Salaam kutoka Dodoma,
Spika Anne Makinda ameonesha kupwaa sana na kutomudu nafasi yake tangu apate cheo hicho.
Wabunge wengi, wa CCM na wa upinzani, wanalalamika kuwa Spika huyo ameshindwa kuliendesha Bunge kwa ufanisi.
Baadhi ya tabia zinazowakera wabunge ni Spika huyo kuwa "mnoko" mno na kukosa uungwana kwenye matamshi yake na amekuwa akiwasema wabunge kama watoto wadogo.
Hata maofisa wa Bunge wanasema kuwa Makinda hafai kabisa kuongoza Bunge na ni mtu ambaye hashauriki kwenye uongozi wake.
Makinda anaelekea kukosa support ya wabunge wengi na huenda wakapiga kura ya kutokuwa na imani naye.
Wabunge wanamlaumu Makinda kwa kuwadhalilisha hadharani kwa kuwakemea kama watoto, kuwanyima uhuru wa kujadili masuala nyeti na kuipendelea/kuilinda sana serikali kwenye maamuzi yake yote hivyo kuling'oa meno Bunge na kulifanya lirudi kuwa "rubber stamp" ya maamuzi ya serikali.
Hili suala linaweza kupelekwa kwenye caucus ya CCM ili ikubaliwe kuwa Makinda ang'oke na nafasi yake ichukuliwe na mbunge mwingine wa CCM, kwa mujibu wa minong'ono ya wabunge wa chama tawala. Inaonekana kuwa wabunge wengi wanakosa uvumilivu wa kungoja mpaka mwaka 2015 ili amalize muda wake. Ni hakika kuwa kama Makinda akifika mwaka 2015, basi hana nafasi tena ya kurudi kama spika kutokana na kuvurunda sana kwenye nafasi hiyo.
"Makinda anawatreat Wabunge kama watoto wadogo. Ni kama mama wa nyumbani anayewaburuza watoto na kuwafokea kila mara wakae kimya, wasitoke nje, waongee kwa ufupi, wasihoji mambo, n.k," alisikika akisema Mbunge mmoja wa CCM.
"Wabunge wengi wa CCM wamefurahia uamuzi wa Tundu Lissu wa CHADEMA kumshitaki Makinda kwenye kamati ya uongozi wa Bunge kwa maamuzi yake ya kupendelea. Kwa kweli tunamkumbuka sana Samuel Sitta kwa viwango alivyoweka alipokuwa Spika."