Waanzilishi wa Bongo HipHop/Flava ni nani?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waanzilishi wa Bongo HipHop/Flava ni nani??

Discussion in 'Entertainment' started by Nzokanhyilu, Jan 6, 2012.

 1. Nzokanhyilu

  Nzokanhyilu JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2012
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,087
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Heri ya mwaka mpya wajameni.
  Naomba kuuliza, nani waanzilishi wa Bongo HipHop/Flava? Mimi nakumbuka mara ya kwanza nasikia tapes za Saleh Jabri akirap juu ya beats za kama Vanilla Ice etc. Tukimwacha huyo, kati ya Kwanza Unit na Sugu, crew gani "imeanzisha" na kuendeleza Hip Hop? Nauliza hivi kwasababu nimegundua kuna mgawanyiko fulani katika MaMC wa Bongo. Sugu mchango wake unaonekana ila naona pia kuna wasanii wanabeef nae sababu tu wako upande wa Kwanza Unit. Lakini kila nikiangalia "maendeleo" haya bongo, naona Sugu anawapiga bao.

  Someone please school me in an unbiased way!!
   
 2. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,155
  Likes Received: 3,346
  Trophy Points: 280
  Kwanza unit nadhani ndo ma legendary wa hiphop hapa bongo. Then akina sugu, balozi, solo thang wanafuata.
   
 3. Nzokanhyilu

  Nzokanhyilu JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2012
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,087
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Legendary kivipi? Kwanini Sugu ana impact zaidi?
   
 4. mpinga shetani

  mpinga shetani JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 3,268
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Duh, hata mimi nawatafuta ... Niwapige risasi
   
 5. F

  Fraddle b JF-Expert Member

  #5
  Jan 6, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 226
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Navyojua salehe jabri alianza halafu ndo kwanza unit na wengine ndo wanafata
   
 6. Nzokanhyilu

  Nzokanhyilu JF-Expert Member

  #6
  Jan 12, 2012
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,087
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Poa, kwahiyo ni sawa kusema kwamba Sugu anafunika wote??
   
 7. n

  namimih Member

  #7
  Jan 12, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kabisa Fraddle b, siku hiyo pale 7 floor New africa ndiyo siku ambayo Saleh Jabir alishangaza alipoingia na Ice Ice Baby lakini kwa kiswahili, wakiwepo akina Marehemu Connie Francis, Ramson na washkaji wengine , enzi hiyo ni new Africa ipo juu sana, ni hayo mashindano ndiyo yaliyoanzisha watu kufikiria kumbe inawezekana kwa kiswahili lakini zaidi ilikuwa kupiga nyimbo za rap za kiingereza, sasa hapa kwenye bongo flava nadhani hao akina Njaidi wanahusika sana, sijajua kama Rap za bongo zimo kwenye kundi la bongo flava, vinginevyo naamini Sugu na akina Balozi wamo katika kundi la kwanza. ni mchango wa habari tu.
   
 8. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #8
  Jan 12, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Ruka Kama Ninja tua kama ndege Airpot huyo ndiye salehe Jabiri aliyewafumbua macho wa Tz. Kwanza unit na Diplomat walikuwa wanatumia za kigeni.
   
 9. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #9
  Jan 12, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,155
  Likes Received: 3,346
  Trophy Points: 280
  wote wameleta impact.
   
 10. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #10
  Jan 14, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Salehe alianza na Ice Ice kisha akaja na OPP ambazo zote nazimiliki ktk CD, salute na heshima kwa huyu kiumbe.
  Kisha Mawingu ya kina Othman Njaidi na nyimbo yao ya Oya msela ooya hawakuwa nyuma, K-U crew, Sugu, Sos B na kukuru kakara zako wewe zitakuponza, the Diplomatz, nakumbuka pia kulikuwa na upanga mashariki na upanga magharibi, kisha wakaja HBC na Gangwe Mobb, Daz Nundaz pia hawakubaki nyuma, Mabaga na wateule nao wakafumuka na kisha na kisha na kisha na kisha na kisha.....
  Kuna mtu nilishawahi kumpa kubwa la bimkubwa wake pale alipomtaja Fid Q kuwa ni Komredi ktk hii game.
   
 11. Mkare_wenu

  Mkare_wenu JF-Expert Member

  #11
  Jan 2, 2014
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  Hii topic nimeipenda iendelee kamavipi
   
 12. Mkare_wenu

  Mkare_wenu JF-Expert Member

  #12
  Jan 2, 2014
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  " Soggy alifanya tracks kama bado nakutesa akiwa
  Bantu Pound Gangsta akiwa na akina Caz T Kipindi
  wapo shule Mbeya lakini si wa kwanza kurekodi.
  Kuna akina Kwanza Album nzima mawingu pale
  Mwenge. Sos B pia Hashim Dogo wa Long time ktk
  Game. MSISAHAU mi toung twista ya Tuff Jam wa
  Hard blaster ngoma kama usiige mambo ya
  mjini ,matapeli ni kati ya ngoma kibao za zamani.
  Kwanza unit Akina Marehemu D Rob, Fresh G, Eazy
  B, Rhymson kuwataja wachache ngoma kama
  Haturap, Amani...... kwa kifupi wa kwanza kurekodi
  akirap kwa kiswahili ni Saleh jabir."

