Wabunge Lema Msigwa na Nassari wawasilisha ushahidi wa rushwa Ofisi za Mkurugenzi wa TAKUKURU

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,224
Wabunge Godbless Lema na Joshua Nassari na Peter Msigwa Wawasilisha ushahidi wa Rushwa Ofisi za Mkurugenzi wa TAKUKURU saa saba mchana leo.




Update
Wabunge wa Chadema, Joshua Nassari (Arumeru Mashariki), Godbless Lema ( Arusha Mjini) na Mchungaji Peter Msigwa(Iringa Mjini) wamewasilisha Takukuru ushahidi wanaodai unaonyesha wa jinsi madiwani wao walivyonunuliwa kwa kupewa rushwa.

Wabunge wao, wamewasilisha ushahidi huo mchana wa leo Jumatatu kwenye ofisi za Makao Makuu ya Takukuru zilizopo Upanga Dar es Salaam.

Wabunge hao wamewasili katika ofisi hizo saa 8.39 mchana na kukutana na waandishi wa habari waliokuwa wakiwasubiri.

Katika kile ambacho waandishi hawakukifikiria, wabunge hao waliwasili kwa miguu na kuelekea moja kwa moja ndani ambapo waandishi walizuiwa kuingia.

Ushahidi huo, wameuwasilisha ikiwa imepita siku moja tangu Lema na Nassari walipofanya mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha kueleza jinsi madiwani wao walivyoshawishiwa na kwa rushwa kuihama Chadema.


Chanzo: Mwananchi
 
Wabunge Godbless Lema na Joshua Nassari Watawasilisha ushahidi wa Rushwa Ofisi za Mkurugenzi wa TAKUKURU saa saba mchana leo.

More to follow.
Hata wasipowasilisha....Wananchi tumeshajua..hilo ndio lilikuwa la muhimu...(Mahakama ya Raia)....Tunajua nini cha kufanya...

Zile rushwa zimetolewa kwa maelekezk kutoka ngazi za juu...Majaji ni wateule wa Rais, Mkurugenzi takukuru ni mteule wa Rais, IGP ni mteule....Unategemea hao wote wammkaange Rais aliyewachagua....????


Sisi wananchi tumejua..inatosha...tutajua cha kufanya
 
Back
Top Bottom