Wabunge CCM wamsafisha Lowassa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge CCM wamsafisha Lowassa.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gumzo, Jul 27, 2012.

 1. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sakata hilo, lilibuka juzi usiku, katika kikao cha Wabunge wa CCM, ambacho kilikuwa kinajadili tatizo la umeme, hali iliyomfanya Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka (CCM), kuibuka na na hoja ya kutaka viongozi wa wizara hiyo wawajibishwe.
  Hoja ya Sendeka, ilimlenga Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi, wawajibishwe kwa kukiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma.

  Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya kikao hicho, kilisema kuwa hoja hiyo ya Ole Sendeka, ilionekana ni mwiba kwake, hali iliyomfanya Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM), kunyanyuka na kumuumbua ole Sendeka.

  Lugola, alisema alifuatwa na Ole Sendeka, huku akiahidi kumhonga fedha ili aweze kumuunga mkono hoja yake ya kutaka Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliachim Maswi, wawajibishwe na Bunge.

  "Hoja ya Ole Sendeka, ilimfanya Kangi Lugola kunyanyuka na kuanza kutoa maelezo ambayo kulikuwa na lengo la kutaka kukwamisha bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini. Alipinga wazi kuwawajibisha viongozi wa wizara hiyo, huku akifananisha kinachotaka kufanywa ni sawa na lililomtokea Lowasa.

  "Alisema katika ripoti ile ya kamati teule ya Bunge, ilipelekea kumwajibisha Lowassa na baada ya muda iligundulika ilijaa upotoshaji mwingi na kusisitiza katu wabunge hawapo tayari kurudia makosa ya mwaka 2008, ambapo vilitolewa vielelezo vya mitaani," alisema mtoa habari huyo.

  Baada ya maelezo ya Lugola, naye Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango (CCM), aliunga mkono hoja hiyo na kusema kuwa mwaka 2008, Bunge liliaminishwa Lowassa, alikuwa mhusika na Richmond, kutokana na jambo hilo kukosa ushahidi alitahadharisha kutorudiwa kwa makosa tena.

  "Kilango, alisema wabunge waliamini alikula fedha kwa kulipwa na Richmond, lakini hakuna ukweli, hivyo hakuna sababu ya kumwajibisha Waziri wa Nishati wala Katibu Mkuu wake.

  BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI GUMZO LA JIJI
   
 2. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Huyu ndie mshika bendera wao, lazima wamsafishe.
   
 3. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Kwa wabunge wa CCM is OK, hakuna atakaye ona ajabu! Lakini wajue LOWASA si msafi hata kidogo!
   
 4. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #4
  Jul 27, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Huyu babu ananafasi huko CDM ndio maana Zitto anapigwa vita.
   
 5. m

  mwamkata muhamad Member

  #5
  Jul 27, 2012
  Joined: Jul 27, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HATIMAYE wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wameibuka na kumsafisha Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, huku wakidai taarifa ya Kamati teule iliyokuwa ikiongozwa na Waziri wa sasa wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ilijaa upotoshaji.

  Yaani wanakumbuka shuka wakati kumekucha.
   
 6. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #6
  Jul 27, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  wamemsafishia wapi ? mtoni au baharini ?
   
 7. A

  Asa79 JF-Expert Member

  #7
  Jul 27, 2012
  Joined: Jul 19, 2012
  Messages: 591
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hee kweli ccm imefika mwisho km lowasa sio fisadi...........yaani watu watatu (lowasa,rostam na kikwet) walijiundia kampuni feki na kujichotea milioni 155 kila siku mnasema hakuhusika?........du!...hii nchi ukifikiria sana unaweza kuwa kichaa ni bora kuvuta unga uwe teja yaani usiwe na akili timamu
   
 8. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #8
  Jul 27, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,125
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Ubinafsi wa hao watu ndo unaoliangamiza taifa, lakini nafurahi kuwa wanazidi kujifuta kwenye mioyo ya Watanzania!!!!
   
 9. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #9
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Asafishiki x 1000
   
 10. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #10
  Jul 27, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Lowasa hasafishiki.
   
 11. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #11
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Wamegundua hakuwa na kosa kwasababu aliamlishwa na Dr Dr Dr Kikwete au bado sijaelewa..
   
 12. m

  mwamkata muhamad Member

  #12
  Jul 27, 2012
  Joined: Jul 27, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni ukweli uliyowazi kuwa kuondoka kwa Lowassa nchi imeshuhudia ombwe la utendaji kazi.Watanzania tuna tabia ya kusahau ya nyuma.Tukumbuke uwanja wa mnazi mmoja ulivyokuwa tayari umeuzwa kwa mwarabu, nani alichukua maamuzi magumu kuzuia na kuwaambia wananchi wachukue mabati yaliyokuwa yamezungushiwa.Nani alivunja mkataba mbovu wa dawasco.Nani alisimama kidete Umoja wa Mataifa kuhakikisha Tanzania inatumia maji ya Ziwa Viktoria, hadi Kenya, Uganda, Ethiopia nazo zinafuata mfano wa Tanzania, Shinyanga wanayaita maji ya Lowassa.Kwa dunia ya sasa, Tanzania inatakiwa kuongozwa na mijitu kama Lowassa haigopi kupitisha maamuzi
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Jul 27, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,606
  Likes Received: 82,206
  Trophy Points: 280
  Magamba wameangalia kundini hawaoni wa kumsimamisha 2015 sasa wanaanza rasmi kumsafisga fisadi kuelekea 2015 kwa matumaini kwamba ikifika 2015 atakuwa msafi sana tena ananukia manukato na akitumia mabilioni yake aliyoyapata kifisadi basi itakuwa rahisi kuchakachua uchaguzi na yeye kutinga Ikulu. Kweli magamba hawajali kabisa maslahi ya nchi bali yale ya chama chao.
   
 14. Ndukidi

  Ndukidi JF-Expert Member

  #14
  Jul 27, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 821
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 80
  BAK, let's be honest.. hivi unajua kuwa asilimia 99.98 ya Wabunge wa CCM ni wabunge wa matumbo yao.. wana uhakika mkubwa wa kutorudi bungeni, na mbaya zaidi ni pale CCM ikikosa urais, kutoka madarakani, wanajua hata hivyo walivyojilimbikizia vitakuwa mashakani, ni lazima sasa hivi watabadirika wote na kuwa pamoja, ili wamuweke mtu atakaye weza kuwahakikishia CCM wanabaki madarakani. Kazi kubwa watanzania tunayo kuondokana na hili kundi la wezi.
   
 15. samilakadunda

  samilakadunda JF-Expert Member

  #15
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 1,701
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  wamesha msafisha amesafishika?????????,mana uchafu alionao hata akichunwa ngozi yake bado atakuwa lowasa fisadi.
   
 16. k

  kimeloki JF-Expert Member

  #16
  Jul 27, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 1,927
  Likes Received: 950
  Trophy Points: 280
  tusubiri tuone
   
 17. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #17
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  zamani issue kama hii ungekuta anne kilango ni anaichachafya serikali lakini siku hizi kila hoja anaikubali sijui ni kanyamazishwa au na yeye yuko kwenye msururu wa hela za tanesco dah si mchezo
   
 18. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #18
  Jul 27, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hawa hakika wanapoteza muda wao. Wanachofanya ni sawa na kumfufua maiti jambo ambalo haliwezekani. Anyway, watakufa na Lowassa wao kama siyo CCM yao.
   
 19. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #19
  Jul 27, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,394
  Trophy Points: 280
  nimeona EL akiwa na vikao na wabunge ndani ya kikao cha bunge!naona wabunge wenzake wanamkubali
   
 20. J

  Jwagu Senior Member

  #20
  Jul 27, 2012
  Joined: Jul 19, 2007
  Messages: 156
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nimeichukia sana CCM kwa uzembe na kutokuwajibika, hasa baada ya kuamua kunyonya wafanyakazi na upuuzi wa SSRA. hata hivyo, tukiacha zazba, nchi ijayo baada ya miaka hii mingi 2.5 (mingi kuliko umri wa uhuru) hivi iliyobaki ya JK, Nikiambiwa nitaje pendekezo la uzalendo na kuangalia mbele na hali tuliyonayo leo, na ukweli wa Mwanakata huu, pendekezo langu ni Zitto, Lowassa (Ubove wake sio sawa na faida zake, watendaji watawajibika, wizi wake kama -upo, ila riba yake sio sawa na asiye mwizi halafu hazalishi), wa tatu ni Dr Magufuli. Dr Slaa, mbowe, Sitta, mwakyembe, mwanry etc nawakubali ila wapewe wizara
   
Loading...