BUKOBA: Sababu za umasikini wa mkoa wa Kagera! #2

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,670
Sababu za umasikini wa mkoa wa Kagera

Thursday September 08 2022

Siku chache zilizopita kumeibuka mjadala mkubwa uliochochewa na kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila kusema kwamba, kuna sababu nyingi za umasikini katika mkoa wa Kagera lakini kubwa mbili ni kuwa kila mwana Kagera ni mwanasheria, wanapenda sana ubishi na kiingereza kingi lakini pia, kuna aina ya “uvivu”.

IN SUMMARY

Na Dk Bullet Ruhinda

Moja ya sababu katika kuelezea uvivu huo ni mfano kuchelewa kufungua maduka ambayo ni moja ya vichocheo vya kiuchumi. Angalau alitaja hizo sababu mbili kati ya nyingi. Chalamila ambaye amewahi pia kuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya na Mwanza, alitoa kauli hiyo wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana. Hata hivyo, jambo la msingi la kujiuliza kisha tujadiliane ni je hizo ni miongoni mwa sababu?

Kitu cha kwanza ambacho kila mmoja wetu anatakiwa kukifahamu ni kwamba bila kujua sababu za tatizo huwezi kuondoa tatizo. Kitu cha msingi kabla ya kuanza kutafuta majibu tujisumbue kujua chanzo cha matatizo.

Tukijua chanzo basi dawa itapatikana bila kutumia nguvu. Pili tujiulize umasikini wa Kagera ni wa asili (natural) au ni wa kutengenezwa (artificial)? Na kama ni wa kutengenezwa je nani aliutengeneza? (who is an architect of Kagera’s poverty?)

Turejee katika historia, miaka ya 1950 mpaka ya 70, Kagera ilikuwa ni miongoni mwa mikoa iliyokuwa imepiga kubwa kimaendeleo. Kwanini? Kwa sababu watu walifanya kazi kwa bidii na bidii ya matunda yao ilionekana kupitia chama chao cha ushirika (BNCU).

Ukipitia maandiko ya Profesa Sam Maghimbi katika tafiti mbalimbali za kisomi, Tanganyika ilikuwa na vyama vichache vya ushirika ambavyo vilifuata misingi ya ushirika kama ilivyoanishwa katika Rochdare Principles of Cooperative.

Vyama hivyo ni BNCU (Kagera) KNCU (Kilimajaro), Nyanza Cooperative (Sukuma land) na Matengo Cooperative. Kati ya hivyo BNCU na KNCU vilikuwa ni vyama vikubwa na vyenye nguvu katika Afrika na ulimwenguni kwa kuwa vilikuwa na nafasi nzuri.

BNCU ilikuwa pamoja na kusomesha vijana wa Kagera kwa ruzuku katika shule za sekondari na ilikuwa ikitoa ufadhili wa masomo popote duniani maadam mwanafunzi awe na barua ya udahili kutoka chuo huskika. BNCU ilikuwa na miradi mingi ya maendeleo, ilikuwa mbioni kujenga Chuo kikuu na barabara katika mji wa Bukoba kwa kutaja miradi michache.

BNCU ilikuwa na mtaji katika pesa za kigeni ambao haukutofautiana sana na akiba ya taifa. Hiyo ndio ilikuwa nguvu ya wana Kagera kutokana na malipo bora ya Kahawa, wakulima waliaanza kujenga nyumba za bati kwenye miaka ya 1940.

Lakini kwa makusudi kabisa, ushirika ule ulipigwa marufuku. Mali na pesa vikataifishwa bila compensation (fidia). Hilo lilikuwa “chepe” la kwanza lililoanza kuchimba kaburi la umasikini katika mkoa wa Kagera.

Mtu atasema mbona ushirika ulirejeshwa, mbona hali ni dhoofu bin hali? Jibu ni rahisi, ulirejeshwa ila si ule Rochdarian bali ni wa kisiasa ambao Cooperative Union ni tawi la chama, kwa hakika ni kitega uchumi cha chama, si cha wananchi. Uongozi wa ushirika lazima uthibitishwe na kudhibitiwa na chama na Serikali.

