Wabunge CHADEMA, Posho mliyoikataa, mnaifanyia nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge CHADEMA, Posho mliyoikataa, mnaifanyia nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jumakidogo, Dec 3, 2011.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Dec 3, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kwa bahati nimeamua kuwa siyo mwanachama wa chama chochote cha siasa bali ni shabiki wa siasa na baadhi ya wanasiasa. Mfano halisi wanasiasa ninao wakubali bila kujali itikadi zao ni Mbowe, Slaa, Mnyika, Lissu, Magufuli, Lowassa nk. Napata fursa ya kuwa makini na kauli za wanasiasa wa nchi hii bila kujali chama atokacho. Wabunge wa CDM Wamekuwa na msimamo wa kutopokea posho zao katika vikao vya bunge. Msimamo ambao wananchi tulio wengi tunauunga mkono mia kwa mia. Lakini utaratibu wa malipo ya posho hizo ni halali kwa mujibu wa kanuni za bunge. Na bahati mbaya hawapewi mkononi hivyo huingizwa moja kwa moja kwenye akaunti zao. Kwa maana ya kwamba watake watapata, wasitake watapata. Ule msimamo wa dhati upo kweli? Manake sijasikia tena wakija na mpango hasi kuhusu posho hizo kuwa, kwa sababu tulizikataa lakini mnatulazimisha. Tunaziingiza katika mradi fulani wa wananchi. Vinginevyo tunarudi kulekule kuwa. Kauli zitokazo midomoni mwa wanasiasa ni tamu masikioni mwa wananchi, lakini kuna dhamira tofauti katika mioyo yao.
   
 2. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #2
  Dec 3, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu pesa ni sabuni ya roho!
   
 3. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #3
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  kama wanalazimishwa kupokea unataka wafanyeje? mi nadhani kitendo chao cha kupinga hizo posho waziwazi kinatosha kuonyesha nia yao ya dhati ktk kupunguza matumizi serkali yasiyo na tija
   
 4. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #4
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hizo posho wazipeleke kwenye mifuko ya majimbo yao!
   
 5. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #5
  Dec 3, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu, wewe ukilazimishwa kuuwa utauwa?
   
 6. R CHUGGA

  R CHUGGA Senior Member

  #6
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 28, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tatizo hamna kiongozi yeyote aliyetoa maelezo yanayoeleweka kuhusu mgomo wa hizo posho.Wananchi tunashindwa kuelewa msimamo wao ni upi katika posho hizo,na wengine ni lazima tuamini kuwa wanazipokea kwa kuwa hamna msimamo wowote uliotolewa!kwa maana hiyo inabaki kuwa ni sanaa tu ya wanasiasa kuwapumbaza wananchi.Kama kweli mna huruma na mtanzania anayeteseka na maisha magumu onyesheni kweli mna nia ya dhati katika hilo!
   
 7. Echolima

  Echolima JF-Expert Member

  #7
  Dec 3, 2011
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 3,169
  Likes Received: 531
  Trophy Points: 280
  Why swali hili ni kwa wabunge Wa CHADEMA tu and why not to Wabunge wengine????
   
 8. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #8
  Dec 3, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo ukilazimishwa kula haramu unakula?
   
 9. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #9
  Dec 3, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Limeulizwa kwa wale waliopinga na kuzikataa posho.
   
 10. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #10
  Dec 3, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Wote wale ni wanafiki walikuwa wanatafuta cheap popularity.
   
 11. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #11
  Dec 3, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,914
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  CHADEMA.......!
  sometimes huwa siwaelewi,
  Bado nawamaind kukubali kufikia makubaliano na JK halafu wanakuja kutulilia kwamba Rais aliwachuuza..!
  Hili la posho usishangae wakija na kauli kuwa hawakuwa na namna ya kukataa manake walilazimishwa kuzipokea...!
   
 12. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #12
  Dec 3, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Eti Siasa maana yake si haswa!!
   
 13. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #13
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kama utatumia nguvu kunishikisha trigger ya bunduki na kisha ukatumia nguvu kunivutisha hiyo trigger na risasi ikafyatuka mimi nitakuwa na kosa gani? we unaambiwa hizo posho huwa zinatangulia wiki moja kabla hata ya kuanza kikao na zinaingia kwenye akaunti moja kwa moja unategemea watazizuiaje?
   
 14. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #14
  Dec 3, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  umesema akilazimishwa eeeh? NDIYO AKILAZIMISHWA NI LAZIMA AUE!
   
 15. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #15
  Dec 3, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  wamezikataa na wamesema waziwazi kuwa hawazitaki lakini zinawekwa kwenye akaunt zao kwanguvu niambie wafanyaje??
   
 16. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #16
  Dec 3, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,820
  Trophy Points: 280
  Huyu naye ni mnafiki? He is refusing to accept this allowance in order to gain cheap popularity for 2015!?

  ~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*

  Makamba ashtushwa
  Mbunge wa Bumbuli, January Makamba, alieleza kushangazwa na ongezeko hilo la ghafla akisema kamwe wabunge wasifikiri kuwa wanaweza kumaliza matatizo yao au ya wapigakura wao kwa fedha ya posho.
  Alisema kitendo cha wabunge kuongezewa posho za vikao kwa asilimia 185.7, kinaleta jazba kwa wananchi ambao wanahangaika kila kukicha kwa ugumu wa maisha.

  "Kwenye jamii lazima kuwe na usawa, kama watu tupo kwenye hali mbaya (ugumu wa maisha) lazima wote tuenende sawa. Wabunge kuongezewa posho kwa asilimia 185 siyo sawa kabisa, tunajiweka mbali na wananchi na wanatuona tunafaidika sana wakati wao wanateseka kwa ugumu wa maisha," alisema Makamba.

  Alisema kuwa, kutokana na msimamo wake huo, Juni mwaka huu alikataa posho iliyotolewa na Wizara ya Nishati na Madini baada ya kuhudhuria semina iliyoandaliwa na wizara hiyo.

  "Tulikaa kwenye semina kwa saa mbili, tunamaliza naletewa karatasi nisaini posho ya Sh280,000. Nilikataa. Nilikataa kwa sababu nilitambua kuwa ile ni kazi yangu kama mbunge, sasa unanilipa hela ya kazi gani?" alihoji Makamba.

  Habari hii imeandaliwa na Fredy Azzah, Frederick Katulanda, Mwanza, Patricia Kimelemeta, Fidelis Butahe na Ellen Manyangu

  SOURCE: Mwananchi.


   
 17. babad

  babad Member

  #17
  Dec 3, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bora wazichukue tu la sivyo wanazila wazee wa magamba for Nothing
   
 18. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #18
  Dec 3, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Sasa mbona wakizikuta wanakaa kimya? Hawasemi wanazitumia vipi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wao.
   
 19. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #19
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Wengine sisi ni kama wachina kila kitu tunapeleka pwani hivyo hakuna haramu
   
 20. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #20
  Dec 3, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Wazipeleke majimboni mwao wakawanunulie vikongwe ubwabwa huko.
   
Loading...