Waanzilishi wa Bongo HipHop/Flava ni nani??

Club Billcana ilifunguliwa rasmi 1994 RTD ikitangaza live kila Friday Night Live na Saturday Night Live, mtangazaji akiwa ni Uncle J. Nyaisanga nilimuonaga Ramsey na Adili Kumbuka, Balozi, Dola Soul na madogo fulani wa Upanga, enzi hizo Rap ilikuwa ni watoto wa maisha bora fulani!. Sugu nilikuja mfahamu baadae kidogo, boom ilikuja baadae ya watoto wa uswazi kuingia kwenye game wakianza na Babu, inspector na kina Kalama na Neture enzi za Kigheto ghetto na Mtoto wa geti kali. Ile bifu ya East Coast na West Coast ilichangia kuibua vipaji lukuki.

Pasco
You're right mkuu Pasco....enzi za mwanzo, muziki ulitawaliwa sana na watoto wa ushuani...sana sana, kama sio wote ni wale waliokuwa skul hadi pale makundi kibao kibao yalipoibuka mitaa ya TMK....makundi kama GWM, LWP, Manduli Mob, Gangwe n.k! Dah, nakumbuka enzi zile; una-make hela ya skul, ikatimia hesabu unaenda kuibuka na jeans mpauko, unaiongeza upana chini; linakuwa bonge la bwanga...chini buti; stail ya Naughty By Nature!!
 
Last edited by a moderator:
Na kwa kweli hawa wadau wa mwanzo ndiyo hata hawa wanaoleta majivuno leo hii wanatakiwa kuwashukuru sana. Itakumbukwa enzi zile muziki wa dansi wa bendi mbalimbali ulikuwa uko juu sana. Hivyo ilikuwa ni jitihada za pekee za wakongwe hao kuweza kuwabadilisha wapenzi wa muziki kutoka kwenye ule wa dansi ambao kwa wakati huo ulibamba sana, hadi kuwapeleka kwenye muziki wa KUFOKAFOKA.Wakati ule ilikuwa ni Hip Hop hasa ya kiswahili, kubana pua hamna, ni mistari mikavu bila kupepesa maneno, verse zimeshiba facts, bila kufichA. Na hiyo kwangu nahisi ndo Original Bongo flavor. Wadogo zetu hawa wa Modern Bongo Flavor( labda tuite hivyo) kiukweli wanatakiwa wawaheshimu sana hawa kaka zao. EATV wangeweza kuwatafuta Sugu, na wengine wa Hip Hop ya mwanzo hapa Tanzania wakawaelimisha wadogo zao ni ugumu gani walikumbana nao, lakini ni jitihada gani za kiushawishi walitumia kuwabadilisha Watanzania ambao musiki wa dansi wa bendi za Tanzania na Congo- Zaire ya wakati ule!
Dah! Umekumbusha muziki wa Congo....ilikuwa ni noma; sikutarajia kama jamaa tungewafukuza kwenye soko! Kwa kweli Sugu alifanya kazi kubwa sana kuendeleza huu muziki coz' pamoja na ukweli kwamba akina Salehe Jabir, KU walikuwa wa mwanzo zaidi, lakini hawakudumu sana kwenye game; Sugu ndo alifanya kazi kubwa zaidi kiasi cha kuanza kuwavuta wengine! Halafu kuna Profesa J, hata kama alikuja baadae kidogo lakini yeye alisaidia sana kuufanya huu muziki uheshimike hata na watu wazima wenye heshima zao hususani aliposhuka na Chemsha Bongo..!!
 
Gang Chomba ebu weka basi hizo nyimbo tupate burudani.

1.Kukuru kakara zako wewe zitakuponza acha we achaaa sos b around the country,s to s to the b
2.Wakati wa kujilinda sasa utaenya utakoma na kithaa thaaa Jos mtambo
3.Ni mimi akili inanituma kusema nimesimama ni mimi 2proud
4.Pepsi mirinda mkono ume martin na gari yangu 504 ukisikia naitwa wewe njoo ice ice beibe jabri

Noma sana long tym mwenye mipini ya 80's-90's ya hiphop bongo aziweke humu.
 
Last edited by a moderator:
W.W.A -weusi wagumu asilia, lakini pia kabla yao alikuwepo dika sharp, mukama muganda, con francis hii ni mwaka 1989 pale lang'ata sasa hivi fm sterio...baadae KU kwanza unit wakaja akina nigga one..
 
