Wabongo wengi wanaojinadi ni hackers huwa ni kelele tu, kwenye vitendo ni sifuri

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,034
Picha linaanza unakuta profile picture yake ni ya kibabe

1685805179729.png


Ila kwa vitendo sasa unaona kabisa ni sifuri

Wanajua zaidi kupiga domo kwenye misamiati na vitu maneno technical ila vitendo 0, utasikia naweza kupiga sql injection nipate password zote, System naweza kuitungua ddos ile, nikikaa man in the middle attack huchomoki, system ikiwa ngumu kupenya natumia reverse social engineering, n.k. haya sasa mwambie atekeleze, visingizio ataanza ooohh sina bando, Ohh unajua hii system ni mpya. dah sema nina mambo memngi haya mambo inabidi ufocuss.. blablabla.

Laptops zao huwa wanaweka windows wanaongezea na Linux, hio linux inakuwa ya kuzugia tu kujimwambafai "mimi ni hacker siwezi tumia hizo toys za windows" na hapo sasa mwambie aitumie hio linux kufanya chochote tu cha kuhack, mtapoteana !! Kwenye simu nako si haba wana vi apps vya kuzugia, app maarufu ni turmux,

Mafanikio yao wengi huwa ni kupata mafaili ya ha - tunnel, na hapo wameyachukua kwa wahindi na wanaijeria, faili likikubali yani atawasumbua sana, mitandao ikijua kuna file la vpn wakilipiga pini kunaweza kukawa na ukame wa free unlimited interenet kwa miezi hata sita, mda huo hulazimika kutumia vpn zenye kikomo cha MB mfano kwa siku MB 200 tu au kutumia vpn zenye speed ya kobe.
 
Picha linaanza unakuta profile picture yake ni ya kibabe, yani unaweza kudhani hiki chuma kinaweza kutungua system nzima ya jf. 😂😂

View attachment 2644904

Ila kwa vitendo sasa unaona kabisa ni sifuri

Wanaishia tu kujitamba kuinstall termux kwenye simu.

wanaishia kututambia wao hawatumii windows wanatumia kali linux

Mafanikio yao wengi huwa ni kutumia internet kwa free vpn, yani hapo atajiona ni mwamba na nusu.
Wengi ma keyboard warriors tu
 
Wanadakwa kimya kimya mzee acha kabisa nimeshuhudia hii issue jamaa alipenetrate kwenye system ya bank moja hapa nchini inayoanza na herufi N before aliwahi kuingilia mifumo ya mtandao wa simu giant tu hapa TZ na siku hiyo mifumo ya huo mtandao ilisumbua masaa kadhaa na hakuna aliejua zaidi ya tuliokua tunamjua anayoyafanyaga na hakutangazwa kwenye vyombo ya habari afu ni janki tu hivi huwezi kumdhania kabisa... Alidakwa mwezi wa 3 baada ya hilo jaribio la kuvuta mpunga kwa illegal way kwenye hiyo bank sijajua keshi ake imeishia wapi mpaka sasa! Acha kuwachukulia wabongo in general man kuna vijana wanauwezo sema tu niseme sijui huwa wanafanya hacking kwa uoga au nini kinawaponza hata sielewagi...
Shida pia ma it wa bongo wengi vilaza wachache sana wapo vizuri ila wengi oya oya
 
Reverse Eng wa Tz ni script kiddies tu ukiwauliza ili uwe hacker unahitaji Fundamentals zipi ndio utajua kanjanja ni nini ?

Mtu kajikunja na Wireshark yake akihama kahamia kwenye Angry Ip scanner ila nae anasimama na kujiita Hacker.
Afu anaanza na kutangaza kua anaongeza followers insta na kurudisha data za computer kwa bei nafuu kabisa karibu DM.
 
Reverse Eng wa Tz ni script kiddies tu ukiwauliza ili uwe hacker unahitaji Fundamentals zipi ndio utajua kanjanja ni nini ?

Mtu kajikunja na Wireshark yake akihama kahamia kwenye Angry Ip scanner ila nae anasimama na kujiita Hacker.
Kila mfumo una namna ya kuingia na kutoka, sio lazima ujue mamboo mengi, kuingia kwenye mfumo illegal au legal.. unacho hitaji kuulewa vizuri sana utendaji kazi wa huo mfumo..
 
Back
Top Bottom