Nakubaliana na wewe.
Lakini njia moja na pekee kabisa kuonyesha kuwa wapiga kura ni waelewa ni kufanya mabadiliko katika masanduku ya kura jambo ambalo litaweza hata kuwastua wanasiasa kwamba hawakuchaguliwa wao katika majimbo yao bali vyama vingine.
Kwa mfano jimbo la Kawe wakisema hatumtaki tena Mbunge fulani kwa sababu hakufanya hivi na hivi, ni lazima wapiga kura wafanye hivyo kwenye sanduku la kura.
Mwaka wa 2025 watakiwa kuwa ni mwaka wa mabadiliko katika kupiga kura ambayo hayakuwahi kutokea tangu nchi ipate uhuru.