Wabunge CCM wawafunga goli CHADEMA, Sendeka amzidi kete Mnyika

Wabunge CCM wawafunga goli CHADEMA, Sendeka amzidi kete Mnyika

umeandika na kufafanua vizuri sana mkuu habarindiyihiyo,achana nao,wajinga wanaotaka habari za kuwasifia na kuponda wenzao.Tumeshawazoea uwezo wao wa kupambana na hoja ni mdogo sana ndio maana hukimbilia katika kubeza na kukimbia hoja.Angalia ulichoandika na wanachochangia.Tatizo ni yale makovu ya uchaguzi mkuu 2010
 
Mkuu itakubidi ujibebe manake sijaona kitu hapa!!! Pamoja nakudonoadonoa muda mrefu hujatoka na kitu hapa!!!!
 
ndugu yangu unaniuangusha......yaani pamoja na kuwa seasoned JF member (2008) kweli hujaweza kujifunza kutoka kwa mwagwiji humu jamvinini ku-tap namna nzuri ya ku-present mada?
mbona ulichaandika ujaeleweka hoja yako unajichanganya
 
tulikwisha sema kuwa humo ndani ya magamba hakuna kitu,Mh Ole Sendeka naye ni wale wale tu.Hawezi kujitapa kuwa wamewazidi ujanja CDM huku akijifanya kiranja wa kupinga ufisadi.Huwezi pinga ufisadi wakati huo huo una pinga adhabu watakayopewa kama nawe si fisadi.Sana sana kinacho fanyika ni mchezo wa kuigiza.Unaimba kijamaa huku unacheza kibepari.Mh Tundu Lissu aliwahi kutabanaisha wakati anapinga makada wa chama kuingizwa katika tume ya maadili ya mahakama,kuwa wananchi wenyewe wanaona nani yupo kwa ajili ya wananchi na nani yupo kwaajili ya manufaa binafsi.Leo hii hujapita hata mwaka mafisadi wanazidi kujitambulisha. Najua kuwa JF itapigwa vita sana lakini ipo siku haki itajulikana ipo upande upi.Mungu siku zote huwa alifanikishi jambo mpaka wanafiki wote wajulikane.Leo wapambanaji wa ufisadi ndani ya CCM wameingia mkenge kwa kupinga adhabu iliyopendekezwa,kisa tu imependekezwa na mpinzani.Si Ole Sendeka pekee yake,bali hata kitendo cha mwenyekiti wa kamati iliyoteuliwa na bunge mheshimiwa Mkufunzi wa sheria wa chuo kikuu naye alisema kuna mengine wameyaweka chini ya kapeti,sisi tunasema hayo yaliyofichwa nayo ni ufisadi ule ule.Hakuwa na dhamira ya kweli, alichojali zaidi ni kukinusuru chama chao cha CCM. Kitendo cha aliyekuwa spika wa bunge kuizima skendo ya Richmond nacho ni ufisadi ndo maana naamini hakuna aliyemsafi ndani ya chama chao cha CCM.Mh M/kiti wa jumuiya ya wazazi alikwisha sema kuwa hakuna aliyemsafi ndani ya CCM isipokuwa wanazidiana kiufisadi,hakuna hata mmoja miongoni mwao aliyetoka na kukanusha kauli ile,Kwakuwa kipindi hicho ndiye aliyekuwa na dhamana ya usalama wa taifa pamoja na tume ya maadili ya utumishi wa umma.Ndo maana mpaka kesho ataendelea kuwatetea mapacha watatu kwa kujua kuwa kwenye msafara wa mamba na kenge nao wamo. Kitendo alichofanya mh huyo hakikuwa cha kizalendo hasa kwa nchi kama yetu iliyopoteza maadili ya utumishi wa umma,ilitakiwa ikithibitika kiongozi amehujumu uchumi wetu alitakiwa anyongwe hadharani kwa kukosa imani kwa wananchi wenziwe walio mpa dhamana.Maxmillan Bushoke aliwahi kuimba kama wote tungekuwa maofisa nani wangefanya kazi zingene!basi tuheshimu dhamana tuliyopewa kwani hayo yote ni mgawanyo wa madaraka
 
Kama ulifuatilia mjadala wa bunge wa jioni ya Ijumaa.. Hutakuwa na haj ya kuhoji uandishi wake...
 
Back
Top Bottom