Bei hazifuati tena soko, zinapangwa na bodi. Kahawa ikawekewa tozo luluki, hiyo yote ikaondoa hamasa ya wakulima kupenda zao hilo na ushirika wao (ambao kwa hakika ni mchwa unawatafuna badala ya kuwanufaisha).

Mfano mzuri wa kurejeshwa kwa ushirika ni mkulima aliyekatwa miguu na mikono, baada ya muda mrefu wa kuuguza vidonda aliyemkata viungo anapatia miguu na mikono ya bandia kisha anamwabia haya nenda kalime!

Chepe la pili katika kaburi la umasikini wa Kagera ni vita vya Kagera ambavyo vilipiganwa ndani ya ardhi ya Kagera.

Mkoa ulisimamisha uzalishaji kipindi chote cha vita. Mashamba yaliharibika, mifugo ikapotea pia kuna vifo vilitokea, baadhi ya wakazi wakawa wakimbizi. Mkoa ukawa kama unatawaliwa kijeshi au chini ya “state of emergence”.

Baada ya vita hapakuwa tena na mkakati maalum wa kiserikali na kitaasisi kuunasua mkoa na athari za vita. Ukaachwa upambane wenyewe kama vile hakuna kilichotokea, bado tutegemee mkoa huo uliorudi nyuma hadi hatua sifuri kimaendeleo usimame na kushindana na mikoa mingine kwa usawa.

Kama hiyo haitoshi mwanzoni mwa miaka ya 1980 au mwishoni mwa miaka ya 70 ukaingia ugonjwa wa ukimwi, madhara yake kwa Kagera yanajulikana kimataifa.

Kufikia mwaka 1985 karibu kila ukoo au familia zilishapoteza nguvu kazi iliyotegemewa na hivyo kuanzisha kizazi na watoto yatima wanaotegemea misaada ya NGOs. Athari za ugonjwa huo bado zipo.

Kama mapigo hayo hayatoshi, mwaka 1984 ulikuwa mwaka wa vita ya uhujumu uchumi. Kwa hakika, vita ile ni kama ililengwa kwa ajili ya mkoa wa Kagera.

Waliokuwepo watashuhudia. Mkoa ulipoteza mitaji. Watu walifungwa hata waliokuwa na viduka vidogo, mali zikataifishwa bila huruma.

Matajiri wakakimbia, mimi nilimshuhudia mhindi mmoja akiitwa Rostamali akikimbia nafikiri kuelekea Canada au Uingereza. Mitaji yote hiyo ikaondoka Kagera.

Bado mtu anasema watu wa Kagera hawafayi maendeleo kwao. Kwa mitaji gani? Yaani wana Kagera ni watu wa kuanza upya kila siku? Je, kwa mambo tajwa hapo juu, Kagera ni masikini kwa asili au kwa kuchongwa?

Tujadili kidogo ufunguaji wa maduka kuanzia saa tatu kwani, watu wameshikia bango kwamba ndio uvivu. Zipo sababu za kisosholojia na anthropolojia kwa nini watu hawafungui maduka nyakati za alfajiri.

Kwanza wakazi wa Bukoba na miji mingine ya Kagera ni wakazi wenyeji (pale ndio kwao), hivyo mahitaji yao yote wanayapata nyumbani mfano kifungua kinywa. Tofauti na mikoa mingine, wakazi wa Kagera si wanunuzi wa vitu katika “vibaba”.

Mfano sukari wengi hununua kuanzia nusu kilo au kilo moja na si vijiko. Mtu anayenunua kilo ya sukari hana haja ya kuamkia kwenye duka la Mangi kununua vijiko vya sukari. Maana yake ni kwamba wana Kagera wanapanga mahitaji yao ya kimaisha. Hawaongozwi na matukio kufanya mambo.

Pili maduka mengi Bukoba mjini hasa ya jumla yanawahudumia wafanyabiashara wanaotoka vijijini, wanaonunua kwa jumla ili wakauze rejareja kwenye maeneo yao.

