Bunge la 13, Mkutano wa Pili unaendelea Jijini Dodoma ambapo waheshimiwa wabunge wanaijadili hotuba ya Rais Samia aliyoitoa Novemba, 2025 wakati akifungua bunge hilo tukufu la 13 tangu Uhuru.
Kila mbunge aliyepata nafasi ya kuongea kuhusu hotuba hiyo, aliangalia kile ambacho anaweza kukichakata na kukiwakilisha kwa wananchi kupitia hotuba yake bungeni.
Ilikuwa Jumanne ya Januari 27, 2026 ambapo Kikao cha Pili cha Bunge kilianza baada ya kikao cha kwanza ambacho rais alihutubia mwaka jana na kukiahirisha.
Jumatano, yaani kesho yake Januari 28, kilikuwa Kikao cha Tatu. Ndipo Mbunge wa Gairo kupitia CCM, Ahmed Shabiby alipopewa nafasi ya kuchangia hotuba ya rais ya Novemba mwaka jana, yeye aligusia ufisadi.
Pamoja na kumshukuru Mungu, kumshukuru Rais na kumshukuru Spika, alisema: "Katika nchi hii sasa hivi mafisadi siyo wanapiga kidogo, wanapiga kiuhakika. Ni walaji na ni walafi na wanafanya vitu kama vile wananchi wa sasa hivi hawana elimu.
"Lazima tufahamu sasa hivi ukienda sehemu yoyote hata kama ni kwenye kijiwe cha bodaboda utamkuta mtu wa chuo kikuu, utamkuta wa 'form six', utamkuta 'form four.
"Utamkuta wa darasa la saba na asiesoma wakikaa pamoja pale wakianza kuongea wote wanakuwa wapo chuo kikuu.
"Kwa hiyo hawa watu siyo kwamba hawaelewi mambo.
"Utakuta mtu yupo serikalini ana GPA ya 2.5 na mwendesha bodaboda ana GPA ya 4.
"Sheria za Takukuru kama zimelegea walete (bungeni) tuzibadilishe. Watu kila sehemu wanajenga majumba, watu wanaona. Tunapozungumza mambo ya leo tujue kuna 2030 inakuja tutakwenda kwenye chaguzi zetu.
Aliongeza kuwa, yeye ni mfanyabiashara, amepambana kwa miaka mingi kufika alipo. Lakini wapo mafisadi ambao ghafla tu wanamiliki majengo makubwa na watu wanajua jengo ni la nani.
"Tena wengine wanaandika na majina yao juu, fulani Tower. Na akienda pale anawaagizia mishikaki watu," alisema Shabiby huku akipongezwa na baadhi ya wabunge.
Akasema yeye ni 'usalama wa taifa wa kujitegemea' kwa hiyo anajua mengi kuhusu mafisadi hao, kauli iliyozua kicheko kutoka kwa wabunge wenzake.
Kwenye mitandao ya kijamii, picha mjengeo ya Shabiby na sauti yake vilitrendi akiwapasua mafisadi hao huku wachangia maoni wakimuunga mkono hasa katika kipengele cha 'mafisadi wanapiga (pesa) kiuhakika'.
Kesho yake, ilikuwa Alhamisi, Januari 29, Kikao cha Nne, Mbunge wa Mwibara kupitia CCM, Kangi Lugola, naye alipewa nafasi ya kuchangia hotuba ya rais, alipita mlemle alimopita mheshimiwa Shabiby akiwasogelea zaidi watu wanaoitwa 'machawa'.
Lugola alisema kuwa, kuwepo kwa 'machawa' serikalini ndiyo kiini cha kuwepo kwa ufisadi, ubadhirifu na wizi wa pesa za umma.
Akaongeza kuwa, katika mazingira kama hayo ni muhimu kuwamaliza 'machawa' kwa nguvu zote ili kusiwepo wapigaji wa pesa hizo.
Alikwenda mbele zaidi akisema kuwa, ifike wakati ili kupambana na 'machawa' kwa uhakika, baadhi ya vyombo vya ulinzi viwe huru kabisa katika kutekeleza majukumu yake.
Kangi Lugola alivitaja vyombo hivyo kuwa ni Polisi na DPP (Mkurugenzi wa Mashitaka) akimaanisha ili viweze kupambana na 'machawa' kwa uhakika.
Baadhi ya wananchi mitaani wamezichukulia hotuba za wabunge hao na nyingine zenye mwelekeo huo kuwa ni msaada kwa Rais Samia Suluhu Hassan katika kujenga Tanzania mpya.
Walisema kuwa, kuwepo kwa Wabunge wa CCM wanaokemea ufisadi serikalini unaofanywa na baadhi ya watumishi wasiyowaaminifu, ndiyo sauti ambazo wananchi wanataka kuzisikia kwa sasa.
"Wale wabunge siyo kwamba ni wapinzani bali ni wa kweli. Hata Rais Samia mwenyewe alipolifungua Bunge, Novemba mwaka jana, aliwazungumzia watu hao wanaopiga pesa za umma au za serikali kwa manufaa yao binafsi.
"Ndiyo maana wabunge wote bungeni wameshika vitabu vya hotuba ya rais ambapo katika ukurasa wa 37 kama sikosei, ndipo maneno ya Rais kuhusu ubadhirifu yanapatikana," alisema Allan Shimwe, mkazi wa Buza-Kanisani wilayani Temeke, Dar es Salaam.
Naye Willson Sakafu mkazi wa Kawe, yeye alisema kwa sasa Watanzania wanataka kusikia hotuba kama hizo kwa sababu wanajua wazi kwamba kuna mafisadi serikalini.
"Sisi Watanzania siyo kwamba ni wajinga. Tunajua kuna mafisadi. Hata Rais wetu Samia siyo mjinga. Anajua kuna mafisadi. Anajua kuna viongozi wazembe. Ndiyo maana hachoki kuwabadili viongozi kila kukicha kwa sababu anawaona hawamsaidii wakati ukweli ni kwamba miongoni mwa majukumu yao ni wao kumsaidia Rais," alisema Sakafu.
Wengi wa wananchi walisema kuwa, kwa mitazamo yao, mawaziri legelege kazini watimuliwe. Walisema utendaji wowote mbovu au upigaji wowote wa pesa lazima kuna waziri katika wizara husika ni mzembe kwa hiyo hata yeye kama msimamizi anaingia kwenye kundi la ufisadi.
"Rais hawezi kusimamia kila wizara, kila mkoa, kila wilaya, kila mtaa, ndiyo maana kuna madiwani, kuna wabunge, kuna wakuu wa wilaya, kuna wakuu wa mikoa hadi mawaziri.
"Hawa kazi yao ni kumsaidia Rais. Wakiwa wazembe hawa basi hata serikali itaonekana zembe. Kumbe ni baadhi ya viongozi tu wasiyotaka kuwa msaada kwa Rais," alisema Jumanne Mohanda wa Buguruni Kwa-Mwinyi Amani jijini Dar.
Aliongeza kuwa, CCM yenyewe ina jukumu la kupambana na mafisadi kwa wakati huu, ili wananchi waone nia yao ya dhati. Wakidharau shida itakuja wakati wakitaka kurudi madarakani kwenye uchaguzi ujao, upinzani hutumia kasoro hizo kuikosoa serikali ambayo mawaziri wake walibeba jukumu kubwa la kumsaidia Rais lakini hawakuona umuhimu kwa sababu ya uzembe au kuwa miongoni mwa mafisadi.
"Unakuaje waziri halafu wasaidizi wako wanakula pesa za umma na wewe upo. Ukiondolewa unamwona Rais kakuonea kumbe kagundua uzembe wako. Husimamii majukumu yako," alisema Jumanne na kumpongeza Rais Samia kwa hotuba zake zinazosisitiza kutochoka kufanya mabadiliko kila mara kama viongozi watashindwa kutekeleza majukumu yao.