Wabongo Hawana Nyongo, CCM itashinda Tena! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabongo Hawana Nyongo, CCM itashinda Tena!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by X-PASTER, Jul 31, 2010.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Jul 31, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Wabongo Hawana Nyongo, CCM itashinda Tena!

  WIKI chache zilizopita zilikuwa ni wiki za watu kuchukua fomu za kugombea Urais wa Tanzania. Baadhi ya watu wamejitokeza kuchukua fomu. Hiyo yote ni sawa kabisa. Kilichonivutia zaidi ni wale wagombea wategemewa wanavyojitangazia ushindi kwa jinsi tofauti.

  Unajua sisi wengine tumekuwa na tabia ya kujaribu kupima maneno, hasa katika kujaribu kuelewa mtu ana maana gani anaposema neno au maneno. Kuna wengine huyachukulia maneno juu juu, wakisema tu: "huyu naye, ngoja tuone". Sisi wengine hujaribu kuyaweka maneno katika mizani, kwa sababu lugha ni mfumo mgumu wa mawasiliano, kwani mtu anaweza akasema hivi akamaanisha vile. Vile vile miundo ya maneno inaweza kulingana, lakini ikatofautiana maana. Nitakupa mfano. Mtu akisema: "Makofi!", wale wanaoambiwa hupiga makofi. Lakini akisema: "Kelele!", wale wanaoambiwa hivyo hawapigi kelele, kama ambavyo wangepiga makofi walipoambiwa "makofi!", badala yake hukaa kimya! Ni kwa nini basi wasipige kelele na hali amri yenyewe inafanana na ile ile ya makofi? Ndio maana nasema lugha huwa ni ngumu saa nyingine. Unatakiwa ukae utafakari ili kupata yaliyosemwa, hususan yakiwa ni nyeti, yanayogusa maisha au maslahi yako.

  Kuna mgombea mmoja mtegemewa amenukuliwa akisema tu kwamba atawamshinda wengine, kwa sababu alizoziona yeye. Lakini kuna huyo mwingine, na huyu sikusoma maneno yake gazetini, bali nilimuona na kumsikia mwenyewe kupitia kwenye luninga, akisema kuwaambia washabiki wake kwamba atafanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba chama chake kinashinda. Kauli hii ni nzito kwa watu wanaojua kupima maneno.

  Uzito wa kauli hii unakuja tunapofikiria kwamba kuna ushindani wa vyama mbali mbali, kwa mujibu wa demokrasia. Halafu wanaochagua ni wananchi. Wananchi hawa wanaweza kuamua kwa kura zao kukuchagua wewe au kumchagua mwingine. Sasa unaposema utafanya lolote liwezekanalo kuhakikisha kwamba chama chako kinashinda, hapa kwa wenye kupima maneno pana maswali. Hili "lolote" linalowezekana ni kama lipi? Kwa mfano ikitokea wananchi wengi wakamchagua yule mwingine, hilo "lolote" ni lipi utakalolifanya?

  Kauli hii inanikumbusha zamani kidogo. Baba yetu aliamua kutuchukua likizo moja na kutupeleka kijijini ili tukaelewe kwetu, maana tumekulia mjini. Kijiji chenyewe kilikuwa kinaitwa Komdudu, nasikia siku hizi kimekufa, na kiliuliwa wakati wa kampeni za vijiji vya ujamaa. Kwa hiyo operation vijiji iliua kijiji chetu ili kuleta maendeleo. Sijui yaliletwa!!!??? Tuache hilo.

  Kule kulikuwa hakuna umeme. Wakati wa chakula cha jioni, watu walikuwa wanakaa nje na kula kwa pamoja, huku wakipata mwanga wa kibatari. Saa ya kula alikuwapo mtu wa kudhibiti ulaji wa sisi watoto ili tusile kwa fujo, hasa siku hiyo nyama ikiwa ndio kitoweo. Kaka yangu aliniambia alikuwa akichukia sana kudhibitiwa hasa kwenye kuchukua nyama. Siku moja akaniambia: "Leo kuna nyama. Nitafanya lolote niwezalo nipate nyama nyingi iwezekanavyo". Mimi nilishangaa, hasa nikijiuliza "lolote awezalo" litakuwa nini, atafanyaje na hali kuna udhibiti? Saa za kula zilipofika, nikawa na hamu ya kumuona kaka akifanya hilo "lolote awezalo"

  Kama kawaida, alikuwepo mtu mkubwa wa kutudhibiti, akihakikisha hakuna anayepeleka mkono kwenye nyama, mpaka yeye agawe kwa haki na usawa. Chakula kilikuwa kimezunguukwa na watoto kama nane hivi, na mdhibiti akiwemo. Mara tulishtukia kibatari kimezimika, japo kulikuwa hakuna upepo. Kukawa giza. Mdhibiti wetu akawa anaagiza kibiriti, lakini inaelekea wakati akiagiza kibiriti alikuwa akipapasa kutafuta lile bakuli la nyama, maana alikuwa akiuliza: "Wabwanga! Dibakuli dya nyama dikuhi?" (Yaani: wavulana, bakuli la nyama liko wapi?). Kibiriti kilipofika na taa kuwashwa baada ya kama robo saa hivi, maana ilibidi kitoke uwani huko kwa akina mama, bakuli la nyama lilikuwa jeupe. Nikajua hapa, kaka kafanya "aliloliweza".