Wafanyabiashara hao huanza kuingia mjini saa tatu mpaka nne, hiyo itakuwa ajabu muuza duka la jumla Bukoba mjini kufungua saa 12 alfajiri wakati wateja wake toka Kamachumu, Ihangiro, Karagwe na penginepo ndio wanaanza safari ya kuja mjini.

Lakini, biashara huria haigozwi na muda wa kufungua bali nguvu ya soko. Uhitaji wa kufungua asubuhi, bali muda ukifika watu watafungua. Wakati mwingine wafanyabiasha wana shughuli zaidi ya moja.

Hivyo kuanzia alfajiri anafanya shughuli nyingine za shamba wakati anasubiri wateja wake wafike saa tatu ndio afungue duka lake. Kwa hiyo kabla ya kuwalaumu watu kwa kufungua maduka saa tatu, tujiulize wanafanya nini asubuhi?

Kagera haina kazi nyingi za usiku kama viwanda au vyombo vya usafiri, mfano Meli huondoka saa tatu usiku hivyo shughuli zinazoihusu hufanyika mchana hadi jioni na si asubuhi.

Nimendika mengi yote haya si kutetea kuwa Kagera si masikini, la hasha bali kuonyesha sababu za umasikini na nani mhusika mkuu kuliko kurundika lawama kwa maprofesa na madaktari wanaotoka Kagera kama vile ni dhambi kuwa profesa.

Nini kifanyike ili kuondoa au kupunguza umasikini? Kwa ufupi wana Kagera wameisha fanya yaliyo ndani ya uwezo wao, serikali ifanye kilichobaki ambacho ni kuleta miundombinu ili kuchochea shughuli za kiuchumi. Miundombinu ya umeme, barabara, maji nk.

Watu wanasema stendi ya mabasi inawatia aibu wana Kagera, kitu ambacho si kweli, bali inawasononesha, na kuitia aibu Serikali.

Si kazi ya wananchi kujenga stendi wala soko bali Serikali kupitia kodi za wananchi. Wala si msaada, ni haki yao. Kama masoko na stendi zimejengwa karibu nchi nzima kwa nini si Kagera? Hapo mwana Kagera analaumiwa kwa lipi?

Mwisho, kabla ya kutoa lawama kwa nini Kagera inaitwa masikini, turudi nyuma kuona nani kasababisha umasikini huo.

Waingereza wana msemo wao “means justify the end”, japo inasemekana Wana Kagera wana kiingereza kingi na ubishi wa wanasheria! Kwangu hiyo ni credit. Dunia ipo katika zama za kuhoji, na si kukubali kila kitu. Tupo zama za ushirikishwaji si kutawaliwa, zama za majadiliano si kuamrishwa.

Wana Kagera wanaishi hivyo.

CHANZO: Mwananchi
 
Usoni: Kingereza kingi! Ni utajiri tosha!
 
""Chepe la pili katika kaburi la umasikini wa Kagera ni vita vya Kagera ambavyo vilipiganwa ndani ya ardhi ya Kagera.

Mkoa ulisimamisha uzalishaji kipindi chote cha vita. Mashamba yaliharibika, mifugo ikapotea pia kuna vifo vilitokea, baadhi ya wakazi wakawa wakimbizi. Mkoa ukawa kama unatawaliwa kijeshi au chini ya “state of emergence”.

Baada ya vita hapakuwa tena na mkakati maalum wa kiserikali na kitaasisi kuunasua mkoa na athari za vita. Ukaachwa upambane wenyewe kama vile hakuna kilichotokea, bado tutegemee mkoa huo uliorudi nyuma hadi hatua sifuri kimaendeleo usimame na kushindana na mikoa mingine kwa usawa."""HII INA UKWELI KIASI
 
