Wabunge hawa hawatarudi Bungeni 2015

Wabunge hawa hawatarudi Bungeni 2015

Status
Not open for further replies.
Wewe uliyeleta uzi huu, lazima utakuwa miongoni ya wale vijana mliotoka na division 0 kidato cha nne mwaka jana, ambao mmeingia kwenye payroll ya Nape kwa mkataba wa kuwa muda wote muwe JF, kwa kazi moja ya kuichafua CDM!

Lakini ambacho mmesahau hivi sasa CDM ni kama mafuriko ya El nino, usitarajie kuwa utayazuia mafuriko hayo kwa viganja vyako vya mikono, hutaweza na lazima utasombwa na mafuriko hayo!!
 
pole dear, hao ndio wanaokunyima usingizi eh? jitahidi tu uwapende maana they are there to stay, hizo ulizogusa ndio cream
 
Mkuu unajua hiyo Tsh 600 (per capital income) inapatikanaje ama unaleta sihasa hapa, hivi unajua kwamba hata hiyo 600 wengi hawawezi kuipata kwa siku na imepatakana tu kwa sababu ya wastani maanake hata hela za AZAM tumegawana tukapata hiyo. hivi unajua hata hao graduate waliojaa hapo jijini dar wakitafuta kazi hawana uwezo wa kuzalisha value ya 650 Tsh lakini tume assume tu.

Unaisemea tanzania ipi ambayo unasema haitoshi kusema watu wana maisha magumu, huamini, hujaona ama ni Lumumba ndo inakufanya uwe hivo

Sikiliza mkuu, huu utaratibu wa per capital income sio mzuri kujua kuwa maisha ya mtu mmoja mmoja ni mazuri au magumu, una changamoto nyingi sana huu utaratibu. Maelezo yangu yanajitosheleza na ndio uhalisia wa maisha ya watanzania wengi, wala sio U-lumumba.
 
Hata kama ni kutaka kupima mawazo ya watu, yapasa mtu ukatumia akili badala ya kufanya kitu ambacho hata wewe mwenyewe huna unajua kuwa hakiwezekani. Hayo majina uliyoyataja basis yake ni nini?
 
Watu kuishi kwa Tshs. 600 kwa siku sio kigezo toshelezi kusema kuwa wana maisha magumu, hii ni kwa sababu wananchi wengi wa kijijini hawatumii fedha kwa kiasi kikubwa katika mahitaji yao, mfano mdogo tu, mtu anaelima bustani yake na akaweka mihogo na ikikomaa anachemsha maisha yanaenda, hawa ndio wamejaa huko mikoani, awahitaji fedha kwa kiasi kikubwa ili kuendesha maisha. Hemu elewa hili mkuu na wote wenye fikra kama zako.

Kwanini yeye ale mihogo ya kuchemsha na wewe ule samaki na kuku wa kukaanga kwa wali au ugali..? or rather kwanini wewe usile mihogo ya kuchemsha na yule kijijini akala samaki na kuku wa kukaanga kwa wali au ugali..?
Hivi ulichokiandika umekielewa..? Bustani inaweza kumlisha na kumvisha na kumlipishia ada ya shule kwa watoto wake..? Au kumsaidia atakapokwenda hospital pindi mmojawapo wa kwenye familia yake akipata maradhi..? Jee mkulima huyu hana haki ya kula wali na kuku..? Hana haki wala hadhi ya kunywa chai na mkate au maandazi..? Hana haki wala hadhi ya kunywa soda au juice..? Hana haki wala hadhi ya kusafiri toka pointi A kwenda pointi B..? Hana haki wala hadhi ya kuwa na umeme nyumbani kwake..? au kuwa na radio au tv..?

Hili ndilo ambalo wewe unaweza kujivuna ndo mchango wako kwa nchi yako..?
Sipendi kuwaita watu wengine majina ya kudhalilisha japo wanastahili.. Naamini wapo watakaonisaidia kwa hilo.. Nitakachosema ni kimoja.. Unakera..:angry:
 
Sikiliza mkuu, huu utaratibu wa per capital income sio mzuri kujua kuwa maisha ya mtu mmoja mmoja ni mazuri au magumu, una changamoto nyingi sana huu utaratibu. Maelezo yangu yanajitosheleza na ndio uhalisia wa maisha ya watanzania wengi, wala sio U-lumumba.

