Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,505
- 16,006
Sera za chama na si sera za mtu.......Wao walifata vile chama kinataka,Msigwa alishawahi kusema 'huwezi kutatua kosa kwa kutumia akili hiyo hiyo iliyosababisha kosa hilo'....akaendelea 'haiwezekani akili kubwa kutawala akili ndogo'. Akakazia 'wanaomuunga mkono Lowassa wakapimwe akili'.
Katika kampeni za Mwaka jana hoja kuu ya Chadema ilikuwa 'mabadiliko' ati wote walioongoza serikali katika kipindi cha miaka 50 iliyopita waondolewe sababu 'hawajafanya chochote ndani ya miaka 50 ya uongozi wao. Katika kuhakikisha wanaelekea katika mabadiliko hayo sasa wanalazimika kutumia 'akili ileile iliyosababisha matatizo ili kutatuta matatizo yale yale'. Kwa sasa Chadema hawawezi kufanya lolote bila kupata malekezo toka kwa Lowassa na Sumaye. Sasa akili ndogo inatoa ushauri kwa akili kubwa', wanapewa hadi maneno ya kuzungumza bungeni na kwenye mikutano ya siasa. Amri ni moja tu, ole wake mbunge wa chadema atakayezungumza kauli tofauti na maelekezo ya Sumaye na Lowassa...'atakiona cha mtema kuni'.
Ajizi nyumba ya njaa, wabunge wa chadema wamekubali yaishe kuwa Hemedi Alli ndiye mkuu mpya wa idara ya Habari na Propaganda Chadema. Tafsiri yake ni kwamba Tundu,Lema,Sugu na wenzao watalazimika kujifunza mila na tamaduni za chadema kutoka kwa Hemedi Ali. Hemedi Ali alijiunga Chadema tarehe 29.07.2015 siku Lowassa anatambulishwa kwa wanahabari kama Mgombea wa Chadema na baadaye Ukawa. Huyu alikuwa ni mwenyekiti wa 4U Movement. Ole wake Tundu aropoke, atawajibishwa..Msemaji ni mmoja tu Hemedi Ali.Bavicha mpya inakuja, vijana wa 4U,Ulipo Tupo na TeamLowassa kutawala nafasi za uongozi Chadema.
Katika hatua nyingine wabunge wa CUF wametengwa katika mazungumzo yaliyosimamiwa na Lowassa na Sumaye. Sasa ni kama watoto 'yatima', Seif hana habari nao.
Hakika wiki katika siasa ni sawa na mwaka katika maisha mengine, siku zinaenda kasi.
Mbona Chademaa wanafuata sera za Lowassa? kwani Lowassa ni chama?Kwani Binadamu hawezi kutubu na kubadilika?Lowassa n Sumaye waligundua kuwa hawako kwenye chama sahihi, kumbuku ukiwa kwenye chama unafata sera za chama si sera zako kama Furani anavyifata za kwake.....
Mkaachaga unafiki nyie watu,kama mnaona hatuna wapinzani Tanzania sasa mbona kila kukicha mnawadhibiti na kuwatungia makosa yasiyo na maana wewe sema Tanzania hatuna chama Tawala chama chetu ni polisi utaeleka sio unaonge pumba hapaNakuambia Tanzania bado hatujapata upinzani wa kweli,
Watasema mchawi ni Ccm kumbe ni wao wenyewe.
Mwananchi aliye choka na chama kimoja
Ili umpeleke chama kingine
Ni lazima uwe na mambo mapya
Watu wapya na hoja zenye mashiko
Ajabu
Wale aliye wachoka Ccm aende kuwakuta cdm
Tena ndio waamuzi wa lolote ndani ya chama!!!
MSIGWA MUNGU ANAKUONA KWA KAULI ZAKO ZILE
HUONI AIBU!!!!
CCM wanapelekeshwa kwa sera za mtu m1? Na ukiangalia CDM wanafata sera zao kabla hata Lowassa hajajiunga nao,hata kama Lowassa alikuwa mchafu CCM;kuja CDM ni kama mtu mwenye dhambi aliyejigundua na kuamua kuokoka na kumfata yesu au njia za yesu,unaweza usifanye vzr ukiwa simba ila ukisajiliwa Yanga na ukapewa nafasi unafanya vzr zaidi Binadamu sio mlima.Mbona Chademaa wanafuata sera za Lowassa? kwani Lowassa ni chama?
Ni hivi ''chadema lazima ihitimu kutoka uanaharakati hadi chama cha siasa'.....Hivi huoni jinsi chadema ilivyobadilika kufuata sera za Lowassa?Mbona
CCM wanapelekeshwa kwa sera za mtu m1? Na ukiangalia CDM wanafata sera zao kabla hata Lowassa hajajiunga nao,hata kama Lowassa alikuwa mchafu CCM;kuja CDM ni kama mtu mwenye dhambi aliyejigundua na kuamua kuokoka na kumfata yesu au njia za yesu,unaweza usifanye vzr ukiwa simba ila ukisajiliwa Yanga na ukapewa nafasi unafanya vzr zaidi Binadamu sio mlima.
Dah ni bomu linalosubiri kulipuka.Ilishakula kwao kitambo... Ni suala la muda tu.
Mpaka wakati wa utawala wa George Bush Junior Donald Trump alikuwa ni mwanachama mkubwa tu wa Democrat. Kwenye siasa haya ni mambo ya kawaida tu, yasikuumize sana. Kuna mwanasisa aliwahi kujiapiza hadi Mama yake mzazi iwapo atarudi ccm, lakini alirudi na akapewa usemaji mkuu wa chama.
Kwani Binadamu hawezi kutubu na kubadilika?Lowassa n Sumaye waligundua kuwa hawako kwenye chama sahihi, kumbuku ukiwa kwenye chama unafata sera za chama si sera zako kama Furani anavyifata za kwake.....
Ww ndo urudi hosptali ukamalizie dozi ndo uje hapaumevevulugwa ndio nini? rudi shule kwanza ndio uje uchangie mada.
USITUDANGANYE. KAMA HAMNAXWAPINZANI MBONA TUNAAMBIWA HAKUNA MIKUTANO ILI KUIMARISHA ZAIDI UPINZANI? MBONA KUNA MKAKAKATI WA KUIVURGA CUF ILI KULETA UHAFIFU WA UPINZANI?Mkaachaga unafiki nyie watu,kama mnaona hatuna wapinzani Tanzania sasa mbona kila kukicha mnawadhibiti na kuwatungia makosa yasiyo na maana wewe sema Tanzania hatuna chama Tawala chama chetu ni polisi utaeleka sio unaonge pumba hapa
Siwezi Jenga hoja kwa mabandiko yako yako coz inaonekana uwezo wako wa kufikiri ni Mdogo mno, ila naomba ujifunze kwa wasira alitokea wapi mpaka ccm wakampokea, na wakampa nafc gan kwenye serkali na ndani ya chamaImekugonga,ndio maana unaweweseka...jenga hoja na sio kubwabwaja.
Kupata au kutokupata haikuwa point yangu.mfano wako Wa Donald trump ni sahihi kabisa maana huto trump hapati urais Wa America