  Hayo ni maneno ya BRIAN HAULE from Facebook
   
 13. Mkare_wenu

  Mkare_wenu JF-Expert Member

  #13
  Jan 2, 2014
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  " saleh jabir alitoa album ambayo ni nyimbo zilizohit
  kipindi hicho na yeye kurap kupitia midundo ya hizo
  nyimbo mfano naughty by nature-opp na ghetto
  bustard album ikauzwa mtaani pia fresh g wa kwanza
  unit nae akatoa mix tape yake kama alivyofanya
  salehe jabiri ilikuwa kama dis flani kwa salehe
  jabir,kwa swali la mwandambo nadhani jibu ni salehe
  jabir kama kuna mtu anajibu lingine atupe"

  by Patrick Togorai from Fb
   
 14. mdukuzi

  mdukuzi JF-Expert Member

  #14
  Jan 6, 2014
  Joined: Jan 4, 2014
  Messages: 5,372
  Likes Received: 4,222
  Trophy Points: 280
  diamond anashangaa mnaandika vitu gani ivi alikuwa hajazaliwa utoto raha kila kitu kwako ni historia kama magofu ya kaole
   
 15. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #15
  Jan 8, 2014
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,447
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  kuna nyimbo ilikuwa inaibwa hivi " ukimwi moto chini dawa ya homa ni kwinini dawa ya mapenzi ni ugumu( ugumu dawa yenye.....tunasema" siujui jina sijui waliimba kina nani ni zamani sana kama kuna mwenye idea anikumbushe
   
 16. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #16
  Jan 8, 2014
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,447
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  mkuu mi nilikuwa nanunua tape enzi hizo alafu zinapotea kwenye mazingira ya kutatanisha.....kama vipi nisababishie hiyo ya soleh jabil
   
 17. a

  allydou JF-Expert Member

  #17
  Jan 8, 2014
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 1,485
  Likes Received: 572
  Trophy Points: 280
  Hahaahahahahaa dah nilikuwa sikafurahi kivile. Watu mnamaishairi balaaa.
   
 18. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #18
  Jan 15, 2014
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Dah! Mzazi kama unamiliki hiyo makitu basi nitakutafuta manake nilikuwa na tape tu enzi zile....ilikuwa kila nikitoka skonga naweka tape ya Salehe Jabiri...basi dada jirani angu mmoja akanichapa, akaiharibu...kisa, kuna mistari ilikuwa inasema "sikutaki sikupendi kwa sababu ni feki, huna sura nzuri wala huna; BLACK! Hasa, ukijitia urembo, Haupendezi na hayo manywele ya kalikiti, na masikio kama tembo....!" dah, enzi zile urembo ni full kalikiti!!

  Anyway, kumbukumbu zangu kama zipo sawa, Salehe Jabir ni muanzilishi....KU Crew, wakalisongesha game...Mr. II ndie ametoa mchango mkubwa zaidi! DPT nao huwezi kuwaacha nyuma, halafu kuna washikaji fulani walikuwa wanajiita Weusi Wagumu Asilia-WWA; hawa walitoa album zamani sana...i think back 1994! GWM na Cheza Mbali na Kasheshe walikimbiza mbaya; wakaja Nigers II Public, aka N2P...hawa walikuwa wanapatikana mitaa ya Kurasini!! Kulikuwa na Da Young Mob, long time...bila kuwasahau LWP...utakoma, utaenya, na kidhaa dhaaa, wakati wa kujilinda sasa...!! Jose Mtambo na mwenywe jamaa ni long time; back 1990s bila kuwasahau akina Njaidi na Msela yao!!!

  Fid Q, anatisha lakini kaja juzi tu kwenye game; tena wakati Gangwe Mob wameshatoboa na Ngangari yao!
   
 19. C

  CHAZA JF-Expert Member

  #19
  Jan 15, 2014
  Joined: Dec 21, 2012
  Messages: 6,666
  Likes Received: 2,146
  Trophy Points: 280
  Na kwa kweli hawa wadau wa mwanzo ndiyo hata hawa wanaoleta majivuno leo hii wanatakiwa kuwashukuru sana. Itakumbukwa enzi zile muziki wa dansi wa bendi mbalimbali ulikuwa uko juu sana. Hivyo ilikuwa ni jitihada za pekee za wakongwe hao kuweza kuwabadilisha wapenzi wa muziki kutoka kwenye ule wa dansi ambao kwa wakati huo ulibamba sana, hadi kuwapeleka kwenye muziki wa KUFOKAFOKA.Wakati ule ilikuwa ni Hip Hop hasa ya kiswahili, kubana pua hamna, ni mistari mikavu bila kupepesa maneno, verse zimeshiba facts, bila kufichA. Na hiyo kwangu nahisi ndo Original Bongo flavor. Wadogo zetu hawa wa Modern Bongo Flavor( labda tuite hivyo) kiukweli wanatakiwa wawaheshimu sana hawa kaka zao. EATV wangeweza kuwatafuta Sugu, na wengine wa Hip Hop ya mwanzo hapa Tanzania wakawaelimisha wadogo zao ni ugumu gani walikumbana nao, lakini ni jitihada gani za kiushawishi walitumia kuwabadilisha Watanzania ambao musiki wa dansi wa bendi za Tanzania na Congo- Zaire ya wakati ule!
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  Jan 15, 2014
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,621
  Trophy Points: 280
  Club Billcana ilifunguliwa rasmi 1994 RTD ikitangaza live kila Friday Night Live na Saturday Night Live, mtangazaji akiwa ni Uncle J. Nyaisanga nilimuonaga Ramsey na Adili Kumbuka, Balozi, Dola Soul na madogo fulani wa Upanga, enzi hizo Rap ilikuwa ni watoto wa maisha bora fulani!. Sugu nilikuja mfahamu baadae kidogo, boom ilikuja baadae ya watoto wa uswazi kuingia kwenye game wakianza na Babu, inspector na kina Kalama na Neture enzi za Kigheto ghetto na Mtoto wa geti kali. Ile bifu ya East Coast na West Coast ilichangia kuibua vipaji lukuki.

  Pasco
   
Loading...