Nimekuelewa Mkuu

sasa tukubaliane kwamba kama hautupi uhalisia basi inawezekana hali ni mbaya zaidi kwa wananchi walio wengi hasa ukizingatiwa tu kwamba watanzania waliowengi hawazalishi kitu. kumbuka nchi yetu 74% ya wananchi wanashighulisha na kilimo na wanachangi 25% tu katika uzalishaji wa taifa.
 
Anza kujadili kwanza tutaondoaje umasikini kwa hawa raia wetu wanao ishi kwa Tsh 650 kwa siku i
Mwambie Mchungaji Msigwa aache kuchukua sadaka za waumini wake, siku hizi salafu hawataki wanataka noti tu.

 
Mkuu mimi naona ungekamilisha list kama ungemaliza na Mhe. Mbowe, huyu jamaa wananchi wa Hai walikuwa hawajui kama kala sifuri kidato cha sita (6), sasa wamejua na wamechachamaa kwelikweli, wamesema hata awape Bilicans bungeni awamrudishi.
Huyu yupo katika listi ya waliopewa ubunge kwa huruma tu, kama akina Mrema, Cheyo, Mbatia

 
Mbowe huenda akajiuzulu siasa ikitokea majimbo kupungua. Na nadhani hilo haliepukiki!
 
Ha ha ha ha haaahaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!

Mkuu usinivunje mbavu zaidi; ama kweli huyu mtani wetu wa kijani aliyetundika uzi huu hapa ukutani ama hakumaanisha alichokiandika humu au yeye mwenyewe kiti chake tayari kimewekwa rehani na wabunge wawili watatu waliofunguliwa kimakosa bungeni na kuanza kung'ata kila fisadi paka jimboni mwake kabisa.

Maadam Ndg Ndugai alifanya makosa makubwa kiasi hicho hawa SIMBA Wadogo (CHADEMA Political Puppies), acha MAFISADI wote wakipate kila mmoja katika jimbo anamotoka.


Hata kama ni kutaka kupima mawazo ya watu, yapasa mtu ukatumia akili badala ya kufanya kitu ambacho hata wewe mwenyewe huna unajua kuwa hakiwezekani. Hayo majina uliyoyataja basis yake ni nini?
 
tunashukuru, najua umepata buku 7 ya kula mchana, basi nenda kapumzike, maana ayo mawazo yako hayana uchambuzi wowote, wala vigezo, umeandika tu. ila najua hao ndio wanaowanyima usingizi ccm. na bado poleni sana.

Sio mbaya kupima upepo kwa vinyweleo japo sikushauri kuzoea tabia hyo

Uzi umejaa chuki binafsi kuliko vigezo na sababu za msingi!

Hivi Kiwia ana ubavu wa kupambana na Diallo Ilemela au tunabwabwaja bila ya kujua ushindi wake ulitokana na nn?
 
Watu kuishi kwa Tshs. 600 kwa siku sio kigezo toshelezi kusema kuwa wana maisha magumu, hii ni kwa sababu wananchi wengi wa kijijini hawatumii fedha kwa kiasi kikubwa katika mahitaji yao, mfano mdogo tu, mtu anaelima bustani yake na akaweka mihogo na ikikomaa anachemsha maisha yanaenda, hawa ndio wamejaa huko mikoani, awahitaji fedha kwa
kiasi kikubwa ili kuendesha maisha. Hemu elewa hili mkuu na wote wenye fikra kama zako.
Mkuu unaifahamu vizuri shughuli ya kilimo au waropoka tu? Kilimo sio kazi rahisi kama unavyofikiria!
Ndani ya nchi hii, huwezi kulima popote na zao lolote kwa kipato unachokitetea hapo juu!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom