Wabunge CCM wawafunga goli CHADEMA, Sendeka amzidi kete Mnyika

Wabunge wa CCM jana walifanikiwa kuzinduka na kuwazidi kete wa CHADEMA dakika ya mwisho. Hali hiyo ilitokea wakati wa kupitishwa kwa muswada wa sheria ya fedha haramu. Aliyeokoa jahazi ni kada mpambanaji wa ufisadi Sendeka. Kamanda Sendeka alifanikiwa kabla bunge kuahirishwa mpaka jumatatu kutaka muongozo wa Spika na kumweleza mwenyekiti wa Bunge Mh. Mabumba kuwa alikosea kuhoji 'kifungu kimepita pamoja na marekebisho yake?", hali ambayo iliwafanya wabunge wa CCM kujibu "NDIOOOO" kwa sauti kubwa na hivyo kujikuta wamepitisha marekebisho yaliyowasilishwa na kijana wa Ubungo John Mnyika ambayo yalitaka adhabu ya makosa ya fedha haramu pamoja na kifungo kuongezwa kuwa pia na adhabu ya mali au fedha zilizohusika kuchukuliwa kama sehemu ya adhabu.

Kiongozi wa bunge alisema kwamba yeye sio malaika hivyo anamuomba Mungu amsamehe kwa kuhoji hivyo hali iliyofanya wabunge wa CCM wakosee na kuitikia ndio pamoja na wenzao wa CHADEMA na hivyo kufanya kifungu hicho kupitishwa wakati bunge lilipokaa kama kamati. Kutokana na hali hiyo alisema kwamba maneno "pamoja na marekebisho yake' yafutwe kwenye hansard ili marekebisho ya Mnyika yasiingizwe katika sheria.

Awali baada ya kifungu hicho kupitishwa wabunge wa CHADEMA walianza kushangilia hali ambayo iliwagutua wabunge wa CCM kuwa walikosea kusema ndio. Kutokana na hali hiyo Mwanasheria Mkuu wa Zamani Mtaalamu Andrew Chenge alikwenda kwa mwanasheria mkuu wa sasa Jaji Werema, akiwa na mazungumzo naye mwanasheria wa sasa alitaka mwenyekiti ampe nafasi Sendeka ili aweze kuzungumza.

Hata hivyo mwenyekiti hakumpa nafasi hiyo awali, bunge likamaliza kukaa kama kamati muswada ukapitishwa mara ya pili, na mara ya tatu na hatua zake zote na hivyo Mabumba kutangaza kwamba ni muswada halali uliopitishwa na bunge pamoja na marekebisho yake.

Kauli hiyo ilifanya wabunge wa upinzani wakiongozwa na CHADEMA kumshangilia kwa sauti kubwa na mwenyekiti huyo akawatakia weekend njema wabunge. Kabla ya kutangaza kikao kimeahirishwa Sendeka na Werema wakata tena kuzungumza ndio kamanda alipofanikiwa kusawazisha bao katika dakika za mwisho.

Sendeka alisema kwamba bunge haliwezi kutunga sheria yenye adhabu kali inayopingana na penal code kama alivyosema mwanasheria mkuu wa serikali. Katika utetezi wake juu ya sheria kuongezewa adhabu kijana Mnyika alidai kuwa adhabu ya miaka mitatu kwa fedha haramu ni chache na penal code haiwezi kuwa kizuizi kwa kuwa haikuwa kizuizi wakati Mwanasheria Mkuu wa Serikali alipolazimisha kifungo cha watoa maoni au elimu ya katiba kuwa miaka saba jela. Hata hivyo Mwanasheria Mkuu alidai kwamba katiba ni suala la muhimu hivyo ni lazima kuweka kifungo kikali zaidi hivyo fedha haramu zizichanganywe na katiba. Kutokana na maelezo hayo, Werema akasema kifungu kipite bila marekebisho. Mwenyekiti akahoji wabunge huwa kifungu kipite pamoja na marekebisho nao bila kujua wakaitikia NDIO kabla ya Kamanda Sendeka kuokoa jahazi.

....ndiyohiyo

ndugu yangu unaniuangusha......yaani pamoja na kuwa seasoned JF member (2008) kweli hujaweza kujifunza kutoka kwa mwagwiji humu jamvinini ku-tap namna nzuri ya ku-present mada?
 
sasa magoli gani waloyafunga? Wakati kilichotokea ni ubabe wa mwenyekiti kutomruhusu olesendeka kuzungumza aliposimama mara ya kwanza. Hata alipofuta,alifuta kienyeji!
 
ndugu yangu unaniuangusha......yaani pamoja na kuwa seasoned JF member (2008) kweli hujaweza kujifunza kutoka kwa mwagwiji humu jamvinini ku-tap namna nzuri ya ku-present mada?
hawezi kujifunza huyo na ushahidi kwamba hawezi ni maada aliyo toa kuanzia kwenye title inamuonesha jinsi gani alivo kichwani, msaada wangu kwake nitamuombeatu a evolve +Vely lakini
 
hawa wabunge wetu wamefundishwa jibu moja ktk chama tawala,kwamba wasipinge ndo maana wanaijua ndioo!hawajali maslahi,hata sendeka ana matatizo ya akili anapinga adhabu...au naye ndo kundi la watuhumiwa? bunge letu halina msaada tena...
 
Maelezo ya mtoa mada hayaendani na ukweli anaouelezea. Katika maelezo yake mengi inaonesha kuwa Mh. Mnyika ndiye mshindi hata kama amepokonywa ushindi baadaye. Iweje wabunge wa CCM waitikie katika kitu wasichofahamu wakati wale wa CDM wanajua wanaitikia ndiyo katika kitu wanachokifahamu. Basi ina maana kama Mh. Ole Sendeka alikuja kuzinduka baadaye wakati tayari wabunge wa CCM walishaitika ndiyo huku wenzao CDM wanajua wanalofanya, hilo bao la wabunge wa CCM liko wapi?
 
Tuliofungwa goli ni watanzania wote wanaoitakia mema nchi yao, lakini kama hao wanapatikana CDM tu, basi mwandishi atakuwa sahihi.

CCM wanatetea mafisadi na wale wanajihusisha na biashara ya fedha haramu wasiadhibiwe au wapewe adhabu Kidogo!!! CHADEMA wanatetea wananchi ili Mafisadi waadhibiwe halafu Masisiem wanashangilia eti wameshinda!!!! Sijui akili zao zimehamia wapi??
 
kweli nimeamini usingizi ni noma,zamani tukiwahi kulala kabla ya chakula mama alikuwa anatunawisha uso kwanza kabla ya kula nilipomuuliza ni kwa nini?aliniambia unaweza ukaweka chakula puani.

ccm kwishney.
 
Wabunge wa CCM jana walifanikiwa kuzinduka na kuwazidi kete wa CHADEMA dakika ya mwisho. Hali hiyo ilitokea wakati wa kupitishwa kwa muswada wa sheria ya fedha haramu. Aliyeokoa jahazi ni kada mpambanaji wa ufisadi Sendeka. Kamanda Sendeka alifanikiwa kabla bunge kuahirishwa mpaka jumatatu kutaka muongozo wa Spika na kumweleza mwenyekiti wa Bunge Mh. Mabumba kuwa alikosea kuhoji 'kifungu kimepita pamoja na marekebisho yake?", hali ambayo iliwafanya wabunge wa CCM kujibu "NDIOOOO" kwa sauti kubwa na hivyo kujikuta wamepitisha marekebisho yaliyowasilishwa na kijana wa Ubungo John Mnyika ambayo yalitaka adhabu ya makosa ya fedha haramu pamoja na kifungo kuongezwa kuwa pia na adhabu ya mali au fedha zilizohusika kuchukuliwa kama sehemu ya adhabu.

Kiongozi wa bunge alisema kwamba yeye sio malaika hivyo anamuomba Mungu amsamehe kwa kuhoji hivyo hali iliyofanya wabunge wa CCM wakosee na kuitikia ndio pamoja na wenzao wa CHADEMA na hivyo kufanya kifungu hicho kupitishwa wakati bunge lilipokaa kama kamati. Kutokana na hali hiyo alisema kwamba maneno "pamoja na marekebisho yake' yafutwe kwenye hansard ili marekebisho ya Mnyika yasiingizwe katika sheria.

Awali baada ya kifungu hicho kupitishwa wabunge wa CHADEMA walianza kushangilia hali ambayo iliwagutua wabunge wa CCM kuwa walikosea kusema ndio. Kutokana na hali hiyo Mwanasheria Mkuu wa Zamani Mtaalamu Andrew Chenge alikwenda kwa mwanasheria mkuu wa sasa Jaji Werema, akiwa na mazungumzo naye mwanasheria wa sasa alitaka mwenyekiti ampe nafasi Sendeka ili aweze kuzungumza.

Hata hivyo mwenyekiti hakumpa nafasi hiyo awali, bunge likamaliza kukaa kama kamati muswada ukapitishwa mara ya pili, na mara ya tatu na hatua zake zote na hivyo Mabumba kutangaza kwamba ni muswada halali uliopitishwa na bunge pamoja na marekebisho yake.

Kauli hiyo ilifanya wabunge wa upinzani wakiongozwa na CHADEMA kumshangilia kwa sauti kubwa na mwenyekiti huyo akawatakia weekend njema wabunge. Kabla ya kutangaza kikao kimeahirishwa Sendeka na Werema wakata tena kuzungumza ndio kamanda alipofanikiwa kusawazisha bao katika dakika za mwisho.

Sendeka alisema kwamba bunge haliwezi kutunga sheria yenye adhabu kali inayopingana na penal code kama alivyosema mwanasheria mkuu wa serikali. Katika utetezi wake juu ya sheria kuongezewa adhabu kijana Mnyika alidai kuwa adhabu ya miaka mitatu kwa fedha haramu ni chache na penal code haiwezi kuwa kizuizi kwa kuwa haikuwa kizuizi wakati Mwanasheria Mkuu wa Serikali alipolazimisha kifungo cha watoa maoni au elimu ya katiba kuwa miaka saba jela. Hata hivyo Mwanasheria Mkuu alidai kwamba katiba ni suala la muhimu hivyo ni lazima kuweka kifungo kikali zaidi hivyo fedha haramu zizichanganywe na katiba. Kutokana na maelezo hayo, Werema akasema kifungu kipite bila marekebisho. Mwenyekiti akahoji wabunge huwa kifungu kipite pamoja na marekebisho nao bila kujua wakaitikia NDIO kabla ya Kamanda Sendeka kuokoa jahazi.

....ndiyohiyo

Hongera mkuu kwa taarifa yako na kutoa sifa lukuki kwa huyo kamanda Mhe. Sendeka!!!???
Hivi mkuu, kwa akili zako timamu, na nadhani ni mtu ambaye umekwenda shule na kuelimika, unaelewa kitu kinachoitwa uchumi?
Kweli kwa akili iliyotulia na yenye uelewa japo kidogo, unaweza kushabikia adhabu ndogo kwa wanaotaka kuharibu uchumi wa nchi kwa hela haramu/chafu.

Au labda uelewa wako ni mdogo sana kujua hela haramu ni nini, na madhara yake ni yepi kwa uchumu wa nchi na ndiyo maana unashabikia?
Pole sana mkuu. Wakati mwingine mwulize jirani yako akupe ufafanuzi kwanza wa jambo usilolijua kabla ya kuleta mada za kujiaibisha ndani ya jukwaa kama hili la great thinkers.
Kaaaaazi kweli kweli, lakini Tz na wa-Tz watafika tu.
 
Kila siku tunaendelea kuwafahamu vema wale waliokua wanajiita makamanda wa kupambana na ufisadi akiwemo Sendeka! Uwongo wao ulisambaa haraka sana wakaonekana mashujaa fulani,sasa ukweli umeanza kutoka nje tumeanza wafahamu ni watu wa aina gani!
 
Maamuzi yako palepale maana mwenyekiti hakuhoji kwa mara nyingine,kwa hiyo maamuzi yako pale pale
 
Hakika Mrisho Wa hawa majuha umefika,unawezaje kushabikia upumbavu Kama huu? Ole Sendeka na co wote watatuonyesha rangi zao halisi, it's just a mater of time
 
Pingu ni pombe mbaya sana na hasa ukiinywa mapema na wewe ni tu wa bara maana hii ni pombe ya wavivu pwani .Ukisha inywa hata akili zako zinachoka kama zako sasa .Pole sana naona umechemka karibia unaiva .
 
Nilikuwa nasikia tu kuwa wabunge wengi wa tawala muda mwingi wanachapa usingizi. Aisee leo ndo nimeamini. Kwa hiyo tawala walisema ndiyo huku wakiwa hawajui maana yake? Unanikumbusha enzi za depo, tulifika tu tukaambiwa hapa kambini kila kitu ni ndiyo afande. Siku moja afande akaja parade amefura ile mbaya na mazungumzo yakawa kama ifuatavyo:
Afande: Mnanitania eeh?
Sisi : Ndiyo afande
afande: Mnasemaje? Mnanifanya mimi mjinga, si ndivyo?
Sisi : Ndiyo afande

unaonekana kama unawasifu tawala, maskini kumbe ndo unafichua ujuha wao! Pole sana. Tukiwaambia gwanda 1= tawala 50 mnabisha. Vijisen ti kwanini baada ya kubaini akamwambia sendeka, kwa nini asingesema yeye?
 
Hakika Mrisho Wa hawa majuha umefika,unawezaje kushabikia upumbavu Kama huu? Ole Sendeka na co wote watatuonyesha rangi zao halisi, it's just a mater of time
 
mgeni ...aamuzi yako palepale maana mwenyekiti hakuhoji kwa mara nyingine said:
ndugu apa umeleta point nzito,kwa kuwa mwenyekiti hakuwahoji wajumbe kwa mara ya pili,ina maana sheria imepitishwa kwa kura za awali ambapo wajumbe wengi walijibu ndiyo kukubali marekebisho...labda j3 wakihojiwa tena ili wakanushe,vinginevyo sendeka na mwenyekti hawawezi kubatilisha kura za wabunge...
 
Back
Top Bottom