Wabunge na Waziri wanamnadi Mtulia | Page 4 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge na Waziri wanamnadi Mtulia

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Hivi punde, Feb 11, 2018.

 1. Hivi punde

  Hivi punde JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2018
  Joined: Apr 1, 2017
  Messages: 1,350
  Likes Received: 3,026
  Trophy Points: 280
  Wabunge na mawaziri kutoka CCM wamejitokeza katika mkutano wa hadhara wa kampeni kumnadi mgombea ubunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia.
  Waliohudhuria mkutano huo uliofanyika leo Februari 11,2018 katika mtaa wa Idrisa, Magomeni ni Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson; Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako; na Naibu Waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile.


  Wabunge waliohudhuria ni Hussein Bashe wa Nzega Mjini, Azzan Zungu (Ilala), Livingstone Lusinde 'Kibajaji’ (Mtera), Halima Bulembo (Viti Maalumu) na Oliver Semuguruka (Viti Maalumu).
  Wengine ni Sixtus Mapumba (Mbinga Mjini), Steven Ngonyani 'Profesa Majimarefu' (Korogwe), Joseph Musukuma (Geita Vijijini) na Rita Kabati (Viti Maalumu).


  Kabla ya viongozi hao kupanda jukwaani, burudani ilitolewa na vikundi vya ushereheshaji huku waliohudhuria mkutano huo wakisimama kucheza na kuwatuza waliokuwa wakiburudisha.


  Halima amesema mwanzoni Mtulia alikuwa mbunge wa upinzani na katika baraza la madiwani hakuweza kushauriana na meya lakini sasa yuko CCM hivyo kuwaomba wananchi wamchague.
  Mapunda amesema wananchi wa Kinondoni hawakuwa na tatizo na mchezaji bali timu anayochezea.


  “Mchezaji mzuri akitoa pasi inaharibika na ndiyo maana Mtulia ni mchezaji mzuri na sasa amekuja timu bora ya CCM mleteni tumalize mchezo mapema,” amesema.
  Mbunge Zungu amesema wabunge wa CCM hawana ujanja bali ni ilani ambayo imejenga kuwajali wananchi.


  Dk Ndugulile ambaye pia ni mbunge wa Kigamboni amesema, “Mtulia nitampa ushirikiano katika kutatua matatizo ya afya, wazee na maendeleo ya jamii yatapatiwa ufumbuzi kwa kumchagua Mtulia.”
  Mwisho.
   
 2. kanali mstaafu

  kanali mstaafu JF-Expert Member

  #61
  Feb 11, 2018
  Joined: May 17, 2015
  Messages: 2,196
  Likes Received: 1,807
  Trophy Points: 280
  Ma Zero brain
   
 3. K

  Kasongo JF-Expert Member

  #62
  Feb 11, 2018
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 2,080
  Likes Received: 1,443
  Trophy Points: 280
  Kwa mazingira yalivyo,hilo jimbo CCM wanaweza kulibeba.Mm si mpenzi sana wa siasa.Tunaomba amani
   
 4. M

  Mnasihi JF-Expert Member

  #63
  Feb 11, 2018
  Joined: Oct 9, 2013
  Messages: 4,120
  Likes Received: 2,456
  Trophy Points: 280
  Mange anawapiga huko aliko na hakuna wa kuweza kujibu hata hoja yake moja! Mwalimu anakubalika bila nguvu kubwa na kama huamini tucheze kamari mimi na wewe yaani uweke jiwe miye naweka m1 tshs kama Salim hajamlamba mtulia tena kwa tofauti kubwa ya kura! Hata mkiiba bado ccm haitoboi kinondoni na siha!
   
 5. Magonjwa Mtambuka

  Magonjwa Mtambuka JF-Expert Member

  #64
  Feb 11, 2018
  Joined: Aug 2, 2016
  Messages: 11,789
  Likes Received: 6,665
  Trophy Points: 280
  Kwenda zako huko wewe lofa. Hiyo m1 uitoe wapi; ufipa?
   
 6. Mafwi Munda

  Mafwi Munda JF-Expert Member

  #65
  Feb 11, 2018
  Joined: Nov 30, 2017
  Messages: 1,766
  Likes Received: 1,507
  Trophy Points: 280
  Hahaha yani ccm polisi wasiposhiriki wanatia huruma sana, nasikia mawaziri wameambiwa mtulia asiposhinda wanavunja baraza la mawaziri, sasa huko tandale wana haha hawaeleweki.
  Yani eti wanajidai hawaelewi kwanini wananchi haeaipendi ccm,
   
 7. josephat manyenye

  josephat manyenye JF-Expert Member

  #66
  Feb 11, 2018
  Joined: Dec 3, 2017
  Messages: 544
  Likes Received: 675
  Trophy Points: 180
  Hawa watu wanafiki sana hata shetani anawashangaa
   
 8. K

  Kasongo JF-Expert Member

  #67
  Feb 11, 2018
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 2,080
  Likes Received: 1,443
  Trophy Points: 280
  Anapumulia mashine kivipi?Waandika vitabu wanasema atashinda kwa kishindo.Ila nakubaliana na wewe-Very awkard gambling by Mhe.Mtulia
   
 9. share

  share JF-Expert Member

  #68
  Feb 11, 2018
  Joined: Nov 22, 2008
  Messages: 2,816
  Likes Received: 3,299
  Trophy Points: 280

  Kama mgonjwa ni HIV positive, hakuna dawa. Hebrew University ya Israel ndiyo taasisi pekee duniani iliyoghundua dawa ya HIV japo haijapata uthibiti wa shirika la afya duniani (WHO). CCM kwa uchaguzi wa Kinondoni ni mgonjwa wa HIV. Hana dawa. Huyu mtulia (herufi ndogo maana ni mgonjwa kisiasa) ameliingiza Taifa bilioni moja kurudia huu uchaguzi. Dawa yake haina uthibiti wa WHO. Mwache afe kifo cha mende kwa kulisababibshia hasara Taifa la Tshs. 1 bn. Hatutaki wahuni wasio na uchungu na nchi. Bilioni moja zingefanya mambo mangapi ya maendeleo? Huyu mtulia ni shithole individual.
   
 10. bs group

  bs group JF-Expert Member

  #69
  Feb 11, 2018
  Joined: Apr 28, 2017
  Messages: 835
  Likes Received: 497
  Trophy Points: 80
  ata mje wote...lenu alipo kinondon wala siha..
   
 11. M

  Mnasihi JF-Expert Member

  #70
  Feb 11, 2018
  Joined: Oct 9, 2013
  Messages: 4,120
  Likes Received: 2,456
  Trophy Points: 280
  Wafikiri wote ni wategemezi wa lumumba kama wewe? Kama unaitaka tuma namba yako ya tigo pesa or whatever nikurushie zaidi ya hiyo ukamalize matatizo yako ila akishinda wa cdm unairejesha kwa riba!
   
 12. Magonjwa Mtambuka

  Magonjwa Mtambuka JF-Expert Member

  #71
  Feb 11, 2018
  Joined: Aug 2, 2016
  Messages: 11,789
  Likes Received: 6,665
  Trophy Points: 280
  Huna lolote wewe mzungusha mikono. Nenda kampe hiyo m1 Mashinji imsaidie kwenye kumnadi Salum Mwalimu hapa Kinondoni.
   
 13. M

  Mnasihi JF-Expert Member

  #72
  Feb 11, 2018
  Joined: Oct 9, 2013
  Messages: 4,120
  Likes Received: 2,456
  Trophy Points: 280
  Wewe umempa ngapi mtulia, kibajaji na ile crew ya leo magomeni? Huku cdm tulishazoea kuchanga tena bila kuombwa, lumumba mna utamaduni huo zaidi ya kukwapua hazina?
   
 14. Magonjwa Mtambuka

  Magonjwa Mtambuka JF-Expert Member

  #73
  Feb 11, 2018
  Joined: Aug 2, 2016
  Messages: 11,789
  Likes Received: 6,665
  Trophy Points: 280
  Nimekutambia kuwa nina m1?
   
 15. M

  Mnasihi JF-Expert Member

  #74
  Feb 11, 2018
  Joined: Oct 9, 2013
  Messages: 4,120
  Likes Received: 2,456
  Trophy Points: 280
  Hizi sio tambo bali ni uhalisia! Hatufanani mjomba. Wakati wewe unahangaika na magu wako kukubania vijiposho na vijinyongeza vya mishahara mikia ya mbuzi mie nilishajikomboa kabla ya ujio wake na mbinu za kumake ninazo hivyo siusubiri mwisho wa mwezi aslan! Kama vipi karibu nikufunde acha kupoteza muda huko lumumba st! Njoo tuuze mitumba.
   
 16. Magonjwa Mtambuka

  Magonjwa Mtambuka JF-Expert Member

  #75
  Feb 11, 2018
  Joined: Aug 2, 2016
  Messages: 11,789
  Likes Received: 6,665
  Trophy Points: 280
  Lofa tu wewe, mwenye mali hapigi kelele.
   
 17. M

  Mnasihi JF-Expert Member

  #76
  Feb 11, 2018
  Joined: Oct 9, 2013
  Messages: 4,120
  Likes Received: 2,456
  Trophy Points: 280
  Sikatai kuitwa lofa na sio mara ya kwanza kuitwa hivyo kwani hata babako mkapa aliniita hivyo pale jangwani! Na sina mali za wizi wala ufisadi bali nina pesa ninayoiringia! Na uzuri wa pesa inakutangaza na mwenyenayo anaitangaza vilevile! Sijifichi kwani tra wananitambua. Nakutangazia tena, wewe nakumudu kwa pesa niliyokuwa nayo na naweza kukununua uhamie cdm! Inabisha wewe njaa kali kama sigara kali? Haya tangaza dau kesho nikakunadi kwenye mkutano wa kampeni na kukuvalisha T-shirt ya cdm!
   
 18. owomkyalo

  owomkyalo JF-Expert Member

  #77
  Feb 11, 2018
  Joined: Dec 26, 2017
  Messages: 1,689
  Likes Received: 2,766
  Trophy Points: 280
  Ataiba kura ...labda ...ila ata akitoboa itakuwa nifunzo kubwa maana sahv yuko ICU...alidhan wananchi watampa feva apite kama anasukuma mlevi.
   
 19. Erythrocyte

  Erythrocyte JF-Expert Member

  #78
  Feb 11, 2018
  Joined: Nov 6, 2012
  Messages: 47,549
  Likes Received: 30,176
  Trophy Points: 280
 20. owomkyalo

  owomkyalo JF-Expert Member

  #79
  Feb 11, 2018
  Joined: Dec 26, 2017
  Messages: 1,689
  Likes Received: 2,766
  Trophy Points: 280
  Njaa inakusumbua elfu 7 mnazolipwa na Lumumba ...zinakutesa
   
 21. Magonjwa Mtambuka

  Magonjwa Mtambuka JF-Expert Member

  #80
  Feb 11, 2018
  Joined: Aug 2, 2016
  Messages: 11,789
  Likes Received: 6,665
  Trophy Points: 280
  Vizuri sana kukubali kuitwa lofa, tena kilaza mkubwa unayejidai una hela kumbe fukara tu, kazi kupewa bando na Mashinji ili uje kuzungusha mikono huku.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...