Ubinafsi na ujuaji mwingi ni ugonjwa mbaya sana unaowamaliza wahaya....unapokuwa unatafuta kitu kizuri jishushe..........mimi nakumbuka mwaka 2001 nilikuwa nafanya kazi hospital moja binafsi huko mkoani tabora...mmiliki wa hospitali ile alikuwa na elimu ya kidato cha nne tu na hakuwa mtaalamu wa afya kama mimi, kuna wakati alituingilia katika maamuzi ya kimatibabu ....mgonjwa anatakiwa achome sindano ya kutibu ugonjwa wa kutibu maambukizi ya njia ya mkojo( UTI)..Kwa siku tano na kila siku mara moja, lakini yeye alikuwa anatulazimisha tupunguze dozi ili apige faida kwenye dawa..kwa kuwa nilikuwa nataka nipige hatua ya kimaisha nitoke pale nilipokuwa ili nibidi nijishushe nikitambua hapa napita, nikijisemea moyoni kuwa ipo siku taaluma yangu nitakwenda kuitumia vizuri sehemu husika na panapofaa..
 
..Je, "ulijishusha" na kufuata mashinikizo ya mwenye hospitali ukamchoma mgonjwa dozi ndogo?
 
Usoni: Kingereza kingi! Ni utajiri tosha!
🤣🤣🤣 kung'atwa ka mkia kidogo.

Kagera umaskini wanautoa wapi na showoff zao ni nyingi huku mtaani?

🤣🤣mi siamini hawa jamaa wanasingiziwa tu. Huko kagera nasikia gari aina ya IST ni kagari tu ka mlinzi wa getiii🤣🤣🤣
 
Wahaya sijuhi nani kawaroga, ardhi yote mmepanda miti (pine) hakuna sehemu ya kulima mazao ya muda mfupi kama karanga, njugu, mihogo, viazi vitamu, nk mashamba ya urithi (ekibanja) yamezidiwa na wingi wa watu pia yamechoka hayana rutuba. Hili nalo mtasingizia serikali....yaani hata kwenye chemichemi na misitu asili mmefyeka na kupanda mikaratusi...hili janga ni la kujitakia
 
Hii ishu iko overrated kwamba utafirkia huko bukoba ni maskini wa kutupa wakati ni miuondombinu tu!!! Ishakuwa kubwa
Napenda ibaki hivi kabisa...acha wauverrate..wakufurahi wafurahi...

Lakin ndo itawasukuma wafanya maamuzi kupeleka hizo huduma mkoani humo..Tanzania ukikaa kimya nothing will be done kwako...

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Ubinafsi na ujuaji mwingi ni ugonjwa mbaya sana unaowamaliza wahaya....unapokuwa unatafuta kitu kizuri jishushe..........mimi nakumbuka mwaka 2001 nilikuwa nafanya kazi hospital moja binafsi huko mkoani tabora...mmiliki wa hospitali ile alikuwa na elimu ya kidato cha nne tu na hakuwa mtaalamu wa afya kama mimi, kuna wakati alituingilia katika maamuzi ya kimatibabu ....mgonjwa anatakiwa achome sindano ya kutibu ugonjwa wa kutibu maambukizi ya njia ya mkojo( UTI)..Kwa siku tano na kila siku mara moja, lakini yeye alikuwa anatulazimisha tupunguze dozi ili apige faida kwenye dawa..kwa kuwa nilikuwa nataka nipige hatua ya kimaisha nitoke pale nilipokuwa ili nibidi nijishushe nikitambua hapa napita, nikijisemea moyoni kuwa ipo siku taaluma yangu nitakwenda kuitumia vizuri sehemu husika na panapofaa..
Sasa apo unaona kujishusha kwako KWa kijinga au KWa manufaa, kwanza ulishiriki wizi kumpunguzia mgojwa dawa ambayo tiyari amelipia, Mbili umeumiza watu Sana kisa pesa, umewasabishia usugu wa magonjwa yao ,
Kifupi wewe, na Bosi wako mlitakiwa kuwa ndani ,ila jinai haifi
 
Sababu za umasikini wa mkoa wa Kagera

Thursday September 08 2022

Siku chache zilizopita kumeibuka mjadala mkubwa uliochochewa na kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila kusema kwamba, kuna sababu nyingi za umasikini katika mkoa wa Kagera lakini kubwa mbili ni kuwa kila mwana Kagera ni mwanasheria, wanapenda sana ubishi na kiingereza kingi lakini pia, kuna aina ya “uvivu”.

