wa Kinondoni hawakuwa na tatizo na mchezaji bali timu anayochezea.


  “Mchezaji mzuri akitoa pasi inaharibika na ndiyo maana Mtulia ni mchezaji mzuri na sasa amekuja timu bora ya CCM mleteni tumalize mchezo mapema,” amesema.
  Mbunge Zungu amesema wabunge wa CCM hawana ujanja bali ni ilani ambayo imejenga kuwajali wananchi.


  Dk Ndugulile ambaye pia ni mbunge wa Kigamboni amesema, “Mtulia nitampa ushirikiano katika kutatua matatizo ya afya, wazee na maendeleo ya jamii yatapatiwa ufumbuzi kwa kumchagua Mtulia.”
  Mwisho.
   
 2. Magonjwa Mtambuka

  Magonjwa Mtambuka JF-Expert Member

  #81
  Feb 11, 2018
  Joined: Aug 2, 2016
  Messages: 11,787
  Likes Received: 6,660
  Trophy Points: 280
  Njaa zinawasumbua viongozi wa ufipa, kila kukicha ni kujiuza tu tena kwa bei ya reja reja.
   
 3. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #82
  Feb 12, 2018
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 12,955
  Likes Received: 5,786
  Trophy Points: 280
  Sawa tumekusikia wewe mzungusha makalio
   
 4. o

  olyanu JF-Expert Member

  #83
  Feb 12, 2018
  Joined: May 30, 2017
  Messages: 1,843
  Likes Received: 1,056
  Trophy Points: 280
  Mbona hawampeleki mwenyekiti na katibu mkuu? Tuna hamu ya kuwasikiliza
   
 5. Muyobhyo

  Muyobhyo JF-Expert Member

  #84
  Feb 12, 2018
  Joined: Oct 9, 2014
  Messages: 7,520
  Likes Received: 5,371
  Trophy Points: 280
  mfano akipita mbunge wa upinzani, ina maana Ndugulile hatatoa ushirikiano? kumbe kuwabomolea nyumba zao mnajua mlifanya kosa, inawauma sasa serikali nzima kujaa kino, tunaomba tu mfanye fair na msitumie ubavu na risasi, Kino nyie ndio waamuzi,
   
 6. Muyobhyo

  Muyobhyo JF-Expert Member

  #85
  Feb 12, 2018
  Joined: Oct 9, 2014
  Messages: 7,520
  Likes Received: 5,371
  Trophy Points: 280
  anawaona wana kindondoni ni fafafa kama yeye
   
 7. M

  Mnasihi JF-Expert Member

  #86
  Feb 12, 2018
  Joined: Oct 9, 2013
  Messages: 4,110
  Likes Received: 2,436
  Trophy Points: 280
  Niite utakavyo but siombi pesa wala bando kwa polepole wala bashite! Halafu wewe, hebu jaribu kutafuta wa size yako eeh! Naona unaleta mazoea ya kipumbavu hapa!
   
 8. Tukundane

  Tukundane JF-Expert Member

  #87
  Feb 12, 2018
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 8,588
  Likes Received: 2,934
  Trophy Points: 280
  Kushuhudia kifo cha Mtulia ambaye mazishi yake yatafanyika tarehe 17.
   
 9. Magonjwa Mtambuka

  Magonjwa Mtambuka JF-Expert Member

  #88
  Feb 12, 2018
  Joined: Aug 2, 2016
  Messages: 11,787
  Likes Received: 6,660
  Trophy Points: 280
  Acha kuzungumza mambo ya kipuuzi.
   
 10. Magonjwa Mtambuka

  Magonjwa Mtambuka JF-Expert Member

  #89
  Feb 12, 2018
  Joined: Aug 2, 2016
  Messages: 11,787
  Likes Received: 6,660
  Trophy Points: 280
  Lazima utakua unajua kuzungusha makalio. Sijui yanazungushwaje.
   
 11. Ntolonyonyo

  Ntolonyonyo JF-Expert Member

  #90
  Feb 12, 2018
  Joined: Jul 11, 2015
  Messages: 1,416
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Nguvu kubwa sana....
  CHADEMA na CUF watagawa kura za wananchi....Hiki kitu kilitokea Jimbo la Segerea 2015...
  Ilibidi wasimamishe CUF tu pale...Hivi nyie Upinzani huwa mnaakili kweli??Mbowe atakua agent wa CCM si bure
   
 12. R

  Ralph Tyler JF-Expert Member

  #91
  Feb 12, 2018
  Joined: Jul 31, 2015
  Messages: 1,032
  Likes Received: 896
  Trophy Points: 280
  Mnashangaa mawaziri? Mwaka 1996 Rais Mkapa alimnadi Abdul Cisco Mtiro kwenye uchaguzi mdogo Temeke dhidi ya Augustine Mrema wakati huo akiwa NCCR Mageuzi. Kama mnamkumbuka Sheikh Ali Mtopea aliyekuwa mpiga debe mkuu wa Mrema, huyu Sheikh alikuwa anasikilizwa kuliko Mkapa. Watu wa Temeke wakamtosa Cisco mbele ya Mkapa na vyombo vyake vyote.
   
 13. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #92
  Feb 12, 2018
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 12,955
  Likes Received: 5,786
  Trophy Points: 280
  CHEMA CHAJIUZA KIBAYA CHAJITEMBEZA.
   
 14. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #93
  Feb 12, 2018
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 12,955
  Likes Received: 5,786
  Trophy Points: 280
  FB_IMG_1517511805694.jpg
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...