Kwanza nimewaomba wabunge wa CDM kwasababu nikiwaomba wale WAGONGA MEZA (WABUNGE WA CCM) hawataweza kuuliza hili swali kwasababu ya SERA ya chama chao KULINDANA.
Ninafahamu umuhimu wa kuendelea kuwahudumia viongozi wetu wakuu wa kitaifa hata baada ya kustaafu. Lakini pia ninataka kufahamu hii KEKI ya TAIFA tunaigawaje kama TAIFA.Isisje ikawa tunawahudumia hao viongozi wakuu wastaafu at the expense of common Tanzanians like me.
Ninafahamu katiba yetu imeruhusu viongozi wote wakuu wa mihimili ya DOLA, yaani SERIKALI, BUNGE na MAHAKAMA waendelee kuhudumiwa na serikali hata baada ya kustaafu. Wanalipwa mishahara posho za wafanyakazi wa ndani, madereva, walinzi ete. Katiba ilikuwa inasema viongozi wastaafu wataendelea kuhudumiwa na serikali hadi watakapofariki. Lakini baada ya Sophia Simba kutembelea familia ya marehemu Sokoine (baada ya JK kuingia madarakani) na kukuta mjane wa Sokoine anaishi maisha ya shida iliamuliwa, kwamba mjane wa kiongozi wa kitaifa aendelea kuhudumiwa na serikali kama alivyokuwa akihudumiwa marehemu mme wake.
Viongozi wakuu wastaafu wanaopaswa kuendelea kuhudumiwa na serikali kwa mjibu wa katiba yetu hata baada ya kustaafu ni RAIS, VP, WAZIRI MKUU, SPIKA WA BUNGE na JUDGE MKUU.
Ninaloomba wabunge wa CDM wanisadie ni kuuliza ktk bunge lijalo, Je ni kiasi gani cha pesa kwa mwezi serikali inatumia kuwahudumia hao viongozi wastaafu ili na sisi walalahoi walipa kodi tufahamu jinsi kodi yetu inavyotumika kuwahudumia hao waheshimiwa na familia zao. WABUNGE WA CDM PLEASE. Habari nilizonazo ni kwamba, sasa hivi imekuwa mzigo mkubwa kwa serikali kuwahudumia hao viongozi wakuu wastaafu (HAI na MAREHEMU). Kwa kumbukumbu zangu ndogo nitawa orodhesha hapa ili muona ni kiasi gain tulivyokuwa na mlolongo mrefu wa wastafu hao, naomba wana JF mnisadie wale nitakaokuwa nimewasahau.
SERIKALI
- Julius Kambarage Nyerere (Rais)
- Ali Hassan Mwinyi (Rais)
- Benjamin William Mkapa (Rais)
- Abeid Amani Karume (VP)
- Aboud Jumbe Mwinyi (VP)
- Abdul Wakili Juma (VP)
- Omari Ali Juma (VP)
- Rashid Mfaume Kawawa (PM)
- Edward Moringe Sokoine (PM)
- Cleopa David Msuya (PM)
- John Samuel Malecela (PM)
- Salim Ahmed Salim (PM)
- Joseph Sinde Warioba (PM)
- Edward Ngoyayi Lowasa (PM)
- Frederick Tuluway Sumaye (PM)
BUNGE (Spika)
- Adamu Sapi Mkwawa
- Pius Msekwa
- Samuel Sitta
MAHAKAMA (CJs)
- Francis Nyalali
- Augustino Ramadhani
Ninafahamu pia ma CDF (Chief of Defense Force) nao wana hudumiwa na serikali hata baada ya kustaafu, ulinzi, mishahara, posho watumishi wa ndani, gari na mafuta etc kama hao wa kitaifa (ingawa sina uhakika kama wao wanatambuliwa na katiba). Bahati mbaya siwafahamu wote lakini nitataja wale ninaowafahamu
CDFs
- Abdallah Twalipo
- David Msuguri
- Marwa
- Waitara
- Mboma
Wengine wamenitoka. Ninaomba wabunge wa CDM. Please, Zitto, Mnyika, Regia, Lema, Wenje etc WALE WA MAGAMBA siwataji, Je serikali inatumia kiasi gani cha pesa kwa mwezi kuwahudumia hawa viongozi wakuu wastaafu wa kitaifa kwa mwezi? Je, mchanganuo wa kila mmoja eg RAIS, VP, PM, SPIKA, CJ na CDF ni Tsh ngapi kwa mwezi? Je, huu utaratibu utakuwa na ukomo? Becuase I'm afraid itafikia mahala watakuwa wengi kiasi serikari itakosa uwezo wa kuwahudumia. Hesabu zangu za haraka mpaka hadi hii leo 2011, tunao
25. JK naye 2015 ataondoka na kundi lake idadi itazidi kuongozeka. Mwisho jamani haya ni mambo MUHIMU ambayo inabidi yaelezwe vizuri kwenye katiba mpya.
Naomba kuwakilisha wabunge wa CDM