IN SUMMARY

Siku chache zilizopita kumeibuka mjadala mkubwa uliochochewa na kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila kusema kwamba, kuna sababu nyingi za umasikini katika mkoa wa Kagera lakini kubwa mbili ni kuwa kila mwana Kagera ni mwanasheria, wanapenda sana ubishi na kiingereza kingi lakini pia, kuna aina ya “uvivu”.

Na Dk Bullet Ruhinda

Siku chache zilizopita kumeibuka mjadala mkubwa uliochochewa na kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila kusema kwamba, kuna sababu nyingi za umasikini katika mkoa wa Kagera lakini kubwa mbili ni kuwa kila mwana Kagera ni mwanasheria, wanapenda sana ubishi na kiingereza kingi lakini pia, kuna aina ya “uvivu”.

Moja ya sababu katika kuelezea uvivu huo ni mfano kuchelewa kufungua maduka ambayo ni moja ya vichocheo vya kiuchumi. Angalau alitaja hizo sababu mbili kati ya nyingi. Chalamila ambaye amewahi pia kuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya na Mwanza, alitoa kauli hiyo wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana. Hata hivyo, jambo la msingi la kujiuliza kisha tujadiliane ni je hizo ni miongoni mwa sababu?

Kitu cha kwanza ambacho kila mmoja wetu anatakiwa kukifahamu ni kwamba bila kujua sababu za tatizo huwezi kuondoa tatizo. Kitu cha msingi kabla ya kuanza kutafuta majibu tujisumbue kujua chanzo cha matatizo.

Tukijua chanzo basi dawa itapatikana bila kutumia nguvu. Pili tujiulize umasikini wa Kagera ni wa asili (natural) au ni wa kutengenezwa (artificial)? Na kama ni wa kutengenezwa je nani aliutengeneza? (who is an architect of Kagera’s poverty?)

Turejee katika historia, miaka ya 1950 mpaka ya 70, Kagera ilikuwa ni miongoni mwa mikoa iliyokuwa imepiga kubwa kimaendeleo. Kwanini? Kwa sababu watu walifanya kazi kwa bidii na bidii ya matunda yao ilionekana kupitia chama chao cha ushirika (BNCU).

Ukipitia maandiko ya Profesa Sam Maghimbi katika tafiti mbalimbali za kisomi, Tanganyika ilikuwa na vyama vichache vya ushirika ambavyo vilifuata misingi ya ushirika kama ilivyoanishwa katika Rochdare Principles of Cooperative.

Vyama hivyo ni BNCU (Kagera) KNCU (Kilimajaro), Nyanza Cooperative (Sukuma land) na Matengo Cooperative. Kati ya hivyo BNCU na KNCU vilikuwa ni vyama vikubwa na vyenye nguvu katika Afrika na ulimwenguni kwa kuwa vilikuwa na nafasi nzuri.

BNCU ilikuwa pamoja na kusomesha vijana wa Kagera kwa ruzuku katika shule za sekondari na ilikuwa ikitoa ufadhili wa masomo popote duniani maadam mwanafunzi awe na barua ya udahili kutoka chuo huskika. BNCU ilikuwa na miradi mingi ya maendeleo, ilikuwa mbioni kujenga Chuo kikuu na barabara katika mji wa Bukoba kwa kutaja miradi michache.

BNCU ilikuwa na mtaji katika pesa za kigeni ambao haukutofautiana sana na akiba ya taifa. Hiyo ndio ilikuwa nguvu ya wana Kagera kutokana na malipo bora ya Kahawa, wakulima waliaanza kujenga nyumba za bati kwenye miaka ya 1940.

Lakini kwa makusudi kabisa, ushirika ule ulipigwa marufuku. Mali na pesa vikataifishwa bila compensation (fidia). Hilo lilikuwa “chepe” la kwanza lililoanza kuchimba kaburi la umasikini katika mkoa wa Kagera.

Mtu atasema mbona ushirika ulirejeshwa, mbona hali ni dhoofu bin hali? Jibu ni rahisi, ulirejeshwa ila si ule Rochdarian bali ni wa kisiasa ambao Cooperative Union ni tawi la chama, kwa hakika ni kitega uchumi cha chama, si cha wananchi. Uongozi wa ushirika lazima uthibitishwe na kudhibitiwa na chama na Serikali.

