Wabunge na Waziri wanamnadi Mtulia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge na Waziri wanamnadi Mtulia

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Hivi punde, Feb 11, 2018.

 1. Hivi punde

  Hivi punde JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2018
  Joined: Apr 1, 2017
  Messages: 999
  Likes Received: 2,283
  Trophy Points: 180
  Wabunge na mawaziri kutoka CCM wamejitokeza katika mkutano wa hadhara wa kampeni kumnadi mgombea ubunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia.
  Waliohudhuria mkutano huo uliofanyika leo Februari 11,2018 katika mtaa wa Idrisa, Magomeni ni Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson; Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako; na Naibu Waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile.


  Wabunge waliohudhuria ni Hussein Bashe wa Nzega Mjini, Azzan Zungu (Ilala), Livingstone Lusinde 'Kibajaji’ (Mtera), Halima Bulembo (Viti Maalumu) na Oliver Semuguruka (Viti Maalumu).
  Wengine ni Sixtus Mapumba (Mbinga Mjini), Steven Ngonyani 'Profesa Majimarefu' (Korogwe), Joseph Musukuma (Geita Vijijini) na Rita Kabati (Viti Maalumu).


  Kabla ya viongozi hao kupanda jukwaani, burudani ilitolewa na vikundi vya ushereheshaji huku waliohudhuria mkutano huo wakisimama kucheza na kuwatuza waliokuwa wakiburudisha.


  Halima amesema mwanzoni Mtulia alikuwa mbunge wa upinzani na katika baraza la madiwani hakuweza kushauriana na meya lakini sasa yuko CCM hivyo kuwaomba wananchi wamchague.
  Mapunda amesema wananchi wa Kinondoni hawakuwa na tatizo na mchezaji bali timu anayochezea.


  “Mchezaji mzuri akitoa pasi inaharibika na ndiyo maana Mtulia ni mchezaji mzuri na sasa amekuja timu bora ya CCM mleteni tumalize mchezo mapema,” amesema.
  Mbunge Zungu amesema wabunge wa CCM hawana ujanja bali ni ilani ambayo imejenga kuwajali wananchi.


  Dk Ndugulile ambaye pia ni mbunge wa Kigamboni amesema, “Mtulia nitampa ushirikiano katika kutatua matatizo ya afya, wazee na maendeleo ya jamii yatapatiwa ufumbuzi kwa kumchagua Mtulia.”
  Mwisho.
   
 2. Kulupura

  Kulupura JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2018
  Joined: Apr 13, 2017
  Messages: 1,520
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  Wana poteza muda tyuuu
   
 3. Tukundane

  Tukundane JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2018
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 8,358
  Likes Received: 2,730
  Trophy Points: 280
  Chombo kinakwenda mrama nini ndo maana Lumumba watakuwa wamejazana kujaribu kukiokoa.
   
 4. Erythrocyte

  Erythrocyte JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2018
  Joined: Nov 6, 2012
  Messages: 45,503
  Likes Received: 27,042
  Trophy Points: 280
  CCM Maji ya shingo Kinondoni , Tegemeo kubwa ni Kailima .
   
 5. Maboso

  Maboso JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2018
  Joined: Feb 18, 2013
  Messages: 4,208
  Likes Received: 2,434
  Trophy Points: 280
  Matokeo yakitoka hamchelewi kusema mmeibiwa kura nyie wazee wa kupinga marudio ya chaguzi kuokoa pesa huku ninyi wenyewe mkishiriki chaguzi hizo hizo zinazotumia pesa nyingi.
   
 6. Waterloo

  Waterloo JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2018
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 12,292
  Likes Received: 12,356
  Trophy Points: 280
  hali tete
   
 7. e

  eddy JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2018
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 9,725
  Likes Received: 4,023
  Trophy Points: 280
  Musukuma na kibajaj wamesemaje leo? Nawakubali sana
   
 8. K

  Kasongo JF-Expert Member

  #8
  Feb 11, 2018
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 1,946
  Likes Received: 1,332
  Trophy Points: 280
  Asante kwa taarifa.Kampeni za Chadema zimesimama?Siwasikii siku hizi
   
 9. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #9
  Feb 11, 2018
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,390
  Likes Received: 419
  Trophy Points: 180
  Doh! Haijawahi kutokea nguvu kubwa namna hiyo. Ukiona hivyo ujue huko chini mambo si mazuri, ama Chadema wamekaba mpaka penalty
   
 10. Magonjwa Mtambuka

  Magonjwa Mtambuka JF-Expert Member

  #10
  Feb 11, 2018
  Joined: Aug 2, 2016
  Messages: 10,118
  Likes Received: 5,273
  Trophy Points: 280
  Safi sana. Mtulia tosha.
   
 11. mafinyofinyo

  mafinyofinyo JF-Expert Member

  #11
  Feb 11, 2018
  Joined: Nov 29, 2012
  Messages: 3,460
  Likes Received: 1,721
  Trophy Points: 280
  Ccm ni laana kwa Wa Tz. Wanajitamba eti wana Timu nzuri wakati kwa zaidi ya miaka 50 wameshindwa kuboresha maisha ya wananchi na ndio kwanza umasikini, ujinga, maradhi vinazidi kuongezeka
   
 12. Granted Peter

  Granted Peter JF-Expert Member

  #12
  Feb 11, 2018
  Joined: Aug 17, 2015
  Messages: 1,134
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  Nimeona kuna mama mmoja amewapigia magoti wananchi
   
 13. Baba Mtakatifu

  Baba Mtakatifu JF-Expert Member

  #13
  Feb 11, 2018
  Joined: Dec 31, 2017
  Messages: 284
  Likes Received: 374
  Trophy Points: 80
  Hatumchagui ili mje mmalizie kabisa na vibanda vyetu tulivyojenga kujisitiri baada ya kutubomolea nyumba zetu
   
 14. Twamo

  Twamo JF-Expert Member

  #14
  Feb 11, 2018
  Joined: May 27, 2017
  Messages: 398
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 180
  Ha ha ha! Hawa kwisha habari yao! Waandae tu mikakati ya kuiba kura lakini kwa Mtulia hadanganywi mtu!
   
 15. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #15
  Feb 11, 2018
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 12,148
  Likes Received: 5,130
  Trophy Points: 280
  Na bunduki na mabomu.
   
 16. Pharm D

  Pharm D JF-Expert Member

  #16
  Feb 11, 2018
  Joined: Feb 17, 2017
  Messages: 823
  Likes Received: 1,262
  Trophy Points: 180
  Na hapo bado mpaka tunataka mpaka mwenyekit wao atoke ikulu apande jukwaan kumnadi huyo mburula wao
   
 17. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #17
  Feb 11, 2018
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 12,148
  Likes Received: 5,130
  Trophy Points: 280
  FB_IMG_1517511805694.jpg
   
 18. Magonjwa Mtambuka

  Magonjwa Mtambuka JF-Expert Member

  #18
  Feb 11, 2018
  Joined: Aug 2, 2016
  Messages: 10,118
  Likes Received: 5,273
  Trophy Points: 280
 19. T

  TIBIM JF-Expert Member

  #19
  Feb 11, 2018
  Joined: Dec 1, 2017
  Messages: 820
  Likes Received: 604
  Trophy Points: 180
  Ikipigwa kihalali hawatoboi
   
 20. Magonjwa Mtambuka

  Magonjwa Mtambuka JF-Expert Member

  #20
  Feb 11, 2018
  Joined: Aug 2, 2016
  Messages: 10,118
  Likes Received: 5,273
  Trophy Points: 280
  Muiteni da'Mange aje kumnadi Mwalimu.
   
Loading...