  Cha kushangaza ni kwamba bakuli lilikuwa halina kitu, lakini lilikuwa mbali na kaka, ila limesogezwa kati kati ya miguu ya mdhibiti. Amshuku nani? Mimi nilijua ni kaka aliyekula nyama zile, kwani alinikonyeza, lakini nikauchuna. Sana sana wengine walidhani mdhibiti ndiye aliyecheza ile rafu. Alipojaribu kuuliza kama jikoni kulikuwa na nyama nyingine, akaambiwa: "Zisila" (yaani zimekwisha). Tukala ugali na mchuzi mtupu. Baada ya kula kaka peke yake ndiye alikuwa na vijiti vya kuchikolea meno.

  Hofu yangu ni kwamba, hii kauli iliyotoka hapa, ya kufanya lolote mtu aliwezalo hadi chama chake kishinde, isijekuwa lolote ni lile lile la kuzima kibatari. Tahamaki taa ikija kuwashwa, nyama zisila!

  Lakini sina hofu sana na wabongo, kwa sababu nimeona wabongo ni kabila moja la ajabu na la kipekee. Kwa kawaida watoto wote duniani wana nyongo. Ukiwafinya wanalia, akiwatekenya wanacheka. Lakini wabongo wao huwa hawana nyongo, hawajui kulia.

  Ukiwatekenya wanacheka, ukiwafinya wanacheka, ndio maana watu wanaweza kufanya lolote waliwezalo ili wapate wanayoyataka, hata kwa rafu, na wao wakahamaki lakini wakacheka tu, kama sisi na mdhibiti wetu tulivyocheka tu, nyama zilipoondoka.

  Wagombea fanyeni lolote muwezalo mpaka vyama vyenu vishinde. Wabongo hawana nyongo. Ukiwatekenya wanacheka, ukiwafinya wanacheka.
   
 2. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Ulitaka iwe kama Kenya walikjochinjana na kuuana Mkuu.
  Mbona lengo la thread yako haina mantiki inayoeleweka ?
  Mfano wako wa kijiji ulichotoka , sijui wapi, ni wa kusadikika.Na mimi na umri wangu sikuwahi kusikia juu ya hilo unalo propound.
   
 3. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #3
  Jul 31, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kwa baadhi ya watu, fasihi simulizi/andishi ni msamiati mgumu sana kueleweka.
   
 4. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #4
  Jul 31, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Nakubaliana na wewe mkuu. Simulizi yako ilikuwa na ujumbe mzito kwa wale waliouelewa; fasihi simulizi na kimpumu ni vitu mbalimbali!! Lakini safari hii inaelekea wadanganyika hawatakubali kula ugali na mchuzi bila nyama hata wakizima vibatari; kama inavyofanyika na MURAA wa kule Tarime!!
   
 5. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #5
  Jul 31, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,682
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Hebu tueleweshe una maanisha nini Mkuu..:shock:
   
 6. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #6
  Aug 1, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Nina maanisha kwamba kuelewa na kujadili ni kazi ya wasomaji, kutafakali kile kilicho andikwa hapo juu.
   
 7. a

  alibaba Senior Member

  #7
  Aug 1, 2010
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 185
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Mkuu X P,
  Kifupi cha tafakari ni kuwa Uwezo na Mikakati ya vyama vya upinzani ni Mdogo dhidi ya CCM, kwa hali hiyo sidhani kama CCM wana haja ya kuzima Kibatari, CCM watashinda mchana kweupe. Takriban kuna vyama 16 vya siasa ukiondoa CCM abacho ndio kikubwa na tayari kimeshika mpini kwa kuwepo serekalini toka Alfajiri ya Taifa hili. Njia pekee ni kuunganisha vyama ili kuwa na nguvu ya kuikabili CCM. Vinginevyo kuna hatari ya kukosa hata huo mchuzi!!
   
 8. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #8
  Aug 1, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  YOU ROCK; UFISADI HUPOFUSHA MKUU USISHANGAE Huenda kakuelewa ila sasa hana macho akilini
   
 9. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #9
  Aug 2, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mkuu waandika fasihi isiyoeleweka na kujisifu mwenyewe yakhe!
  Kama miye sikuilewa na nikakukosoa ni heri ungejibu yale niliyo kukosoa basi mkuu.
  Kwa vile umeandika fasihi iliyokaaa kimanga'munga'mu basi miye nitaendelea kuku kandamiza!
  Nyongo kama nyongo tunayoifahamuni hatari ikimuingia mtu,
  Nyongo ya kisiasa ndo kasisa usiseme.
  Sasa mtu akiingiwa nyongo haendi kucheza taarab au kunywa gahawa!
  Nyongo ikimkolea mtu anapanda jazba na ustaarabu, akili vyatokea dirishani.
  Hapo tena ni mapanga shaa shaa, virungu moto wa matairi na vinginevyo.
  Sasa mkuu kichwa cha habari yako na nyongo wapi na wapi.Ili CCM itoke wabongo inabidi wapandishe mashetani? na nyongo kufanya kazi yake!
  Ustaarabu umeshasheni kule Kenya na hata kwetu hapa Zenj.
  Mkuu nyongo noma!
   
 10. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #10
  Aug 2, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kumbe kiswahili kazi Kukielewa, pole nilikuwa sifahamu kuwa wewe ni mwana fasihi. Ongera sana mkuu...! Kumbe naweza kujifunza mengi sana kutoka kwako Insha'Allah.
   
 11. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #11
  Aug 2, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  I

  Insha'Allah Maalim, ujumbe usha fika natumai-msg sent
   
 12. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #12
  Aug 2, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ah ah ah hope umenielewa...!
   
 13. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #13
  Aug 2, 2010
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Nimekuelewa fika Maalim,ujumbe ndo uko kibarazani kwako atii,sasa ukiamua kuipekua nguo ya mjumbe basi huo uamuzi wako,ashakum si matusi Maalim
   
 14. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #14
  Aug 3, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Sawa mkuu...! Tupo pamoja.
   
Loading...