Wabunge CCM kuunda chama?

Kwanza muda wa kuanzisha chama cha siasa na kupata usajili wa kudumu na kisha kushiriki katika uchaguzi utakaofanyika mwaka huu upo? Wanachoweza ni kujiunga na vyama vilivyopo; wachague pa kuweka uzito wao; CUF? Chadema? TLP? NCCR? etc... I bet kama wapo, wataingia NCCR mageuzi, halafu wakishaingia madarakani utagundua ni chama kile kile!!
 
Hakuna wabunge na wanachama vigogo watakaoondoka ccm..wote waoga na wanafiki kuacha mafao yao ndani ubunge pia hawana support wa wapiga kura kama watarudi ccm...anaeweza kuhama na chama kikayumba ni EL pekee....nae ataogopa atawekwa ndani alipuliwe na richmonduli yake!!wengine wote waoga JK alikuwa tayari ana card ya chadema angetoswa(kura zisingetosha) angeibukia chadema apewe agombee urais!!waliobaki waoga na wanafiki?!!!!
 
Mie sichangii kupoteza muda mana katika wale wote hakuna msafi na hakuna shujaa wa kuweza kuihama CCM.Wao wangojee humo humo . Kama unaweza kubwata hadi povu latoka then unamiza kwa kusema unaunga hoja mia kwa mia leo unaweza kuondoka uanzishe Chama? Acheni tu bwana .
 
Hawapaswi kuhama CCM, wapiganie mumo humo. Kuanzisha chama kingine ni kupoteza muda na nguvu zao.
 
wabunge gani hawana nafasi ndani ya CCM, na lini wataenguliwa ili tujue CCM wasafi

Mkuu unatumiwa nini hapa?? JK huyuhuyu unasema kuna wana CCM wamekamatwa kooni, wakati kuanzia JK waliingia madarakani kwa rushwa?? wadanganye haohao!

Suwala la kutumwa kwangu halipo na wala suwala la kuangalia mambo kwa chuki au upepo halipo kwangu na ndio maana naeleza ukweli kwa mujibu wa mambo yalivyo.
Kwani wewe hujuwi kuwa kuna mgawanyiko huko CCM?
Hivyo wewe hujuwi kuwa wanajiita wapiganaji hawana bao CCM?
Hivyo wewe hujuwi kuwa wanaodaiwa kuwa mafisadi ndio wanao sauti CCM?
Ivyo wewe huoni kuwa wanaojiita wapiganaji ndio wanaolalama kuwa wanafanyiwa hujuma majimboni mwao? na wale watuhumiwa wametulia tuli?
Fanya hesabu halafu rudi tena kwenye mjadala.
 
EEH MUNGU bariki jio wa chama kipya, bariki vurugu ndani ya CCM, WAFANYE WASIELEWANE KUELEKEA uchaguzi mkuu, naomba CCM iwafukuze uanachama wapigaji wote, iwafukuze Uanacham,a kina Mengi, Malecela ,Idd Simba, Warioba, quares, na wengine, eeh Mungu baba mfanye Kikwete apatane na Lowassa tena...ili CCM wengine wamkatae kwa sauti moja, nikiomba hayo nikataraji shehe Yahya aaibike yeye nA mapepo yake.....AAMEN.
Kama una dhambi nyingi kama mimi sala hii haitasikilizwa. Wengi wa uliowataja kwenye sala yako hii hawana nafuu wala ahueni yoyote kwa Taifa hili. Wakipata nafasi utawashangaa.
 
hakuna lolote wanachoweza kufanya ni kuhama chama lakini sio kuanzisha chama kipya. Huo ni mkwara mbuzi tu. Hakuna atayefukuzwa chama kwa tuhuma za ufisadi kwanza ufisadi bado haujawekwa kwenye sheria za nchi kwa hiyo hukumu ya ufisadi bado haipo kisheria.
Labda nchi ya enzi za mwalimu lakini siyo hii ya kibepari
 
- Hapa ndipo CCM inapopiga bao kwenye uchaguzi na hizi propaganda zao za kampeni sounds like Ruhinda, sasa tayari ameshashika tena ile kazi yake ya kampeni na Mtandao!

Respect.

FMEs!

Huyu bado ana infulence?Nasikia utu uzima na afya vinamsumbua kwa sasa.Kila jioni jamaa yake(BWM) anaelekea Mikocheni kumjulia hali
 
Mtabiri Maarufu enzi hizo Mr. Naustradamus' alitabiri mambo mengi yaliyotokea moja likiwa-Kutakuja kutokea Kiongozi Maarufu aitwaye Histler ambaye atawaangamiza watu wa kabila moja. Kitendo hicho kitazua vita kubwa ulimwenguni na hatimaye Kiongozi huyo atashindwa vita hiyo. Muda mwingi ulipita baada ya utabiri huo then akaibuka Hitler lakini Mr.Naustradamus katika utabiri wake alikosea herufi moja na kumwita Histler, Hitler aliwaua wayahudi popote pale alipowafikia na akasambaza vita (WWII) kwenye mataifa mengine, jinsi vita ilipozidi kupiganwa Hitler alionyesha kudhoofika, basi watu wakarejea kwenye utabiri wa Mr. Naustradamus kwamba Kiongozi huyo hatimaye lazima atashindwa vita basi Marekani na Waingereza wakajipanga kumtwanga Hitler na kumshinda na utabiri ukawa umetimilika.SASA KWA TANZANIA: Nyerere alisema upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM, wabunge wajaja wameshaliona hilo na wanalifanyia kazi. Waendelee bila kukata tamaa CCM imo mbioni kuanguka na haitaanguka na wote itaanguka na wale ambao ni waumini wake wengine watajiengua na kutegneza chama kingine kitakachoshika madaraka. Kazeni boot
 
hakuna wa kuondoka CCM na kwenda kuanzisha chama...yale yale ya akina Mrema
 
Ni uzushi tu!!! Hakuna mwenye ubavu wa kufanya hivyo ndani ya si si emu.
 
hakuna lolote wanachoweza kufanya ni kuhama chama lakini sio kuanzisha chama kipya. Huo ni mkwara mbuzi tu. Hakuna atayefukuzwa chama kwa tuhuma za ufisadi kwanza ufisadi bado haujawekwa kwenye sheria za nchi kwa hiyo hukumu ya ufisadi bado haipo kisheria.
Labda nchi ya enzi za mwalimu lakini siyo hii ya kibepari

Kwenye hiyo red si kweli kwamba hakuna sheria za ufisadi zipo kuna sheria ya uhujumu uchumi ukiisoma inaeleza mambo hayahaya ya ufisadi ingawa haitaji neno mafisadi, tatizo hapa ni utekelezaji na hasa mtekelezaji wa hizo sheria. Enzi za Mwalimu na Sokoine sheria hizi zilitumika ipasavyo na sisi wananchi tuliziona zikifanya kazi lakini si leo ambapo anayetakiwa kuzitekeleza yeye mwenyewe hajiamini kama ni msafi, hapo ndipo kwenye tatizo na si sheria.
 
Uwezo wa wanasiasa wa CCM kuhama chama upo. Tena ni mkubwa kuliko unavyodhaniwa. Mbona waliwahi kuhama wengi tu, tena katika kipindi ambacho Upinzani ulikuwa unaonekana kama usaliti?

Wanachotakiwa kufanya wanasiasa hao ni kuzingatia muda. Na ili waweze kufanikiwa, litakuwa jambo la ajabu kama wataanzisha chama. Kwa maana, haitakuwa rahisi kwa chama hicho kipya kushiriki uchaguzi mkuu ujao (2010). Wanachoweza ni kutafuta chama ambacho hakina malumbano, ambacho wanaweza kwa haraka kukikuza na kutafuta kura kwa wananchi bila kuanza logistics za usajili.

Kila kitu kinawezekana.

Ukweli ni kwamba, ndani ya CCM hakuna mtu anaeweza kusema yeye peke yake anaweza kukitingisha chama sana kama atahama mwenyewe. Hata JK akiamua kuhama chama hawezi kufanikiwa kushinda uchaguzi Mkuu (hata kama angehama mwaka 2005). Kinachotakiwa ni kundi kubwa kuhama kwa pamoja, na kuingia kwenye chama kimoja wote. Lakini pia, ni lazima watu hao wawe na nguvu ya kuweza kupiga kampeni kali, na wawe wanakubalika kwa kiasi kikubwa (mtaji) kwa wananchi. Maana, kama ni wala rushwa, au watu wasio na uwezo mkubwa kisiasa, hawata leta mabadiliko makubwa sana.

Kundi linalopingana na ufisadi ndani ya CCM linaweza kuleta madhara makubwa kwa CCM, endapo litaamua kukiacha chama hicho.
 
Mtabiri Maarufu enzi hizo Mr. Naustradamus' alitabiri mambo mengi yaliyotokea moja likiwa-Kutakuja kutokea Kiongozi Maarufu aitwaye Histler ambaye atawaangamiza watu wa kabila moja. Kitendo hicho kitazua vita kubwa ulimwenguni na hatimaye Kiongozi huyo atashindwa vita hiyo. Muda mwingi ulipita baada ya utabiri huo then akaibuka Hitler lakini Mr.Naustradamus katika utabiri wake alikosea herufi moja na kumwita Histler, Hitler aliwaua wayahudi popote pale alipowafikia na akasambaza vita (WWII) kwenye mataifa mengine, jinsi vita ilipozidi kupiganwa Hitler alionyesha kudhoofika, basi watu wakarejea kwenye utabiri wa Mr. Naustradamus kwamba Kiongozi huyo hatimaye lazima atashindwa vita basi Marekani na Waingereza wakajipanga kumtwanga Hitler na kumshinda na utabiri ukawa umetimilika.SASA KWA TANZANIA: Nyerere alisema upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM, wabunge wajaja wameshaliona hilo na wanalifanyia kazi. Waendelee bila kukata tamaa CCM imo mbioni kuanguka na haitaanguka na wote itaanguka na wale ambao ni waumini wake wengine watajiengua na kutegneza chama kingine kitakachoshika madaraka. Kazeni boot

Yale yale tu ya Ford Kenya na Ford Asili na hatimaye NARC kule Kenya. Watu walewale, mawazo yao yaleyale, hakuna kipya. Ni sawa na mvinyo wa zamani kwenye chupa mpya!!

Nilishasema hapa, Waafrika tutajikomboa siku moja kutoka kwenye lindi hili ya ujinga na umasikini, lakini kizazi chetu hakitalishuhudia hili, labda watoto wetu!
 
huyu shekhe naye anadanganya watu ,tunasubiri hayo mapinduzi ya wabunge,,Lakini je wana jeuri ya kufanya hivyo?
 
Mtabiri Maarufu enzi hizo Mr. Naustradamus' alitabiri mambo mengi yaliyotokea moja likiwa-Kutakuja kutokea Kiongozi Maarufu aitwaye Histler ambaye atawaangamiza watu wa kabila moja. Kitendo hicho kitazua vita kubwa ulimwenguni na hatimaye Kiongozi huyo atashindwa vita hiyo. Muda mwingi ulipita baada ya utabiri huo then akaibuka Hitler lakini Mr.Naustradamus katika utabiri wake alikosea herufi moja na kumwita Histler, Hitler aliwaua wayahudi popote pale alipowafikia na akasambaza vita (WWII) kwenye mataifa mengine, jinsi vita ilipozidi kupiganwa Hitler alionyesha kudhoofika, basi watu wakarejea kwenye utabiri wa Mr. Naustradamus kwamba Kiongozi huyo hatimaye lazima atashindwa vita basi Marekani na Waingereza wakajipanga kumtwanga Hitler na kumshinda na utabiri ukawa umetimilika.SASA KWA TANZANIA: Nyerere alisema upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM, wabunge wajaja wameshaliona hilo na wanalifanyia kazi. Waendelee bila kukata tamaa CCM imo mbioni kuanguka na haitaanguka na wote itaanguka na wale ambao ni waumini wake wengine watajiengua na kutegneza chama kingine kitakachoshika madaraka. Kazeni boot

Hivyo unafananisha utabiri huu wa Nyerere na watabiri wengine?

Hivyo ulikuwa hujuwi kuwa wakati wa Nyerere hata mwanafunzi ulilazimika kuwa mwanachama wa CCM?
Kama unalijuwa hilo basi huo wa nyerere haukuwa utabiri bali ni kitu obvious na mbona kimeshatokea? You name it viongozi wetu wa upinzani si walikuwa wanachama wa CCM hata kule vyuoni?

Panga panguwa hadi tufute Generation hii wote tulikuwa CCM au Vijana wa CCM.
 
Back
Top Bottom