Wabunge kumng'oa Spika Anne Makinda?

Wabunge kumng'oa Spika Anne Makinda?

Makinda hawezi kutolewa kama Spika licha ya malalamiko ya Wabunge kwa sababu anaungwa mkono na Rais Jakaya Kikwete kwa vile yuko loyal 100% kwa serikali na kukubali Bunge (legislature) liwe linapokea maagizo kutoka kwa serikali (executive) badala ya Bunge na serikali vyote kuwa na nguvu sawa kama pillars of the state.

Pia, Makinda amewekwa kwenye nafasi yake na Rostam Aziz na Edward Lowassa, hivyo watatumia pesa na mtandao wao kumlinda asitoke kwenye cheo chake. Kwa maagizo ya Rostam, Makinda aliwateuwa Lowassa, Januari Makamba na Peter Serukamba kwenye kamati nyeti za Bunge na wakatwaa uenyekiti wa kamati hizo. Hivyo basi, Lowassa, Serukamba na Januari wako kwenye kamati ya uongozi wa Bunge na watafanya kila juu kutupilia mbali hoja yoyote ya kumng'oa Makinda.
 
Back
Top Bottom