Saleh Jabir ni wa kwanza kutambulisha bongo flavour. Enzi hizo hata redio moja ya fm hakuna. Alikua akitumia beats za wanamziki wa nje kisha yeye abaweka sauti na maneno yake. Alikua akiuza/wakiuza tape zake kariakoo msimbazi st.Sugu,kwanza unit,prof jize,sos b,gwm,bwp,nature,gangwe mob na wengineo walifuata baadae wakiwa promoted na media house za kwanza kama radio one,itv,ctn nk !kukiwa na kina Deo Mshigeni,Ebony Moalim,Flora Nducha,Rankim Ramadhani,Jacko Guda,Gotta Airie nk. Vijana wengi wa sasa hawajui historia hizo!
 
Salute kwa majembe yote yaliyoufanya muziki wa hiphop uwe juu. Salehe jabir.sugu.ku,dar young mob,gangwe momb,tmk,ect ,mike muhagama,taji liundi,pfunky majani,master jay,bon luv na wengineo. Hip hop ya bongo ipo salama katika mikono ya kina fid q.
 
a k a Afande mwoga!! anaogopa ma under ground balaa.
 
W.W.A -weusi wagumu asilia, lakini pia kabla yao alikuwepo dika sharp, mukama muganda, con francis hii ni mwaka 1989 pale lang'ata sasa hivi fm sterio...baadae KU kwanza unit wakaja akina nigga one..

Umenikumbusha mbali sana mazee, siku ya mashindano Lang'ata Major General Fresh XE alirap alivyopitia vyeo vyote vya jeshi mpaka kufikia hapo
 
Mkuu Mungu akubariki sana sana kama ulikuwepo siku hiyo. Maana ni watu wachache sana watakuwa wanakumbuka siku hiyo. Akina fresh xe mimi nawaheshimu sana ktk bongo hiphop. Hawa wasanii wanaodai wao ni wahasisi wa hiphop bongo wanatudanganya. Sugu hawezi kuwa muhasisi wa hiphop wakati dar young mob niliyoianzisha mimi walimpa deal 1995 alipotoka mbeya kuja dar kabla ya kuwa maarufu.
 
W.W.A -weusi wagumu asilia, lakini pia kabla yao alikuwepo dika sharp, mukama muganda, con francis hii ni mwaka 1989 pale lang'ata sasa hivi fm sterio...baadae KU kwanza unit wakaja akina nigga one..

dadeki,mkuu huo mwaka (1989) mi nilikuwa naanza standard one.
 
Mkuu Mungu akubariki sana sana kama ulikuwepo siku hiyo. Maana ni watu wachache sana watakuwa wanakumbuka siku hiyo. Akina fresh xe mimi nawaheshimu sana ktk bongo hiphop. Hawa wasanii wanaodai wao ni wahasisi wa hiphop bongo wanatudanganya. Sugu hawezi kuwa muhasisi wa hiphop wakati dar young mob niliyoianzisha mimi walimpa deal 1995 alipotoka mbeya kuja dar kabla ya kuwa maarufu.

kuna post moja nilisoma hapa jf ikaniacha na kicheko mno.ilikuwa inasema kipindi hicho sugu alikuwa na pair moja tu ya kiatu,ulikuwa humkosi na sneaker ya DH mguuni.LOL
 
dadeki,mkuu huo mwaka (1989) mi nilikuwa naanza standard one.

Mi nlikua namaliza form four....hahaha. hizo billlicanas, twiga, maggot, pool side, motel agip, kote tumekula bata mbayaa......na coco beach pale kwa alphonsi miaka hiyo ndo palikua mahali pa kuuuza sura kila jumapili. Siku za wiki viwanja vya basket masaki mwisho jeshini. Hao akina nigga one walikuwa wanakaa obay mitaa ya morogoro stores...kwa sasa nikisema q-bar ndo utaelewa zaidi....anyway...yote maisha..
 
For real sugu alipokuja dar alikuwa mshamba sana. Dar young mob walipompa deal ndo akawa maarufu. Yote tisa lakini ukweli unabakia pale pale kuwa sugu siyo mmoja wa waasisi wa hiphop bongo. Professor jay yes alikuwepo enzi zile ingawa alianza rasmi miaka ya 1990. Sambamba na Waasisi wa madj bongo kuanzia 1989: chris phabby, kali kali, choggy sly....
 
sugu alikua na kismati
 
Mi nlikua namaliza form four....hahaha. hizo billlicanas, twiga, maggot, pool side, motel agip, kote tumekula bata mbayaa......na coco beach pale kwa alphonsi miaka hiyo ndo palikua mahali pa kuuuza sura kila jumapili. Siku za wiki viwanja vya basket masaki mwisho jeshini. Hao akina nigga one walikuwa wanakaa obay mitaa ya morogoro stores...kwa sasa nikisema q-bar ndo utaelewa zaidi....anyway...yote maisha..

umetisha kaka. wewe ni real old tymer.nakumbuka ktk makuzi yangu,show ya kwanza kuwashuhudia live kwanza unit waki-perform ilikuwa ni kati ya 1995/6 pale mambo club oysterbay.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom