Wabunge na Waziri wanamnadi Mtulia

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,551
Wabunge na mawaziri kutoka CCM wamejitokeza katika mkutano wa hadhara wa kampeni kumnadi mgombea ubunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia.
Waliohudhuria mkutano huo uliofanyika leo Februari 11,2018 katika mtaa wa Idrisa, Magomeni ni Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson; Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako; na Naibu Waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile.

Wabunge waliohudhuria ni Hussein Bashe wa Nzega Mjini, Azzan Zungu (Ilala), Livingstone Lusinde 'Kibajaji’ (Mtera), Halima Bulembo (Viti Maalumu) na Oliver Semuguruka (Viti Maalumu).
Wengine ni Sixtus Mapumba (Mbinga Mjini), Steven Ngonyani 'Profesa Majimarefu' (Korogwe), Joseph Musukuma (Geita Vijijini) na Rita Kabati (Viti Maalumu).

Kabla ya viongozi hao kupanda jukwaani, burudani ilitolewa na vikundi vya ushereheshaji huku waliohudhuria mkutano huo wakisimama kucheza na kuwatuza waliokuwa wakiburudisha.

Halima amesema mwanzoni Mtulia alikuwa mbunge wa upinzani na katika baraza la madiwani hakuweza kushauriana na meya lakini sasa yuko CCM hivyo kuwaomba wananchi wamchague.
Mapunda amesema wananchi wa Kinondoni hawakuwa na tatizo na mchezaji bali timu anayochezea.

“Mchezaji mzuri akitoa pasi inaharibika na ndiyo maana Mtulia ni mchezaji mzuri na sasa amekuja timu bora ya CCM mleteni tumalize mchezo mapema,” amesema.
Mbunge Zungu amesema wabunge wa CCM hawana ujanja bali ni ilani ambayo imejenga kuwajali wananchi.

Dk Ndugulile ambaye pia ni mbunge wa Kigamboni amesema, “Mtulia nitampa ushirikiano katika kutatua matatizo ya afya, wazee na maendeleo ya jamii yatapatiwa ufumbuzi kwa kumchagua Mtulia.”
Mwisho.
 
Safi sana. Mtulia tosha.
 
Safi sana. Mtulia tosha.
FB_IMG_1517511805694.jpg
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom