Wabunge chadema tusaidieni: Serikali kugharamia viongozi wa kitaifa wastaafu

Ndugu wana JF

Nimefurahia mrejesho wenu. Lakini kuna mambo hapa tuna confuse. Sitaongelea wakuu wa majeshi because I'm not conversant with it. Nitaongelea hawa wakuu wa mihimili ya dola, yaani SERIKALI, BUNGE na MAHAKAMA. Katiba yetu (sijui ibara ya ngapi) inasema kwamba ukiwa hata kwa siku MOJA RAIS, VP, PM, SPIKA au CJ basi serikali ita kuhudumia mshahara, posho na marupurupu mengine hadi mwisho wa uhai wako.

But very controversial mwanzoni mwa utawala wa JK, Sophia Simba baada ya kutembelea familia ya marehemu Sokoine sheria hiyo ikabadilishwa tena na kusema kwamba wajane wa viongozi wa kitaifa pia wataendelea kuhudumiwa na serikali, kama walivyokuwa wanahudumiwa waume zao wakati wa uhai wao.

Ni kwamba hawa viongozi wa kitaifa sio kwamba hawapati pension kama watumishi wengine. Wakistaafu wanapata pensheni kama watumishi wengine. Bahati nzuri wao siku hizi wako PSPF. Hivyo mafao yao wanapata kutoka katika mfuko huo, kulingana na sheria za mfuko huo.

Lakini on top of that ya hiyo pension, bado serikali inaendelea kuwapatia mishahara, posho za walinzi, wafanyakazi wa ndani, matibabu, gari na mafuta yake nk.

Nakumbuka wakati wa utawala wa Mkapa Alhaji Mwinyi aliwahi kucheleweshewa hayo malipo na ilizuwa mtafaruku mkubwa. Magazeti yalilipoti.

Sasa swali langu je serikali itaendelea kuwahudumia hao waheshimiwa wastaafu na familia zao (wajane)hadi lini, taking into consideration kwamba idadi yao inazidi kuwa kubwa miaka inavyoongezeka?.

Kwanini labda serikali isipunguze idadi yao mathalani tukasema kwamba seriklia itawahudumia RAIS, SPIKA na CJs tu. Wegine wategemea pension zao kama wafanyakazi wengine?.

Na hapo ndio kilio cha wafanyakazi kuhusu malipo ya uzeeni kitakaposikilizwa maana sasa hawa vingunge wakianza kuonja joto ya jiwe watakapopokea ka-pension kiduchu ambako ndiko hako hako, bila kutegemea msaada wa serikali, basi serikali italazimia ku-review malipo ya pension.

Jamani mizigo mingine serikali inajitakia, na mambo haya yote yanaweza kuwa solved na KATIBA MPYA na wala sio CCM au CDM!
 
Back
Top Bottom