Wabunge chadema tusaidieni: Serikali kugharamia viongozi wa kitaifa wastaafu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge chadema tusaidieni: Serikali kugharamia viongozi wa kitaifa wastaafu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bobuk, May 31, 2011.

 1. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Kwanza nimewaomba wabunge wa CDM kwasababu nikiwaomba wale WAGONGA MEZA (WABUNGE WA CCM) hawataweza kuuliza hili swali kwasababu ya SERA ya chama chao KULINDANA.

  Ninafahamu umuhimu wa kuendelea kuwahudumia viongozi wetu wakuu wa kitaifa hata baada ya kustaafu. Lakini pia ninataka kufahamu hii KEKI ya TAIFA tunaigawaje kama TAIFA.Isisje ikawa tunawahudumia hao viongozi wakuu wastaafu at the expense of common Tanzanians like me.

  Ninafahamu katiba yetu imeruhusu viongozi wote wakuu wa mihimili ya DOLA, yaani SERIKALI, BUNGE na MAHAKAMA waendelee kuhudumiwa na serikali hata baada ya kustaafu. Wanalipwa mishahara posho za wafanyakazi wa ndani, madereva, walinzi ete. Katiba ilikuwa inasema viongozi wastaafu wataendelea kuhudumiwa na serikali hadi watakapofariki. Lakini baada ya Sophia Simba kutembelea familia ya marehemu Sokoine (baada ya JK kuingia madarakani) na kukuta mjane wa Sokoine anaishi maisha ya shida iliamuliwa, kwamba mjane wa kiongozi wa kitaifa aendelea kuhudumiwa na serikali kama alivyokuwa akihudumiwa marehemu mme wake.

  Viongozi wakuu wastaafu wanaopaswa kuendelea kuhudumiwa na serikali kwa mjibu wa katiba yetu hata baada ya kustaafu ni RAIS, VP, WAZIRI MKUU, SPIKA WA BUNGE na JUDGE MKUU.

  Ninaloomba wabunge wa CDM wanisadie ni kuuliza ktk bunge lijalo, Je ni kiasi gani cha pesa kwa mwezi serikali inatumia kuwahudumia hao viongozi wastaafu ili na sisi walalahoi walipa kodi tufahamu jinsi kodi yetu inavyotumika kuwahudumia hao waheshimiwa na familia zao. WABUNGE WA CDM PLEASE. Habari nilizonazo ni kwamba, sasa hivi imekuwa mzigo mkubwa kwa serikali kuwahudumia hao viongozi wakuu wastaafu (HAI na MAREHEMU). Kwa kumbukumbu zangu ndogo nitawa orodhesha hapa ili muona ni kiasi gain tulivyokuwa na mlolongo mrefu wa wastafu hao, naomba wana JF mnisadie wale nitakaokuwa nimewasahau.

  SERIKALI

  1. Julius Kambarage Nyerere (Rais)
  2. Ali Hassan Mwinyi (Rais)
  3. Benjamin William Mkapa (Rais)
  4. Abeid Amani Karume (VP)
  5. Aboud Jumbe Mwinyi (VP)
  6. Abdul Wakili Juma (VP)
  7. Omari Ali Juma (VP)
  8. Rashid Mfaume Kawawa (PM)
  9. Edward Moringe Sokoine (PM)
  10. Cleopa David Msuya (PM)
  11. John Samuel Malecela (PM)
  12. Salim Ahmed Salim (PM)
  13. Joseph Sinde Warioba (PM)
  14. Edward Ngoyayi Lowasa (PM)
  15. Frederick Tuluway Sumaye (PM)
  BUNGE (Spika)

  1. Adamu Sapi Mkwawa
  2. Pius Msekwa
  3. Samuel Sitta
  MAHAKAMA (CJs)

  1. Francis Nyalali
  2. Augustino Ramadhani
  Ninafahamu pia ma CDF (Chief of Defense Force) nao wana hudumiwa na serikali hata baada ya kustaafu, ulinzi, mishahara, posho watumishi wa ndani, gari na mafuta etc kama hao wa kitaifa (ingawa sina uhakika kama wao wanatambuliwa na katiba). Bahati mbaya siwafahamu wote lakini nitataja wale ninaowafahamu

  CDFs

  1. Abdallah Twalipo
  2. David Msuguri
  3. Marwa
  4. Waitara
  5. Mboma
  Wengine wamenitoka. Ninaomba wabunge wa CDM. Please, Zitto, Mnyika, Regia, Lema, Wenje etc WALE WA MAGAMBA siwataji, Je serikali inatumia kiasi gani cha pesa kwa mwezi kuwahudumia hawa viongozi wakuu wastaafu wa kitaifa kwa mwezi? Je, mchanganuo wa kila mmoja eg RAIS, VP, PM, SPIKA, CJ na CDF ni Tsh ngapi kwa mwezi? Je, huu utaratibu utakuwa na ukomo? Becuase I'm afraid itafikia mahala watakuwa wengi kiasi serikari itakosa uwezo wa kuwahudumia. Hesabu zangu za haraka mpaka hadi hii leo 2011, tunao 25. JK naye 2015 ataondoka na kundi lake idadi itazidi kuongozeka. Mwisho jamani haya ni mambo MUHIMU ambayo inabidi yaelezwe vizuri kwenye katiba mpya.

  Naomba kuwakilisha wabunge wa CDM
   
 2. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  .tuwatose tu kwani hawakuwa na pensheni?
  mizigo mingine ni yakujitakia wengine ni vibaka tuwateme wote isipokuwa marais
   
 3. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Lowasa nae yumo
   
 4. t

  think BIG JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2011
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 236
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  listi ya wastaafu wanaolipwa baada ya kustaafu ni wengi. Kwenye listi yako ongeza:
  (1) ma-meja jenerali na ma-jenerali wote wastaafu
  (2) ma-jaji wastaafu wote

  Hawa hulipwa ulinzi, mishahara, watumishi wa ndani, gari, mafuta ya gari pamoja na matengenezo ya gari.


  Mungu ibariki Tanzania.
   
 5. p

  pointers JF-Expert Member

  #5
  May 31, 2011
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  hii ndo nchi ya wadanganyika, hiyo hoja ni lazima itapingwa vilivyo na watu wa CCM........
   
 6. fige

  fige JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli mkuu hapo una hoja hasa kwa mfano kiongozi kastaafu kama seif au Lowasa analipwa kama mstaafu na wakati huohuo ni m/raisi au ni mbunge.

  Inabidi tujue watu kama hawa wanalipwa nini.

  Lakini ni muhimu kuangalia mafao ya wastaafu wetu wote sio viongozi peke yao kwa umakini mkubwa, kwa sababu kama mafao au pensheni itakuwa ndogo inaweza sababisha ufisadi kwa hofu ya maisha baada ya kazi.

  Nachelea kusema si watu wote wamekuwa mafisadi kwa kupenda,bali hata mishahara wanayopata na pensheni zao
  Zinasababisha kuingia kwenye mkumbo.
   
 7. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280

  Mkuu watu hawa wana mishahara na marupurupu mengi sana ambayo mengine hayakatwi hata kodi na kumbuka baadhi yao hawa mishahara na marupurupu yao yanatoka kweney mfuko mkuu wa hazina (consolidated fund) ambapo huwa hayakatwi kodi
  Tukisema watu kama hawa wataingia kweney ufisadi ni kama tunakosea mkuu maana kwako mishahara na marupurupu ni makubwa na hata hizo pension zao ni kubwa sana
   
 8. God bell

  God bell JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2011
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 581
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Hata wale mafisadi papa watakaoondoka na JK muda wake ukiisha watapewa hiyo mihela na posho kwa muda wa maisha yao yote? Hivi inawezekana uchote maji kwene mfereji uyamwage mtoni?
   
 9. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #9
  May 31, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Atleast basi wangefanya hivi

  Ile siku ya saba saba kila mkoa ukatoa jina la mkulima bora wa mwaka naye angeluwa analipiwa Pnesheni tena ya kawada ya mfanyakaziw a kima cha kati na serikali.

  I meana kila mwaka mkulima 1ja kwenye kla mkoa hata kila wilaya anaingiziwa kupewa japo penshion ya laki kila mwezi. Maabo kama haya ndo yanaonesyha kweli tuko serius na ilimo kwanza.

  I Always wonder taifa hili linawafanyia nini wakulima zaidi ya kuwakamua tu.

  Anyway nimetoka nje ya mada but nahani itakuwa vizuri CCM wamrudishe MKapa may be hata wakichakachua mwaka 2015 basi tutakuwa hatuna hasara sana kwenye Taifa kuhudumia msururu wa viongozi.
   
 10. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #10
  May 31, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Tumekwisha! Hapo bado wachakachuaji wa matumizi ya serikali. Kweli hapa mtanzania wa kawaida atakuwa na uwezo wa kusomesha mtoto wake?
   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  May 31, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Aliyeibua hoja hii ni nzuri, ila ninachoweza kuongezea ni kwamba utaratibu wa ulipwaji wa mafao yao uwe utaratibu ule ule kwa wafanyakazi wengine waliokatwa mafao ya uzeeni wakati wanafanya kazi. Utaratibu wa sasa hauwasaidii na kwa upande fulani wananyonywa au kupunjwa haki zao.

  Wafanyakazi wastaafu wasipewe mafao ya uzeeni yote kwa wakati mmoja kwa mkupuo, bali, wapewe kila mwezi hadi watakapokufa ili wawe na uhakika wa kupata pesa ingawa kidogo kila mwezi. Hii ni kutokana na kwamba pesa wanayokatwa wanapofanya kazi huwekezwa katika rasilimali mbalimbali na huzalisha. Mfano wanaofanya hivyo ni Taasisi ya Social Security ya Marekani, mtu akishaikisha umri wa miaka kati ya 62 early retirement na 71 maximum retirement. Mtu anakuwa na hakika ya kupata kiasi fulani cha pesa kila mwezi. Kupata zote kwa mkupuo ni vigumu kwa wengi kupanga bajeti ya pesa hizo hadi watakapokufa.
   
 12. p

  politiki JF-Expert Member

  #12
  May 31, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  kuna haja ya kuwalipa lumpsum payment moja ya nguvu wakati wa kustaafu kwake ili aweze kujiajili kwenye shughuli za mashamba au biashara na kutoa ajira kwa watu huku naye akiendelea kula pesa yake kulingana na namna hatakavyoitumia pesa yake au pia anaweza kuweka benki akawa anakula interest kila mwezi yeye na familia yake. nchi yetu ni maskini sana hatuwezi kuendelea na mfumo huu wa OPEN ENDED COMITTMENT halafu wakati huohuo tukaendelea kuhudumia nchi kuna haja ya kutafuta njia mbadala ya kuwafanya wahusika hawa wakaweza kujitegemea badala ya kutegemea seriakali for the rest of their lives that is impossible. hili swala inabidi liwekwe wazi kwa wale wote wanaotaka kugombea urais na nafasi zote zilizoelezwa hapo juu hili wahusika wajue kabla hawajachukua hiyo kazi.
   
 13. U

  Utatu JF-Expert Member

  #13
  May 31, 2011
  Joined: Dec 31, 2008
  Messages: 436
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 60
  Huyu Lowassa kaiibia nchi halafu, yeye ni mstaafu? Au ni Mwizi? Acha kuendelea KUNYONYA wa Tanzania wenzako!
   
 14. U

  Utatu JF-Expert Member

  #14
  May 31, 2011
  Joined: Dec 31, 2008
  Messages: 436
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 60
  Kwa manufaa ya UMMA.

  Kwanza wanalipwa kiasi gani? DATA Tafadhali......ni haki ya Wananchi na walipa kodi kujua.
   
 15. U

  Unstoppable JF-Expert Member

  #15
  May 31, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,049
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  By the way kwanini Lowassa aitwe mstaafu? Ina maana na mawaziri wote waliokumbwa na scandal nao ni wastaafu?
   
 16. U

  Unstoppable JF-Expert Member

  #16
  May 31, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,049
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Alafu anasemekana ni mzalendo, mchapakazi ambaye akipitishwa kugombea uraisi ana- support ndani ya chama. Hapa kwakweli kazi ipo.
   
 17. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #17
  May 31, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hii ni hoja nzito na nzuri sana japo naona uliowaomba bado hawajaingia kutoa neno
  ngoja tuone labda wanajipanga
   
 18. U

  Unstoppable JF-Expert Member

  #18
  May 31, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,049
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hapana mkuu, si sahihi kuwaita mafisadi hata kidogo. Sheria zilizotungwa na wabunge "tuliowachagua" ndio zinazowalinda. Hatuwezi tukazikubali/tumia sheria kwenye mambo fulani lakini tukazikataa kienyeji kwenye certain issues. Inatakiwa pale sheria kama hizo zikipitishwa tuzisimamie kidete wakati ule ule. However it is not too late naamini tunaweza kupigania mabadiliko ya hizi sheria mfano: kuna baadhi ya position zilizotajwa wastaafu wanalipwa kuliko mtu mwenye nafasi hiyo hiyo aliyeko kazini i.e. Augustino Ramadhani is getting paid/has more benefits than Othman Chande. Sasa sijui vigezo ni nini hasa.
   
 19. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #19
  May 31, 2011
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,522
  Likes Received: 2,108
  Trophy Points: 280
  Jibu ni kuongeza umri wa kustaafu kwa lazima kwa viongozi wa majeshi ya ulinzi na usalama kuwa miaka 70 labda tu pale afya inapolazimisha astaafu mapema na baada ya kustaafu watunzwe mpaka kufa:
  • Mkuu wa JWTZ na majenerali wake umri miaka 70 kustaafu
  • Mkuu wa Polisi IGP na makamishna wake umri miaka 70 kustaafu
  • Mkuu wa Usalama wa Taifa na Wakurugenzi wake umri miaka 70 kustaafu
  • Mkuu wa Magereza na makamishna wake umri wakustaafu miaka 70.
  • Mwendesha mashitaka mkuu wa serikali miaka 70.
  Kuhusu majaji wakuu, majaji wa mahakama kuu na rufani
  • Hawa inasemekana wanapata hekima zaidi umri unavyokuwa mkubwa basi kustaafu kwa hiyari iwe miaka 71 na kwa lazima iwe miaka 80 labda afya iwe mgogoro na wakistaafu watunzwe mpaka kufa.
  Wale wa nyadhifa za kisiasa kama Marais, makamu wa Rais, Mawaziri Wakuu na Spika (Kutokana na vyama) wao lazima kuwawekea fixed term sije wakachakachua demokrasia kwa kukaa madarakani bila mbanno wa mihula ya kiuongozi na Waendelee kutunzwa mpaka kufa sije wakawa mafisadi kwa kupora mali za umma.

  Pia kwa wale viongozi wa nyadhifa za ulinzi na usalama waendelee kutunzwa mpaka kufa iliwawe huru na kutofikiria kujiingiza ktk siasa kwa kupindua nchi au kufuata amri potofu za viongozi wa kisiasa.

  Watumishi wa juu wa umma wakistaafu ktk umri mkubwa gharama nzima za kuwatunza zitapungua kwani kundi la watakaobakia hai kwa muda mrefu litapungua ( fikiria jaji kustaafu miaka 80 au jenerali/kamishna wa polisi miaka 70) na pia kuongeza ufanisi kwa kutumia hekima zao.
   
 20. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #20
  May 31, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Hoja hii ni muhimu ijadiliwe kwa kina kwani mzigo wa hawa wastaafu unazidi kuwa mzito kwa taifa; ni wakati muafaka sheria ya mafao ya viongozi ikaangaliwa upya iendane na wakati tulionao kwani it is not cast in stone!! Ile sheria ina mapungufu mengi kwa mfano kwanini kiongozi aliyeondoka madarakani kwa kashfa apewe pension wakati mfanyakazi wa serikali aliyeondoka kazini kwa kashfa hunyimwa pension yake?
   
Loading...