Bei hazifuati tena soko, zinapangwa na bodi. Kahawa ikawekewa tozo luluki, hiyo yote ikaondoa hamasa ya wakulima kupenda zao hilo na ushirika wao (ambao kwa hakika ni mchwa unawatafuna badala ya kuwanufaisha).

Mfano mzuri wa kurejeshwa kwa ushirika ni mkulima aliyekatwa miguu na mikono, baada ya muda mrefu wa kuuguza vidonda aliyemkata viungo anapatia miguu na mikono ya bandia kisha anamwabia haya nenda kalime!

Chepe la pili katika kaburi la umasikini wa Kagera ni vita vya Kagera ambavyo vilipiganwa ndani ya ardhi ya Kagera.

Mkoa ulisimamisha uzalishaji kipindi chote cha vita. Mashamba yaliharibika, mifugo ikapotea pia kuna vifo vilitokea, baadhi ya wakazi wakawa wakimbizi. Mkoa ukawa kama unatawaliwa kijeshi au chini ya “state of emergence”.

Baada ya vita hapakuwa tena na mkakati maalum wa kiserikali na kitaasisi kuunasua mkoa na athari za vita. Ukaachwa upambane wenyewe kama vile hakuna kilichotokea, bado tutegemee mkoa huo uliorudi nyuma hadi hatua sifuri kimaendeleo usimame na kushindana na mikoa mingine kwa usawa.

Kama hiyo haitoshi mwanzoni mwa miaka ya 1980 au mwishoni mwa miaka ya 70 ukaingia ugonjwa wa ukimwi, madhara yake kwa Kagera yanajulikana kimataifa.

Kufikia mwaka 1985 karibu kila ukoo au familia zilishapoteza nguvu kazi iliyotegemewa na hivyo kuanzisha kizazi na watoto yatima wanaotegemea misaada ya NGOs. Athari za ugonjwa huo bado zipo.

Kama mapigo hayo hayatoshi, mwaka 1984 ulikuwa mwaka wa vita ya uhujumu uchumi. Kwa hakika, vita ile ni kama ililengwa kwa ajili ya mkoa wa Kagera.

Waliokuwepo watashuhudia. Mkoa ulipoteza mitaji. Watu walifungwa hata waliokuwa na viduka vidogo, mali zikataifishwa bila huruma.

Matajiri wakakimbia, mimi nilimshuhudia mhindi mmoja akiitwa Rostamali akikimbia nafikiri kuelekea Canada au Uingereza. Mitaji yote hiyo ikaondoka Kagera.

Bado mtu anasema watu wa Kagera hawafayi maendeleo kwao. Kwa mitaji gani? Yaani wana Kagera ni watu wa kuanza upya kila siku? Je, kwa mambo tajwa hapo juu, Kagera ni masikini kwa asili au kwa kuchongwa?

Tujadili kidogo ufunguaji wa maduka kuanzia saa tatu kwani, watu wameshikia bango kwamba ndio uvivu. Zipo sababu za kisosholojia na anthropolojia kwa nini watu hawafungui maduka nyakati za alfajiri.

Kwanza wakazi wa Bukoba na miji mingine ya Kagera ni wakazi wenyeji (pale ndio kwao), hivyo mahitaji yao yote wanayapata nyumbani mfano kifungua kinywa. Tofauti na mikoa mingine, wakazi wa Kagera si wanunuzi wa vitu katika “vibaba”.

Mfano sukari wengi hununua kuanzia nusu kilo au kilo moja na si vijiko. Mtu anayenunua kilo ya sukari hana haja ya kuamkia kwenye duka la Mangi kununua vijiko vya sukari. Maana yake ni kwamba wana Kagera wanapanga mahitaji yao ya kimaisha. Hawaongozwi na matukio kufanya mambo.

Pili maduka mengi Bukoba mjini hasa ya jumla yanawahudumia wafanyabiashara wanaotoka vijijini, wanaonunua kwa jumla ili wakauze rejareja kwenye maeneo yao.

Wafanyabiashara hao huanza kuingia mjini saa tatu mpaka nne, hiyo itakuwa ajabu muuza duka la jumla Bukoba mjini kufungua saa 12 alfajiri wakati wateja wake toka Kamachumu, Ihangiro, Karagwe na penginepo ndio wanaanza safari ya kuja mjini.

Lakini, biashara huria haigozwi na muda wa kufungua bali nguvu ya soko. Uhitaji wa kufungua asubuhi, bali muda ukifika watu watafungua. Wakati mwingine wafanyabiasha wana shughuli zaidi ya moja.

Hivyo kuanzia alfajiri anafanya shughuli nyingine za shamba wakati anasubiri wateja wake wafike saa tatu ndio afungue duka lake. Kwa hiyo kabla ya kuwalaumu watu kwa kufungua maduka saa tatu, tujiulize wanafanya nini asubuhi?

Kagera haina kazi nyingi za usiku kama viwanda au vyombo vya usafiri, mfano Meli huondoka saa tatu usiku hivyo shughuli zinazoihusu hufanyika mchana hadi jioni na si asubuhi.

Nimendika mengi yote haya si kutetea kuwa Kagera si masikini, la hasha bali kuonyesha sababu za umasikini na nani mhusika mkuu kuliko kurundika lawama kwa maprofesa na madaktari wanaotoka Kagera kama vile ni dhambi kuwa profesa.

Nini kifanyike ili kuondoa au kupunguza umasikini? Kwa ufupi wana Kagera wameisha fanya yaliyo ndani ya uwezo wao, serikali ifanye kilichobaki ambacho ni kuleta miundombinu ili kuchochea shughuli za kiuchumi. Miundombinu ya umeme, barabara, maji nk.

Watu wanasema stendi ya mabasi inawatia aibu wana Kagera, kitu ambacho si kweli, bali inawasononesha, na kuitia aibu Serikali.

Si kazi ya wananchi kujenga stendi wala soko bali Serikali kupitia kodi za wananchi. Wala si msaada, ni haki yao. Kama masoko na stendi zimejengwa karibu nchi nzima kwa nini si Kagera? Hapo mwana Kagera analaumiwa kwa lipi?

Mwisho, kabla ya kutoa lawama kwa nini Kagera inaitwa masikini, turudi nyuma kuona nani kasababisha umasikini huo.

Waingereza wana msemo wao “means justify the end”, japo inasemekana Wana Kagera wana kiingereza kingi na ubishi wa wanasheria! Kwangu hiyo ni credit. Dunia ipo katika zama za kuhoji, na si kukubali kila kitu. Tupo zama za ushirikishwaji si kutawaliwa, zama za majadiliano si kuamrishwa.

Wana Kagera wanaishi hivyo.

CHANZO: Mwananchi
Jamaa kaandika kongole kwake
 
Kitu ambacho Chalamila anatakiwa aelewe ni kuwa Tanzania practically ilitakiwa iwe na timezones (GMT +2 na GMT +3) mbili!
Yani wakati Dar Es Salaam ni saa tatu kamili asubuhi, Western Tz ni sawa sawa na saa mbili kamili asubuhi ukifuatilia parameters za mawio na machweo.
Kwa hiyo mtu aliyefungua duka lake Dar Es Salaam au Tanga saa mbili asubuhi na kufunga saa kumi na mbili jioni ni sawa na yule aliyefungua duka lake Bukoba au Kigoma saa tatu asubuhi na kufunga saa moja jioni.

Tukiwaambia watu nchi yetu ni kubwa, 'hawaelewi'! Kwenye hii ramani ya Dunia unaweza kujionea Tz ikiwa katika GMT mbili tofauti. Msitari 'umeikata' nchi katikati kwenye GMT mbili tofauti, even though officially tunatumia timezone ya GMT +3.
download.jpeg
 
Chepe lingine watu wanao nunua Kahawa kwa magendo na wanatoka mbali bei yao mala2nanusu au kwa bei ya vyama vya shilika!
 
Back
Top Bottom