Wabunge Kagera wamsusia mkuu wa mkoa kuadhimisha miaka 50

Poleni sana wenzangu wa Kagera. Mtawakumbuka sana hawa wabunge (Mtungirehi, marehemu Kabuye na Rwakatare).

Hawa watu wa Kagera nao njaa ilishakuwa nyingi na ubinafsi umewatawala sana.
Kila kiongozi anaeletwa wao udhani atamaliza shida zao. Wameshapita pale wakuu wa mikoa wa kila design na hakuna mabadiliko zaidi ya kwamba wanakuja chuma na kuondoka. Sasa wanadhani Masawe ataleta mabadiliko gani zaidi ya vitisho vya kiaskari?
Kila mtu ana jinsi yake ya kupata matatizo ya watu wake na kuyafikisha panakotakiwa na si lazima wapate amri ya Masawe. Ninachojua Masawe analinda maslahi ya bwana wake na wabunge wanalinda ya wananchi.
Hata hivyo mkataa pema pabaya panamwita. Watu wa Kagera walipenda sana kuhongwa na wataishia kubongwa.
 
Kaa la moto, kwakweli umenikuna: ni kweli kabisa watu wa kagera waliendekeza upuuzi kwamba mgombea anayetokeza na kuwapa 2000 au kulipa michango midogomidogo ya wanafunzi walioko primary basi yeye ndiye atachaguliwa kuwa mbunge na akishapata nafasi hiyo ni kutokomea kusiko julikana huku wana Kagera wakibaki wanagugumia tu, mfano nzuri hasa ni ktk jimbo la Bukoba vijijini; akina Karamagi na sasa Rweikiza wamekuwa wakifanya hivyo na baadae kuacha Jimbo/wilaya na Umasikini wa kutupwa; inasikitisha sana Bkb vijini hadi sasa asilimia 80 wananchi hawajui umeme japokuwa nyaya zinakatisha kwenye migomba na nyumba zao , barabara hazipitiki, makao makuu pa wilaya/jimbo hapajulikani, zaidi ya mkuu wa Wilaya kuishi Bkb mjini. mambo hayo yamepelekea wanakagera wengi wahishi uhamishoni kwenye miji mikubwa ya Dsm na Arusha; lkn kama wangepatikana viongozi wenye nia kabisa ya kimaendeleo wakashirikiana vyema na wasomi lukuki wanaotokea kagera ni hakika kagera ingekuwa Ulaya ndogo ya Tanzania.
 
Watu wakagera bana wanaonekana wajanja lakini mkoa wao umechoka sana. Poleni na Ccm yenu!
 
Na hapa ndipo unaweza kuona kisomo kilivyoporomoka Kagera. Wasomi wa Kagera sio wa sasa, bali sasa hivi watu ni njaa tu. Vijana wengi hawajaenda shule, wanahongeka kirahisi kwa mlo wa siku moja kuuza uhuru wao. Wanadanganywa kwa khanga, vikofia, tshirt, vitambaa vya kichwani na sh.2000.
Hongo katika chaguzi hapa zinafanywa wazi tena wanatumiwa wajanja wachache wanaokula commission.
Sasa hivi kila mtu anayetokeza kutaka kugombea kwanza upiga kambi na kugawa vijipesa eti anachochea maendeleo na huyo kila mtu ataweka macho kwake, watu watapeleka vishida vyao kwake naye atajifanya anawapa vipesa. Hakuna maendeleo tena Kagera, kahawa kama dhahabu ya Kagera sasa hivi ni kama takataka maana haina thamani Tanzania lakini inathamani nchi jirani ingawa si ruhusa kuiuza huko. Watu wamekuwa mafukara kweli kweli. Walio matajiri ni wachuuzi wa bidhaa. Hakuna uwekezaji!
JAMBO LINALONIUMIZA SANA NI KWAMBA SASA HIVI KAGERA WAGOMBEA WENGI WALIKUWA NI VIONGOZI KATIKA VYAMA VYA USHIRIKA NA WALIKUWA WEZI NA WABADHIRIFU WA MAZAO KWA MANUFAA YAO. HAWA NDIO VIONGOZI WALIO KATIKA CHAMA HIKI CCM NA NDIO UGOMBEA VYEO VYOTE KATIKA JAMII KWA KUWA WANA PESA ZA WIZI. WATU WANAWAHUSUDU WEZI HAWA NA KUWAONA WATU WALIOFANIKIWA SANA BILA KUJUA MAFANIKIO YOTE HAYA YALITOKANA NA WIZI WA MAZAO YAO. WANAWAKENULIA MENO NA KUWAPA UONGOZI.
Wako wapi watu waliovaa viatu vya wazee wetu kama wakina mzee Ishengoma, Kawamala na wengine wachache waliochochea elimu Kagera? wako wapi? Leo tuna wezi tupu, wabunge wote wezi.......kama hakuna aliye mwizi kwa nini watake kutumia raslimali zao kupata uongozi? tukiwaacha hutawaona wakirudi kuchochea maendeleo? Yuko huyu bwana alikuwa mbunge miaka mingi iliyopita na wananchi wakaona hana kitu katika represantation na wakampiga chini anaitwa Rutalaka, ukimuona anazungumza Star Tv utadhani ana msaada wowote kwa wana Kagera. Utamsikia akisifia chama chake kilichokufa kwa misifa mingiiii? muulize anausaidia vipi mkoa wa kagera kimaendeleo kama x mbunge, hutasikia lolote. Mbabaishaji tu.
Sitaki hata kusema mengi maana naweza kutukana matusi mazito hapa!
 
Msitake kunipandisha presha mimi,mkoa wa Kagera kweli hauna mbele wala nyuma.Nimeshuduia mbunge Rweikiza akionga wananchi kwa kuwapa vipesa,kawachinjia ngombe pamoja na diwani wa Kata Karabagaine anaitwa Makwabe basi huyu jamaa aliwachinjia ng'ombe akawa amemaliza kazi.
Kagera mpaka ipate viongozi wenyewe maono na uzalendo kama mimi ndo itaweza songo mbele.
Nipeni kula zenu 2015 kupitia CDM Bukoba Vijijini.
 
Tatizo lenu mnaandika, mnalalama yanaishia hapa. Tuchukue hatua! Na tuwe chumvi ya hao wasiobadilika, hao wanaodhani maendeleo ni misaada wakati wa mazishi au hongo wkt wa uchaguzi.
 
Back
Top Bottom