Wabunge na Waziri wanamnadi Mtulia

Wabunge na Waziri wanamnadi Mtulia

Wabunge na mawaziri kutoka CCM wamejitokeza katika mkutano wa hadhara wa kampeni kumnadi mgombea ubunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia.
Waliohudhuria mkutano huo uliofanyika leo Februari 11,2018 katika mtaa wa Idrisa, Magomeni ni Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson; Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako; na Naibu Waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile.


Wabunge waliohudhuria ni Hussein Bashe wa Nzega Mjini, Azzan Zungu (Ilala), Livingstone Lusinde 'Kibajaji’ (Mtera), Halima Bulembo (Viti Maalumu) na Oliver Semuguruka (Viti Maalumu).
Wengine ni Sixtus Mapumba (Mbinga Mjini), Steven Ngonyani 'Profesa Majimarefu' (Korogwe), Joseph Musukuma (Geita Vijijini) na Rita Kabati (Viti Maalumu).


Kabla ya viongozi hao kupanda jukwaani, burudani ilitolewa na vikundi vya ushereheshaji huku waliohudhuria mkutano huo wakisimama kucheza na kuwatuza waliokuwa wakiburudisha.


Halima amesema mwanzoni Mtulia alikuwa mbunge wa upinzani na katika baraza la madiwani hakuweza kushauriana na meya lakini sasa yuko CCM hivyo kuwaomba wananchi wamchague.
Mapunda amesema wananchi wa Kinondoni hawakuwa na tatizo na mchezaji bali timu anayochezea.


“Mchezaji mzuri akitoa pasi inaharibika na ndiyo maana Mtulia ni mchezaji mzuri na sasa amekuja timu bora ya CCM mleteni tumalize mchezo mapema,” amesema.
Mbunge Zungu amesema wabunge wa CCM hawana ujanja bali ni ilani ambayo imejenga kuwajali wananchi.


Dk Ndugulile ambaye pia ni mbunge wa Kigamboni amesema, “Mtulia nitampa ushirikiano katika kutatua matatizo ya afya, wazee na maendeleo ya jamii yatapatiwa ufumbuzi kwa kumchagua Mtulia.”
Mwisho.
Hiki ni "KIWEWE" Bado joto ya "JIWE" inakuja!?
 
Huku akija Mr II tu basi kinondoni itazizima. Acha wao wakusanyane huko CCM..
Ngwe hii CCM chali...
Tupo kinondoni kampeni vijana nyumba kwa nyumba ni moto.
 
Muiteni da'Mange aje kumnadi Mwalimu.

Hatuna shida naye. Kwetu wanasema; Fimbo ya mbali haimuui nyoka. Sumaye atosha kumaliza kazi. Vunjeni bank; atoke pale magogoni, bado hampati kitu. Umemwona nani CDM akipiga magoti kuomba kura??
Chema chajiuza chenyewe
 
Chadema Nao wakutane hivyo hivyo ,si wanawabunge na serikali kivuli?[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ccm ni laana kwa Wa Tz. Wanajitamba eti wana Timu nzuri wakati kwa zaidi ya miaka 50 wameshindwa kuboresha maisha ya wananchi na ndio kwanza umasikini, ujinga, maradhi vinazidi kuongezeka
Kwa sababu hakuna mwingine wa kutawala.
 
Na hapo bado mpaka tunataka mpaka mwenyekit wao atoke ikulu apande jukwaan kumnadi huyo mburula wao
Aje asije mtulia anaingia bungeni kwa sababu tayari mtangzaji wa matokeo ni wa kwao.
 
Hatuna shida naye. Kwetu wanasema; Fimbo ya mbali haimuui nyoka. Sumaye atosha kumaliza kazi. Vunjeni bank; atoke pale magogoni, bado hampati kitu. Umemwona nani CDM akipiga magoti kuomba kura??
Chema chajiuza chenyewe
Umesahau silaha ya mwisho mkurugenzi?
 
Hatuna shida naye. Kwetu wanasema; Fimbo ya mbali haimuui nyoka. Sumaye atosha kumaliza kazi. Vunjeni bank; atoke pale magogoni, bado hampati kitu. Umemwona nani CDM akipiga magoti kuomba kura??
Chema chajiuza chenyewe
Ok, hamna tabu.
 
Aje asije mtulia anaingia bungeni kwa sababu tayari mtangzaji wa matokeo ni wa kwao.
Tutakua tunaelekea walipofika wenzetu waDRC na sudan kusin na nina uhakika tutafika either sooner or later
 
Back
Top Bottom